JE WAJUA? Kuhusu Bacteria Wanaoishi Kwenye Kinywa Chako.

Kuna bacteria wengi wanaoishi kwenye kinywa chako zaidi ya idadi wa watu wanaoishi duniani.

Bacteria pia wapo kwenye ngozi yako, utumbo mpana na hata sehemu ya uke.

Kwa bahati nzuri bacteria hawa hawana madhara na wapo hapo kukukinga na bacteria wabaya.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA

Sasa unajua kwamba sio bacteria wote wanaoishi kwenye mwili wako ni hatari.

Mambo Matano Ya Kushangaza Kuhusu Siku Ya Jumatatu

Jumatatu ni siku ya kwanza ya wiki. Ni siku ambayo watu wanatoka kwenye mapumzimko na kuanza tena wiki ya kazi. Na kwa kuwa watu wengi hawapendi kazi wanazofanya, jumatatu inaonekana kuwa siku mbaya sana.

Haya ni mambo matano ya kushangaza ambayo hutokea sana siku za jumatatu tofauti na siku nyingine za wiki.

1. Zaidi ya asilimia 50 ya wafanyakazi huchelewa kazini.

Tafiti nyingi zinaonesha jumatatu ndio siku ambayo inaongoza kwa watu kuchelewa kufika kazini au kuwa watoro kazini.

SOMA; Mambo matano ya kufanya siku ya jumatatu ili uwe na wiki yenye mafanikio.

2. Asilimia kubwa ya watu hujiua.

Tafiti zilizofanywa hasa kwenye nchi zilizoendelea zinaonesha kwamba jumatatu ndio siku ambayo inaongoza kwa watu kujiua.

3. Asilimia kubwa ya watu hupata shambulio la moyo.

Jumatatu ndio siku ambayo watu wengi hupata shambulio la moyo(heart attack) zaidi ukilinganisha na siku nyingine za wiki. Hii inaweza kusababishwa na shinikizo kubwa la damu kutokana na kurejea kwenye kazi.

4. Mvua hainyeshi sana.

Inasemekana siku za jumatatu haina mvua sana ukilinganisha na siku nyingine za wiki. Hii inatokana na kwamba mwisho wa wiki watu wengi hawafanyi kazi na hivyo hakuna uchafuzi mkubwa.

5. Ni siku nzuri ya kununua gari.

Jumatatu ni siku nzuri ya kununua gari kwani wauzaji wa magari wanakuwa wameuza sana mwishoni mwa wiki na hawategemei wateja wengi siku ya jumatatu hivyo kuwa tayari kupunguza bei kwa kiasi kikubwa.

Nakutakia jumatatu njema na epuka mambo yanayoweza kukuharibia maisha yako hasa yanayotokea siku za jumatatu.

Tuko pamoja.

NENO LA LEO; Kuhusu Kuupuuza Ukweli.

I've learned that to ignore the facts does not change the facts.

 

Nimejifunza kwamba kuupuuza ukweli haibadilishi ukweli.

Ukweli ni ukweli hata kama utaamua kuupuuza. Kubaliana na ukweli na angalia jinsi ya kuutumia kupata kile unachotaka.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Kuanza Upya.

Though no one can go back and make a brand new start, anyone can start from now and make a brand new ending.

 

Japokuwa hakuna anayeweza kurudi nyuma na kuanza upya, mtu yoyote anaweza kuanza sasa na kuwa na kesho nzuri.

Usikatishwe tamaa na makosa uliyofanya nyuma, anza leo kufanya yale yatakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.

JE WAJUA? Mambo Kumi Usiyojua Kuhusu Kupumua.

1. Mtu mzima anapumua mara 23,000 kwa siku.

2. Kazi kubwa ya kupumua sio kupata oxygen, bali kuondoa kabon dayoksaidi.

3. Kupumua kwa kutumia mdomo ni hatari kwa afya yako.

4. Unavyopumua kwa kasi ndivyo inavyozidisha njaa na acid kwenye mwili wako.

5. Unatakiwa kufanya mazoezi kwa kiwango ambacho utaweza kupumua ukiwa umefunga mdomo.

6. Pua ina ngazi nne za kuchuja hewa inayoingia, ukipumua kwa mdogo unenda moja kwa moja kwenye ngazi ya nne.

7. Kama mapafu yako yangetandazwa yanafiki ukubwa wa uwanja wa tennis.

8. Kupumua kunaendeshwa na mfumo wa fahamu usio wa hiari(involuntary).

9. Ukijizuia kupumua unaongeza kabon dayoksaidi kwenye mwili.

10. Ukijizuia kupumua unatibu kwi kwi.

Sasa umeshajua mambo muhimu kuhusu kupumua, pumua vyema.

Nakutakia kila la kheri.

Ushauri Kwa Wajasiriamali Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Facebook.

Mmoja wa waanzilishi wa Facebook Dustin Moskovitz, ambaye amekuwa bilionea kupitia kampuni hiyo, sasa anamiliki kampuni nyingine inayotoa ushauri kwa wajasiriamali na wanaotaka kuingia kwenye ujasiriamali.

Anasema tofauti na vyombo vya habari vinavyoonesha kwamba ujasiriamali ni kitu cha ufahari na rahisi, ni kazi ngumu sana ambayo inahitaji ujitoe sana.

Anasema hivi ndivyo vyombo vya habari vinavyoaminisha watu ujasiriamali ukoje;

so-a-scene-from-the-social-network-this-is-us-partying-and-working-at-the-same-timesomebodys-spraying-champagne-everywhere

Na hivi ndivyo uhalisia ulivyo;

dustin-moskovitz-startup-entrepreneurship-launch-advice-deck

Na hapa ametoa ushauri wa vitabu sita ambavyo kila mjasiriamali au anayepanga kuingia kwenye ujasiriamali ni muhimu kuvisoma;

heres-moskovitzs-recommended-reading-list-for-aspiring-entrepreneurs

Tafuta vitabu hivyo na uvisome, vitakusaidia katika safari yako ya ujasiriamali.

Nakutakia kila la kheri, TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Kinachokurudisha Nyuma.

It's not who you are that keep's you back, it's who you think you're not. So start believing in yourself!

 

Kinachokurudisha nyuma sio vile unavyofikiri upo bali vile unavyofikiri haupo. Anza kujiamini sasa na amaini unaweza kufanya mambo makubwa.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

Mambo 10 Unayotakiwa Kujua Kuhusu Uwekezaji.

Moja ya njia za kuelekea kwenye utajiri ni kuwa mwekezaji. Unapokuwa mwajiriwa unawasaidia wengine kuwa matajiri. Unapojiajiri au kufanya biashara unaanza kujijengea utajiri. Unapokuwa mwekezaji unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kufikia utajiri.

Hivyo ni muhimu sana wewe kuwa mwekezaji. Ila kabla hujawa mwekezaji, JIONGEZE na mambo haya kumi muhimu unayotakiwa kujua kuhusu uwekezaji.

1. Akiba uliyoweka benki sio uwekezaji. Hela iliyoko benki inazalisha kiasi kidogo sana na wakiondoa makato ni kama hakuna unachopata. Hata ukiwa na nyingi kiasi gani benki, sio uwekezaji.

2. Uwekezaji ndio njia pekee ya kuenda na mfumuko wa bei. Ukiweka hela benki, inapungua thamani kutokana na mfumuko wa bei. Ukiwekeza hela thamani yake inaongezeka jinsi mfumuko wa bei unavoongezeka.

3. Uwekezaji ni hatari. Kupitia uwekezaji unaweza kutengeneza fedha nyingi na pia unaweza kupoteza fedha nyingi.

4. Kununua hisa ni kumiliki kampuni. Unaponunua hisa za kampuni fulani unakuwa unamiliki sehemu ya kampuni hiyo. Ikipata faida na wewe unapata na ikipata hasara na wewe unapata.

5. Vipande ni kukopesha fedha. Unaponunua vipande ni kama umeikopesha taasisi fedha na hivyo kuweza kuitumia kwenye shughuli nyingine za kibiashara. Baadae unapata faida kutokana na vipande vyako.

6. Kuanza mapema ni faida kubwa. Kama utaanza kuwekeza ukiwa na umri mdogo ukifikia uzeeni utakuwa umefaidika sana na umejifunza sana.

7. Uwekezaji maarufu sio mzuri kwako. Kitu ambacho ni maarufu sana na ambacho kila mtu anawekeza hakina faida kubwa.

8. Usiwekeze fedha utakayoihitaji karibuni. Uwekezaji una changamoto nyingi sana na kama thamani imeshuka sana ukisubiri itapanda tena. Kama unawekeza fedha ambayo unatarajia kuitoa huwezi kunufaika.

9. Hakuna awezaye kutabiri soko la kesho. Ni vigumu sana kuweza kutabiri ni nini kitatokea siku zijazo, lakini unaweza kujipanga vizuri.

10. Unahitaji kujifunza kila siku kuhusu uwekezaji na mbinu mbali mbali za mafanikio kwenye uwekezaji. Soma kitabu THE INTELIGENT INVESTOR, utajifunza mengi.

Anza sasa kuwekeza au kuweka mipango ya kuwekeza. Jinsi utakavyoanza mapema ndivyo utakavyonufaika zaidi. Kwa hapa tanzania unaweza kuwekeza kwa kununua hisa, kununua vipande vya UTT, kununua ardhi, Kujenga nyumba za kuuza na kupangisha na hata kununua kampuni au biashara.

Nakutakia kila la kheri, TUPO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Kushinda Vikwazo Kwenye Maisha.

Nobody trips over mountains. It is the small pebble that causes you to stumble. Pass all the pebbles in your path and you will find you have crossed the mountain.

 

Hakuna mtu anayeuvuka mlima kwa hatua moja. Ni mawe madogo madogo ndio yanayokuzuia. Yavuke mawe yote kwenye njia yako na utajikuta umeshauvuka mlima.

Tatizo lolote kubwa linalokukabili linaweza kutatulika vizuri sana kama utaligawa katika sehemu ndogo ndogo.

Nakutakia kila la kheri.

Ukiacha Kuangalia Facebook Kila Mara Mambo Haya Matano Yatatokea.

Facebook ni mtandao mkubwa sana wa kijamii ambao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi. Facebook imekuwezesha kujuana na watu wengi, kukutana na marafiki mliopotezana zamani na hata kujifunza mambo mengi. Hata makala hi unaweza kuwa umeipata kupitia facebok.

Pamoja na faida hizi, facebook imekuwa chanzo kikubwa cha watu wengi kupoteza muda kwani ina utegemezo mkubwa. Unaweza kujikuta kila siku unaangalia ni nini kinaendele kwenye facebook.

Kama utaacha kuangalia facebook kila mara, mambo haya matano yatatokea.

1. Utaacha kufa akili.

Kila mara unapotumia facebook ni kama akili yako inakuwa imekufa. Kwa sababu unajikuta akili yako yote imeingia kwenye mtandao huo na hivyo kushindwa kuona na kufikiria mambo mengine yanayoendelea. Kwa mfano unaweza kuwa umepanda gari safari nzima uko kwenye facebook tu na hivyo kushindwa kuona vitu vingine ambavyo vingekufanya ufikiri zaidi.

2. Utakamilisha kazi nyingi.

Kila mara unapoingia facebook hasa kwenye kuda wa kazi ni kama unajiibia muda wako wa kazi. Hivyo ukiweza kujidhibiti na ukapunguza muda unaoingia kwenye mtandao huu utakamilisha kazi nyingi.

3. Utawajua marafiki zako wa kweli ni kina nani.

Kupata marafiki kwenye mtandao ni rahisi sana. Unaweza kulike post zao au kuweka maoni kila mara na tayari mkawa karibu. Ila urafiki wa ukweli unahitaji zaidi ya hapo. Hivyo punguza muda unaotumia kwenye mtandao na ujue marafiki zako wa kweli ni watu gani.

4. Utaacha kujilinganisha na wengine na hivyo kujikubali.

Facebook inaweza kuwa sehemu ya kukufanya uone hakuna unachofanya cha maana. Hii inatokana na kuona wengine wakifanya mambo makubwa. Wakati mwingine unachokiona sio kweli.

SOMA; HIvi ndivyo mitandao ya kijamii inaharibu akili yako, kuwa makini.

5. Utagundua ulikuwa unatumika kibiashara.

Facebook zamani ilikuwa nzuri sana ila kwa sasa hivi wanatumia taarifa zako kuwauzia watu wa matangazo. Hivyo kila utakapoingia utakutana na matangazo na post nyingi za marafiki zako hutaziona tena. Kwa njia hii facebook wanakutumia wewe kibiashara.

Tumia mitandao ya jamii lakini usikubali mitandao hii ikutumie wewe.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

Sehemu Tano Unazoweza Kupata Mtaji Wa Kuanzia Biashara.

Kisingizio kikubwa cha watu kushindwa kuanza biashara kimekuwa ni mtaji. Kila siku watu wanalalamika wanapenda kuanza biashara ila mtaji hawana. Lakini wakati huo hawafanyi jitihada zozote za kupata mtaji huo au kuanza kidogo na kufikia makubwa.

Kulalamika kwamba taasisi za fedha hazitoi mkopo kwa watu ambao hawana dhamana ni kupoteza muda wako. Nikuulize wewe akija mtu yeyote akakuambia nipe elfu kumi nitakurudishia nikiipata utampa? Ni vigumu sana. Kwa kuwa ni vigumu kupata mkopo kwenye taasisi za fedha leo JIONGEZE na sehemu hizi tano ambazo unaweza kupata mtaji wa kuanzia biashara.

1. Akiba zako mwenyewe.

Kama huna kazi ya kukupatia kipato tafuta hata kazi ya kibarua, ifanye na weka akibakatika kila unachopata, baada ya muda tumia akiba hii kuanza biashara.

2. Michango kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki.

Unaweza kukusanya mchango kutoka kwa ndugu jamaa na hata marafiki. Wape wazo lako na omba wakuchangie.

3. Kuanza na biashara ambayo haihitaji mtaji.

Kuna biashara nyingi ambazo unaweza kuanza bila ya mtaji. Anza na biashara hizi na ukishaanza kupata kipato kikubwa unaweza kuhamia kwenye biashara unayoitaka.

SOMA; Biashara tano unazoweza kuanza kufanya bila mtaji.

4. Kuandaa wazo zuri.

Kama una wazo zuri sana ambalo linaweza kufanyika ila huna mtaji, liandae wazo hilo vizuri sana na kisha angalia kampuni ambazo zinaweza kufaidika na wazo hilo kisha wauzie wazo hilo au wakupe sehemu ya faida itakayopatikana kwa wazo lako.

ANGALIZO; Sajili wazo lako kwenye mamlaka husika(BRELA) ili usije ukaibiwa wazo hilo.

5. Shiriki mashindano mbalimbali.

Kuna mashindano mengi sana yanafanyika siku hizi ambayo yanapambanisha mawazo bora ya kibiashara. Andaa wazo lako na ingia kwenye mashindano haya. Ukiweka wazo lako vizuri unaweza kuwa mshindi na ukapata mtaji.

Tumia njia hizo tano kupata mtaji wa kuanzia biashara. Kama unaona njia hizi hazifai au haziwezekani kwako endelea kukaa nyumbani na kuperuzi mitandao ya kijamii huku ukiendelea kupoteza muda.

Amua sasa kubadili maisha yako, chukua hatua.

NENO LA LEO; Kuhusu Kufikia MAFANIKIO MAKUBWA.

The greatest oak was once a little nut that held its ground!

 

Mti unaaonekana mkubwa siku moja ulikuwa mbegu ambayo ilishikilia ardhi.

Shilikia misingi yako na siku moja utafikia mafanikio makubwa. Usiyumbishwe wala kukata tamaa.

TUPO PAMOJA.

Mambo Matano(5) Ambayo Ni Marufuku Kufanya Kwenye Eneo La Kazi.

Kazi ndio msingi wa maendeleo. Na ili uweze kufikia mafanikio makubwa ni lazima ufanye kazi kwa bidii na maarifa. Sifa moja kubwa ya kufanikiwa kwenye kazi yoyote ni kupenda unachofanya. Kuna mambo mengi sana ambayo ukiyafanya kwenye kazi yako yanakuzuia kufikia mafanikio.

Leo JIONGEZE mambo haya matano ambayo ni marufuku kuyafanya eneo la kazi kama unataka kufikia mafanikio makubwa.

1. Kuonesha tabia ya hasira au kulipiza kisasi.

Mara kwa mara mtapishana kauli na mfanyakazi wako, mfanyakazi mwenzako au bosi wako. Kwa vyovyote vile tafuta njia ya kumaliza tofauti zenu kwa amani, ukiongea au kufanya mambo kwa hasira au kupanga kulipiza kisasi utaingia kwenye matatizo makubwa.

2. Majungu na kusengenya.

Maeneo mengi ya kazi hapa Tanza ia kuna majungu mengi sana. Usianzishe wala usishiriki kumpiga jungu mtu yeyote aliyepo kwenye eneo lako la kazi. Ni kumkosea heshima na hii itakufanya uingie kwenye matatizo.

3. Kudanganya.

Wafanyakazi wengi wamezoea kudanganya hapa na pale. Tatizo kubwa la kudanganya kwenye eneo lako la kazi ni kwamba itakubidi uishi uongo huo kwa muda mrefu kitu ambacho kitakuumiza.

4. Kuchukua sifa za wengine.

Kuna watu wanasubiri wengine wafanye kazi halafu wao ndio wanaokuwa wa kwanza kusema kama sio mimi hiki kisingewezekana. Usifanye hivi, utakosa ushirikiano kutoka kwa wengine. Kila mtu ana nafasi kubwa kwenye kukamilika kwa jambo lolote.

5. Usichome daraja.

Watu wengi wanaojiajiri wanatokea kwenye ajira. Zamani kidogo watu walikuwa wakiondoka kwenye ajira zao kwa ugomvi mkubwa na hivyo kuondoa kabisa ushirikiano. Wewe usifanye hivi, kama unakwenda kujiajiri hakikisha unakuwa na uhusiano mzuri na mwajiri wako kwani anaweza baadae kuwa mteja wako au akakuletea wateja. Mafanikio ya sasa yanatokana na ushirikiano mzuri uliojenga na watu.

Epuka kufanya mambi hayo matano kwenye kazi yako kama kweli unataka kupata mafanikio kupitia kazi hiyo.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

Watu Watatu(3) Waliofukuzwa Kwenye Kampuni Walizoanzisha Wenyewe.

Unaweza kufikiri kuingia kwenye biashara na kujiajiri mwenyewe ndio njia nzuri ya wewe kuwa na uhuru kwa kile unachofanya. Inaweza isiwe kweli kwa sababu kwa jinsi hali ya biashara za kisasa ilivyo unaweza kujikuta kwenye hali ngumu sana.

Tena pale unapofikia kampuni ikawa kubwa na kuanza kuuza hisa, wenye hisa nyingi wanaweza kufanya maamuzi hata ya kukufukuza wewe japo wewe ndiye uliyeanzisha.

Hapa ni orodha ya watu watatu ambao walifukuzwa kwenye kampuni walizoanzisha wenyewe;

1. Steve Jobs, Apple

Steve Jobs alianzisha kampuni ya apple ila baadae alifukuzwa kwenye kampuni hiyo. Alikuja kurudishwa kwenye kampuni hiyo na kuleta mapinduzi makubwa ya kiteknolojia.

2. Ted Tunner, CNN

Ted Tunner alianzisha CNN, shirika la habari la marekani lakini baadae alikuja kufukuzwa kwenye shirika hilo.

3. Jack Dorsey, Twitter

Jack Dorsey ni mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa kijamii unaoitwa twitter ila kwa sasa anaonekana hayupo tena kwenye mtandao huo kwani ameanzisha kampuni nyingine ya teknolojia.

Kuwa makini pale unapoanzisha kampuni yako yasije kukutokea mambo ambayo hukutarajia.

Nakutakia kila la kheri.

NENO LA LEO; Kuhusu Lifti Ya Kuelekea Kwenye Mafanikio.

There is no elevator to success. You have to take the stairs.

 

Hakuna lifti ya kuelekea kwenye mafanikio, ni lazima upande ngazi.

Watu wengi wamekuwa wakidanganywa sana kwamba kuna njia ya kupata mafanikio haraka, kama vile mtu anavyopanda lifti na kufika ghorofa ya kumi haraka.

Ukweli ni kwamba hakuna njia yoyote inayoweza kukuletea mafanikio haraka. Kama ilivyo kwamba itakuchukua muda kupanda ngazi mpaka ufike ghorofa ya kumi.

Usikate tamaa, SONGA MBELE.

Sababu 5 Kwa Nini Ni Marufuku Wewe Kukata Tamaa.

Katika maisha kuna wakati ambapo mambo huwa magumu sana. Ni katika nyakati hizi ambapo watu wengi hukata tamaa na kuacha kile ambacho walikuwa wanafanya.

Kwa kukata tamaa unashindwa kufikia mafanikio na pia unaona maisha yako kama hayana maana.

Leo JIONGEZE na sababu hizi tano kwa nini ni marufuku wewe kukata tamaa.

1. Bado hujafa.

Kama bado unaishi hii ina maana kwamba kila kitu kinawezekana. Hata iwe umeshindwa au kupoteza kiasi gani, jipange tena na utafikia mafanikio.

2. Kuna watu wengine walishafanya.

Katika jambo lolote ambalo linakushinda kufanya, kuna watu wengine walipitia changamoto kama zako ila waliweza kufikia mafanikio. Na kwa bahati nzuri sana watu hawa wameandika yote hayo kwenye vitabu, vitafute na uvisome.

3. Kuna watu wana hali mbaya kuliko wewe.

Wakati wewe unalalamika huna viatu kuna mwenzako hana miguu kabisa. Hivyo kukata tamaa na wakati kuna watu wana matatizo makubwa kuliko wewe na bado wanaishi utakuwa hujitendei haki.

USIKATE TAMAA2

4. Utawahamasisha wengine.

Kama ukiweza kufikia mafanikio licha ya changamoto unazokutana nazo utawahamasisha wengine nao kuweza kufikia mafanikio. Kama utakata tamaa na kuacha utawakatisha na wengine tamaa na kuwafanya wasijaribu kabisa.

5. Unastahili kuwa na furaha.

Kila mmoja wetu anastahili kuwa na furaha kwa sababu furaha hupewi na mtu bali inatoka ndani yako. Unapokata tamaa huwezi kuwa na furaha, badala yake utaona maisha yako kuwa kisirani. Ila kama utakomaa na kufanikiwa utakuwa na furaha idumuyo.

Sasa umeshajiongeza na sababu hizi tano za kutokata tamaa. Endelea kukomaa na utafikia mafanikio makubwa. Kama mambo yanazidi kuwa magumu badilisha mbinu ila sio kuacha kufanya kabisa.

Nakutakia kila la kheri.

Mambo 5 Muhimu Ya Kufanya Kabla Hujalala Leo.

Siku ya leo ndio inaelekea kuisha na kwa siku nzima ya leo umepitia mambo mengi sana. Kuna mengi umefanikiwa kufanya leo na pia kuna ambayo umepata changamoto kubwa.

Hata kama siku yako ilikuwa mbaya kiasi gani, kuna mambo mazuri uliyojifunza kwa siku hii.

Hapa kuna mambo matano muhimu unayotakiwa kufanya kabla ya kulala.

1. Fanya tathmini ya leo.

Fanya tathmini ujue umeitumiaje siku ya leo. Ni mambo gani umefanikiwa kufanya na ni yapi umeshindwa. Chukua kalamu na karatasi uandike mambo matatu uliyofanikiwa kufanya leo ambayo yamekusogeza kwenye mafanikio. Pia andika mambo matatu ambayo inabidi uyarekebishe.

2. Pangilia kesho yako.

Kabla ya kulala pangilia siku yako ya kesho. Andika mambo makubwa matatu unayohitaji kukamilisha kesho na uanze kuyafanyia kazi mapema kesho.

3. Pata muda wa kujisomea.

Tenga muda mchache wa kusoma kitabu, ndio kusoma kitabu cha kawaida.

4. Lala mapema.

Kwa kawaida watu wengi huchelewa kulala kwa sababu ambazo sio za msingi. Inaweza kuwa kuangalia tv au movie, kuperuzi mitandao mbalimbali na kadhalika. Ukilala mapema unaweza kuamka mapema ukiwa na nguvu.

5. Kaa mbali na mwanga wa vifaa.

Sasa hivi tunatumia vifaa vingi vinavyotoa mwanga mkali. Simu, kompyuta, tv hivi vinatoa mwanga mkali sana. Mwanga huu unakufanya uchelewe kupata usingizi. Hivyo ni vyema usitumie simu au kompyuta kitandani.

Anza kufanya mambo hayo matano leo na utaona mabadiliko kwenye maisha yako.

Tuko pamoja.

Faida 5 za matikiti maji kiafya

Tikiti maji  ni tunda ambalo linapatikana kwa wingi sana katika maeneo mbalimbali. Hili ni moja ya tunda ambalo linapatikana kila msimu wa mwaka.

TIKITI

Hata bei ya tikiti maji sio kubwa sana kiasi cha kwamba kila mtu anaweza kupata tunda hili.

Kuna faida nyingi sana za kula tikitimaji. Hapa utazijua faida tano za kiafya.

 

1. Inapunguza magonjwa ya moyo.

Matikiti maji yana kirutubisho ambacho huondoa sumu zinazosababisha magonjwa ya moyo na shinikizo la damu.

2. Ni nzuri kwa mifupa yako.

Kirutubisho hiko kilichopo kwenye matikiti maji kinaweza pia kulinda mifupa na kupunguza magonjwa ya mifupa hasa kwa wazee.

3. Inapunguza mafuta mwilini.

Tafiti zinaonesha kwamba matikiti maji yana virutubisho ambavyo vinazuia mafuta kujikusanya mwilini.

4. Yanaongeza maji mwilini.

Unatakiwa kunywa maji mengi sana kwa siku. Ila ni wachache sana wanaoweza kunywa kiwango kikubwa cha maji. Ukila matikiti maji yanaongeza maji mengi mwilini.

5. Yanaimarisha kinga ya mwili.

Matikiti maji kama yalivyo matunda mengine yana vitamin c kwa wingi ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha kinga ya mwili.

Hizo ndio baadhi ya faida nyingi za matikiti maji. Ongeza idadi ya vipande unavyokula kila siku ili unufaike zaidi.

TUKO PAMOJA.

Biashara 5 Unazoweza Kuanza Kufanya Bila Ya Kuwa Na Mtaji.

Kikwazo kikubwa cha watu wengi kuingia kwenye biashara kimekuwa ni mtaji. Japo sio kweli kwamba mtaji pekee ndio kikwazo, lakini wengi wanaamini mtaji tu ndio unawazuia.

Lakini pia wakati huo ambao mtu hana mtaji hakuna juhudi kubwa anazofanya ili kuhakikisha anapata mtaji huo.

Sasa kufupisha habari leo JIONGEZE na biashara hizi tano unazoweza kuanza kuzifanya bila ya kuanza na mtaji wa fedha.

1. Biashara ya mtandao(Network marketing).

Hii ni biashara ambayo ni mkombozi kwa mtu yeyote ambaye ana kiu ya kufikia mafaniki. Hapa tanzania kuna makampuni mengi yanayofanya biashara hii kamA Forever living, Oriflame, GNLD, na mengineyo. Katika makampuni haya kuna ambayo unaweza kuanza na kiasi cha chini sana ambacho ni sawa na bure.

2. Biashara ya ushauri.

Je kuna kitu ambacho una utaalamu nacho? Je kuna kitu ambacho unapenda sana kukifuatilia na hivyo unakijua sana? Vizuri, kuna mtu anataka kukijua ila hajui aanzie wapi. Kwa wewe kutoa ujuzi na uzoefu wako unaweza kulipwa fedha.

3. Biashara ya taarifa(internet marketing).

Hii ni biashara ya kutoa taarifa kwa kupitia mtandao wa intanet. Unaweza kuwa na blog yako ambayo ni bure kuiendesha na baadae ukaanza kupata kipato kizuri kupitia mtandao.

Soma; jinsi ya kutengeneza fedha kwa kutumia mtandao wa intaneti.

4. Biashara ya uwakala wa mauzo(salesman.)

Kuna makampuni mbalimbali ambayo yanatumia mawakala kuuza bidhaa au huduma zao. Kwa wewe kujifunza na kuwa wakala wao unaweza kupata kipato kizuri kwa njia ya kamisheni.

5. Biashara ya udalali.

Hii ni biashara ambayo wewe unamsaidia mtu kupata kitu anachotaka na hana muda au uzoefu wa kukipata. Kama ukiweza kuifanya biashara hii kwa mbinu nzuri unaweza kutengeneza kipato kizuri.

Angalizo; Biashara hizi zinahitaji wewe ufanye kazi kwa bidii na maarifa na pia unaweza usione faida mapema. Ila ukiweka malengo na mipango mizuri utaona mafanikio makubwa baadae.

Uzuri ni kwamba unaweza kuanza biashara hizi ukiwa bado umeajiriwa au upo masomoni.

Nakutakia kila la kheri.

TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Zawadi Kubwa Uliyopewa.

Everyone is gifted - but some people never open their package!

 

Kila mtu amezawadiwa, lakini baadhi ya watu hawafungui maboksi yao.

Kama unajiona wewe ni mtu ambaye huna bahati au huna kipaji chochote na kuna wengine ndio bora zaidi basi hujajijua vizuri. Kaa chini na utafakari kwa kina utaiona zawadi kubwa iliyoko ndani yako.

Nakutakia kila la kheri.

TUKO PAMOJA.

Mambo Matano(5) Ya Kufanya Siku Ya Jumatatu Ili Kuwa na Wiki Yenye Mafanikio.

Jumatatu ndio siku inayochukiwa na watu wengi kuliko siku nyingine yoyote ya wiki. Siku hii imepewa majina mabaya sana likiwemo BLUE MONDAY.

Jumatatu ni siku ambayo watu wanatoka kwenye mapumziko na kuanza tena kazi. Ni siku ambayo watu wanajua kuna siku tano za kazi mbele, na kama hupendi kazi yako ndio unazidi kupata msongo wa mawazo.

Leo JIONGEZE na mambo haya matano ambayo ukiyafanya siku ya jumatatu utakuwa na wiki yenye mafanikio makubwa.

1. Amka mapema na fanya mazoezi.

Kama mwishoni mwa wiki ulipumzika au kustareheka sana, jumatatu amka mapema na fanya mazoezi. Itakuwezesha kuianza wiki vizuri. Pia tumia muda huo wa asubuhi kupitia malengo na mipango yako ya wiki nzima.

Soma; faida 5 za kukimbia dakika 5 kila siku 

2. Pata kifungua kinywa.

Watu wengi sana hukosa muda wa kupata kifungua kinywa hivyo kuianza siku yao wakiwa wamechoka. Pata kifungua kinywa ili uianze wiki yako ukiwa na nguvu za kutosha.

3. Wahi kazini au kwenye biashara zako.

Tafiti zinaonesha jumatatu ndio siku ambayo watu wengi wanachelewa au kutokuhudhuria kabisa kazini au kwenye biashara zao. Sasa wewe usiwe mmoja wao, fika eneo lako la kazi mapema.

4. Jiandae kwa mambo usiyotegemea.

Kama umeajiriwa jumatatu unaweza kukutana na mabadiliko mengi sana kwenye eneo lako la kazi. Unaweza kukuta jukumu ulilokuwa unafanya unatakiwa uache na kukamilisha lingine lenye uhitaji wa haraka. Hata kama umejiajiri kutakuwa na mabadiliko ya hapa na pale tofauti na ulivyotegemea.

5. Kumbuka kuna jumanne.

Jumatatu inaweza kuwa siku ngumu sana kwako. Unajikuta na majukumu mengi na huku ukiwa haupo kwenye hali nzuri ya kufanya kazi. Usijiumize sana pale unaposhindwa kumaliza yote, kwa sababu sio mwisho wa dunia, kuna jumanne. Fanya kwa uwezo wako na endelea siku ya jumanne.

Naamini haya matano yataifanya jumatatu na wiki yako kuwa ya mafanikio.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

HIZI NDIO HATUA KUMI ZA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE MAISHA YAKO



Angalia video hii fupi ambayo itakupatia hatua kumi za kuboresha na kubadilisha kabisa maisha yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Ugumu Wa Kufanya Maamuzi.

It's not hard to make decisions when you know what your values are.

 

Sio vigumu kufanya maamuzi kama unaijua thamani yako au malengo yako.

Tunakosea katika kufanya maamuzi mengi kwa sababu tunayafanya bila ya kujua yataathiri vipi malengo yetu.

Nakutakia siku njema.

Mambo Matano Ambayo Watu Waliofanikiwa Hufanya Mwisho Wa Wiki.

Kwa taratibu nyingi za kazi kwa walioajiriwa na hata aliojiajiri mwisho wa wiki huwa ni siku za mapumziko. Kwa walioajiriwa wanaweza kuwa na siku mbili za mapumziko na waliojiajiri wanaweza kuwa na muda mfupi zaidi ya hapo.

Jinsi unavyoweza kutumia siku hizo za mwisho wa wiki inaweza kukufanya ufikie mafanikio au ushindwe kufikia mafanikio.

Hapa utaona mambo matano ambayo watu wenye mafanikio makubwa hufanya mwisho wa wiki.

1. Hupumzika.

Japokuwa siku hizi ni za mapumziko bado sio watu wote wanapumzika. Wengine hutumia muda huu kufanya kazi nyingine zaidi. Watu wenye mafanikio hupata muda wa kupumzika mwisho wa wiki.

2. Hufanya tathmini wa wiki inayoisha.

Watu wenye mafanikio hutenga muda mwisho wa wiki na kufanya tathmini ya wiki inayoisha. Huangalia ni kipi walishofanikiwa na ni wapi waliposhindwa.

3. Hupanga wiki inayoanza.

Watu wenye mafanikio hutumia mwisho wa wiki kuweka malengo na mipango ya wiki inayofuatia. Mipango hii huwawezesha kuwa na wiki yenye mafanikio makubwa.

4. Hujumuika na ndugu na jamaa.

Watu wengi wenye mafanikio huwa na kazi nyingi sana katikati ya wiki na hivyo kukosa nafasi ya kuonana na ndugu jamaa na marafiki. Hutumia mwisho wa wiki kujumuika na watu ambao hawajakuwa nao kwa muda mrefu.

5. Hukata mawasiliano.

Watu wenye mafanikio hutenga masaa machache mwisho wa wiki kukata mawasiliano yote. Hutumia muda huu kukaa na kutafakari maisha yao zaidi. Katika kukata mawasiliano huondoka kwenye mtandao, huzima simu na vifaa vingine vyote vya mawasiliano.

Na wewe unaweza kufanya mambo haya kila mwisho wa wiki na ukaboresha maisha yako zaidi.

Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Kufikia Ndoto Zako.

If you are facing in the right direction, all you have to do is keep on walking in order to reach your dreams.

 

Kama upo kwenye uelekeo sahihi, unachotakiwa kufanya ni kuendelea na safari ili kufikia ndoto zako.

Ukishachagua njia yako usirudi tena nyuma, endelea kukaza mwendo ili uweze kufikia malengo yako.

TUKO PAMOJA.

Hivi Ndivyo Mitandao Ya Kijamii Inavyoharibu Akili Yako, Kuwa Makini.

Tunaweza kukubali kwamba mitandao ya kijamii ndio mapinduzi ya sasa. Yaani kama ilivyokuwa mapinduzi ya viwanda, sasa tuna mapinduzi ya mitandao ya kijamii. Mitandao kama facebook, twitter, instagram, linked in na mingine mengi imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Mitandao hii imekuwa na faida kubwa sana, kuwaleta watu karibu zaidi ya ilivyowahi kutokea. Watu wengi wamefahamiana kupitia mitandao hii na wengine wanatengeneza kipato kupitia mitandao hii.

Kama tunavyojua, chochote chenye faida huwa kina hasara. Leo tutaangalia hasara ya mitandao ya kijamii kwenye akili yako na hivyo kuharibu maisha yako.

Kwenye mitandao hii ya kijamii kwa mfano facebook au instagram, watu huweka picha zao mbalimbali wakiwa katika hali ya furaha au kustarehe. Kupitia picha hizi kama na wewe hujapata nafasi ya kuwa katika hali hizo unaweza kuona maisha yako sio mazuri kama ya wale ambao wanaweka picha nzuri.

Kwa mfano mtu anaweka picha anakula vyakula vizuri anakuandikia I AM HAVING LUNCH, wakati huo wewe unakula makande au wali maharage ni manyanyaso makubwa sana kisaikolojia. Hali kama hii inakufanya wewe ujione maisha yako sio mazuri kama ya watu hao.

Kitu unachotakiwa kukumbuka ni kwamba watu hawa wameweka picha hizo nzuri chache tu, kuna siku wanakula makande kama wewe ila hawaleti picha zao kwenye mitandao. Kuna siku wanashinda njaa ila hawatakuandikia kwamba wameshinda njaa.

Hivyo acha kujilinganisha na chochote unachokiona kwenye mtandao wa kijamii. Kama mtu kaweka picha anakula vizuri au kavaa vizuri au yuko kwenye kiwanja kizuri usijaribu kujilinganisha hata kidogo. Maisha yako wewe yanaweza kuwa bora kuliko hata ya watu hao.

Tumia mitandao ya kijamii kujumuika na wengine ila isiwe sehemu ya wewe kujilinganisha na wengine na hatimaye kuona maisha yako hayana thamani.

TUKO PAMOJA.

Faida Tano Za Muziki Kiafya Na Mziki Mzuri Unaoweza Kusikiliza Leo.

Watu wengi wanapenda kusikiliza mziki ili kuburudika, ila mziki una faida nyingi sana ukiacha kuburudika tu.

Mziki una faida kiafya kwa yeyote anayesikiliza. Ila mziki tunaozungumzia hapa ni mziki laini.

Zifuatazo ni faida tano za mziki kiafya.

1. Mziki husaidia hupunguza maumivu.

Watu ambao wanateseka na maumivu makali wameonesha kupata afadhali wanaposikiliza muziki laini.

2. Mziki unaimarisha kinga ya mwili.

Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi zinaonesha kwamba kusikiliza muziki kunaimarisha kinga ya mwili.

3. Mziki unawasaidia watoto njiti.

Watoto njiti ambao wamezaliwa kabla ya muda wa kawaida wa mtoto kuzaliwa wanaweza kunufaika sana na mziki uliopangiliwa vizuri na unaoendana na sauti zilizopo kwenye tumbo la mama.

4. Mziki unasaidia wazee.

Wazee mara nyingi hujisikia wapweke na kuwa na sononeko. Kwa kusikiliza mziki wanapata ahueni kwa kipindi kidogo.

5. Mziki unaweza kukusaidia kupunguza huzuni.

Kama una huzuni au umekasirishwa ukisikiliza mziki laini hasira zako zinaweza kupungua kwa kiasi kikubwa.

Anza kusikiliza mziki laini sasa na upate faida hizo na nyingine nyingi kiafya. Unaweza kuanza kwa kusikiliza mziki huo hapo chini.

PICHA; Nchi Zilizotawaliwa Na Uingereza Na Miaka Zilipopata Uhuru.

UK

NILICHOJIFUNZA LEO; Sababu Za Kihistoria Kwa Nini Scotland Ilitaka Kujitenga Na Uingereza.

Jana tarehe 18/09/2014 wananchi wa Scotland walipiga kura ya kuamua kama Scotland ijitenge na kuwa na mamlaka yake kamili au iendelee kuwa sehemu ya Uingereza(United Kingdoms). Matokeo ya kura hiyo yaliyotangazwa leo asubuhi yanaonesha kwamba asilimia 55.3 wamekataa kujitenga na asilimia 44.7 walipiga kura ya kutaka kujitenga. Kwa matokeo hayo Scotland inaendelea kuwa sehemu ya Uingereza.

 

Nilitaka kujifunza zaidi juu ya muungano huu wa Scotland na England.

Mwaka 1602 malkia Elizabert I wa England alifariki dunia bila ya kuacha uongozi kwa watu wa familia yake. Mfalme James I wa Scotland alikuwa msimamizi wa ncho zote mbili lakini kila nchi ilikuwa na uhuru wake.

Mwaka 1707 viongozi wa Scotland walikubali kuungana moja kwa moja na England kutengeneza United Kingdoms. Baadhi ya wananchi wa Scotland hawakufurahishwa na maamuzi haya ni hivyo yalitokea maandamano mengi kupinga muungano huo. Kwa miaka mingi baadhi ya wananchi wa Scotland wamekuwa wanajaribu kujitoa ila wanashindwa.

Mwaka 1999 Scotland waliweza kuwa na bunge lao. Uingereza waliruhusu Scotland kuweza kufanya maamuzi yao juu ya mambo kama afya, nyumba na elimu, lakini bajeti walipangiwa na Uingereza.

Bado wananchi wengi wa Scotland hawakufurahishwa na hili na hivyo manunguniko ya chini chini yalikuwa yakiendelea. Chama cha upinzani kiliposhika nafasi ya kuongoza bunge la Scotland viongozi wake walipendekeza ipingwe kura ya kuamua kuendelea kuwepo chini ya Uingereza au kujitegemea wenyewe.

Haya yote ndiyo yaliyopelekea kwenye kura iliyofanyika jana. Na kama tulivyoona kwenye matokeo asilimia 44 ya wanaotaka kujitenga sio ndogo na hivyo huenda chokochoko zikaendelea.

Tunaweza kujifunza nini hapa kwenye muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar? Karibu kwa maoni.

Faida Tano (5) Za Kulala(Kusinzia) Mchana.

Katika jamii zetu kulala mchana inaweza kuonekana kama uvivu. Yaani mtu anayelala mchana anaonekana ni mvivu na hapendi kazi. Kinyume na imani hii kulala mchana kuna faida kubwa sana kuliko ulivyowahi kufikiri.

Leo utajifunza faida tano za kulala mchana na kama utaweza uweke ratiba hiyo kwenye kila siku yako.

1. Inapunguza stress.

Kufanya kazi kwa siku nzima inaweza kukufanya uwe na stress nyingi sana. Kupata dakika chache za kulala inapunguza stress hizi.

2. Inaongeza uwezo wa kujifunza na kumbukumbu.

Ni rahisi sana kujifunza na kukumbuka yale uliyojifunza kama akili inakuwa imepumzishwa. Kulala mchana kunaipumzisha akili.

 

3. Inaongeza ubunifu.

Kama unafanya kazi ambazo zinahitaji ubunifu wa hali ya juu kuwa na utaratibu wa kulala mchana na unapoamka unakuwa katika nafasi nzuri ya ubunifu.

4.  Ni bora kwa afya yako.

Tafiti zinaonesha kwamba watu wanaolala mchana wanauwezekano mdogo wa kupata magonjwa ya moyo ukilinganisha na ambao hawalali mchana.

5. Inaongeza ufanisi.

Watu ambao wanalala mchana huamka wakiwa na ufanisi mkubwa kuliko ambao wanafanya kazi siku nzima.

Ni muda gani ulale?

Muda wa wewe kulala mchana ni mfupi sana kati ya dakika 20 mpaka 25. Hivyo hata kama unafanya kazi unaweza kutenga dakika 20 baada ya chakula na ukasinzia au kulala kidogo. Sio lazima ulale kitandani, hata kkuinamisha kichwa chako kwenye meza inakutosha kunufaika na usingizi huo. Anza sasa kujilaza dakika 20 na uboreshe maisha yako.

Nakutakia kila la kheri.

NENO LA LEO; Kuhusu Muonekano Wako Wa Nje.

How things look on the outside of us depends on how things are on the inside of us.

 

Jinsi mambo yanavyoonekana kwa nje inategemea na jinsi tulivyo ndani yetu.

Anza kubadili kilichoko ndani yako ili kuona mabadiliko ya nje. Anza na mawazo yako, ukibadili mawazo yako utaona mabadiliko kwa nje.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Kuhusu Uerevu

A wise man does in the beginning, what a foolish man does in the end.

 

Mtu mwerevu hufanya mwanzoni, kile ambacho mpumbavu hufanya mwishoni.

Kuwa mwerevu sasa kwa kujifunza kupitia makosa ya wengine na usiyarudie.

Nakutakia kila la kheri.

Mambo 10 Unayotakiwa Kuacha Kufanya Ili kuboresha Maisha Yako.

Maisha yetu ya kila siku yana changamoto nyingi sana. Lakini sehemu kubwa ya changamoto hizi tunasababisha wenyewe kutokana na maamuzi tunayofanya au tabia zetu wenyewe.

Hapa kuna mambo kumi ambayo unatakiwa uache kuyafanya ili uweze kuwa na maisha bora.

1. Acha kulalamika sana kwenye maisha yako. Kulalamika hakutakusaida zaidi ya kukufanya ujione huna msaada. Kama kuna kitu hukipendi kibadilishe, kama huwezi kukibadilisha achana nacho.

2. Acha kujiongezea msongo wa mawazo. Usijipe kazi nyingi kupiata uwezo wako, usiahidi mambo mengi na usijaribu kufanya kila kitu.

3. Acha kujutia makosa uliyofanya zamani. Kuendelea kujutia kila siku na kukumbuka ulichopoteza au ulichokosa hakutakusaidia chochote zaidi ya kukuumiza. Jifunze kutokana na makosa hayo na songa mbele.

4. Acha kuhofia kesho yako na anza kufanyia kazi ndoto zako. Hofu ni kitu ambacho hakipo ila kinakuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa. Achana na hofu sasa na fanya kitu kufikia ndoto zako.

5. Acha kusogeza mambo mbele na anza leo. Umesema unataka kuanza biashara ila utaanza kesho, kesho haitafika, anza leo kuweka mipango yako na anza kuifanyia kazi.

6. Acha kutegemea watu wengine ndio wakupe furaha, kumbuka furaha inatoka ndani yako.

7. Acha kulinganisha maisha yako na ya watu wengine. Hakuna mtu mwenye uwezo ambao unao wewe. Kazana kuwa bora kila siku ila sio kujilinganisha na wengine.

8. Acha kusubiri muda muafaka. Unasubiri muda muafaka ndio uanze biashara? Muda muafana ndio sasa, hutapata muda mwingine mzuri kama huu kufanya kile ambacho unataka kufanya.

9. Acha kukimbia matatizo yako. Kukimbia matatizo sio kuyasuluhisha, yataendeleakukufata ulipo. Yakabili matatizo yako na uyatatue.

10. Acha kukaa na watu wanaokurudisha nyuma. Watu unaokaa nao wana ushawishi mkubwa sana kwako. Kama unakaa na watu waliokata tamaa na wanaolalamika tu na wewe utakuwa hivyo hivyo.

Boresha maisha yako kwa kuacha kufanya mambo haya ambayo yanakurudisha nyuma.

TUKO PAMOJA.

Fanya Mambo Haya Matano Kila Siku Asubuhi Na Utakuwa Na Siku Yenye Mafanikio.

Kila siku inayoanza ni siku mpya kwako kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na dunia kwa ujumla. Hijalishi siku ya jana ilikuwaje kwako, ila leo unayo kwenye mikono yako na ni uamuzi wako kama unataka kuifanya siku yenye mafanikio au unataka kuipoteza.

Fanya mambo haya matano kila siku asubuhi na utakuwa na siku yenye mafanikio makubwa.

1. Amka asubuhi na mapema. Unapoamka asubuhi na mapema unakuwa na faida ya kuwa macho kabla ya watu wengine. Muda huu ni muda wenye utulivu na unaweza kufanya mambo yako vizuri.

2. Soma nusu saa kila siku. Baada ya kuamka mapema, tumia nusu saa ya kwanza akujisomea kitabu kizuri kitakachokufundisha na kukuhamasisha. Kama huna kitabu bonyeza hapa na uweke email yako utatumiwa vitabu.

3. Pangilia siku yako. Andika ni mambo gani matatu ambayo ukiyakamilisha siku ya leo yatakuletea mafanikio makubwa. Pangilia jinsi utakavyofanya mambo hayo.

4. Fanya mazoezi. Unapofanya mazoezi asubuhi unauweka mwili wako katika hali ya uchangamfu na ukakamavu, hata akili yako inaweza kufanya kazi vizuri.

SOMA; Faida 5 za kukimbia dakika 5 kila siku.

5. Pata kifungua kinywa. Ni muhimu sana kupata kifungua kinywa asubuhi. Hii ni kwa sababu unapolala ni kama unakuwa umefunga na hivyo unapoamka mwili unakuwa hauna chakula cha kutosha.

Haya ni mambo ambayo unaweza kuanza kuyafanya mara moja na ukaona mabadiliko kwenye maisha yako. Hebu anza kuyafanya sasa na upate mafanikio kwneye maisha yako.

TUKO PAMOJA.

Mambo Matano(5) Ya Kufanya Wakati Unaelekea Kukata Tamaa.

Maisha yana changamoto nyingi sana. Kuna wakati mambo yanaweza kuwa magumu sana kwako na kuona kama vile huo ndio mwisho wa dunia. Huu ndio wakati ambao unakata tamaa na kuona haiwezekani tena. Kabla ya kufikia hali hii ya kukata tamaa kuna mambo matano ya kufanya ambayo yatabadili kabisa hali yako.

1. Pitia tena malengo yako. Ni kipi hasa kinakusukuma ufanye hicho unachofanya? Ni nini hasa kinakufanya utake kufikia malengo hayo. Ukijua sababu hii itakusukuma zaidi hata mambo yanapokuwa magumu.

2. Kumbuka mafanikio yako. Kabla hujakata tamaa hebu kumbuka ni mambo mangapi umeshafanikiwa mpaka sasa. Kama unafikiri hujafanikiwa kwa lolote, fikiri tena kwa kina.

3. Kumbuka kwamba vikwazo ni sehemu ya maisha. Hakuna safari ya maisha iliyonyooka, kila mtu aliyefikia mafanikio makubwa alikutana na vikwazo vikubwa sana.

4. Fanya kile unachoweza kufanya kwa ubora. Wakati mambo yanapokuwa magumu badala ya kutumia muda mwingi kufikiria kwa nini mambo yanakwenda hivyo, tumia muda wako kufanya kile unachoweza kufanya kwa ubora wa hali ya juu. Utaongeza thamani na kuweza kuondoka kwenye magumu.

5. Kumbuka kwamba hauko peke yako. Kuna watu wengi sana ambao wako tayari kukusaidia katika hali unayopitia. Moja ya njia rahisi za kupata msaada wa watu hawa ni kusoma vitabu vya kukuhamasisha. Kuna vitabu vingi sana vinavyoweza kukuhamasisha na kubadili kabisa mtazamo wako. Soma nusu saa kila siku na utaona mabadiliko makubwa. Kama huna kitabu cha kusoma bonyeza hapa na uweke email yako utatumiwa vitabu.

Fanya mambo haya machache unapokuwa unapitia hali ngumu yenye kukatisha tamaa. Kumbuka ya kwamba kama utakata tamaa ndio unakuwa umeaga mashindano. Ila kama ukiendelea kuvumilia utaibuka mshindi.

Nakutakia kila la kheri.

NENO LA LEO; Kuhusu Uwezo Wako Mkubwa.

If you think you are too small to be effective, you have never been in the dark with a mosquito!

 

Kama unafikiri wewe ni mdogo sana kuweza kuleta mabadiliko makubwa, hujawahi kukaa kwenye giza ukiwa na mbu.

Kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa ulioko ndani yake. Ujue uwezo wako na utumie kufikia mafanikio makubwa.

TUKO PAMOJA.

Faida 5 Za Kukimbia Dakika 5 Kila Siku.

Kila mtu anafahamu kwamba mazoezi ni kitu muhimu sana kwa afya njema na maisha kwa ujumla. Lakini inapokuja kwenye kufanya mazoezi, watu wengi hufikiri ni lazima kwenda kwenye eneo maalumu la mazoezi au kununua vifaa maalumu. Kwa hiyo ukosefu wa vifaa hivyo na ukosefu wa muda pia hufanya watu wengi kushindwa kufanya mazoezi.

Leo utajifunza faida tano za kukimbia dakika tano kila siku. Nani ambaye hana dakika tano kwenye siku yake? Nani ambaye hana eneo la kukimbia dakika tano? Jibu ni hakuna.

Hizi ndio faida 5 za kukimbia dakika 5 kila siku.

1. Inapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Magonjwa ya moyo sasa hivi yamekuwa tishio sana kutokana na watu kutofanya mazoezi.

2. Utaishi muda mrefu. Kwa kufanya mazoezi utakuwa na afya imara na hivyo utaweza kuishi muda mrefu zaidi.

3. Inakusaidia kuwa katika hali nzuri. Kwa kufanya mazoezi unakuwa katika hali nzuri inayokuwezesha kufanya majukumu yako kwa ufanisi zaidi.

4. Unapata usingizi mzuri. Kwa kufanya mazoezi, mwili unapata nafasi nzuri ya kupumzika unapolala, na hivyo kuwa na usingizi mzuri.

5. Kuongeza ufanisi wa akili. Mazoezi hasa yanapofanywa asubuhi huifanya akili kuwa katika ufanisi wa hali ya juu.

Hizi ndio faida tano unazoweza kuzipata kwa kukimbia dakika tano kila siku. Anza leo jioni au kesho asubuhi ili kuepuka magonjwa na pia kuongeza ufanisi wa akili yako.

TUKO PAMOJA.

Mbinu 5 Zitakazokufanya Uwe Mbunifu Zaidi.

Iwe umeajiriwa au umejiajiri unalipwa kulingana na ubunifu wako. Kama unataka kulipwa zaidi, yaani kupata wateja wengi zaidi au kupata kipato kikubwa zaidi ni muhimu kila siku kuongeza ubunifu wako kwenye kile unachofanya.

Hizi hapa ni mbinu tano zitakazokufanya uwe mbunifu zaidi;

1. Pata muda wa kupumzika. Tafiti zinaonesha kwamba mtu anapokuwa amechoka, uwezo wake wa kufikiri unakuwa chini sana.

2. Fikiria kama mtoto. Watoto wana ubunifu mkubwa sana kwa sababu hufikiri bila ya kujiwekea mipanga. Anza kuondoa mipaka kwenye fikra zako na ufikiri kwa uhuru zaidi.

3. Fanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana ili kuweka akili yako katika ufanisi wa hali ya juu.

4. Jipe muda wa mwisho wa kukamilisha kitu. Kama kuna jukumu unafanya jipe muda ambao ni lazima uwe umemaliza. Jinsi muda unavyokaribia kuisha utajikuta unapata mawazo mazuri ya kufanya.

5. Usikatae mawazo mabaya haraka. Wakati unafikiri unaweza kuja na mawazo mengi sana. Usianze kujiwekea mipaka kwamba hili ni zuri na hili ni baya, yaangalie yote vizuri na ujue ni kipi cha kufanya.

Tumia mbinu hizi kila siku na utaona ubunifu wako ukiongezeka.

Muhimu; Kila siku fanya unachofanya kwa ubunifu zaidi.

TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Kutabiri Kesho Yako.

The best way to predict your future is to create it!

Njia bora ya kutabiri kesho yako ni kuitengeneza leo.
Usihangaike kupata utabiri kwamba maisha yako ya baadae yatakuwaje. Unao uwezo wa kuyatengeneza na kuwa kama vile unavyotaka wewe. Kujifunza zaidi tembelea AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Kila la kheri.

Sheria 10 Za Kuzingatia Kwenye Maisha.

Kuna sheria nyingi sana ambazo tunaishi nazo kwenye maisha yetu. Kuna ambazo tumezikuta kwenye jamii kwa asili na kuna ambazo zinatungwa na mamlaka husika.

Hapa kuna sheria kumi ambazo unatakiwa kuishi nazo kila siku ili kurahisisha maisha yako.

1. Ukifungua kitu, hakikisha unakifunga.

2. Ukiwasha kitu, hakikisha unakizima.

3. Ukivunja kitu, kubali umekivunja.

4. Kama huwezi kurekebisha ulichokivunja, mtafute anayeweza akirekebishe.

5. Ukikopa lipa.

 

6. Kama kuna kitu unakithamini, kijali.

7. Ukichafua, safisha.

8. Kama kitu sio chako, omba ruhusa kabla ya kukitumia.

9. Kama hujui jinsi ya kutumia kitu, jifunze kwanza au achana nacho.

10. Kama hakikuhusu usikiulizie maswali.

Kama unavyoona hizi ni sheria rahisi sana ambazo kama ukianza kuzifuata utaepukana na matatizo mengi sana. Anza kuzitumia sasa.

TUKO PAMOJA.

Mambo 10 Rahisi Unayoweza Kuanza Kufanya Leo Na Ukaboresha Maisha Yako.

Safari ya maisha ni safari yenye changamoto nyingi sana. Katika safari hii kuna milima na mabonde na hata visiki vinavyoweza kukukwamisha. Ili kuweza kushinda changamoto hizi kuna vitu vidogo vidogo sana unavyoweza kufanya kila siku na ukaboresha maisha yako.

 

Haya hapa ni mambo 10 unayoweza kuanza kufanya leo na ukaboresha maisha yako.

1. Kuwa na mtazamo chanya. Katika kila jambo linalotokea jua kuna kitu kizuri cha kujifunza au kunufaika.

2. Kunywa maji mengi. Sehemu kubwa ya mwili wako ni maji, ukosefu wa maji unaweza kukufanya upate matatizo ya kiafya.

3.  Jenga tabia ya kujisomea. Tabia hii itakufanya uweze kufikiri zaidi na pia utajifunza zaidi. Kama huna kitabu cha kusoma bonyeza hapa na uweke email yako utatumiwa vitabu.

4. Jifunze kusema hapana. Matatizo mengi unayokutana nayo kwenye maisha yako yanatokana na wewe kukubali kila kitu unachokutana nacho au unachoambiwa. Anza leo kusema hapana.

5. Acha kutumia simu yako kwa muda. Simu za kisasa zimetufanya tuwe watumwa wa kila mara kuangalia nini kinaendelea. Anza leo kuzima simu yako japo kwa saa moja na utumie muda huu kufanya mambo mengine.

6. Pata kifungua kinywa. Watu wengi wanakosa kifungua kinywa kwa sababu ya haraka au kupunguza matumizi, usifanye hivi.

7. Usitumie zaidi ya unachopata, hakikisha matumizi yako yanakuwa pungufu ya kipato chako.

8. Acha kulalamika. Kama kuna kitu hukipendi kibadilishe, kama huwezi kukibadilisha achana nacho.

9. Omba msaada. Huwezi kufanya kila mwenyewe, unahitaji msaada wa watu wengi.

10. Kaa mbali na watu wenye kukatisha tamaa. Ukiwa karibu nao watakurudisha nyuma.

Maisha unayoishi ni yako na una uwezo wa kuyabadili na kuyafanya vile unavyotaka wewe. Anza leo kwa kufanya mambo hayo rahisi na utaona mabadiliko makubwa.

TUKO PAMOJA.

Njia 10 Rahisi Za Kuondoa Msongo Wa Mawazo.

Msongo wa mawazo ni kitu kibaya sana kwa afya yako na hata kwa kazi au biashara yako. Unapokuwa na msongo wa mawazo huwezi kufanya maamuzi sahihi na hivyo kujikuta ukipata matatizo zaidi.
Japokuwa hakuna anayependa kuwa na msongo wa mawazo, maisha yetu ya kila siku yanatutengenezea msongo wa mawazo. Msongo huu unaweza kutokana na watu wanaotuzunguka au hata kazi tunazofanya.
stress2

Fanya mambo haya kumi ambayo ni rahisi sana na utaweza kuondoa msongo wa mawazo.

1. Pata muda wa kutosha wa kupumzika. Ukiweza kulala inakuwa bora zaidi.
2. Fanya matembezi ya taratibu ukiwa mwenyewe kwa muda usiopungua nusu saa. Tembea sehemu ambayo unaweza kuona vitu vya asili kama majani au miti.
3. Chukua karatasi na uandike vitu kumi kwenye maisha yako ambayo unafurahi kuwa navyo, cha kwanza furahi kwamba bado unaishi.
4. Sikiliza mziki ambao unaupenda sana. Kila mtu ana aina yake ya mziki anaipenda.
5. Kaa kimya kwa dakika tano, usifikirie chochote kwa dakika hizo tano tu. Kuhakikisha hufikirii chochote hesabu pumzi zako.
6. Nyoosha misuli yako. Kama umekaa kwa muda mrefu nyanyuka na ufanye mazoezi kidogo yatakachangamsha misuli yako.
7. Fanya kazi ya kujitolea, tenga siku moja au muda wako na ufanye kazi za jamii za kujitolea. Kwa kutoa unajisikia vizuri zaidi.
8. Panga kukutana na marafiki zako uliopotezana nao muda mrefu. Kwa kukutana nao na kukumbushana mambo mliyokuwa mnafanya utajisikia vizuri.
9. Nenda sehemu ambayo hujawahi kwenda. Utaona mambo mapya na kujifunza mambo mapya yatakayokufanya uwe na mawazo mapya.
10. Angalia vichekesho, utacheka na kubadili hali yako ya msongo.
Fanya mambo haya kuondoa msongo wa mawazo. Sio lazima ufanye yote kwa wakati mmoja. Chagua machache unayoweza kuyafanya na yakabadili hali yako ya msongo wa mawazo.
Kila la kheri.

NENO LA LEO; Kuhusu Kufanya Mambo Mengi.

It's important to focus on one thing at a time. Even in the Roman times they understood this with their Proverb; "The man who chases two rabbits catches none."

 

Ni muhimu kufanya jambo moja kwa wakati. Hata wakati wa Roma walielewa hili kwa msoemo wao; mtu anayekimbiza sungura wawili, hushindwa kumsiha hata mmoja.

Chagua mambo machache na uyafanye kwa ufanisi mkubwa na utapata mafanikio makubwa sana.

TUKO PAMOJA.

Hili Ndilo Kosa Kubwa Tunalokwenda Kufanya Watanzania 2015.

Mwaka 2015 ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu sana na watanzania wengi umekaribia kabisa kufika. Huu ni mwaka ambao uchaguzi mkuu wa nchi yetu utakwenda kufanyika na hivyo wananchi kupata nafasi ya kuchagua diwani, mbunge na raisi ambaye tunaona anatufaa.

Mwaka 2015 umekuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu kwa sababu wananchi wengi tumeaminishwa na kuamini kwamba baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 na chama tawala kuondoka madarakani maisha yetu yatakuwa mazuri sana. Ni imani nzuri sana ambayo tumekuwa nayo hasa ukizingatia hali ya nchi kiuchumi ipo chini sana ukilinganisha na rasilimali tulizonazo.

Pamoja na kuwa na imani hii nzuri, kuna kosa kubwa sana ambalo watanzania tutakwenda kulifanya mwaka huo 2015. Kosa hili litatugharimu tena miaka mingine mitano au hata zaidi ya hapo kama hatutaendelea kujifunza.

Kosa hili kubwa ni kutokuwa na vigezo vya kiongozi tunayemtaka sisi wananchi. Na kwa kukosa vigezo hivi tutarudia makosa ambayo tuliyafanya nyuma kwa kuchagua watu kutokana na umaarufu wao. Kutokana na kuangalia umaarufu tumechagua viongozi wengi ambao wameishia kutuangusha na kushindwa kutimiza ahadi zao wenyewe.

Ni lazima sisi kama wananchi bila hata ya kuambiwa na wanasiasa, tuwe na vigezo vya aina ya kiongozi tunayemtaka. Na hii ni kuanzia udiwani, ubunge na uraisi. Lazima sisi tuwe na vigezo vyetu kisha wale watakaojitokeza kuomba nafasi hizo tuwachuje kwa kutumia vigezo vyetu.

SIASA

Ilivyo sasa ni kwamba wananchi hatuna vigezo vyetu, ila tunatumia vigezo vya wagombea watakavyotuletea na hivyo tunaweza kulinganisha baina ya mgombea na mgombea na kuamua kumchagua mmoja wao. Hapa ina maana kama wagombea wote ni wabovu tutamchagua ambaye ni ahueni. Na hapa ni kwa sehemu ndogo, shemu kubwa itatumia kigezo cha umaarufu.

Ni kigezo hiki cha umaarufu ambacho kinawafanya watu sasa hivi kuitisha mikutano ya waandishi kila kukicha kutangaza nia zao za kugombea uongozi. Ni kigezo hiki cha umaarufu ambacho kinawafanya watu kuzunguka huku na kule kutoa misaada ili waonekane wanajali sana.

Sasa watanzania tuache kufanya kosa hili ambalo litaendelea kugharimu maisha yetu.

Katika makala zijazo tutazungumzia ni vigezo gani tunaweza kuvitumia katika kila nafasi ya uongozi ili tuweze kupata viongozi bora.

Tanzania ni nchi yetu sote, unapopata ujumbe huu wajulishe na wenzako wote unaowafahamu ili tuweze kuleta mabadiliko kwenye nchi yetu.

Usisahau kuweka email yako ili upate makala hizi moja kwa moja kwenye email yako.

TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Yasiyowezekana.

“Most things that we think are impossible in life, is because we have never tried them. So go for every dream and opportunity before making a judgement.”

“Mambo mengi tunayofikiri hayawezekani ni kwa sababu hakuna aliyewahi kujaribu kuyafanya, hivyo fanyia kazi kila ndoto yako kabla ya kujihukumu kwamba haiwezekani”

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Kuhusu upatikanaji wa FURSA

"Opportunities are found by those who look for them! The bee has a sting but honey too... so look at every negative and make a positive out of it."
"Fursa zinapatikana kwa wale wanaozitafuta, nyuki anauma ila ana asali pia.... hivyo angalia kwenye kila tatizo kuna njia ya kutokea"
Nakutakia siku njema.

NILICHOJIFUNZA LEO; Viongozi Mashuhuri Walioibadili Dunia.

Karibu kwenye kipengele hiki cha mambo niliyojifunza kwa siku husika. Kwa siku zinazokuja nitakuwa nakushirikisha yale ninayojifunza kuhusu uongozi kupitia kitabu WORLD FAMOUS LEADERS WHO RESHAPED THE WORLD.

Hiki ni kitabu kilichoeleza kwa kifupi baadhi ya viongozi ambao walifanya mambo makubwa duniani. Unaweza kujipatia kitabu hiki na ukaendelea kujifunza zaidi. Kava lake naweka kwenye picha hapo chini;

viongozi

Viongozi hawa kuna waliofanya makubwa kwa wema kama Nelson Mandela na wengineo na kuna waliofanya makubwa kwa ubaya kama Adolf Hitler aliyesababisha vifo vya zaidi ya wayahudi milioni sita.

Kuna mengi ya kujifunza kupitia maisha na uongozi wa watu hawa.

Nakukaribisha katika safari hii ya kujifunza.

TUKO PAMOJA.

NENO LA LEO; Kuhusu Hazina Ya Mwanadamu.

“More gold has been mined from the thoughts of men than has been taken from the earth. So dust off the cobwebs and use all those great ideas you have!”

“Dhahabu nyingi imechimbwa kwenye mawazo ya wanadamu kuliko iliyochimbwa ardhini. Hivyo futa futa utando uliokinga mawazo yako na anza kuyatumia mawazo yako kuleta mabadiliko.”

Nakutakia siku njema.

Je Vijana Wanaoingia Kwenye Siasa Wanaweza Kuwa Wakombozi Wetu?

Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana hapa Tanzania ambao wanaingia kwenye siasa. Na kwanzia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo baadhi ya vijana waliogombea ubunge walipata kuchaguliwa kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa vijana kuingia kwenye siasa.

Na hata kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 vijana wengi wameonesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali za udiwani na ubunge katika maeneo mbalimbali. Na kwa kuwa mpaka sasa hatuna sheria inayoruhusu mgombea binafsi, vijana hawa wote ambao wana nia ya kugombea inawalazimu kupitia vyama vya siasa. Kwa sasa tuna vijana wengi sana ambao wameingia kwenye vyama mbalimbali vya siasa na wengine wamepata nafasi kubwa kwenye vyama hivi.

siasa

Swali kubwa la kujiuliza ni je vijana wengi kuingia kwenye siasa wanaweza kuwa wakombozi wa nchi yetu Tanzania? Natumia neno ukombozi kwa sababu naamini nchi yetu inahitaji ukombozi ili kutoka hapa ilipo. Inahitaji ukombozi kwa sababu tumefika hapa tulipo kutokana na uongozi mbovu na siasa na sera mbovu zilizowekwa na viongozi hawa wabovu. Na ukiangalia viongozi hao umri wao umekwenda sasa na hivyo vijana ndio watakwenda kuchukua nafasi zao siku za mbeleni.

Najiuliza swali hili kwa sababu tumeona baadhi ya vijana ambao wameingia kwenye siasa hizi wakiishia kutumiwa na baadhi ya watu na hivyo kujikuta wakishindwa kuleta mabadiliko yoyote. Tumeona baadhi ya vijana ambao walikuwa wakilalamikia uongozi mbovu ila wamepewa uongozi kwenye sehemu mbalimbali na kushindwa kuleta mabadiliko yoyote. Na vibaya zaidi wanaishia kuwa sehemu ya kitu walichokuwa wanakipinga.

Sina tatizo na kijana ambaye ameingia kwenye chama chochote cha siasa alichopenda yeye. Iwe ameingia CCM, CHADEMA, CUF au hata CHAUSTA. Kikubwa ambacho wananchi wanataka kuona ni mabadiliko ya kweli katika siasa zetu na hatimaye uongozi wa nchi yetu. Naamini mabadiliko haya yanawezekana kupitia vijana kama watajua ni kitu gani wanakwenda kufanya kwenye siasa hizi na kuepuka kutumika na wale ambao wapo kwenye mifumo hii kwa muda mrefu.

Wewe kama ni kijana ambaye umeingia kwenye siasa jiulize swali hili mara kwa mara na hakikisha unakuwa sehemu ya mabadiliko popote unapokuwepo.

Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuleta mabadiliko katika taifa letu Tanzania.

TUKO PAMOJA.

Hakikisha hukosi makala mpya kila inapowekwa kwenye blog hii. Weka email yako hapo juu ili upate makala moja kwa moja kwenye email yako.

NILICHOJIFUNZA LEO; Vita Kubwa Kuwahi Kutokea Afrika Ukiacha Vita Vya Pili Vya Dunia.

Ukiacha vita vya pili vya dunia vita kubwa ambayo imewahi kutokea Afrika ni vita ya pili ya Congo(Second Congo War)
Vita hii ilianza August 1998 na kutangazwa kumalizika July 2003 baada ya serikali ya mpito kushika madaraka.
congo war
Pamoja na kutangazwa kumalizika kwa vita hii bado mapigano na choko choko zinaendelea katika majimbo ya Kivu na Ituri.
Ni katika vita hii ambapo raisi wa Congo Laurent Kabila aliuawa na mtoto wake Joseph Kabila kushika madaraka ya kuongoza nchi.
Vita hii ilihusisha mataifa tisa ya Afrika na vikundi zaidi ya 20 vya wapiganaji.

Sababu ya vita hii.

Sababu kubwa iliyochangia vita hii ni mgogoro wa kimaslahi katika uchimbaji na biashara ya madini.

Madhara ya vita hii.

Vita hii ndio vita kubwa zaidi kutokea barani Afrika ukiacha vita vya pili vya dunia. Mpaka kufika mwaka 2008 zaidi ya watu milioni 5.4 walikuwa wamepoteza maisha kutokana na vita hii. Vifo vingi vilitokana na mauaji ya kuvita, huduma mbovu za afya na ukosefu wa chakula.
Kuna mengi sana ya kujifunza katika vita hii. Kwa kifupi nimeweza kukuandalia haya kwa leo.
Tukutane tena wakati mwingine. Usisahau kuweka email yako ili upate makala hizi moja kwa moja.

Vyanzo;

WIKIPEDIA; Second Congo War.

Nilichojifunza Leo.

Nilichojifunza Leo ni kipengele kipya kitakachokuwa kinakujia mara kwa mara kupitia blog hii Makirita Amani. Ningependa kipengele hiki kiwe kinakujia kila siku ila siwezi kuahidi hilo kwa sasa.
Kupitia kipengele hiki utajifunza mambo mengi kuhusiana na UONGOZI, SIASA, UCHUMI, MAENDELEO na hata HISTORIA za nchi yetu Tanzania, bara letu Afrika na hata Dunia kwa ujumla.
Tutajifunza mambo mengi yatakayotusaidia kuelewa zaidi nchi yetu na dunia kwa ujumla wakati tunajiandaa kuwa viongozi bora wa nchi yetu.
Kupitia kipengele hiki mimi na wewe tutajifunza mambo yatakayotuandaa kuweza kuisaidia nchi yetu, wakati huo mimi naendelea kujiandaa kuwa raisi wa nchi yetu Tanzania.
Karibu sana katika blog hii maalumu kwa maswala ya uongozi na kuhakikisha hukosi machapisho yanayowekwa, weka email yako kwenye box hapo juu na utapokea makala moja kwa moja kwenye email yako kila zinapowekwa.
Naamini tutaendelea kuwa pamoja kwenye safari hii.
Nakutakia kila la kheri.