Hatua Saba (7) Za Kuweka Malengo Na Kuweza Kutimiza Ndoto Zako.
Kuweka malengo ni sawa na kuchora ramani ya sehemu uendako. Bila kuwa na ramani ni sawa na kutembea safari usiyoijua. Ni rahisi zaidi kufanikiwa katika hali ngumu ukiwa na malengo kuliko kufanikiwa katika hali rahisi bila malengo. Ni ngumu sana kufika uendako kama hujui njia. Bila malengo madhubuti ni ngumu sana kwako kufikia ndoto zako. Anza kuweka malengo yako leo, usichelewe kwani hakuna kesho ambayo imewahi kufika. Ukiweka malengo utapata msukumo kutoka ndani mwako na hivyo kuwajibika/kulazimika kutimiza ndoto zako.
1. Amua unachokihitaji katika maisha yako
Ili uweze kufanikiwa ni lazima uamue ni kipi cha kuwa nacho katika maisha yako. Kama unahitaji pesa jaribu kuweka kiasi ambacho unahitaji baada ya muda fulani. Mfano milioni moja kwa mwezi au milioni hamsini kwa mwaka. Hii itakufanya muda wote uone kama una deni na hivyo kufanya kila linalowezekana kufikia malengo yako. Weka malengo yako kama kuwa na afya njema, kujenga, biashara, siasa na kadhalika. Hakikisha vile unavyoamua kutoka moyoni ni vile vyenye faida kwako.
SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.
2. Andika malengo yako kenye karatasi/daftari
Baada ya kuamua unachokitaka maishani mwako sasa ni wakati wako wa kuweka malengo na kuandika kwenye karatasi au daftari dogo maarufu kama diary. Nakushauri uandike kwenye daftari maana ukiandika kwenye karatasi ni rahisi kupotea kuliko kwenye daftari dogo. Hakikisha unasoma vile ulivyoandika mara nyngi ili uweze kukumbuka na kuona kama deni kwako. Ukishaandika malengo yako ni kama umechora ramani ya vita, hivyo una sehemu ya kuanzia katika mapambano yako. Kuna siri kubwa iliyopo baina ya kuandika na ubongo wako.
3. Weka muda wa mwisho kwa kila lengo ulilojiwekea
Weka mwisho wa kila lengo ambalo utajiwekea, kama lengo ni kubwa inakubidi uligawanye katika vipande vidogo vidogo na hivyo kuwa rahisi kulimiza. Ukiweka muda wa mwisho (deadline) unapata msukumo kutoka ndani mwako. Weka muda wa mwisho kwa kila lengo. Usijiwekee malengo makubwa mno katika muda mfupi kwani ukishindwa kulitimiza unaweza kufa moyo.
4. Orodhesha vitu vitakavyokufanya ufikie lengo lako
Kila siku buni njia mpya zitakazokufikisha katika malengo yako. Waza na fikiria njia mpya kila mara. Orodhesha vitu na mawazo yako katika daftari dogo. Kumbuka bila kuandika vitu hivyo hutaweza kufikia lengo lako kwa urahisi. Orodha ya vitu vitakavyokufikisha katika ndoto zako ni sawa na barabara katika ramani.
SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
5. Chukua hatua/weka katika matendo
Baada ya hatua hizo nne sasa ni wakati wa wewe kuchukua hatua na kufanya katika matendo. Weka katika mpangilio kiasi kwamba unaanza na vile vyenye umuhimu zaidi mpaka vile vyenye umuhimu mdogo. Hii ni kwamba utaweza kutimiza vile vyenye kukufikisha katika kilele cha ubora wako. Ukianza kufanya vile visivyo na umuhimu kwanza basi utakuwa katika nafasi ngumu sana kufikia ndoto zako. Usiahirishe kwani uhairishaji (procrastination) hufanya usifanikiwe na hivyo kula muda wako bure. Chukua hatua leo kwani hakuna siku nyingine unayoijua zaidi ya leo.
7. Fanya jambo moja kila siku kutimiza malengo yako
Pengine hili ndilo jambo kubwa na la muhimu zaidi katika malengo yako kuweza kufikia ndoto zako. Ukiweka malengo bila kufanyia kazi itakuwa ni kazi bure. Fanya jambo moja kila siku ambalo litakupeleka hatua moja mbele zaidi ya jana. Maneno bila matendo ni kazi bure. Waswahili walisema ‘’maneno matupu hayavunji mfupa’’. Unatakiwa pia kuwa madhubuti na kuamua kutoka moyoni (commitment) mwako kufikia ndoto zako.
Ndugu msomaji nakuhimiza kuweka malengo yako leo na kuanza kufanyia kazi. Kama hutaweka malengo, ni sawa na kwenda vitani bila kuwa na ramani ya vita. Ni rahisi sana kushindwa bila ramani kwani kamwe hutajua unakoenda na hivyo utaishia usipopenda kuwepo.
Nakutakia kila la kheri katika kutimiza ndoto zako.
Makala hii imeandikwa na Nickson Yohanes
Unaweza kuwasiliana na nae kwa kwa: simu: 0712 843030/0753 843030
e-mail: nmyohanes@gmail.com
Pia unaweza kutembelea blog yake: www.lifeadventurestz.blogspot.com kujifunza zaidi
Pia unaweza kujiunga na email list yetu kwenye Life Adventures uweze kupata Makala kila zinapotoka.
5/19/2015 07:30:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Sifa Sita(6) Unazohitaji Ili Kuwa Mjasiriamali Bora.
Kumekuwa na maswali mengi sana katika mitazamo tofauti juu ya ujasiriamali kwa mfano ujasiriamali ni nini? Na mjasiriamali ni mtu mwenye sifa gani?. Basi mpenzi msomaji wa makala hii ya leo utapata kujua nini maana ya ujasirimali na sifa mjasiriamali ni zipi.
Ujasiriamali nini?
Ujasiriamali ni uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi zinazojitokeza na kugeuza au kutumia changamoto hizo kama fursa. Kwa mfano eneo A kuna shida kubwa ya maji basi mjasiriamali atakabiliana changamoto hiyo kwa kuchimba kisima cha maji na hatimaye atakuwa ametupia changamoto hiyo ya maji na kugeuza kuwa fursa.
Sifa za kuwa mjasiriamali bora
- Uwezo wa Kuona Fursa
Mjasiriamali lazima uwe na jicho la kuona fursa au uwezo wa kuona fursa katika jamii yako inayokuzunguka. Mjasiriamali anatumia changamoto zinazojitokeza katika jamii yake na kutumia changamoto hiyo kama fursa kwake. Kwa mfano sehemu unayokaa watu wanauhitaji wa huduma za kibenki kama vile tigo pesa, m-pesa ,airtel money nk. Basi mjasiriamali anaona hiyo fursa kwake kwa kuanzisha vibanda hivyo vya kutolea huduma za kibenki.
SOMA; Njia Rahisi Ya Kutengeneza Matatizo Makubwa Kwenye Maisha Yako.
- Ubunifu
Kama mjasiriamali yakupasa uwe mbunifu. Baada ya kuona fursa sasa katika eneo Fulani buni kitu tofauti, kuwa wa kipekee kwa mfano kama unatengeneza chapati basi zifanye chapati hizo kuwa tofauti na za wengine. Mshawishi mteja onesha utofauti wako katika ubunifu wa bidhaa au huduma unayotoa.
- Kuwa Mvumilivu
Mjasiriamali siyo mtu wa kukata tama, mjasiriamali ni mtu mvumilivu. Tutambue kuwa hakuna mafanikio ya haraka na mafanikio hayatokei kama vile radi au ajali. Bali mafanikio katika jambo lolote lile yakupasa uwe mvumilivu sana, vilevile katika safari ya mafanikio kuna changamoto nyingi sana. Mafanikio yoyote yale yana changamoto hivyo basi uweke hili akilini mwako.
SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uweze Kufikia Malengo Yako.
- Mtu Mwenye Malengo
Mjasiriamali ni mtu mwenye malengo. Lazima uwe na malengo ya muda mrefu na mfupi huwezi kuwa mjasiriamali bora kama huna malengo. Lazima ujiwekee malengo kwa mfano ndani ya mwaka mmoja unahitaji ufike wapi, kama umekosa kuwa na malengo umekosa sifa ya kuwa mjasiriamali bora.
- Ari ya Kufanya Kazi/Kujituma
Mjasiriamali unatakiwa kuwa mtu mwenye ari ya kufanya kazi au kujituma kwelikweli ,mtu wa kujitoa unahitaji masaa ya ziada katika kujitoa kwako . Ondoa uvivu, unabidi uweke juhudi ya kufanya kazi, lazima upende kazi yako usiwe mtu wa kusukumwa bali kuwa mtu wa kujituma.
SOMA; Upya Wa Biashara Mpya Na Unavyoweza Kuutumia Vizuri…
- Mtu Anayependa Kujifunza
Kama wewe ni mjasiriamali halafu huwezi kujifunza basi unapitwa na mengi sana. Mjasiriamali unatakiwa kujifunza kila siku kitu kipya, soma vitabu mbalimbali ,jifunze kwa watu waliofanikiwa kila siku kwani kujifunza hakuna mwisho na elimu haina mwisho, hudhuria semina mbalimbali upate maarifa mapya.
Hivyo basi,mjasiriamali anatakiwa awe mtu wa kuongeza thamani na mtu mwenye jicho la kuona fursa katika jamii inayomzunguka.
Makala hii imendikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com
5/18/2015 07:30:00 AM | Labels: UJASIRIAMALI | 0 Comments
Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani - 2
Karibu tena kwenye mwendelezo wa makala hii . Kama haukusoma makala iliyopita unaweza kusoma kwa kubonyeza maandishi haya; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani
1. Sio kila wakati utakua sahihi.
Tambua kuwa sio kila wakati utakua sahihi. Kuna nyakati unaweza kukosea na usitambue kuwa umekosea. Sikiliza maoni ya wengine na ushauri wao pia. Maisha ni kujifunza, tunajifunza kila kukicha kutokana na matukio na kutoka kwa watu mbalimbali wanaotuzunguka. Ili kubadilika na kukua ni vizuri kukubali kwamba sio lazima kila wakati tuwe sahihi. Kuna wakati mwingine tunakosea na wanaotuzunguka wanaweza kutushauri na tunatakiwa kufanya maboresho katika maeneo husika.
2. Waza juu ya mambo mazuri kuhusu wengine.
Fikiri juu ya mambo mazuri kuhusu wengine. Wawazie mema watu wengine, usiwaze mabaya juu yao. Ukiwaza kuwatendea vizuri wengine basi utawatendea hivyo. Ukiwaza vibaya ni lazima utawatendea vibaya.
Hata kama wale wanaokuzunguka wanakutendea vile usivyopenda, usiwawazie mabaya. Endelea kuwatendea na kuwawazia mazuri. Kama kila mmoja angefanya hivi basi sisi sote tungeishi kwa amani. Anza wewe kufanya hivi na ulete mabadiliko mahali ulipo.
SOMA; BIASHARA LEO; Usianze Biashara Upya Kila Siku…
3. Usiingilie kati mwingine aongeapo.
Jitahidi kuwa msikivu wakati mtu mwingine aongeapo na wewe. Subiri mwenzio aongee mpaka mwisho ndipo umjibu. Kuingilia kati mtu mwingine aongeapo ni dalili ya kudharau kile anachoongea na kuona kuwa yale unayotaka kuongea wewe ndiyo ya maana zaidi. Lakini hii pia ni dalili kuwa haumsikilizi ila kuna vitu unawaza kichwani mwako kwa wakati huo huo.
Kama mtu anakuambia kitu ukamwingilia kwa kumalizia sentensi yake na yeye hakutaka kuimalizia kama hivyo ulivyoimalizia, unamnyima mnyima mtu huyo nguvu ya kuendelea kuongea na wewe tena. Hivyo unaweza kukuta watu wengi hawapendi kukaa na kuongea na wewe kwakuwa kila mara wewe hupenda kuwa muongeaji mkuu.
4. Jifunze kuwa na huruma, kusamehe na kuomba msamaha.
Katika maisha ya kila siku mambo mbalimbali hutokea ikiwemo kuudhiwa na watu wengine. Ni vizuri kuwa na huruma , kuwahurumia wanaotukosea na kuwasamehe pia. Kwakuwa kama mtu akikukosea na ukakasirika anayebaki na maumivu ni wewe na si mkosaji. Hivyo kwa usalama wako mwenyewe ni bora kuamua kusamehe na kuendelea na maisha yako ya furaha.
Lakini pia ni vizuri kuomba msamaha pale tunapokosea. Kuomba msamaha haimaanishi kuwa umejidhalilisha kwa mtu uliyemuomba msamaha ila ni ishara kuwa hukupenda kufanya jambo ulilolifanya na ungependa yule uliyemfanyia aliachie na muendelee na maisha ya amani na furaha kama hapo awali.
SOMA; Mambo 20 niliyojifunza Kwenye Kitabu LITTLE BETS.
5. Usiwe mtu wa lawama.
Usiwalaumu wengine kwa kila baya linalotokea. Kwa kuwa na lawama utajikuta ukigombana na kila mtu anayekuzunguka. Chukua jukumu kwa vitu ambavyo havikwenda sawa na uangalie ni nini haukukamilisha au haukukifanya kilichosababisha kwa namna moja au nyingine mambo kwenda tofauti na ulivyotarajia. Ukiwalaumu wengine huwezi kubadilika , huwezi kukua na huwezi kufanya marekebisho pale ulipokosea.
6. Kumbuka kuwa chanzo cha furaha yako ni wewe mwenyewe.
Usisahau kuwa wewe mwenyewe ndiye mwenye jukumu la kujipa furaha na sio mtu mwingine yeyote au kitu chohote kile. Ukishakua na furaha basi ni rahisi hata watu wanaokuzunguka kuendelea kuidumisha furaha yako na hata wakifanya kinyume na hivyo basi endelea kuwa na mtazamo chanya ndani yako na utaweza kuitunza furaha uliyonayo.
SOMA; Njia Rahisi Ya Wewe Kuondokana Na Tabia Usiyoipenda.
7. Usipende kuongelea habari za wengine.
Jitahidi usikae kati ya watu na kuanza kumjadili mtu mwingine na kumzungumzia mambo mabaya. Fanya shughuli zako ukimaliza soma, sikiliza kanda nzuri zinazojenga. Ongea na watu kuhusu mambo ya maendeleo na vitu vitakavyokufanya ukue. Kujiepusha na kuongelea mambo ya watu kutakuweka mbali na chuki na ugomvi na watu wengine.
Kumbuka kua ulimwengu huu unachangamoto nyingi. Zipo kila sehemu, hakuna mahali utakapokwenda kuishi ambapo kutakuwa hakuna changamoto. Hivyo ni vizuri kuwa makini na kujifunza kuishi na watu vizuri ili uweze kukamilisha majukumu yako ya kila siku na kufikia malengo ya maisha uliyojiwekea. Maisha ni mtihani ni vizuri kutafuta ujuzi kila siku wa namna ya kufaulu mtihani huu.
Nakutakia utekelezaji mwema wa haya uliyojifunza.
Kama una swali, maoni au ushauri usisite kuwasiliana nami.
MWANDISHI: ESTHER NGULWA
MAWASILIANO: 0767 900 110 / 0714 900 110
5/15/2015 07:30:00 AM | Labels: MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Kanuni Sita(6) Muhimu Za Kushinda Tatizo Lolote Unalokutana Nalo.
Matatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hapati A au B lakini anafaulu. Kwa mwanafunzi anaweza akalipuuzia kwa kigezo kuwa hajafeli.
Kamwe usilipuuze tatizo wala usipuuze uwezo wako wa kukabiliana na tatizo. Tambua kuwa tatizo unalokutana nalo kuna mamilioni ya watu duniani wameshapitia tatizo kama hilo. Ukiwa na mtazamo chanya kuhusu tatizo utabadili tatizo na litakupatia uzoefu. Na unapokosa mtazamo sahihi kuhusu tatizo unalokumbana nalo itasababisha tatizo husika kuwa kubwa zaidi.
SOMA; UKURASA WA 75; Kila Mtu Ana Matatizo…
Siri kubwa ambayo imewafanya watu waliofanikiwa kuendelea vizuri ni mtazamo juu ya matatizo wanayokutana nayo. Hapa nakuletea kanuni sita kuhusu matatizo na ambazo ukizifanyia kazi ipasavyo wewe pia utakuwa mshindi kwa kuwa kila unapokutana na tatizo utakuwa sehemu ya utatauzi wa tatizo husika.
1. Kila mtu anayo matatizo
Usifikiri ukishafanikiwa utakuwa ndio umeyaaga matatizo, kadiri unavyofanikiwa ndivyo matatizo unayatengeneza mapya. Mafanikio huwa hayaondoi matatizo bali hutengeneza matatizo mapya. Kwa mfano inawezekana unafikiri ukipata kazi fulani ndo utakuwa umefanikiwa Sana, lakini kumbe unaweza kupata hiyo kazi lakini bosi wako akawa ni mkorofi. Sawa suluhisho unaweza kufikiri ni kujiajiri hapo pia utakutana na matatizo ya kushughulika na wafanyakazi wako ili wazalishe zaidi. Kubaliana na uhalisia kuwa Hakuna mtu ambaye yuko huru hana matatizo bali kutegemeana na shughuli unayojishughulisha nayo basi utakutana na matatizo yanayoendana na shughuli husika
2. Kila tatizo lina ukomo wake
Hakuna tatizo ambalo ni la kudumu yaani litakuwepo milele. Muda wa uhai wa tatizo ukiisha litakufa kwa kuisha/kutokuwepo kabisa na litapita. Kila tatizo huwa lina muda wake ambao kiuhalisia ni mdogo kwa hivyo hakuna haja ya kukwepa au kukimbia tatizo kwa kuwa ukikwepa tatizo sio kuwa unatatua tatizo bali unatengeneza matatizo mapya.
SOMA; Kila Suluhisho Linatengeneza Tatizo, Chagua Ni Tatizo Gani Unataka.
3. Kila tatizo lina fursa
Tatizo linaweza kuwa tatizo kwa mtu mmoja ila kwa mtu mwingine linaweza kuwa fursa. Mfano hospitali zipo kwa sababu watu wanaumwa au wanasheria wapo kwa sababu kuna matatizo ya kisheria. Kwa hiyo kwa mgonjwa ana tatizo la kuumwa lakini mtu mwingine amabaye anafikiria kuhusu kutatua matatizo ya magonjwa mbalimbali atafungua hospitali kutibu magonjwa yanayosumbua jamii na hivyo kumpatia fursa kwa kuwa atalipwa anapotoa huduma hiyo.
4. Kila tatizo litakubadilisha
Hakuna tatizo ambalo litakuja katika maisha yetu na kutuacha kama lilivyotukuta. Tatizo litakufanya uamke au uchangamke na usonge mbele. Na hii ni kwa sababu ya wewe kuwa na uwezo wa kuchagua tatizo husika likkufanyie nini katika ujuzi wako, uzoefu wako, au likufundishe nini ili uweze kuwa na uwezo stahihi wa kutatua tatizo husika.
SOMA; Usinunue Matatizo Ya Watu.
5. Unao uwezo wa kuchagua tatizo likuathiri vipi/kwa kiwango gani
Namna ambavyo unavyolikabili tatizo linavyokutokea inaamua pia athari ya tatizo husika kwako.Inawezekana usiwe na uwezo wa kuchagua tatizo linalokutokea lakini unao uwezo wa kuchagua namna unavyolikabili tatizo.
6. Kuna namna chanya na hasi jinsi ya kukabili kila tatizo
Mara zote chagua namna chanya ya kutatua tatizo kuliko namna hasi ya utatuzi wa tatizo. Jambo la msingi ni kuwa kama huwezi kutatua tatizo basi unahitaji kulisimamia kwa ubunifu. Unapotatua tatizo leo unakuwa ni sehemu ya suluhisho la tatizo na hivyo itakupelekea kufaidika na faida zinazoambayana na kutatua tatizo husika.
Kumbuka utatuzi wa matatizo hufanywa rahisi kama matatizo yatachukuliwa au kutazamwa kama changamoto.
Mwandishi: Goodluck Moshi
Mawasiliano:
Whatsapp: +255 753 201 994, Telegram: +255 658 201 994, Barua pepe: eng.gmoshi@gmail.com Facebook: Goodluck Moshi
Pia unaweza kutembelea blog yake www.stadizamafanikio.blogspot.com kujifunza zaidi.
5/14/2015 07:33:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Jinsi Unavyoweza Kutumia Changamoto Kama Fursa Ya Kujifunza Zaidi.
Kuna wakati katika maisha tunakutana na changamoto ambazo zinatulazimisha kuacha au kusimama kabisa kuishi ndoto zetu au kuzitimiza.
Ndugu yangu huenda kweli unapitia kitu ambacho ukikiangalia unaona ni kweli hutakiwi kuendelea na mambo mengine, pengine kwa kuwa hauna uwezo tena na nguvu za kufanya hayo mambo, lakini hata katika hali hiyo kipo unachoweza kujifunza, kipo unachoweza kufanya kama tu utaamua kubadili namna unavyoangalia mambo na kuyachukulia. Unaweza tumia hiyo changamoto kama fursa ya kupata au kujifunza mambo mengine hata kwa watu wengine unaokutana kutokana na changamoto hiyo. Usiiangakie changamoto hiyo tu mpaka ukashindwa kupata kile ulitakiwa upate hapo, bali hakikisha unapata kile ulikusudiwa kukipata kwenye changamoto hiyo, hakikisha unaelewa somo, hakikisha unapotoka hapo unakuwa ni mtu mwingine , unakuwa umejifunza kitu, unakuwa una kitu kipya cha kujifunza au hata kushirikisha wengine. Hata kama ni tatizo kubwa kiasi gani bado lipo unaloweza kujifunza hapo kama tu utaamua kubadili namna unavyotazama mambo ndugu yangu.
SOMA; Najua Umeshasikia Hili Mara Nyingi, Sio Vibaya Ukasikia Tena Na Leo.
Unaweza kuwa unaumwa , umelala kitandani huwezi lakini bado unaweza kujifunza hata kwa kulala kwako pale maana bado unakuwa na uwezo wa kufikiri na kutafakari mambo na pengine hata kuona jinsi mambo yanavyoenda. Unaweza jifunza hata kwa kuangalia wale wanakuhudumia au wanaokuja kukutembelea jinsi wanavyochukulia hali yako, lipo unaloweza kujifunza pale ndugu, maana mfano ukiangalia wewe ndiye unayeumwa na pengine unaelewa zaidi maumivu unayopitia, unaelewa zaidi hali unayoipitia lakini mtu mwingine anaweza jidai au dhani kwamba kwa kuwa alishawahi ona mtu mwenye tatizo kama lako basi atafikiri anayaelewa hata maumivu yako, kwa kuwa analinganisha na ya yule huyu unatakiwa kumwelewa na kwenda naye kama alivyo. Mwingine atajidai ni mtaalamu zaidi ya daktari hivyo anaweza akatumika kukuchanganya zaidi badala ya kuwa pale kukufariji, mwingine atakuja pale kuona jinsi gani unaumwa na apate cha kwenda ijuza jamii au naye aonekane alikuja na anakujali lakini kumbe lengo ni apate tu cha kwenda kuongea kwa watu. Lakini mwingine ni kweli anajali, anakupenda anaumizwa na hali unayopitia anatamani kuona ukiinuka,ukisimama tena na kuendelea na harakati za maisha huyu ni mtu mwema kwako, ni ndugu/rafiki mwema anakupenda kweli, anakutakia mema na huyu anakufanya hata wewe usiangalie kile unapitia na kujifunza hata kwa huyu kwa namna anachukulia hali yako na kwa upendo anakuonyesha katika wakati huu, anakufanya uone kama una deni kwake na jamii kwa ujumla kwa namna amekubeba katika hali unayopitia, katika jamii hawa ni wachache sanaa.
SOMA; Hiki Ndio Kitakachotokea Miaka 100 Ijayo..
Lakini wakati mwingine unapokuwa kwenye changamoto au niseme mitihani ya maisha inaweza kuwa wanaokuzunguka ndio wanakatishwa tamaa zaidi na hali unayopitia hivyo badala ya wewe kutaka au kutegemea kuhurumiwa zaidi unaweza geuka msaada kwao kwa kuwafariji, kuwatia moyo kuwafanya wasikate tamaa, waamini kwamba inawezekana kuinuka tena, inawezekana kusimama tena na hata isipowezekana wanatakiwa kukubali kuwa haijalishi nini kinatokea , haijalishi wanakutana na nini maisha huwa ni lazima yaendelee, kuwafanya wasiwe watu wa kukata tamaa, kuwafanya hata katikati ya huzuni waweze kuona sababu ya kucheka, sababu ya kufurahi, wasiangalie ukubwa wa kile wanapitia , wasiangalie pale wanapitishwa bali wahakikishe wanaelewa kwanini wanapita pale, lengo haswa ni nini? Wahakikishe wameelewa lengo la kupita pale, wahakikishe wameelewa somo sawasawa ili liwafae katika maisha yao.
SOMA; Siku Ya Furaha, Kifo Cha Furaha…
Wanatakiwa wajifunze kuwa kusikitika, kuumia, kulalamika juu ya hali fulani ngumu unayopitia haiwezi kubadili kitu , haiwezi badili ukweli bali wanatakiwa kujifunza kukabiliana na hali zilizopo wakiwa na mtazamo sahihi , wanatakiwa kuwa watu wa kushukuru hata katika magumu, unaweza kuona pengine unahangaika kutafuta kazi wakati umesoma na ukaumia sana , kumbuka kuna mwingine hata hiyo elimu hakupata neema ya kuipata, hivyo acha kulalamika na kusikitika kama kweli umesoma tumia hiyo elimu kuweka maisha sawa, Jifunze kumshukuru Mungu kwa kuangalia vile amekujaalia, kwa kuangalia vile unavyo sasa, mshukuru hata kwa nyakati ngumu unazopitia maana angeweza angezuia, lakini karuhusu kwa kuwa anajua unaweza kuhimili, unaweza ukijiamini.
Makala imeandikwa na Beatrice Mwaijengo, anapatikana kwa namba +255 755 350 772 au kwa bberrums@gmail.com, unaweza pia kumsoma zaidi kwenye http://jitambueunani.blogspot.com
5/14/2015 07:17:00 AM | Labels: MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Jambo Moja Muhimu Unalotakiwa Kujua Kuhusu Miasha Na Kulitumia Kila Siku Ili Kufanikiwa.
Ndugu msomaji wa JIONGEZE UFAHAMU napenda nikushirikishe jambo moja la muhimu sana katika maisha yako na maisha ya kila binadamu. Kama unaweza kukumbuka miaka kadhaa nyuma ulipokuwa mdogo na usiyejua mambo mengi kama ilivyo sasa hivi. Ulipokuwa mdogo sana ulikuwa hujui kusoma wala kuandika. Lakini unaposoma hapa sasa hivi ni ushuhuda tosha kwamba sasa hali ni tofauti kwani umeweza kusoma nilichokiandika. Pengine kuna vingi sana unavyojua na bado unaendelea kuvijua kadiri siku zinavyosonga mbele. Ulikuwa hujui kuendesha baskeli au gari lakini sasa unajua. Naomba uelewe kwamba ulizaliwa bila kujua chochote na kila kitu umejifunza hapa duniani. Ni ushahidi tosha kwamba kama ukiamua kujifunza kitu chochote hapa duniani utaweza kwani hakuna jambo lisilowezekana wala jambo jipya chini ya jua.
SOMA; Kozi 1100 Unazoweza Kujifunza Bure Kupitia Mtandao.
Ushauri wangu kwa leo basi ni kuhusu kujielimisha. Waswahili walisema elimu ni kama bahari na haina mwisho. Maana yake ni kwamba kujifunza na kujielimisha ni mambo ambayo yanatokea kila siku katika siku zote za maisha yako. Jaribu kujitathmini na kujiuliza kwa siku ya leo umejifunza kitu kipi kipya ambacho ulikuwa hukijui na kitakusaidia katika kusonga mbele kuelekea katika mafanikio yako. Ninaposema mafanikio sizungumzii mafanikio ya kipesa au kiuchumi peke yake bali mafanikio katika ujumla wake kuanzia afya, mahusiano, kielimu, kimaisha na yanayofanana na hayo. Hivyo basi kwa kila siku iendayo kwa Mungu kaa chini na ujitafakari ni kwa kiasi gani umeweza kujifunza kitu kipya. Kuna mtu aliwahi kusema kwamba ‘’Mtu yeyote asiyejifunza ni mzee hata kama ana miaka 20, na mtu yeyote anayejifunza ni kijana hata kama ana miaka 100’’. Maana yake ni kwamba muda na siku yoyote ambayo utaacha kujifunza unaanza kuhesabiwa kama mzee. Epuka uzee kwa kuwa tayari kujielimisha na kujifunza.
SOMA; UKURASA WA 13; Jifunze Kila siku.
Vitu vya kujifunza katika maisha ni vingi mno kiasi kwamba mpaka unafikia mwisho wa maisha yako utakuwa hujavimaliza. Kuna vyenye faida na visivyo na faida. Nakushauri ujifunze vile ambavyo unavihitaji katika maisha yako na si kujifunza vitu ambavyo vitakupotezea muda wako bure. Jifuze vitu vya kukujenga kama namna ya kuwa tajiri, namna ya kuwa na afya bora, namna ya kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa, namna ya kuwa bora katika fani yako na namna ya kuwa na uhusiano mzuri, namna ya kujenga familia bora na vingi vinginevyo.
Unaweza ukajiuliza kama umechelewa kujifunza au huwezi tena kujifunza. Kumbuk hakuna mtu yeyote aliye mkubwa kuweza kujifunza mambo mapya na hakuna umri wa ukomo wa mafanikio. Anza leo na utaona mafanikio yake kesho. Pia unaweza kujiuliza ni wapi unapoweza kujifunza vitu hivi. Jibu ni rahisi sana, unaweza kujifunza kutoka kwa watu wengine;kwa waliofanikiwa utajifunza mbinu walizotumia kufikia mafanikio makubwa na hivyo na wewe uzitumie na kwa watu walioshindwa utatumia makosa wanayofanya kama funzo kwako ili usiyarudie. Pia unaweza kujifunza kwa kusoma vitabu mbalimbali. Watu wengi hawasomi hata angalau kitabu kimoja kwa mwaka.
SOMA; Uwekezaji Muhimu Kwako Kufanya Na Unaolipa Sana.
Unaweza kuanza kusoma kitabu kimoja kwa mwezi na baadae vitabu kadhaa kwa mwezi. Watu wengi waliofanikiwa ni wasomaji wazuri wa vitabu kwani vitabu ni hazina isiyofilisika. Pia unaweza kujifunza kwa kutumia mtandao wa internet. Tumia mtandao kwa faida yako kwani ukiutumia vibaya utageuka adui wako, kwani utapoteza muda wako mwingi ambao ungeutumia kuzalisha au kujifunza. Pia unaweza kujifunza kwa kufanya mwenyewe kitu fulani na kupitia makosa utajifunza kitu na siku ukikifanya tena kitu hicho utakuwa bora zaidi. Pia unaweza kujifunza kupitia vyombo vya habari kama televisheni,magazeti na hata redio. Kama utaona inafaa unaweza pia kuingia darasani uliweze kujifunza mambo mapya au kuongeza ujuzi kwa kile unachikifahamu. Kumbuka hakuna njia moja iliyo sahihi zaidi na hakuna njia moja ya kujifunza. Jua kuwa njia hizo na zingine ambazo sijazitaja zinaweza kufanya kazi kwa pamoja ama kwa kushirikiana.
Kumbuka kuwa huwezi kuwa bora kama hujielimishi. Jifunze na jielimishe kila siku.
Makala hii imeandikwa na Nickson Yohanes
Unaweza kuwasiliana na nae kwa kwa: simu: 0712 843030/0753 843030
e-mail: nmyohanes@gmail.com
Pia unaweza kutembelea blog yake: www.lifeadventurestz.blogspot.com kujifunza zaidi
5/13/2015 08:00:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Kwanini ni Muhimu kuwekeza kwa Muda Mrefu.
Unapofanya uwekezaji au jambo lolote unashauriwa kuwa na malengo ambayo utakuwa unayafuata katika utekelezaji wako. Na ukifanya uwekezaji hasa katika hisa ni vyema ukawa na malengo ya kukaa na Hisa zako kwa muda Fulani. Uwekezaji katika Hisa unamanufaa ikiwa utawekeza kwa muda mrefu na utapata manufaa makubwa.
Kwanini uwekeze kwa muda mrefu?
Ukiwekeza kwa muda mrefu uwekezaji wako utakua kwa kiwango kizuri, uwekezaji wa kuanzia mwaka 1 au 2 au zaidi ni rahisi kwa mwekezaji kuona ukuaji wa uwekezaji wake katika ongezeko la thamani. Mara nyingi ongezeko la bei ni rahisi kulitambua katika uwekezaji wako ikiwa utawekeza kwa muda mrefu. Vile vile katika kipindi hicho ni rahisi kwa mwekezaji kupata gawio la mwaka au miezi sita.
SOMA; Kinachokufanya Ukwame, Na Uwe Na Maisha Magumu.
Ukiwekeza kwa muda mrefu unaondoa hatari ya kupata hasara, kama utafanya uwekezaji wa muda mrefu katika Hisa ni rahisi kuondoa hatari ya kupata hasara kutokana na kupanda na kushuka kwa bei za hisa. Bei za hisa hupanda na kushuka, kwa hiyo ikiwa utawekeza kwa muda mfupi ni rahisi kupata hasara kama utauza kipindi ambacho bei zimeshuka ndani muda mfupi.
Ukiwekeza kwa muda mrefu una nafasi nzuri ya kupata gawio, kama utawekeza kwa miezi miwili ni vigumu kupata gawio kwa kuwa kampuni nyingi hutoa gawio kila baada miezi sita au mwaka. Kwa mwekezaji ambaye atawekeza kwa muda mrefu ana nafasi nzuri ya kupata gawio na kunufaika na uwekezaji wake.
Muda ambao mwekezaji anashauriwa kuwekeza na kukaa na uwekezaji wake
Unashauriwa kuwekeza kwa muda wa mwaka 1 au zaidi na uwekeze katika kampuni zaidi ya moja. Ukiwekeza kwa mwaka mmoja au zaidi na kwa kampuni tofauti unazuia hatari ya kupoteza pesa yako na uwekezaji kukua kwa kiwango kizuri.
Mwandishi: Emmanuel Mahundi
Mawasiliano: emmanuelmahundi@gmail.com au 0714 445510
Kwa kujifunza zaidi tembelea www.wekezamtanzania,blogspot.com
5/13/2015 07:30:00 AM | Labels: SOKO LA HISA(DSE) | 0 Comments
Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Design Your Best Year Ever.
Habari rafiki, ni matumaini yangu waendelea vizuri. Wiki hii tunaendelea na utaratibu wetu wa kushirikishana mambo 20 nilijifunza kwenye kitabu. Leo tunajifunza kutoka kwenye kitabu kinachoitwa DESIGN YourBestYear EVER. Kitabu kimeandikwa na DARREN HARDY.
1. Kwanza fahamu “Kwanini” kabla hujapotea kwenye kufahamu “Namna gani”. Kama Kwanini yako ni kubwa vya kutosha, namna gani ya kufikia malengo itakua rahisi. Wengi tunahangaika kutafuta njia za kufia malengo yetu, mwishowe tunapotelea huko. Know “Why” beforeyougetlostin “How.”
2. Anza kwa shukrani. Unapotaka kutengeneza mafanikio anza kwa kushukuru kwanza kwa wingi wa vitu ulivyonavyo tayari. Ukiwa na shukrani kwa vile ulivyonavyo, vitavutia upatikanaji wa vingine vingi zaidi. Tazama vitu ulivyonavyo, mali ulizo nazo, fursa ulizo nazo, kua na moyo wa shukrani kwanza kwa ulivyonavyo ndipo utakapoona njia nyingine zikifunguka.
3. Huwezi kupiga/kulenga mahali usipopaona. Kama hujui unakokwenda unaweza kuishia popote pale. Kuweka malengo kunakusaidia kuona unakotaka kwenda, kunakusaidia kulenga kisawasawa
4. Weka malengo ambayo yanakupa changamoto. Ukiona malengo uliyojiwekea hayakuumizi kichwa basi rudi jipange upya.
SOMA; Dunia Ya Wingi Na Dunia Ya Uhaba…
5. Andikamalengo yako. Usipoandika ni rahisi kusahau pindi unapokutana na changamoto au matatizo. Hatua ya kuandika ni ya kujasiri kuonyesha umedhamiria. Ukishaandika weka mahali ambapo utaweza kuona kila mara. Isipite siku hujasoma Malengo yako.
6. Jifunze kufanya tathmini ya mwaka uliopita. Kabla ya kuweka malengo mapya hebu fanya tathimini ya wakati uliopita. Orodhesha mambo kama 10 hivi yaliyotokea, na pia andika mambo uliyojifunza kutokana na hayo mambo 10.
7. Janga kubwa la maisha sio umasikini au njaa au kifo. Janga kubwa ni kushindwa kutumia uwezo wetu tulio nao.
8. Acha Mafanikio yako yahamasishe na kua ushuhuda kwa wengine. Mulika njia za wengine kwa tochi ya mafanikio yako ili na wao waone kwamba inawezekana kufanikiwa.
9. Hakikisha malengo yako ni yako kweli. Usiweke malengo kwa kufurahisha marafiki au ndugu. Usikubali mawazo ya watu au wana familia ndio ya kuongoze kuweka malengo hakikisha unafuata kile unachokitaka hasa.
10. Andaa orodha ya mambo/(malengo) 10 kisha kati ya hayo 10 chuja hiyo orodha na ufikishe malengo 3. Anza kuweka mpango wa utekelezaji wa hayo matatu.
11. Anza kwa kuligawa Lengo kubwa kwenye vipande vidogovidogo. Ukilivamia kama lilivyo lengo lako kubwa kwa ukubwa wake utekelezaji unakua mgumu. Ukitaka kumla tembo unamkata vipande vidogovidogo unaanza kutafuna taratibu mpaka anaisha. Vivyo hivyo kwa yale malengo makubwa fanya hivyo.
SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uweze Kufikia Malengo Yako.
12. Anza kufanya kama vile tayari umeshafikia lengo lako. Kama ungekua tayari ni Milionea ungetembeaje, ungeongeaje ungeshikanaje mkono na watu au ungeingiaje nyumbani kwako? Anza kufanya vile ambavyo ungefanya ukiwa umefikia malengo yako
13. Mafanikio ya kweli na utoshelevu wa maisha ni pale unapokua na mafanikio nyumbani, katika masoko, mafanikio katika mwili wako, akili pamoja na roho yako. Mafanikio ya kweli ni yale yenye uwiano (balance).
14. Weka malengo yako katika hali ya sasa. Usiseme nataka kua Bilionea tarehe 14 Feb 2030, bali sema mimi ni Bilionea 14 Feb 2030, kusema wewe ni bilionea kutaumba nguvu ambayo itakwenda kutenda kazi kutengeneza kile ulichokiri.
15. WEWE ndio wakufanyia kazi na sio malengo yako. Unapoweka malengo wengi wetu tunamtazamo wa kufanya kazi kwa bidii ili kuyafikia malengo tuliyojiwekea, na asilimia kubwa hatuyafikii maana kuna kitu hua tunakosea. Swala hapa sio hayo malengo (afya njema, fedha nyingi, ndoa bora, biashara kubwa n.k) swala hapa ni WEWE. Kama utaendelea kufanyia kazi malengo yako halafu ukasahau kujifanyia kazi wewe, utaendelea kukimbizana nayo na hutayashika. Anza kwanza kujifanyia kazi WEWE. Kama unataka kua bilionea, anza kujitengenezea tabia za kibilionea, kusema kwako, kuwaza kwako kufanane na bilionea. Ufahamu wako wa ndani unatakiwa ushawishike kua wewe ni bilionea. Bila hivyo, ukajisumbua tu kukimbizana na malengo utafanikiwa kwa muda tu ila utarudi kwenye hali yako ambayo ndio umeizoea. Na ndio maana maskini akishinda bahati nasibu ya mamilioni baada ya muda anarudia hali yake umaskini. Weka nguvu yako kubwa katika kujiboresha WEWE na mafanikio yatakuja kulingana na kiwango cha ubora wako
16. Andika madhara utakayoyapata pindi utakaposhindwa kufikia malengo yako. Ni muhimu kufahamu sio tu ahadi utakazopata utimizapo malengo, bali ni muhimu vilevile kutambua maumivu ambayo utayapata pale utakaposhindwa kufikia malengo.
SOMA; Mambo 20 niliyojifunza Kwenye Kitabu LITTLE BETS.
17. Ni muhimu kufurahia mafanikio madogomadogo unayoyapata kwenye njia unayoelekea kwenye mafanikio makubwa. Usisubiri mpaka ufikie lengo ndiyo ufurahie, bali katika hatua unazopiga jifunze kufurahia hatua zenyewe. Hii itakupa nguvu kuendeleza mapambano kuelekea kwenye lengo lako kubwa. Jipongeze kwa kila hatua unayopiga
18. Washirikishe wengine (ndugu, marafiki au wafanyakazi wenzio) malengo yako. Pale utakapojua kwamba watu wanaelewa ulichojiwekea ahadi kukifikia, utajisikia kuwajibika zaidi. Ila kama malengo yako unayafahamu wewe tu, hata wakati fulani ukisikia kutokuendelea unaweza kufanya hivyo, maana hakuna anayejua.
19. Tafuta picha zitakazokuhamasisha na uweke sehemu utakapoweza kuziona kila wakati. Mfano tafuta picha ya gari unalotaka au nyumba ambayo unataka kuishi.
20. Hakikisha malengo yako yanaendana na tunu zako za msingi (Corevalues) pamoja na viwango vyako. Kama lengo haliendani na misingi yako au viwango uliyojiwekea basi mara moja weka pembeni, rudi jipange upya
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com
5/12/2015 07:30:00 AM | Labels: UCHAMBUZI WA VITABU | 0 Comments
Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uweze Kufikia Malengo Yako.
Afya siyo neno geni kabisa katika akili yako. Na wala siyo mara yako ya kwanza kuliona neno hili au kusikia watu wakiongelea kuhusu afya kupitia vyombo vya habari kama vile radio, Luninga (TV) na nk.
Nini maana ya afya ?
Afya ni hali ya kuwa mzima kiakili,kimwili,kijamii na kiuchumi pia. Hivyo basi, kama binadamu yakupasa uwe na afya bora ili uweze kufikia malengo yako uliyojiwekea kwa sasa au kwa baadaye.
Wamiliki wa vyombo vya moto kama vile gari, pikipiki na nk. Wamekuwa wakifanyia huduma au service vyombo vyao vya moto kila baada ya muda Fulani. Kwanini wanafanyia vyombo vyombo vyao service au huduma?
Wanafanyia sevirce au huduma kwa sababu ili visiharibike na viendele kuwasaidia katika maisha yao ya usafiri wa kila siku. Wasipo vifanyia service au huduma vitakufa au kuharibika kabisa.
SOMA; USHAURI; Usianzishe NGO Anzisha Kampuni.(Usianzishe Msaada Anzisha Biashara)
Swali, je kwa binadamu wa kawaida tunafnayia service au huduma miili yetu? Kumbe basi , watu wanapasa kutunza afya zao sana kuliko kitu chochote .Ukiwa na afya mbaya na usipojali mwili wako utadhoofika na kushindwa kutimiza malengo au mipango yako uliyojiwekea kufikia sehemu fulani ya maisha unayohitaji kufikia.
Tunahitaji kula vizuri na kwa wakati ili tuwe na afya bora. Kula vizuri kuna hitaji mlo kamili wa chakula ambacho kinajenga mwili na siyo kubomoa. Je vyakula unavyokula vinajenga mwili au vina bomoa mwili? Nafikri jibu unalo mwenyewe.
Tunahitaji tunywe maji mengi kwa siku ,tunahitaji pia tupate muda wa kupumzika ili kufanya afya yako iwe nzuri katika Nyanja zote , tafiti nyingi zinasema kuwa binadamu anatakiwa kulala masaa 7-8 kwa usiku. Pia unahitaji upate muda wa kupumzika mchana ,unaweza ukasinzia kwa dakika 10-15-30 na pumzika pale mwili unapohitaji kupumzika usijilazimishe kufanya kazi wakati mwili umechoka.
SOMA; BIASHARA LEO; Kuhusu Wateja Wasionunua Kwako.
Faida za kuwa na afya bora
Ø Inakuongezea ufanisi wa kazi
Ø Unakuwa imara kiakili na kimwili
Ø Unakuwa mchangamfu
Ø Unakuwa na furaha
Hizi ni miongoni mwa faida chache kati ya nyingi za wewe kuwa na afya bora. Kumbuka kuwa huwezi kufikia au kutimiza malengo yako uliyojiwekea kam hauna afya bora, hivyo basi jail sana afya yako na fanyia huduma au service mwili wako mara kwa mara.
Makala hii imendikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com
5/11/2015 10:00:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani
Mara nyingi tumekuwa tukiwalaumu watu wanaotuzunguka kuwa wao ndio chanzo cha sisi kutoishi kwa furaha na amani na kwamba watu hawa ni chanzo cha sisi kutofikia mafanikio yetu. Wakati mwingine unaona watu waliopo katika mtaa, ofisi au nyumba unayoishi ni wabaya mno hata unatamani kwenda kuishi mahali pengine ukiwa na imani kuwa watu utakaowakuta huko watakua wa tofauti na kufanya maisha yawe rahisi.
Lakini ukweli ni kwamba kubadili mazingira au eneo ulipo sio suluhisho. Suluhisho ni kubadili namna unavyochukulia mambo. Kubadilika wewe kwanza kwakua hauwezi kumbadili mtu mwingine kama yeye hajaamua kubadilika. Sisi wenyewe ndiyo wenye jukumu la kuleta furaha na kuleta uwezekano wa ama kufikia au kutofikia mafanikio tuliyojiwekea.
SOMA; Ukiwa Na Kitu Hiki Ni Mwanzo Mzuri Wa Kufanikiwa Katika Uwekezaji.
Tunaweza kuamua kuishi kwa amani au kuishi kwa majuto na kuwalaumu wengine kwa kutofanikiwa kwetu. Kwa kulalamika hatuwezi kuleta tofauti yoyote ile zaidi ya kuendelea kuumia na kuwaona wengine wabaya.
Sasa ufanye nini ili kuhakikisha mambo yanakwenda kama ulivyopangilia na kuzuia mtu yeyote asikutoe nje ya mstari? Mambo haya hapa chini yatakusaidia sana kukufikisha mahali pazuri na utaishi vizuri na mtu yeyote Yule.
1. KUWA MSIKIVU.
Jitahidi kuwa msikilizaji badala ya kuwa mwongeaji. Ukiongea sana unaweza ongea vitu ambavyo si vizuri na kuwafanya watu wengine kujihisi vibaya na ukasababisha ugomvi au chuki. Kumbuka kuwa ukiongea kitu mtu anakiweka kichwani na haiwezekani kukifuta kichwani mwake tena. Hivyo kama utaongea jambo baya kwakua ulikua huwa unaongea tu hauna namna ya kubadili kauli yako. Hivyo ni vizuri kujifunza kuwa msikivu.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
2. KUBALI KUKOSOLEWA.
Usijisikie vibaya ukikosolewa unapokuwa umekosea. Jitahidi kutobishana sana unapoambiwa umekosea. Kukosea ni sehemu ya kujifunza. Ukiambiwa umekosea kaa chini na uangalie kwa umakini ni kwa nini ulikosea ili wakati mwingine usirudie kosa ilo hilo. Kila mmoja anakosea katika maeneo fulani nyakati fulani, iwe katika mahusiano, ofisini, shuleni, kwenye jamii nk. Hivyo ukikosolewa usione kama umeonewa. Jua kuwa kukosea ni sehemu ya maisha na ni nafasi nzuri yakuweza kujifunza na kujipanga kufanya vizuri zaidi.
3. USIPENDE KUBISHANA
Jitahidi kuepuka kubishana kusiko na sababu hata kama unajua kuwa upo sahihi. Kubishana sana huleta ugomvi na chuki. Kama upo sahihi hata ukikaa kimya haiubadili ukweli unaoufahamu kuwa uongo. Usiwe mwenye kubishana bishana utaishi kwa amani.
4. TAMBUA KUWA KILA MTU ANAMAWAZO YAKE.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
Tambua kuwa kila mmoja ana namna anavyotafsiri mambo. Kila mmoja ameumbwa tofauti na anamawazo yake. Heshimu mawazo ya wengine kwa kuwa tofauti ndio unaofanya ulimwengu usonge mbele. Kama wote tungekuwa na namna moja tunavyotafsiri vitu ulimwengu ungekua hauvutii hata kidogo. Ukitambua na kuheshimu uko tofauti wa mwingine huwezi kuumia kichwa. Utaishi kwa amani na furaha.
Tuonane wiki ijayo kwenye sehemu ya mwisho ya makala hii. Asante sana.
Kama unaswali, maoni au ushauri usisite kuwasiliana nami.
MWANDISHI: ESTHER NGULWA
MAWASILIANO: 0767 900 110 / 0714 900 110
estherngulwa87@gmail.com
Makala imepitiwa kwa lugha fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makalaza Kiswahili na Mjasiriamali barua pepe: rumishaelnjau@gmail.comsimu 0713 683422.
5/08/2015 07:46:00 AM | Labels: MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Mambo 20 niliyojifunza Kwenye Kitabu LITTLE BETS.
Habari rafiki, ni matumaini yangu waendelea vizuri. Karibu sana katika utaratibu wetu wa kushirikishana mambo 20 niliyojifunza kwenye kitabu. Leo tunajifunza kutoka kwenye kitabu kinachoitwa LITTLE BETS. Kitabu hiki kimeandikwa na Peter Sims
1. Matatizo hupelekea kupata shuluhisho mpya ambazo hukuwahi kufikikiria. Unapokumbana na matatizo au changamoto chukulia kama vile ni fursa ya wewe kugundua njia mpya.
2. Unapopoteza mwelekeo usikate tamaa kamwe hakikisha unatafuta njia mpya kwa kutumia uzoefu ulio nao... kama alivyofanya SteveJob. katika kuanzisha kampun nyingne ya next computer baada ya kufukuzwa kwenye kampuni ya apple aliyoianzisha
3. Ukianza biashara ukiwa na mtaji mdogo ukafeli ni rahisi kuinuka kuliko kuanzisha biashara ukiwa na mtaji mkubwa ukafeli.
4. Waweza kuanza na wazo dogo. Wazo dogo laweza zaa matokeo makubwa, hakikisha unafanyia kazi wazo lako.
SOMA; Kuna Jambo Moja La Ziada La Kufanya.
5. Kubali kuwa kuna mawazo hayatafikia mafanikio lakini usiache kuwaza. Unapojizoesha kuwaza mawazo ya biashara, mwanzoni utakua unapata mawazo ya kawaida, na pengine mengi hayatafikia kwenye mafanikio, Lakini baada ya muda akili inaanza kuleta mawazo mazuri zaidi.
6. Kukosea ni moja ya hatua ya kufanikiwa. Ukiwa unakwepa kukosea au kushindwa itakuwia vigumu kufika unakotaka kwenda maana hutajaribu kwa hofu ya kushindwa.
7. Ubunifu ni kuunganisha vitu unavyovijua... unganisha doti za uzoefu wako
8. Unaposhindwa usichukilie kushindwa bali chukulia kwamba umefahamu njia ambayo haitkufikisha, alafu tafuta njia nyingne
9. Mafanikio yanaficha matatizo
10. Maswali ni majibu mapya, ukiwa na utaraibu wa kujiuliza maswali na kujaribu kuyajibu kwa utendaji kutakupelekea kupata majibu mapya. Kabla ya majibu hutangulia maswali ubora wa majibu unategemea ubora wa maswali.
SOMA; Hii Ndio Hatari Kubwa Kuliko Zote.
11. Katika mafanikio hakuna njia ya mkato, lazima uzingatie kanuni na ukubali kwenda hatua kwa hatua
12. Tafuta msaada kwa waliokutangulia...hakuna anayefanikiwa peke yake
13. Kujaribu mara kwa mara kunasahihisha makosa, na pia kunapelekea kwenye jibu sahihi. Jaribu tena na tena
14. Sio lazima ujue kila kitu ndio uanze biashara. Hata kama utajua kila kitu yapo mambo ya mapya (surprises) utakuna nayo kwenye biashara unayotaka kufanya. Kama ni hivyo basi ukishafahamu yale ya msingi anza mara moja, mengine utajifunza kwa vitendo zaidi ya nadharia.
15. Usikatishwe tamaa na wasikilizaji au watu wa pembeni, ukishinda hakuna hata mmoja atakayekumbukwa, bali wewe ndiye utakayekua shujaa. Wako wapi waliomkatisha tamaa Nyerere wakati akipigania uhuru wa Tanganyika, walikuwepo waliomkatisha tamaa, lakini leo hii hakuna anayekumbukwa hata mmoja. Follow your heart
16. Ugunduzi mdogo unaweza kukupelekea kua na biashara kubwa sana.
SOMA; Kinachoamua Maisha Yako Sio Unachozungumza, Bali Hiki…
17. Ukamilifu ni kizuizi cha ubunifu. Kusubiri mpaka ukamilike kunafanya watu wengi wanashindwa kua wabunifu maana wanatamani muda wote waonekane wamekamilika
18. Mipango mizuri hujengwa ama hubomolewa na mazungumzo na kukutana na watu wengne. Unapokua na wazo au mipango yako jua ni nani wa kumshirikisha
19. Wajasiriamali wanofanikiwa ni wale wenye mtazamo wa majaribio. Hufanya majaribio mapya kila wakati. Hujaribu mawazo mapya bila kujali ni madogo kiasi gani. Katika kujaribu huko ndiko kunako wapa uwezo wa kutambua njia sahihi ni ipi
20. Akili au ubongo unakua kwa kujifunza vitu vipya kila siku. Unapojifunza vitu vipya seli za ubongo wako zinakua. Uwezo wa kufikiri pia unakua.
Asanteni sana. Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com
5/07/2015 07:39:00 AM | Labels: UCHAMBUZI WA VITABU | 0 Comments
Fanya Uwekezaji Huu Ambao Ni Rahisi Kwako Na Una Faida Kubwa.
Watu wengi wamekuwa wakitamani kufanya biashara au shughuli yoyote ambayo itakuza kipato chao, lakini wengi wao hukatishwa tamaa jinsi gani ataweza kusimamia biashara hiyo. Changamoto ya usimamizi wa biashara ni kubwa sana kwa watu wengi hasa wale ambao ni wafanyakazi katika serikali na kampuni binafsi. Na wengi ambao wamejaribu kufanya biashara wameshindwa kutokana na usimamizi mbovu wa biashara zao. Wengi wanatamani kukuza vipato kwa njia nyingine. Nini kifanyike?
Uwekezaji katika hisa ni suluhisho kwa wale wote ambao wanakutana na changamoto ya muda wa usimamizi wa biashara zao. Uwekezaji katika hisa ni rahisi, unahitaji muda mdogo wa usimamizi, unakua na kuongeza kipato kwa mwekezaji.
SOMA; Haya Ndio Mapinduzi Makubwa Tunayohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Kilimo.
Uwekezaji huu unafanyikaje?
Mtu yoyote Yule anaweza kuwa mwanahisa akiwa popote pale Tanzania. Unaweza kununua hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam kupitia mawakala wake ( Brockers) au kupitia Benki ya CRDB ukiwa mkoa wowote ule hapa Tanzania. Wasiliana wakala utapata utaratibu wowote jinsi ya kununua hisa. Unachotakiwa kuwa nacho ni pesa yako kwa ajili ya kununua hisa, akaunti yako ya benki na mawasiliano ya Mawakala wa soko la Hisa au Benki ya CRDB.
Kwanini uwekezaji huu ni rahisi?
Ni uwekezaji ambao unaweza kuufanya ukiwa katika mkoa wowote ule hapa Tanzania kwa gharama ndogo na wewe kuwa mmiliki wa hisa na kutengeneza faida. Ukihitaji kununua au kuuza hisa zako unachotakiwa kuwasiliana na mawakala wa soko la hisa ukiwa mkoani au sehemu yoyote ile kwa njia ya mtandao ( simu, barua pepe na benki). Utapata utaratibu wote kuhusu kuuza na kununua hisa.
Uwekezaji huu unahitaji muda mdogo wa usimamizi
Ukiwekeza katika hisa Mfano CRDB, TBL au SWIS hutahusika katika shughuli za kila siku za Kampuni. Wewe kama mwanahisa unahitajika kufuatilia utendaji wa Kampuni katika taarifa za fedha ambazo hutolewa kila baada ya miezi mitatu, sita na mwaka. Kama mwekezaji utasubiri katika kushiriki katika mkutano mkuu wa mwaka kwa ajili ya kutoa kushiriki katika vikao vya maamuzi ya wanahisa. Baada ya hapo unasubiri hisa zako kuongezeka thamani na kupata gawio.
SOMA; Huoni Kwa Sababu Hutaki Kuona.
Ni uwekezaji ambao unakua na mwekezaji anapata kipato
Ukiwa mwekezaji katika hisa, huku ukiwa unaendelea na kazi yako kama mwajiriwa au mfanyabiashara hisa zako zinaongezeka thamani na wewe mwekezaji utapata gawio kila baada ya miezi sita au mwaka. Utafaidika kwa haya ikiwa utaamua leo kwa kununua hisa za Kampuni ambazo zimesajiliwa katika soko la Hisa.
Faida ya Kuwa mmiliki wa Hisa
- Gawio
Ukiwa miliki wa hisa utapata gawio ikiwa Kampuni itapata faida katika kipindi hicho cha mwaka na wanahisa wakaridhia utoaji wa gawio. Gawio hutolewa mara mbili au moja kwa mwaka kutokana sera ya kampuni na maamuzi ya wanahisa.
- Ongezeko la thamani
Wanahisa pia huweza kupata faida itokanayo na ongezeko la thamani iwapo bei ya hisa itaongezeka kwenye soko la hisa. Ikiwa ulinunua hisa moja kwa Tsh 800 na baada ya mwaka hisa hizo sokoni zikauzwa kwa Tsh 1,400 basi unakuwa umepata ongezeko la thamani ya shilingi 6,00 kwa kila hisa. Hii ni faida tofauti na gawio, ikiwa utawekeza katika kampuni nzuri utapata gawio na ongezeko la thamani ndani ya mwaka mmoja. Vile vile ikiwa bei itashuka na kufikia Tsh 600 utapata hasara ya Tsh 200. Ila ukiwekeza katika kampuni nzuri ni vigumu kupata hasara na unakuwa na uhakika wa bei kuongezeka kwa 20% au 40% au zaidi kwa mwaka.
- Dhamana
Hisa kwa mwekezaji anaweza kuzitumia kama dhamana anapohitaji kupata mkopo.
- Huokoa muda wa usimamizi
Ni uwekezaji ambao humpatia mwekezaji uhuru wa kufanya shughuli nyingine na kwa wale ambao hawana muda wa usimamizi katika biashara huu ni uwekezaji mzuri kwao.
- Ni mali inayohamishika kwa urahisi
Ni mali ambayo inahamishika ki urahisi na kwa haraka pale mwekezaji anapohitaji pesa yake kwa ajili ya shughuli nyingine.
- Akiba
Njia ya kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye.
- Ushiriki wa jamii katika Uchumi
Inasaidia kuongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za kifedha na kukuza uchumi.
Kama unahitaji kushiriki katika Uwekezaji katika hisa kwa kununua hisa soma makala hii Hivi ndivyo unavyoweza kununua hisa katika soko la Hisa
Mwandishi: Emmanuel Mahundi
Mawasiliano: emmanuelmahundi@gmail.com au 0714 445510
Kwa kujifunza zaidi tembelea www.wekezamtanzania.blogspot.com
5/06/2015 07:30:00 AM | Labels: SOKO LA HISA(DSE) | 0 Comments
Kama Umeajiriwa Na Hujaanza Kufanya Hili Jua Kuwa Unapotea.
Kupata ajira imekuwa ndoto ya watu wengi na mafanikio kama sehemu tu ya maisha yao. Kama umeajiriwa na umekuwa ukitamani kuajiriwa nakupa pongezi kwani umefikia baadhi ya malengo yako. Watu wengi katika kada mbalimbali, wenye elimu na wasio na elimu wamekuwa wakitamani kuajiriwa na kuwekeza nguvu kubwa katika hilo. Sisemi kwamba wamekosea wala sisemi kwamba wamepatia kwani yote yanaweza kuwa sahihi kwa mtazamo wa muhusika. Lakini kama umeajiriwa au una mpango wa kuajiriwa ni muhimu zaidi kujua kuwa kufanikiwa ama kutofanikiwa kupo mikononi mwako mwenyewe na si kwa serikali wala mwajiri wako. Watu wamekuwa wakitafuta ajira nzuri na yenye kutoa pesa nyingi ili waweze kukidhi mahitaji yao lakini hata baada ya kupata ajira hizo bado tatizo la fedha lipo kwao.
Robert Kiyosaki katika mfululizo wa vitabu vyake vya Richdad, Poordad, anasema kuwa tatizo siyo pesa bali tatizo kubwa ni elimu kuhusu pesa (Financial education). Kwa leo sitajadili kuhusu hili bali nitajadili kidogo jambo linalofana na hilo japo kwa mbali kidogo. Watu wengi walioajiriwa wamekuwa wakitumia nguvu na akili nyingi katika kuwaletea watu wengine utajiri huku wenyewe wakibaki masikini ama watu wa hali ya kati katika maisha yao yote ya utumishi na hata baada ya utumishi na kuishia kutegemea mafao baada ya kustaafu. Wengi pia wamekuwa wakiingia kwenye ajira na kujiahidi kutoka katika ajira na kujiajiri lakini wanakuwa watumishi maishani mwao kwani hawakuwa na dira na mwelekeo wa kuweza kuwatoa huko kwani hujikuta wameshaingia katika mtego wa panya na kujishindwa kujinasua. Hutamani kutoka lakini woga wa kupata pesa unawashikilia. Naamini unajua methali hii ‘’mbio za sakafuni huishia ukingoni’’ndizo mbio ambazo walioajiriwa wengi wamekuwa wakizikimbia, mbio ambazo mwisho wake sote tunaujua kuwa ni kutosonga mbele na wengine kutumbukia katika lindi la madeni kila uchao.
SOMA; Tofauti ya mtazamo Kati ya Mtu wa Hali ya kati na Mtu wa hali Juu.
Naomba sasa nirudi katika lengo halisi la makala hii, kama umeajiriwa ni muda sasa wa kuanza kufanya mambo yako (mind your own business). Mbali na ajira ya kila siku ambayo umekuwa ukiifanya kupata kipato kila baada ya muda fulani mathalan siku, wiki na mwezi ni muda sasa wa wewe kutenga muda wa kufanya shughuli zako mwenyewe za kukufikisha katika kilele cha mafanikio. Tafuta kitu ambacho unaweza kukifanya mbali na ajira yako ya kila siku ili uweze kujiongezea kipato. Mishahara imekuwa haijitoshelezi na ndio maana migomo na ari ndogo makazini haiishi. Hivyo basi kuendelea kulalamika kuwa mshahara ni mdogo bila kufanya juhudi za kuongeza kipato hakutakusaidia lolote.
Unaweza ukaanza kufanya shughuli zako mwenyewe baada ya muda wako wa kazi kuisha unaporejea kutoka kazini. Wakati huu ambapo mradi au biashara yako inakua inahitaji usimamizi wako mkubwa ili iweze kusimama. Kwa muda huu si vizuri kuwaachia watu biashara yako waisimamie bila wewe kuwepo ili kuweza kuikuza zaidi. Wakati huu pia uwe na nidhamu ya fedha ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima. Ikiwezekana usitumie kipato chochote unachopata kwenye mradi wako ama biashara yako kwa muda wa hata miezi sita ili ikue na utazame pia kuhusu mwenendo wake. Naomba nikushauri kitu kimoja unapoamua kujifanyia shughuli zako, kama una familia na unategemea ajira yako ikupatie kipato sikushauri uache kazi unayoifanya mapema mpaka biashara yako itakaposimama kama lengo lako ni kujiajiri na kuacha kazi. Kama utaamua kuendelea na kazi baada ya shughuli zakokusimama kuacha kazi na kurudi kusimamia miradi yako itakuwa juu yako mwenyewe kulingana na utashi wako.
SOMA; Dalili Kwamba Unaweza Kufikia Mafanikio Makubwa.
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kuchukua hatua za kuweza kujitegemea na si kutegemea ajira kutokana na woga na kushindwa kufanya maamuzi magumu kwa maisha yao. Kumbuka haya maisha ni yako na hakuna wa kukufanyia maamuzi. Watu wamekuwa wakishindwa kufanya biashara kwa kuogopa madhara (taking risk) na kuamua kuwa kama walivyo. Nikuambie kuwa hakuna mafanikio ya haraka na yasiyokuwa na hatari. Hata katika kusoma kuna hatari zake, muda wowote unaweza kufeli na kila kitu ulichofanya kuwa historia. Unapoanguka hupaswi kukaa chini na kuanza kulia bali kunyanyuka na kusonga mbele huku ukijifunza kutokana na makosa yako. Nikupe mfano katika elimu, katika darasa la watu mia labda walifanikiwa kufaulu sitini kuingia elimu ya sekondari huku arobaini wakishindwa na kurudi mtaani kuendelea na maisha mengine. Kufika sekondari ishirini wanafanikiwa kupata alama za kuendelea na kidato cha tano huku arobaini wakibaki nyuma na wengine kwenda katika vyuo vya kati. Baada ya safari ya miaka miwili ya elimu ya sekondari ya juu wanafaulu kumi na mbili kati ya waliochaguliwa kidato cha tano ambapo kumi kati yao kwenda vyuo vikuu na wawili kwenda vyo vya kati. Kumbuka kuwa watatu hawakufanikiwa kusonga mbele na hivyo kurudi mtaani kupambana na maisha mapya. Baada ya kufika vyuo vikuu saba kati ya wale kumi wanafanikiwa kupata shahada zao na watatu kati yao wakishindwa safari na wao kuungana na hao wengine walioshindwa kuanzia shule ya msingi. Kwa mfano huu nikuambie kuwa kukabiliana na hatari ndio njia nzuri zaidi kuliko kuogopa kujaribu kutimiza ndoto zako kwa kufanya jambo litakalokuletea mafanikio. Kama wale wote walishindwa kuanzia shule ya msingi na hata sekondari waliweza kufanya uwekezaji ni dhahiri kuwa hata wale waliosoma watakuwa wameachwa nyuma. Kwa mfano huu naamini umeelewa kuwa wanaofikia mafanikio makubwa ni wachache sana, naamini na wewe ni mmojawapo. Mwisho basi kwa wewe unayetaka kufanya biashara au mradi fanya tu, usitishwe na hali iliyopo, tafuta kitakachokufanya uwe tofauti na wengine na utaona mafanikio.
Kabla ya kuhitimisha nipende kuzungumzia kuhusu muda. Kila mtu ana muda sawa na kila mtu katika hii dunia na ni bidhaa pekee ambayo kila mtu anayo katika kiasi sawa yaani saa 24 kila siku. Hivyo basi jitahidi kuutumia muda wako kwa faida na si kwa hasara. Kumbuka muda ndio maisha yako. Muda ulionao unakutosha sana kama utaamua kuupangilia. Kama ukitoka kazini punguza mijadala isiyo na tija, punguza kufuatilia mitandao ya kijamii, punguza kuhudhuria sehemu za starehe kama baada hasa baada ya kazi na utumie muda huo kujijenga. Kumbuka hukuja duniani kulipa bili bali kuishi na kufurahia kila siku yako ya maisha. Kama hutafanya shughuli zako (minding yourown business), utakuwa mlipaji wa bili daima na hutafurahia maisha yako.
Mwisho kabisa nikutakie usomaji mwema na mafanikio mema nategemea kukuona katika kilele cha ubora.
Makala hii imeandikwa na Nickson Yohanes ambae ni mjasirimali na mhamasishaji.
Unaweza kuwasiliana na naye kwa: simu: 0712 843030/0753 843030
e-mail:nmyohanes@gmail.com
Pia unaweza kutembelea blogu yake: www.lifeadventurestz.blogspot.comkujifunza zaidi
5/05/2015 07:30:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Tofauti ya mtazamo Kati ya Mtu wa Hali ya kati na Mtu wa hali Juu.
Kuna tofauti nyingi sana kati ya tajiri na masikini jinsi wanavyofikiri na kuwa na mitazamo tofauti. Mitazamo chanya na kufikri kichanya zaidi kwa matajiri kunawafanya wajizidi kuwa juu ukilinganisha na masikini jinsi wanavyofikiria. Zifuatazo ni mitazamo mbalimbali kati ya tajiri(world class ) na watu wa kipato cha kati yaani (middle class).
Masikini huwa wanaamini kuwa pesa ndio mzizi wa maovu yote lakini matajiri huwa wanaamini kuwa umasikini ndio mzizi wa maovu yote. Kwa hiyo amua kujivunia kuwa tajiri na dharau kauli za watu wa kipato cha chini wanaokuambia kuwa tajiri sio sahihi .
Masikini huwa wanaamini kuwa pesa ni ngumu sana kuipata wakati matajiri huwa wanaamini kuwa pesa ni rahisi kuipata kama ukiitega.
Masikini huwa wanaamini kuwa kama wakiwa matajiri watapoteza marafiki wao lakini Matajiri huwa wanaamini kuwa na marafiki kutawaongezea mtandao mkubwa zaidi wa kuwa tajiri.
Masikini huwa wanawafundisha watoto wao jinsi ya kuishi lakini matajiri huwafundisha watoto wao jinsi ya kupata au jinsi ya kuwa tajiri.
Masikini huwa wanaamini kuwa pesa inambadilisha mtu Lakini Tajiri anaamini kuwa pesa inaonesha mtu alivyo.
Tajiri anaamini kuwa kuwajibika au kujituma ndio njia salama pekee ya kupata pesa wakati masikini huwa wanaamini kuwa kazi ndiyo njia salama pekee ya kupata pesa.
SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.
Watu wa kipato cha kati huwa wanaamini kuwa na pesa nyingi inakutengenezea matatizo mengi lakini watu wa kipato cha juu yaani (world class) wenye uhuru wa kifedha wanaamini kuwa na pesa nyingi inakupunguzia kuwa na matatizo mengi au kuwa na matatizo machache.
Masikini huwa wanaamini kuwa ukipata fedha nyingi kutakupelekea kuwa na mawazo (stress) lakini tajiri anaamini kuwa na fedha nyingi inasaidia kupunguza mawazo (stress) au kutokuwa na mawazo .
Matajiri wanafikiri kirefu au kikubwa (think big) wakati masikini wanafikri kidogo u kifupi (think small).
Matajiri wanaishi chini ya kipato chao lakini masikini wanaishi juu ya kipato chao. Hii ndio sababu ambayo inawafanya watu wengi kutofikia malengo yao kwa sababu wanaishi juu ya kipato chao na kupelekea kuwa na madeni mengi.
Watu wa kipato cha kati wanaamini kuwa matajiri lazima wasaidie masikini lakini matajiri wanaamini katika kujitegemea.
Watu wa kipato cha kati wanaamini tajiri wana akili sana lakini watu wa kipato cha juu wanaamini kuwa na akili sana kuna uhusiano mdogo sana katika kupata utajiri au kuwa tajiri.
SOMA; Jambo Muhimu La Kila Mfanyabiashara Kufanya Kila Siku.
Watu wa kipato cha kati wanaamini kuwa na pesa ndio kutengeneza pesa lakini watu wenye uhuru wa kifedha wanaamini kuwa kupitia au kwa kutumia watu wengine kupata fedha au kutengeneza fedha.
Hizi ni baadhi tu ya mitazamo kati ya watu wenye kipato cha kati (middle class) na watu wenye uhuru wa kifedha ( world class).
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au barua pepe deokessy.dk@gmail.com au tembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com
5/04/2015 07:30:00 AM | Labels: FEDHA, MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 3
Leo ni siku ya mwisho ya kujiunga na SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA.
Habari ndugu msomaji karibu tena katika sehemu hii ya mwisho ya makala ya jinsi ya kuondokana na msongo wa mawazo wa kukosa muda katika ulimwengu huu wa utandawazi. Tumeangalia baadhi ya siri hizi wiki mbili zilizopita na kama haukusoma waweza soma hapa; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 2
Siri nyingine ni:
4. PANGA KAZI KUTOKANA NA UMUHIMU NA UHARAKA WAKE.
Kila mara tunakuwa na kazi nyingi sana za kufanya lakini haraka na umuhimu wa kazi hizi hutofautiana. Kuna baadhi ya kazi hata usipofanya haraka hazileti athari yoyote katika kukamilisha malengo yako uliyojiwekea. Ni vizuri sana kufahamu kazi ipi unatakiwa uanze kuifanya ipi ifuate na umalizie na kazi gani. Kwa kufanya hivi unaipa akili uwezo wa kutulia na kufanya kazi kwa ufanisi. Usipofahamu kazi ipi ianze unaweza kujikuta ukifanya kazi ambazo hazina umuhimu sana na kuacha kazi ambazo zinatakiwa kufanyika kwa haraka.
5. HAKIKISHA UNAMALIZA KAZI UNAYOIANZA.
Ukianza kazi basi hakikisha unaimaliza kabisa ili uweze kuendelea na kazi nyingine. Hii inakupa hamasa ya kufanya kazi inayofuata na kuwa na uhakika kuwa utaimaliza pia. Usianze kazi na kuiacha njiani kwasababu yoyote ile isiyo ya msingi sana. Kufanya kazi nusu huleta uvivu wa kuanza kazi nyingine. Kila ukifikiri kuwa kuna kazi haukuimaliza na itakufanya uchanganyikiwe na kushindwa kuendelea na kazi nyingine.
SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.
6. FANYA KAZI HUSIKA.
Jitahidi kuzuia akili yako kukusukuma kufanya shughuli ndogo ndogo na kukwepa kufanya shughuli unayohitaji kuifanya. Mfano umefungua kompyuta unataka kuandika ripoti akili yako inakushawishi uanze kupanga vizuri( folders ) faili zako badala ya kuandika ripoti. Au badala ya kusoma akili inakusukuma ukaloweke nguo kwanza ili ukimaliza kusoma ukafue. Lakini baada ya kuloweka unajikuta umeanza kufua na kuona bora umalize kufua kwanza ndipo ukasome. Ukimaliza kufua ile motisha ya kusoma huna tena na akili inakushawishi kuwa kazi zote zilikuwa muhimu. Baadaye unaona bado unakazi nyingi muhimu zinazokusubiri. Hakikisha unafanya kazi uliyopanga na si vinginevyo.
7. EPUKANA NA MARAFIKI WANAOKUPOTEZEA MUDA.
Marafiki wanamchango mkubwa sana katika maisha yetu ya kila siku. Ni vizuri kuwa na marafiki lakini ni lazima pia kutimiza malengo yako kama vile ulivyokusudia. Ni vizuri kuwaeleza rafiki zako juu ya ratiba yako ili usipoteze marafiki na kama kweli ni marafiki wazuri basi watakuelewa na kukuacha ufanye kazi muhimu. Kama marafiki hawa hawatakuelewa usiharibu ratiba zako ili kuwafurahisha. Kwa kuwa kama unashughuli nyingi hata ukiwa nao kila mara utakumbuka shughuli hizo badala ya kukaa nao kwa furaha. Kuwa makini sana na uepukane na marafiki wanaokupotezea muda.
SOMA; Njia Ya Uhakika Ya Kuondokana Na Hofu.
8. JIPONGEZE UNAPOMALIZA SHUGHULI ZAKO.
Kila mmoja hufurahia anapopongezwa. Ni muhimu pia kujipongeza wewe mwenyewe kila mara unapomaliza shughuli ulizojipangia. Orodhesha shughuli zako na jiandikie ni zawadi gani utajipa baada ya kumaliza shughuli hizo. Ukifanya hivyo unakuwa na hamasa ya kumaliza shughuli hizo ili ujipe zawadi yako. Zawadi yaweza kuwa kitu chochote mfano kula chakula Fulani, kusikiliza muziki, kulala kwa muda, kuangalia video Fulani au kuoga maji ya moto mazuri n.k.
Ni imani yangu kuwa siri hizi zitakusaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza msongo wa mawazo unaotokana na kubanwa na kazi nyingi na kuona kuwa muda hautoshi. Nakutakia utekelezaji mwema na ni imani yangu kuwa shughuli zako zitaenda vizuri tangu sasa
Kama unaswali, maoni au ushauri usisite kuwasiliana nami.
MWANDISHI: ESTHER NGULWA
MAWASILIANO: 0767 900 110 / 0714 900 110
estherngulwa87@gmail.com
5/01/2015 07:30:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments