Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.

Kila mtu ana maelezo yake ya mafanikio. Neno mafanikio lina maana tofauti kw akila mtu. Lakini licha ya utofauti huo bado kwa ujumla mafanikio ni kuwa bora kama unavyoweza kuwa.

Na mafanikio sio kitu ambacho kinatokea mara moja. Hutaamka siku moja asubuhi halafu paa mafanikio hao hapo.

SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kutoka Kimaisha Kwa Kuanza Na Mshahara Mdogo.

Mafanikio yanatokana na jinsi unavyoishi kila siku. Kuna tabia ndogo ndogo unazofanya kila siku ambazo zikikusanyika pamoja ndio zinaleta mafanikio au kushindwa.

Yafuatayo ni mambo matano ambayo wajasiriamali wenye mafanikio hufanya kila siku. Yasome na wewe uanze kuyafanya ili uweze kufikia mafanikio.

1. Wako tayari kujaribu tena hata pale wanaposhindwa.

Haijalishi wameshindwa mara ngapi, wajasiriamali wenye mafanikio huendelea kujaribu tena na tena. Na hawajaribu tu kama wajinga(kwa kurudia kile kile walichofanya) bali wanatumia walichojifunza na kubadili mbinu wanazotumia na hatimaye kupata mafanikio.

SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ni Kitu Unachotakiwa Kufanya Kila Siku.

2. Huzikabili hofu zao.

Moja ya vitu vinavyowarudisha watu wengi nyuma ni hofu. Wajasiriamali wenye mafanikio sio kwamba hawana hofu, wanazo ila wanaamua kuzikabili. Wanaingiwa na hofu ila nwanajua hii ni hofu na wanaipuuza na kuendelea na mipango yao.

3. Wanajitengenezea nidhamu binafsi.

Wajasiriamali wenye mafanikio makubwa wanajua ya kwamba nidhamu binafsi ndio msingi wa mafanikio. Hivyo kila siku hujijengea nidhamu binafsi ili waweze kutekeleza majukumu yao, kuaminika zaidi na kuweza kufikia mafanikio. Wako tayari kufanya kazi ngumu leo ili baadae wapate matunda mazuri. Hawakimbilii kufanya vitu vya kuwafurahisha kwa sasa.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

4. Hutenga muda wa kupumzika.

Pamoja na kupenda kufanya kazi kwa bidii na maarifa, wajasiriamali wenye mafanikio wanajua kwamba miili yao haiwezi kufanya kazi muda wote. Hivyo hutenga muda maalumu kwa ajili ya kupumzika ili kurejesha nguvu kwenye miili yao.

5. Hutoa bila ya kutegema kupokea.

Wajasiriamali wenye mafanikio hutoa kwa wengine bila ya kutegemea kupokea. Kama ni bidhaa au huduma wanatoa, hutoa zaidi ya wanavyolipwa.Kwa njia hii huendelea kuwa bora zaidi na kutengeneza wateja wengi, faida kubwa na mafanikio makubwa.

Hayo ndio mambo matano yanayofanywa na wajasiriamali waliofanikiwa, anza sasa kuyafanya na wewe kila siku. Kitakachotokea utaona mwenyewe.

0 comments: