Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini - 2

Ndugu msomaji karibu tena katika mwendelezo wa makala yangu ya namna ya kujijengea uwezo wa kujiamini. Naamini ulifaidika na machache kati ya mengi ambayo niliyaainisha katika juma lililopita. Nakukaribisha tena tuweze kuongeza ufahamu wetu kupitia jukwaa hili la JIONGEZE UFAHAMU.

Kama hukusoma makala ya wiki iliyopita isome kwa kubonyeza hapa; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini.

9. Tabasamu

Ninaposema tabasamu simaanishi kucheka bali ni hali ya kuonyesha bashasha usoni. Si tu kwamba kutabasamu kutaonyesha kwamba unajiamini bali pia huonyesha kwamba wewe ni mtu mwenye siha njema na hujasongwa na mawazo. Kutabasamu kutakusaidia kuonyesha kwamba wewe ni mkarimu. Ni rahisi zaidi kuwasiliana na mtu aliyetabasamu kuliko kinyume chake. Mtu kutokutabasamu inatuma ujumbe kwa watu kuwa yawezekana yeye hajiamini, mwoga au ana hasira na wakati mwingine husababisha mawasiliano yao na watu wengine kuwa magumu.

10. Mtazame unayeongea naye.

Hili tatizo la kushindwa kumtazama unayezungumza naye usoni linawakabili watu wengi, pengine mimi na wewe. Kumtazama unayeongea naye usoni huweza kutuma ujumbe kwamba uko makini na unayezungumza naye, unajali anachozungumza na kufurahishwa na mazungumzo yake. Pia huonyesha kwamba wewe unajiamini na siyo mwoga. Kumtazama unayezungumza naye haimaanishi kumkodolea macho muda wote kwani unaweza kumfanya akose kujiamini. Jifunze tabia hii kwani wataalamu husema kwamba macho ni lango la moyo na kupitia machoni unaweza kugundua mengi ikiwemo kujua kwamba yanayozungumzwa na msemaji ni ya kweli au uongo. Kumbuka kila mtu ana tabia ya kuona haya/aibu lakini inakupasa uishinde kwa mazoezi.

SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.

11. Jiweke katika hali ya kutoogopwa

Jifunze kujiweka katika hali ya kufanya watu wawe rahisi kuzungumza na wewe. Kuna watu wamejitengenezea mazingira ya kuonyesha kwamba hawako tayari kuzungumza na watu. Watu hawa hujifanya kwamba wanatumia sana simu zao kwa kuongea ama ujumbe mfupi na mengine yanayofanana na hayo. Pia usipende kuzungusha miguu wala mikono yako kwani unatuma ujumbe kwamba hauko tayari kuzungumza. Kumbuka lugha ya alama huzungumza yaliyo ndani mwako hivyo chukua tahadhari. Ulivyo kwa nje inasadifu ulivyo kwa ndani.

12. Fahamu vipaji vyako

Kuna wakati ambao unaweza kujijisikia kukosa thamani. Katika kipindi hiki chukua kalamu na karatasi na uandike kuhusu vipaji vyako na vyote vizuri ulivyowahi kuvifanya. Achana na mabaya ama vitu ambavyo vitakufanya ujidharau. Kumbuka pongezi ulizowahi kupewa na ndugu, jamaa na hata marafiki. Jaribu kusahau mabaya yaliyosemwa juu yako na watu kwani hayana nafasi katika maisha yako. Kumbuka hata ukiwa mfano mbaya watu wengine wanaweza kujifunza kwa mfano wako. Kumbuka kuwa kama vile wewe usivyo mkamilifu ndivyo na watu wengine wasivyo. Fanyia kazi vipaji vyako na punguza au ondoa kabisa mabaya yako na kwa hali hii utakuwa mtu mwenye kujiamini sana. Kumbuka kujiambia kuwa wewe ni mshindi siku zote na acha kujihukumu.

SOMA; Haya Ndio Mambo Matatu Yatakayokuletea Matokeo Ya Kushangaza.

13. Kumbuka ulizaliwa ukijiamini

Unakumbuka ulipokuwa mtoto mchanga? Kipindi hicho ulikuwa mwenye kujiamini na ulifanya vitu uliyoona wewe vinafaa. Ulilia, ulitambaa, ulicheza na mengi kadhalika bila kumwogopa yeyote. Lengo langu kukumbusha haya ni ujue kuwa kutokujiamini kwako kumetokana na kuhukumiwa na watu na kunyooshewa vidole kila ulipokwenda. Lakini lililo jema zaidi ni kwamba kila mtu huja duniani bila kitu na hujifunza vyote hapa duniani. Kama vyote uliweza kujifunza unaweza pia kujifunza kujiamini na kuacha ama kusahau kutokujiamini.

14. Sio tatizo lako peke yako

Kuna msemo unasema kifo cha wengi ni harusi. Msemo huu unakusaidia kujua kuwa kila mtu hukabiliwa na matatizo kama wewe. Tatizo la kujiamini ni la dunia nzima. Kila mtu hukabiliwa na tatizo hili ila wengine wamejifunza kulishinda tatizo hilo na kulificha kwenye macho ya jamii. Kiukweli kila mtu huwa jambo analojiamini kwayo na yapo mengine mengi ambayo wanashindwa kujiamini. La muhimu zaidi acha kujifananisha na watu wengine kwani haya ni maisha yako na hupaswi kuwa sawa na mtu fulani. Hupaswi kuwa sahihi zaidi, mjanja zaidi ama mzuri zaidi bali kuwa mwenye furaha zaidi. Kumbuka kuwa kuweza kujiamini si suala la siku moja na huhitaji muda zaidi. Kuna siku waweza kushindwa lakini usife moyo, jaribu tena na tena.

SOMA; Hizi Ndizo Gharama Unazotakiwa Kuzilipia, Ili Uweze Kupata Kile Unachokihitaji Katika Maisha Yako.

15. Saidia wengine

Kusaidia watu wengine kutakuongezea uwezo wa kujiamini zaidi. Saidia pale unapoweza, pongeza panapostahili na punguza kuhukumu wengine. Kama kuna mtu anahitaji msaada wako jaribu kumsaidia hata kama hajakuomba kwani kuna watu wengine ni waoga wa kuomba msaada. Hii itakusaidia kujiamini, kujenga urafiki na pia kufungua milango ya wewe kusaidiwa kwani kadiri unavyotoa ndivyo unavyopokea. Utajisikia vizuri sana pale utakapojua kuwa Fulani kafanikiwa kwa sababu yangu pia.

16. Achana na wanakufanya ukose kujiamini.

Kuna watu katika hii dunia hupenda kuhukumu wengine kwa kila jambo walifanyalo liwe zuri au baya. Watu wa namna hii kaa nao mbali kwani siku zote utakuwa mdogo tu kwao na hutaweza kujiamini. Hawa hutafuta makosa na mapungufu yako siku zote. Kaa nao mbali kama wenye ugonjwa wa ebola lakini si kuwachukia. Chagua marafiki ambao watakufanya ujisikie vizuri katika ubora wako. Tabia na mafanikio yako huchangiwa kwa kiasi kikubwa na watu unatumia nao muda wako mwingi.

SOMA; Haya Ndio Matumizi Mazuri Ya Mshahara Wako Ambayo Yatakuletea Furaha Na Mafanikio.

17. Ongea na watu wageni kwako

Kujiamini ni zaidi ya kusoma ama kujifunza kupitia vitabu na makala, hii ni tabia ambayo hujifunzwa. Jifunze kuongea na watu wageni usoni kwako kwani huwezi kujua ni wapi utawahitaji. Itakuwia vigumu mwanzoni lakini baadaye utazoea kadiri siku zinavyokwenda na kadiri unavyoongea na wageni. Kuongea na watu usiowafahamu pia ni ukarimu.

18. Tegemea mafanikio

Katika kila jambo unalofanya tegemea mafanikio. Watu wengi sana hushindwa jambo kabla ya kulijaribu, kwa maana nyingine hushindwa mchezo nje ya uwanja. Ukitegemea kushindwa hutaweza kulifanya jambo kwa jitihada kwani huwezi kwenda mbali zaidi ya unavyowaza. Hivyo basi katika kujiamini amini pia kwamba inawezekana. Inawezekana anza sasa, usiahirishe kwani kamwe hutafanya ama utafanya katika hali ya taharuki.

Asante kwa kuuungana nami katika makala hii, tupo pamoja.

Makala hii imeandikwa na Nickson Yohanes ambae ni mjasirimali na mhamasishaji.

Unaweza kuwasiliana na naye kwa: simu: 0712 843030/0753 843030

e-mail: nmyohanes@gmail.com Pia unaweza kutembelea blogu yake: www.lifeadventurestz.blogspot.com kujifunza zaidi.

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na Mjasiriamali Email: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

Hii Ndio Njia Moja Muhimu Ya Kufikia Mafaniko Makubwa.

NJIA MOJAWAPO YA MAFANIKIO NI KUWA MWENYE BIDII

Katika kila jambo kunahitajika bidii. Bidii ni nguvu ambayo inamwezesha mtu kufikia malengo yake aliyojiwekea ili aweze kufanikiwa.

Mpendwa msomaji wa makala hii ukitaka ufaulu katika jambo lolote lile lazima ujijengee tabia ya kujituma ,maana maendeleo yoyote yale katika jambo lolote yanahitaji mtu anayejituma.

SOMA; Kama Tayari Una Ndoto Hiki Ndio Unatakiwa Kufanya.

Mawazo ya mtu mwenye bidii siku zote huelekea utajiri tu. Utajiri unakuja baada ya kufanyia kazi mawazo yako kwa bidii. Mtunzi wa kitabu cha Who will Cry When You Die-Robin Sharma anasema ‘’ Live your life in such away that when you die the world cries while you rejoice’’ maana yake ‘‘ ishi maisha yako kiasi kwamba siku ukifa dunia nzima italia wakati wewe unafurahia’’ hivyo basi usemi huu unatuasa tuweke bidii ili tuweze kufanikiwa na kuleta matokeo chanya katika jamii.

SOMA; Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuishinda Hofu.

Hivyo basi, mafanikio yeyote duniani katika nyanja yeyote ile yanaletwa na bidii yako katika jambo hilo unalowekea bidii, bidii inatumika katika biashara, elimu, michezo, uongozi nakadhalika.

‘’ You can not see, what you don’t look for’’ maana yake huwezi kuona kwa kile ambacho hukitafuti ‘’ mtunzi wa kitabu cha The Compound EffectDarren Hardy amedhihirisha hilo katika usemi wake hapo juu. Hivyo basi, tunapaswa kuwa wenye bidii katika kazi, masomo, biashara nakadhalika ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu na kuleta mabadiliko chanya katika jamii zetu tunazoishi.

SOMA; Kitu Hiki KImoja Kitakufanya Ushindwe Kwenye Biashara.

’Mawazo ya mwenye bidii huelekea utajiri tu bali mwenye pupa huelekea uhitaji’’

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi mhamasishaji na mjasiriamali unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe (E-mail) deokessy.dk@gmail.com

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasahanaRumishael Peterambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na MjasiriamaliEmail: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

Nilichojifunza Leo; Zoezi Moja Litakalobadili Maisha Yako Kabisa.

Nilichojifunza Leo

Leo nilipata wasaa wa kukutana na Mimi mwenyewe. Jana kabla ya kulala nilipanga appointment ya kukutana na Mimi mwenyewe asubuhi na mapema. Mbinu hii ya kukuta na mimi nilijifunza kwa rafiki yangu Amani Makirita . Nilipokutana na mimi tulijadili na kujifunza mambo kadha , kwa leo ngoja nikushirikishe nilijchojifunza kuhusu Mabadiliko.

Karibu kwenye somo

• You must change you self before changing others. The most difficult person to change is yourself
Ni rahisisi sana kumwambia mwenzako “unatakiwa ubadilike bwana” je umeshawahi kukaa peke yako ukajisemesha maneno hayo? Kumbuka ni rahisi kutamani kuona wengine wakibadilika, lakin wengi wetu hatuko tayari kubadilika sisi wenyewe. Kubadilika sio kitu kirahisi unahitaji nguvu ya ziada. Maana akili yako na mwili wako vilishakua na mazoea Fulani (status quo). Sasa katika kubadilisha mazoea hayo kuna kua na upinzani wa hali ya juu, Maana tunapenda kua katika hali tuliyoizoea maana hapo ndipo tunapokua comfortable. Sasa unapojaribu kutoka kwenye hiyo hali lazima uweke mikakati mizuri na uweze kuifutilia kuifanya mara kwa mara bila kujali unajisikia kufanya au hujisikii mpaka pale umepata yale mabadiliko unayoyatamani. Kumbuka ni rahisi kurudia hali ya mwanzo kuliko kufikia kwenye mabadiliko.
Mabadiliko ya kweli ni yale yanayokufanya kua mtu bora zaidi kuliko ulivyokua hapo awali. Katika mchakato wa mabadiliko utaumia, wakati mwingne utaona kama unajitesa vile. Lakini usiyatazame hayo Tazama kule unakotaka kufika, kama wewe ni Daudi, au John au jina lolote, mtazame Daudi au John unayetaka kumuona baada ya mabadiliko hiyo itakutia hamasa ya kuendelea mbele na mchakato wa kubadilika. Pia furahia kuona mabadiliko madogomadogo maana hayo ndiyo yatakayopelekea mabadiliko makubwa.

Fanya appointment na wewe binafsi, jipe muda wa kukutana na wewe mwenyewe. Jipe muda wa kujisikiliza. Mbona hua unapanga appointment na watu kibao. Lakin Je hua unapata wasaa wa kukutana na wewe binafsi? Au wewe sio wa muhimu kwako?

Nafikiri tukutane tena na tutaongelea zaidi jinsi ya kukutana na wewe na ni nini cha kusema unapokuna na wewe na faida zake.
Nakuachia hizi nukuu mbili za watu mahiri kabisa:

1. “Mabadiliko ya kweli lazima yaanze na wewe kubadilika. Kama hujabadilika wewe usijisumbue kumwambia mwingne abadilike” Daudi Mwakalinga

2. Change will not come if we wait for some other person or some other time. We are the ones we've been waiting for. We are the change that we seek. - Barack Obama

Hakuna lisilokua na mwisho. Kinachodumu ni mabadiliko. Nakutakia kila la kheri katika safari ya mabadiliko.

Daudi Mwakalinga
CC:
Makirita Amani
Unaweza pata kitabu kizuri sana kinachohusiana na Mabadiliko. Nashauri sana kitafute. tembelea hapa kujua zaidi JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA.

Makala hii imeandikwa na Daudi  Mwakalinga.

Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka.

Kila mmoja anania ya kufikia mahali fulani katika maisha yaani kuwa na pesa kiasi fulani,kuwa na familia ya aina fulani,kuwa na aina fulani ya uhusiano,kuwa na kiwango fulani cha elimu, au kufikia kiwango fulani cha imani kiroho,kuwa na ainafulani ya marafiki, kupata kitu fulani, au kuona maisha yapo katika kiwango fulani. Hizi zote ni ndoto ambazo hutufanya sisi binadamu kutengeneza malengo mbalimbali katika kila eneo la maisha yetu.

Kunamsemo unasema kuwa mtu ambaye hana ndoto hajui aendako na hawezi kupotea njia, ni kweli kama huna ndoto inamaana kuwa lolote linalokuja mbele yako ni sawa kwakua hujui unataka mambo yako yawe namna gani.

Kwa wale wenye ndoto na malengo kama mimi na wanaopenda kufikia malengo yao naomba tuungane hapa kukumbushana baadhi ya vitu vitakavyokusaidia kwa namna moja au nyingine kukufanya ufikie malengo yako kwa haraka.

1. Fahamu ni nini hasa unataka katika maisha yako.

Ni vizuri kuwa na uhakika wa nini unataka? katika kila eneo la maisha yako . Kiroho,mahusiano, uchumi na kijamii.

Ni vigumu sana kuboresha mahusiano ambayo hujui unataka yaweje kwa kua hutajua mbinu ya kuyafanya yafikie kiwango cha uzuri usichokijua hata wewe. Ni hivyo pia katika upande wa uchumi na kiwango cha elimu. Kwa mfano ukifahamu unahitaji kupata kiasi fulani cha pesa kwa mwaka ni rahisi kujua utatakiwa kupata kiasi gani kwa mwezi,wiki na hata kwa siku ili baada ya mwaka ufikie kiwango unachotaka. Ukijua kiwango unachohitaji kwa siku ni rahisi sasa kutafuta ni nini ufanye ili kukuingizia kiwango unachohitaji kwa siku. Hivyo ni vizuri kujua safari unayoiendea kabla ya kuanza safari hiyo.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

2. Kuwa na bidii

Watu wanaofanya kazi zao kwa bidii mara nyingi hufanikiwa. Katika kila eneo unalotaka kuboresha weka bidii. Weka bidii katika kuhudumia familia yako, kusoma, kufanya kazi za ofisi, kufanya biashara yako, malengo yako ya kufikia kiwango unachotaka yatafikiwa kwa haraka kama utafanya kila jambo kwa bidii na sio kwa mazoea kama watu wengine wanavyofanya.

3. Tumia muda wako vizuri.

Muda ni rasilimali ya thamani sana katika maisha ya binadamu. Kama hautakuwa makini katika kuutunza muda wako na kuutumia vizuri basi utajikuta kila lengo ulilonalo halifikiwi kwa wakati. Pangilia siku yako na mambo muhimu unayotakiwa kuyakamilisha kwa siku hiyo. Usipoteze muda kwa kuangaliakurasa za watu whatsAppna moyo wako unakusuta na kukukumbusha jambo muhimu unalotakiwa kufanya. Au kukaa na wenzio unacheza karata au kuhadithiana mpira au tamthilia ya jana ilikuaje.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Tumia muda wako vizuri kwa kufanya majukumu yako ya siku kutokana na malengo uliyojiwekea, jipe muda wa kupumzika na kutafakari ili ufahamu kama unaelekea unakohitaji. Muda wa kufanya mambo mengine unayodhani ni ya ziada uwe mdogo ili usiathiri ufikiwaji wa malengo yako. Na muda huo usipopatikana usisikitike kwakua hayo mambo mengine yapo nje ya malengo yako.

4. Acha lawama.

Ili uweze kufikia malengo ni lazima uache tabia ya kulaumu wengine. Jione kuwa wewe ndiye mwenye jukumu la kufanya malengo kufikiwa au yasifikiwe na sio kulaumu wengine kwa makosa yako. Binadamu mara nyingi tunapenda kuwalaumu watu wengine kwa makosa yoyote yanayotokea, na kwakufanya hivyo tunashindwa kuona ni wapi tunahitaji kuparekebisha.

Jaribu kujizuia kuwatupia lawama watu wengine kosa linapotokea. Chukua jukumu la kuchunguza na kufanya marekebisho mahali ambapo hukutimiza wajibu ipasavyo. Kwa kufanya hivyo utaona malengo yako yakifikiwa kwa urahisi kabisa. Ukimuachia mtu kazi aifanye, mfano kupika chakula na wewe ni mmiliki wa sehemu ya chakula hakiki kwanza kama chakula kimepikwa vizuri kabla wateja hawajala ili ujue ni nini cha kurekebisha badala ya kuacha wateja walalamike na wewe uwalaumu wapishi bila kujua kuwa ni jukumu lako kuangalia ubora wa chakula kabla ili kuhakikisha kuwa haupotezi wateja.

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

Asante sana kwa kuungana nami kwenye sehemu hii ya kwanza ya makala, tutaonana wiki ijayo katika sehemu ya pili ya makala hii. Naomba uyafanyie kazi yale unayosoma kila siku ili uone mabadiliko.

Nakutakia maisha yenye furaha.

MWANDISHI: ESTHER NGULWA

MAWASILIANO: 0767 900 110/ 0714 900 110

estherngulwa87@gmail.com

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasahanaRumishael Peterambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na MjasiriamaliEmail: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

Mambo Matano Ya Muhimu Kuyafahamu Kabla Ya Kuwekeza Kwenye Kilimo.

Wiki iliyopita tuliweza kuona jinsi ambavyo fikra potofu watu walizo nazo kuhusu kilimo zilivyodidimiza kilimo chetu. Pia tuliweza kupata picha ambavyo nchi tajiri zilivyowekeza kwenye kilimo kupitia teknolojia za kisasa zaidi. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ya wiki iliyopita isome hapa; Haya Ndio Mapinduzi Makubwa Tunayohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Kilimo.

Leo hii napenda tuanze kujifunze mambo matano ambayo kila mtu aliye na ndoto ya kuwekeza kwenye kilimo ni lazima ayafahamu vizuri. Kutotilia maanani moja ya mambo haya kunaweza kupelekea ukakichukia kilimo. Leo tutaanza na mambo mawili.

1. Soko

Hili ndilo jambo la muhimu kwenye kila uwekezaji au kwa maana nyingine biashara yeyote lazima itegemee soko. Na hapa ndipo wengi wanakosea sana wakulima wadogo na hata vijana wanaoingia kwenye kilimo maana wengi wanazalisha kwa kufuata mkumbo kwa vile wengi wanazalisha wakati huo au amesikia labda kilimo cha zao Fulani kinalipa. Kabla ya kuwekeza kwenye kilimo lazima uanze kwa kulitambua soko lako. Lazima uzalishaji wako uwe unaendeshwa na soko. Unatakiwa kua na taarifa za kutosha kuhusu soko, kujua soko linasemaje, ni wakati gani watu wengi wanakua wamezalisha, wakati gani bidhaa hii inakua kwa wingi sokoni, ni wakati gani inakua hadimu na ni kwanini? Usizalishe kwa vile ni msimu wa kuzalisha kwamba unaona mko wengi. Watu wengi wanaofaidika kwenye kilimo ni wale ambao hawafuati mkumbo kwenye kuzalisha wao wanajua kucheza na wakati, wakati bidhaa ile ni hadimu au wakati ambao sio msimu wa kuzalisha, ndio wakati wa wao kuzalisha na hivyo kupelekea kupata faida nzuri zaidi. Hata kampuni kubwa zinazowekeza kwenye kilimo kwanza wanakua na soko la uhakika, aidha baada ya kufanya utafiti wa kutosha au kwa kuingia mikataba na wateja wao. Vyovyote vile lakini wanachokua na uhakika nacho ni kua wanajua ni wapi watauza baada ya kuzalisha. Mfano kwa kampuni zinazozalisha maua Arusha na maeneo mengine soko lao kubwa liko uholanzi (Amsterdam Auction) na ndio maana asilimia kubwa ya wamiliki wa kampuni hizo ni waholanzi maana wanalijua vizuri soko la maua. Ila kwetu hali ni tofauti badala ya kuanzia sokoni sisi tunaenda moja kwa moja shambani kuzalisha baada ya mazao kukomaa na kua tayari kuvuna ndio tunalikumbuka soko, yaaniumeshazalisha ndio unaenda kutafuta soko, bila kujua pengine ulichonacho hakihitajiki na soko.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Wengine wanaweza kusema hatuwezi kuwekeza kwenye kilimo maana soko hakuna, hasa wakulima wadogo wengi wanafahamu soko ni pale kwenye mkusanyiko wa watu wengi kama kwenye minada, magulio au kwenye masoko kama Kilombero, Arusha, Mabibo Dar es salaam n.k.Unachotakiwa kujua ni kwamba kuna aina kadhaa za masoko mfano masoko ya ndani yasiyo rasmi, masoko ya kitaasisi kama mahoteli, mashule na mahospitali. Pia kuna masoko ya kiviwanda; mfano viwanda vya kuongeza thamani kama vya AZAM au REDGOLD Arusha n.k Bila kusahau masoko ya kimataifa kama Ulaya, Asia na hata nchi za jirani kama Sudan ambako kumekua na vita na watu wamekua hawana muda wa kuzalisha. Hata hivyo kuna vitu vingi sana vya kujifunza kwenye upande wa soko naona kwa leo tuishie hapa kwa upande wa soko, tukipata muda huko mbeleni tutajadili kwa kina.

SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya

2. Hali ya hewa inayoruhusu kilimo husika

Kila kilimo cha zao fulani kina hali ya hewa au mazingira yanayo kiruhusu kilimo hicho kustawi vizuri. Kwenye eneo hili tunaangalia maswala ya jotoridi, unyevunyevu kwenye hewa, mvua na sifa za udongo unaosaidia ukuaji wa zao husika. Kuna mazao yanapendelea hali ya joto na kuna mengine yanastawi kwenye hali ya baridi. Mfano kama mananasi yanapendelea ukanda wa joto na ndio maana yana stawi sana ukanda wa pwani huko. Katika sifa za udongo kuna sifa za kikemikali au kifizikia. Mfano wa sifa hizo ni kama pH ambacho ni kipimo cha kiwango cha asidi na alkali ya udongo. Hii ina maana pH ya udongo wako ikiwa ndogo chini ya 5 udongo wako una kiwango cha asidi na ikiwa kubwa zaidi ya 8 maana yake udongo wako una kiwango fulani cha alkali.Katika aina ya udongo inakubidi ufahamu ni udongo mfinyanzi, tifutifu au kichanga. Usije ukapanda mpunga kwenye udongo wa kichanga wakati mpunga unapendelea udongo unaotuamisha maji. Au unapanda vitunguu kwenye udongo unashikamana sana (mfinyanzi) wakati kitunguu kinahitaji udongo wenye kuachia (tifutifu) ili kiweze kujijenga vizuri.Lakini ngoja nisiingie kwa kina sana hapa kwenye udongo maana kuna mambo mengi sana na ndio maana watu wanasomea shahada za chuo kikuu kwenye masuala ya udongo na hata wengine wanakua maprofesa wa udongo.

SOMA; Fanya Mambo Haya Matatu Na Usipokuwa Tajiri Ndani ya miaka 10, sahau kuhusu utajiri kwenye maisha yako.

Lengo la kukupitisha hapa kidogo ni ili ufahamu kwamba baada ya kupata soko la uhakika na kujua ni zao gani kinachofuata ni kujua maeneo gani zao hilo linastawi, ni udongo wa aina gani unaofaa. Unashauriwa kabla ya kupanda uchukue sampuli ya udongo ukapime maabara kujua sifa za udongo wa shamba lako. Zipo taasisi za serikali na binafsi zinazotoa huduma ya upimaji udongo. Taasisi hizo ni kama taasisi za utafiti wa kilimo kama SARI (Arusha) ARI Ukiliguru ( Mwanza), ZARI Kizimbani (Zanzibar), ARI Maruku Kagera, ARI Kibaha n.k Pia zipo taasisi za elimu kama Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro. Ukishapima udongo unapewa ushauri wa zao gani linaweza kustawi vizuri kwenye shamba lako lakini pia unapata ushauri wa aina gani ya mbolea unatakiwa kutumia. Gharama ya upimaji inategemea na wingi wa vitu unavyotaka kupima kwenye huo udongo.

Kwa kifupi maeneo mengi ya nchi yetu ni mazuri sana kwa kilimo na ndio maana tunaona nchi nyingi zinakuja kuwekeza kwenye kilimo nchini kwetu. Hata hapa kwenye jumuiya ya Afrika mashariki wenzetu wanaimezea mate sana ardhi yetu yenye rutuba. Nchi ya Tanzania inauwezo mara kumi ya Kenya au kwa maneno mengine ina hali ya hewa nzuri katika kuzalisha mbogamboga mara kumi zaidi ya Kenya, maeneo mengi ya Kenya ni makame sana.Lakinicha kushangaza wenzetu wanazalisha mazao hayo na kuuza nje ya nchi mara kumi zaidi ya Tanzania. Je ni kwanini? Basi naomba tukutane tena wiki ijayo hapa hapa

Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au 0658 587029 au barua pepe (email)daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na Mjasiriamali Email: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

Maswali ambayo huulizwa mara nyingi kuhusu uwekezaji katika hisa.

Watu wengi wanatamani kufanya uwekezaji katika hisa na kufahamu jinsi ambavyo uwekezaji huu unavyofanyika ila kuna vitu vingi hawavifahamu katika uwekezaji. Maswali haya yatakufungua mwanga jinsi ya kutambua uwekezaji katika hisa, jinsi ambavyo unafanyika na jinsi ambavyo mwekezaji atapata manufaa katika uwekezaji huu.

1. Nini ushiriki wa soko la hisa (DSE) katika kupanda na kushuka kwa thamani ya Hisa?

Soko la Hisa (DSE) haihusiki kabisa katika kuchangia kupanda na kushuka kwa thamani ya hisa. Vitu ambavyo vinasababisha kushuka na kupanda kwa za hisa ni nguvu ya soko (yaani wanunuzi na wauzaji). Wanunuzi wakiwa wengi katika hisa ya kampuni Fulani hupelekea kupanda kwa bei kwa sababu watashindana kwa bei ili kila mtu aweze kununua hisa hizo.

2. Wapi unaweza kupata bei za hisa?

Ili uweze kupata taarifa za bei ya hisa za kila siku tembelea tovuti yao ambayo ni www.dse.co.tz. Katika tovuti yao utaweza kufahamu bei za kampuni ambazo zimeongezeka na kampuni ambazo bei zake zimeshuka.

SOMA; Changamoto Inayokusumbua Kwenye Biashara.

  1. Naweza kununua hisa kuanzia ngapi?

Kiwango cha chini cha kununua hisa katika soko ni hisa 100 ila mwekezaji unaweza kununua hisa chini ya mia moja kwa lugha kingereza huitwa odd lots board. Kwa hiyo mwekezaji yoyote anaweza kununua hisa chini ya mia moja katika soko la hisa yaani unaweza nunu hisa 5, 10, 20 au zaidi.

4. Hisa zinauzwa wapi?

Hisa zinauzwa sehemu mbili i) katika soko la wali, hapa ni pale kampuni ambapo inauza hisa zake kwa mara ya kwanza kabla ya kusajiliwa katika soko la hisa. ii) Hisa zinauzwa kwa madalali wa soko la Hisa au unaweza nunua katika tawi la benki ya CRDB lolote lile. Anwani za madalali wa soko la Hisa zinapatikana katika tovuti ya DSE au soma makala hivi ndivyo unavyoweza kununua hisa.

5. Nalipia hisa mara moja tu au ni kila mwezi kwenye Kampuni husika?

Ukinunua hisa pesa unatoa mara moja tu, ikiwa utahitaji kununua hisa zingine utalipia kwa hisa ambazo unaongeza. Baada ya kununua hisa zako hakuna gharama nyingine zaidi ya kusubiri hisa zako kuongezeka thamani na kupata gawio. Ikiwa utahitaji kununua hisa nyingine utalipia kwa bei ambayo ipo sokoni.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

  1. Kwa sisi tulioko mikoani tunawezaje kununua hisa?

Mmoja wa madalali wa soko la Hisa ameingia ubia na benki ya CRDB kwa hiyo popote lililopo tawi la benki ya CRDB unaweza ukanunua hisa. Vile vile kuna kampuni nyingine za madalali ambalo watafanya utaratibu wa kununua hisa.

  1. Je unaweza kupata taarifa za utendaji na ufanisi wa kampuni unapokuwa mwanahisa?

Kampuni yoyote ambayo imesajiliwa katika soko la hisa ni lazima iweke taarifa zake muhimu kuhusu utendaji wake na taarifa za fedha za kila mwaka, miezi mitatu na miezi sita. Kama mwekezaji taarifa hizi zitakusaidia kujua kampuni ambayo inafanya vizuri na ambayo haijafanya vizuri ili uweze kuchagua kampuni bora ya kuwekeza.

  1. Hisa zinapatikana muda wote au ni kwa muda Fulani tu?

Kuna aina mbili ya masoko ya hisa, soko la awali ambapo hisa huuzwa kwa mara ya kwanza na kwa kipindi maalumu tu na kuna soko la upili ambapo soko la hisa halina kipindi maalum unaweza kununua na kuuza muda wowote iwe tu ni siku ya kazi (Jumatatu hadi Ijumaa). Katika soko la upili ndipo soko la Hisa linapofanya kazi zake kila siku ya kazi ambapo mwekezaji atanunua na kuuza hisa zake.

SOMA; Haya Ndio Matumizi Mazuri Ya Mshahara Wako Ambayo Yatakuletea Furaha Na Mafanikio.

  1. Je gawio hutolewa mara ngapi na kampuni kwa wawekezaji?

Gawio hutolewa kulingana na sera ya kampuni husika. Kuna kampuni ambazo hutoa gawio mara mbili kwa mwaka na kuna kampuni ambazo hutoa gawio mara moja kwa mwaka. Ukiwa mmiliki wa hisa unayo haki ya kupata gawio ikiwa kampuni itatoa gawio hilo kulingana idadi ya hisa ambazo unamiliki.

  1. Je nikifariki hisa zako atamiliki/atarithi nani?

Soko la hisa limeandaa utaratibu ambao kila mwekezaji ambaye ananunua hisa katika fomu ambazo unapewa utajaza mrithi wako. Mrithi wa hisa unaweza kumchagua mtu yoyote Yule ambaye wewe ungependa awe mrithi wako.

Endelea kutembelea mtandao huu kuendelea kupata makala nzuri kuhusu uwekezaji katika Hisa na mfulululizo wa maswali na majibu kuhusu bidhaa ya Hisa.

Mwandishi: Emmanuel Mahundi

Mawasiliano emmanuelmahundi@gmail.com simu 0714445510

Kwa kujifunza zaidi tembelea www.wekezamtanzania.blogspot.com

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na Mjasiriamali Email: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini

Huwezi kupambana na adui unayemuogopa hata siku moja. Yabidi kwanza kutomuogopa adui yako ndio uweze kupambana naye. Sifa ya kwanza inakupasa kumjua adui yako, kujua uwezo na udhaifu wake. Adui mwenyewe wa kumjua ni wewe mwenyewe. Kama nilivyosema katika makala iliyotangulia kwamba chanzo cha matatizo mengi ni woga. Kuogopa kitu ambacho kinaweza kutokea ama kisitokee. Kitokee ama kisitokee hupaswi kukiogopa. Kukosa kujiamini ni tatizo linalowakwamisha watu wengi. Hakuna anayeweza kukuondolea tatizo hili zaidi yako mwenyewe, hivyo basi fanya yafuatayo na utaliepuka tatizo lenyewe.

1. JIPENDE

Labda kuna watu wangeuliza kujipenda vipi? Hakika kuna watu hawajipendi. Kama hujipendi wewe utawezaje kumpenda mtu mwingine? Na unategemea vipi watu wengine wakupende? Ninaposema kujipenda simaanishi kuwa mbinafsi. Namaanisha kwamba inakupasa kujithamini. Jithamini kwa kula vizuri, kujipamba, kujipumzisha na hata kuoga. Kama wewe hujipendi jiandae kutopendwa na watu wengine. Na kitendo cha kutopendwa na watu wengine kinaweza kwa kiasi kikubwa kukuondolea kujiamini na kujaa woga wa kukosolewa. Kwa mfano hakuna mtu anayependa kukaa na mtu mchafu ama anayenuka, anayekasirika bila sababu nk. Jipende nawe utapendwa, pia utajiamini.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

2. VAA VIZURI

Kuvaa vizuri hakukugharimu kitu kwani mavazi ni mojawapo ya mahitaji muhimu matatu ya binadamu. Mengine ni chakula na malazi. Ninaposema kuvaa vizuri nina maana kujua vyema ni nguo zipi zinazokupendeza. Si lazima ziwe za bei ghali. Hata mtumbani unaweza kupata nguo nzuri kwa bei nafuu. Jitahidi pia kuvaa nguo kulingana na mahali na pia utamaduni wa jamii inayokuzunguka. Usipende kuvaa nguo zinazoonyesha sehemu kubwa ya mwili wako ama nguo zinazobana sana mwili wako. Hii itakusaidia kuondokana na wasiwasi wa kujihisi kuvaa vibaya.

3. KUWA NA MAISHA YENYE MTAZAMO CHANYA

Ili uwezekujiaminiinakupasa kujijengea maisha yenye mguso na mtazamo chanya. Kwanza kabisa acha kujiwazia kushindwa. Waza uwezekano wa kitu na akili itakupa jinsi ya kutatua tatizo linalokukabili. Usiseme jambo hili ni gumu ama haliwezekani bali sema jambo hili litafanikiwa ama tatizo hili nitalitatua na kwa hakika akili yako itakupa mbinu nyingi za kulifikia lengo lako. Lakini ukishasema siliwezi akili yako itajifunga na jambo hilo hutafanikiwa. Usijinenee maneno ya kukatisha tamaa. Pia haitoshi tu kuwaza katika hali ya uwezekano (chanya), bali pia anza kuchukua hatua chanya. Jiulize kwanini wenzako wameweza? Kwa kuanza jaribukujitathminina kujijua vizuri, ni vitu gani unaweza kuvifanya, vikwazo unayohisi yapo na uhalisia wa uwepo wake isije ikawakwamba umejiumbia ulimwengu wako mwenyewe wa vikwazo. Kwa hiyo basi jijue na jitambue. Jua adui namba moja wa kushindwa kwako ni wewe.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

4. KUWA MTU WA WATU

Kuwa mtu watu ni kuwa mwema na kuelewana na watu wote kadiri inavyowezekana. Watu kukuona kama adui au mtu asiyeelewana na watu kunaweza kukuondolea ujasiri wako. Simaanishi kwamba uwaachie watu nafasi ya kutawala maisha yako bali simamia yale unayoyaamini wewe. Simamia misingi yako uliyojiwekea. Kujihisi kwamba wewe ni mtu mzuri kutakujenga kuliko kujihisi wewe ni mtu mbaya. Kumbuka Imani huja kwa kusikia, kusikia watu wakikuongelea vibaya kutakuvunja moyo.

5. JIANDAE VYEMA

Katika makala iliyopita nilijaribu kueleza kuhusu suala la kujiandaa kwa jambo lolote. Kujua kitu kutakufanya ujisikie vizuri na hivyo kujiamini. Ndio maana basi wachezajihujiandaa vyema kabla ya kucheza mechi zao na hujiandaa zaidi pale wanapokabiliwa na mechi ngumu. Vile vile mwanafunzi ambae hajajiandaa vyema kwaajili ya mtihani, huwa na wasiwasi mwingi kabla na baada ya mtihani. Kulijua jambo kutakufanya ujiamini zaidi na kuondokana na wasiwasi.

SOMA; NENO LA LEO; Kitu Kimoja Kitakachokujengea Kujiamini Na Kujithamini.

6. ZUNGUMZA TARATIBU

Siku za nyuma kidogo kuna rafiki yangu aliniambia kwamba watu wasiojiamini huongea haraka sana na kwa sauti kubwa. Nilikuja kulithibitisha hili siku moja. Kuongea taratibu kutakufanya uonekane mwenye kujiamini. Watuwasiojiaminihuongea kwa haraka kwani wanahisi wanachokiongea hakina thamani mbele ya msikilizaji. Pia ongea kwa sauti ya kawaida inayosikika. Kuongea kwa sauti kubwa sanakunaonyeshakwamba wewe hujiamini na unataka kuwateka watu wasikie kelele zako na siyo maneno yako.

7. BADILI KUTEMBEA NA KUSIMAMA KWAKO

Labda inaweza kuonekana ni sababu ndogo lakini, lugha ya alama pia inazungumza mengi. Jinsi unavyosimama ama kutembea unawatumia watu taarifa nyingi za jinsi ulivyo ndani. Penda kusimama wima bila kuegemea vitu. Pia jitahidi kutembea mwendo wa kawaida ambao ni wa kikakamavu. Usitembee kwa kunyong’onyea wala kwa kuburuza miguu. Tembea wima huku mabega yakiwa nyuma na usitembee kwa kutazama chini kama afanyavyo kondoo. Kusimama kilegevu ama kutembea kilegevu watu watakusoma na kuhitimisha kuwa hujiamini.

SOMA; SIRI YA 10 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujiamini.

8. TAFUTA MAJIBU YA MATATIZO YAKO

Katika kitabu cha WinnersandWinners (washindi na washindi)mwandishi anatuambia kuwa walalamikaji ni wale watu ambao hutazama matatizo yao bila ya kutafutia majibu. Jua kuwa kulalamikia tatizo sio njia ya kulitatua. Ukiwa na tatizo kaa chini waza na hakika utapata majibu yake. Huna hela? Jibu lake ni kufanya kazi, hujui kusoma? Nenda shule au tafuta mtu akufundishe? Huna ajira? Tafuta ajira ama jiajiri. Majibu ya matatizo yako unayo mwenyewe. Jiamini jikubali usikate tamaa.

Mwandishi ni: Nickson Yohanes ambaye ni mjasiriamali na mhamasishaji. Unaweza kuwasiliana na naye kwa: simu: 0712843030/0753843030 e-mail:nmyohanes@gmail.com Pia unaweza kutembelea blogu yake: www.lifeadventurestz.blogspot.comkujifunza zaidi.

Makala imehaririwa kwa Kiswahili fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na Mjasiriamali Email: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Kama kuna kitu kimoja ambacho tuna uhakika nacho hapa duniani ni kwamba dunia inabadilika kila siku. Ukiangalia historia ya dunia tulikotoka na tulipo sasa kumetokea mabadiliko makubwa sana. Zilianza zama za mawe, zikaja zama za chuma, yakaja mapinduzi ya viwanda na hata sasa tupo kwenye mapinduzi ya kiteknolojia.

Jambo moja la kushangaza ni kwamba pamoja na mabadiliko haya kuwa wazi bado watu wengi ni wagumu sana kubadilika. Watu hawapendi mabadiliko, wanapenda kufanya kile walichozoea kufanya na wanataka maisha yaendelee vile yalivyokuwa jana na leo. Kitu ambacho ni ndoto isiyowezekana.

Katika zama zote ambazo dunia imepita, kuna watu ambao waliweza kubadilika haraka na kupata faida ya mabadiliko, wengine walilazimishwa kubadilika na hivyo kuburuzwa na kuna ambao waliachwa na mabadiliko na hivyo kupotea. Waliofaidika na mabadiliko ni wale waliokuwa tayari kubadilika, walioburuzwa na mabadiliko ni wale ambao walikuwa hawajui kama kuna mabadiliko ila wanakwenda tu na hali ilivyo. Walioachwa na mabadiliko ni wale ambao hata baada ya kuona mabadiliko wao waligoma kubadilika, waliendelea kung’ang’ania kile walichozoea na hatimaye kuachwa nyuma na kupotea.

mabadiliko cover EDWEB

Mabadiliko ni jambo muhimu sana lakini watu wengi hawajalipa msisitizo kwenye maisha na hii inapelekea wengi kuachwa nyuma na mabadiliko haya.

Ni kutokana na umuhimu wa jambo hili nimekuandalia kitabu kinachoitwa JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Katika kitabu hiki utajifunza mambo yafuatayo;

1. Historia fupi ya mabadiliko kwenye maisha ya mwanadamu hapa duniani na kwa nini mabadiliko yataendelea kutokea.

2. Mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye elimu, kazi na hata biashara.

3. Makundi ya aina tatu ya watu ambao wanazalishwa na mabadiliko, kundi linalonufaika na mengine yanayopoteza.

4. Mambo kumi muhimu sana ya kufanya ili na wewe uingie kwenye kundi ambalo linanufaika sana na mabadiliko ambayo yanaendelea kutokea

5. Mabadiliko makubwa yanayokuja kwenye mfumo wa elimu, mfumo wa ajira na hata biashara na ujasiriamali.

Kitabu hiki kitakuandaa wewe na kukupa mbinu za kuweza kuboresha maisha yako zaidi na kufanikiwa licha ya mabadiliko yanayoendelea.

Kitabu hiki ni muhimu sana kwa makundi yafuatayo;

1. Wanafunzi wa vyuo vikuu ambao wanasoma ila hawana uhakika wa kupata ajira. Kitawawezesha kujiandaa mapema ili kujua njia watakayochukua na hivyo kutopoteza muda wakisubiri ajira ambazo hazipo.

2. Wafanyakazi ambao wamekuwa kwenye kazi kwa muda mrefu lakini hawaoni manufaa ya kazi zao kwenye maisha yao.

3. Wafanyabiashara ambao wamefanya biashara kwa muda mrefu ila wako pale pale miaka nenda miaka rudi.

4. Wafanyakazi ambao wamestaafu kazi, wamefukuzwa kazi, wamepunguzwa kazi au wameamua kuacha kazi wenyewe.

5. Watu ambao umri wao umekwenda kiasi na wanaamini kwamba mambo waliyokuwa wanafanya zamani ni bora kuliko yanayofanyika sasa, na wanaendelea kuyafanya licha ya kushindwa kupata majibu makubwa.

6. Mtu yeyote ambaye anataka kuboresha maisha yake zaidi, kwa kujua mambo yanayoendelea na ni yapi yanakuja kwa siku za mbeleni.

Ni muhimu sana wewe kupata na kusoma kitabu hiki, kitaleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako kama utakuwa tayari kufanyia kazi yale ambayo utajifunza.

JINSI YA KUPATA KITABUJINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy yaani pdf na unaweza kukisoma kwenye simu yako kama ni smartphone, unaweza kukisoma kwenye tablet na pia unaweza kukisoma kwenye kompyuta. Kurasa zake zinasomeka vizuri kwenye vifaa hivyo vya aina tatu tofauti.

Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu tano(5,000/=), gharama hii ndogo sio kwa sababu kina mambo madogo ila ni kwa sababu kitabu hiki ni muhimu sana na kila mtu ni muhimu akisome, hivyo gharamaisiwe kikwazo cha watu kushindwa kukisoma.

Kupata kitabu unafanya malipo ya tsh 5,000/= kupitia namba 0717396253 au 0755953887 na kisha unatuma email yako kwenye moja ya namba hizo na unatumiwa kitabu mara moja.

Mambo sasa hivi yanakwenda kidigitali zaidi na huna haja ya kubeba mizigo mingi, kwa kuwa na simu yako tu unaweza kuendelea kujifunza mambo mengi sana.

Karibu sana upate kitabu hiki mapema, kwa sababu jinsi unavyozidi kuchelewa kukipata, mabadiliko yanaendelea kutokea na yanakuacha nyuma. Jinsi utakavyoweza kuchukua hatua haraka ndivyo unavyoweza kuiokoa na kuimarisha kazi yako au biashara yako. Chukua hatua haraka kwa kusoma kitabu hiki leo.

Pia tembelea blog ya VITABU VYA UJASIRIAMALI NA MAFANIKIO ili kupata vitabu vingine vingi na vizuri vya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo lolote unalofanya.

Jipatie kitabu chako leo, maisha hayakusubiri wewe uwe tayari.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kuboresha maisha yako, na kitabu hiki kiwe nguzo muhimu sana kwako.

TUPO PAMOJA.

MAKIRITA AMANI

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Haya Ndio Matumizi Mazuri Ya Mshahara Wako Ambayo Yatakuletea Furaha Na Mafanikio.

Mshahara ni makubaliano ya malipo kati ya mwajiri na mwajira kulingana na kazi anayofanya mwajiriwa. Malipo haya yanakuwa kwa muda au kipindi fulani kutokana na mkataba wao waliojiwekea.

Wakati mwingine unafanya kazi na kupata mshahara lakini hujui au hufahamu sehemu au makundi unayoweza kuugawa mshahara wako.

Zifuatazo ni bahasha tano ambazo unaweza kuugawa mshahara

1.SADAKA(Tithe Fund)

Unapopata mshahara wako asilimia kumi ya kipato chako yaani mshahara weka katika bahasha hii au mfuko huu wa sadaka. Kutoa asilimia kumi ya mshahara wako ni mwongozo wa kuufuata lakini siwezi kukulazimisha uamuzi uko mikononi mwako BO SANCHEZ katika kitabu chake cha My Maid Invest in the Stock Market alikuwa akiwaambiwa wafanyakazi wake yani wasaidizi wake hivi ‘’ You will grow in abundance think’’ usemi huu wa BO SANCHEZ una maanisha kuwa kuna faida sana pale unapotoa sadaka kama alivyonena hapo juu,  utakuwa katika uwezo mkubwa wa kufikiri’

SOMA; Tabia KUMI Za Watu Waliofanikiwa Sana(PICHA)

2. MATUMIZI ( Expense Fund)

Haya ni yale matumizi ya kila siku ya mahitaji ya nyumbani (daily needs) ambapo pia unaweza ukatenga fungu lingine la mshahara wako au kipato chako na kuweka katika bahasha hii ya matumizi.Hii itakusaidia sana kutotumia hela vibaya na kuwa na nidhamu ya pesa katika mshahara wako na itakusaidia kujuwa kwa mwezi matumizi yako yanagharimu kiasi gani.

3. MSAADA ( Support Fund)

Katika jamii zetu kusaidiana ni jambo la kawaida msaada huo unaweza ukatoa kwa ndugu,jamaa,marafiki na nk. Pengine ni kumsaidia mtaji wa kuanzisha biashara au kuboresha biashara na mengine mengi kuhusiana na msaada. Hivyo weka sehemu ya mshahara wako katika bahasha hii ya msaada hii itakusidia kutoharibu bajeti zako nyingine.

SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.

4. DHARURA (Emergence Fund)

Katika maisha yetu ya kibinadamu huwa tunapatwa na dharura sana,na ubaya wa dharura unakuja pale umepatwa na tatizo halafu huna hela ya haraka ya kutatua jambo hilo lakini kama ukiwa umeweka sehemu ya kipato chako katika bahasha hii wala hutopata shida ya kulitatua. Dharura ni nyingi katika maisha na zinatokea kwa ghafla bila taarifa kama vile ajali, radi au kifo kinavyotokea. Ukiwa na fedha ya dharura itakusaidia kuwa na amani ya akili (Peace of Mind).

5. KUSTAAFU (Retirement Fund)

Hii ni njia moja nzuri ya kuweka akiba na kustaafu ukiwa milionea. Weka ,tenga akiba katika bahasha ya kustaafu na iwekeze hela hii katika soko la hisa . Hela hii weka katika bahasha ya kustaafu na usiitumie bali iwekeze katika soko la hisa na mwisho wa siku una staafu ukiwa milionea.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Gawa mshahara wako katika mafungu haya matano na utakuwa na maisha yenye furaha na mafanikio makubwa. Kwa kutoa sadaka utakuwa vizuri kiimani, kwa kutoa msaada utakuwa vizuri kijamii na kwa kuweka akiba na kuwekeza kwenye soko la hisa utajiandaa kwa maisha yako ya baadae.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi Mhanasishaji na Mjasiriamali unaweza kuwasiliana naye kupitia namba namba 0717101595 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria. ( 2)

Ndugu msomaji karibu tena kwenye muendelezo wa makala hii ambayo itakusaidia kukupa ujasiri wa kufanya jambo lolote unalohitaji katika maisha yako. Wiki iliyopita tuliangalia baadhi ya vitu vitakavyosaidia kujenga ujasiri ambavyo ni kuweka malengo, kufanya jambo moja baada ya jingine,kupata taarifa sahihi za kitu unachotaka kukifanya na maandalizi. Kwa maelezo zaidi soma makala ya wiki iliyopita. Tuendelee kuanagalia vitu vingine.

Kama hukusoma makala ya wiki iliyopita hii hapa; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria.

5. Amini kuwa unaweza.

Hakuna jambo lolote lile unaloweza kufanya vizuri kama hata wewe mwenyewe huna imani kuwa unaweza kufanya. Imani ni kitu cha muhimu sana katika kila eneo ili kufikia malengo yako.Ukishindwa kujiamini mwenyewe basi hata watu wanaokuzunguka hawawezi kukuamini kwa lolote unalotarajia kulifanya. Ukishakuwa na wasiwasi ndani yako kwa lile unalohitaji kufanya ujasiri wote huondoka na nguvu ya kufanya jambo lolote lile hata liwe dogo huondoka.

Ukiwa na imani kuwa unaweza kufanya na kufikiri ni namna gani ufanye jambo lako , utaona akili yako ikifunguka na kukupa mbinu mbalimbali za kufanya kitu unachotaka kukifanya. Jiamini kuwa unauwezo wa kufanya mambo makubwa nutapata ujasiri wa kuyafanya mpaka wewe mwenyewe utashangaa kama ni wewe umefanya au ni mtu mwingine?

6. Kila unachogusa kufanya fanya kwa ubora wa hali ya juu.

Unapopanga kufanya kazi yoyote ile, iwe ndogo au kubwa mahali popote pale, hakikisha umeifanya vizuri sana. Ukifanya kazi kwa ubora unasikia amani ndani yako na hivyo kukupa ujasiri wa kufanya kazi nyingine huku ukiwa na imani kuwa nayo utaifanya vizuri.

Ninaimani kuna wakati uliwahi kufanya kitu kizuri na ulifanya kwa kukusudia kabisa kuwa unataka kukifanya vizuri kadiri unavyoweza. Hebu fikiria wakati ule baada ya kufanya tu kitu hicho ulijisikiaje. Ona ujasiri ulioupata ndani yako baada ya kukamilisha kitu kile. Je hauwezi kujipanga na kufanya mambo mengine makubwa unayofikiria kwa kuweka akili yako yote na kutoa muda kwa hayo mambo makubwa ambayo unafikiri yatakufikisha katika malengo yako? Kafanye unalotaka kufanya kwa ubora kabisa na utapata ujasiri wa kuendelea na mambo mengine.

SOMA; Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

7. Usiogope kushindwa.

Kama kuna jambo kubwa linaloweza kumzuia mtu kuwa jasiri na kufanya vitu vikubwa basi uoga ni jambo kubwa moja wapo.

Hakuna mtu yeyote katika maisha yake ambaye hajawahi kushindwa hata mara moja. Watu wengi jasiri uliowahi kuwaona na unaowasikia wamepitia vipindi mbalimbali vya kushindwa pia. Walijipanga kufanya mambo fulani lakini kwa namna moja au nyingine hayakwenda vile wao walivyotarajia.

Inapotokea umeshindwa, usikate tamaa. Jifunze ni wapi vitu havikwenda vizuri na ujipange upya kwa mara nyingine uboreshe pale unapoona palikua na tatizo. Katika jambo lolote unalolifanya kama umefanya maandalizi mazuri kuna matokeo ya aina mbili yaani kushinda na kushindwa, lakini katika uoga na kutofanya, tokeo ni moja tu ambalo ni kushindwa. Je unachagua kuogopa na kujiondolea hata ujasiri kidogo ulionao au kujipanga vizuri na kufanya jambo unalotaka na kuhakikisha kuwa matokeo yake hayakukatishi tama lakini yanakuwa ni njia ya wewe kujifunza na kukufanya uwe jasiri wa kufanya vitu vikubwa zaidi ambavyo vitakusaidia kupata matokeo makubwa baadae?

8. Omba msaada.

Sio rahisi sana kufanya kila jambo wewe mwenyewe na ndio maana Mungu alituumba binadamu wengi. Kila mmoja husaidiwa au kumsaidia mwingine wakati fulani. Usiogope kuomba msaada wakati unapodhani unahitaji kusaidiwa. Fahamu kuwa unaweza kupata msaada wa nguvu kazi, ushauri, au msaada wa kifedha mahali fulani na kwa wakati fulani. Uwepo wa rasilimali zote unazohitaji ili kukamilisha jambo unalohitaji ni muhimu ili kupata ujasiri wa kufanya jambo hilo. Hivyo pale unapodhani kuwa unahitaji kitu fulani usisite kuomba msaada mahala ambapo unadhani utasaidiwa.

SOMA; NENO LA LEO; Haya Ndio Maafa Unayojitengenezea Mwenyewe.

9. Sikiliza ushauri lakini usifanyiwe maamuzi na mtu mwingine.

Watu jasiri ni wazuri sana katika kufanya maamuzi. Hii haimaanishi kuwa huwa hawapati ushauri kutoka kwa wengine. Kama unahitaji ushauri ni vizuri kusikiliza wengine wanakushauri nini lakini baada ya kusikiliza ushauri kaa chini uchambue mambo mazuri katika ushari ulioupata na uamue ni nini unahitaji kufanya. Kumbuka kuwa jambo lolote unalohitaji kulifanya baada ya matokeo wewe ndiye utaonekana katika nafasi ya kufanya na sio washauri wako wala waamuzi wako. Hivyo ni vizuri kusikiliza ushauri na kuamua wewe binafsi ni nini unataka ufanye.

Ukiamua wewe mwenyewe inakupa ujasiri wa kufanya jambo tena kwa wakati mwingine lakini ukiamuliwa unaweza kujikuta ukitupia lawama kwa watu wengine. Kumbuka kuwa katika jambo lolote unalotaka kulifanya wewe ndio mwamuzi wa mwisho.

10. Muombe Mungu wako.

Kutokana na imani yako muombe Mungu wako akupe ujasiri wa kufanya mambo makubwa ambayo unaimani kuwa unaweza kufanya na yataleta mabadiliko chanya katika jamii inayokuzunguka. Amini kuwa kama watu wengine wanaweza kuwa na ujasiri wa kufanya mambo makubwa basi wewe pia waweza kujifunza kutoka kwao na kujijengea ujasiri na kuweza kufanya zaidi ya unavyoweza kufikiri.

SOMA; UKURASA WA 77; Kama Watu Hawakupingi Unakosea Sana.

Nakutakia safari njema ya kujijengea ujasiri nikiwa na imani kuwa unakwenda kukamilisha malengo yako na kufanya zaidi na zaidi kwa kadiri ya utakavyoamua wewe.

Uwe na maisha yenye furaha.

MWANDISHI: ESTHER NGULWA

MAWASILIANO: 0767 900 110 / 0714 900 110

estherngulwa87@gmail.com

Haya Ndio Mapinduzi Makubwa Tunayohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Kilimo.

Sekta ya kilimo ndio sekta inayoajri watu wengi kwa hapa Tanznia inakaridiriwa zaidi ya aslimia 80 ya watanznaia wanategemea sekta hii aidha moja kwa moja au wananufaika kwa namna moja au nyingine. Kwa ujumla hakuna nchi yeyote duniani amabyo iliendelea bila kuwekeza kwenye kilimo, basi kama ipo zitakua ni chache sana. Hata hizo nchi zenye viwanda vikubwa malighafi zake zinatokana na kilimo. Hii inaonyesha kwamba bila kilimo uchumi wa nchi utakua mashakani. Tofauti ya nchi tajiri na nchi masikini(kama zinavyoitwa nchi zinazoendelea) ni kwamba kwa nchi tajiri kilimo ni uwekezaji unatiliwa umuhimu mkubwa sana. Ndio maana huko matajiri ndio wanaolima lakini kwetu kilimo kimechukuliwa ni cha watu masikini. Na ndio maana ukiwa unalima unaonekana kuwa wewe ni mtu wa kaliba ya chini au uliyeshindwa maisha. Mfano unawezakuta watu mjini wakitoa kauli zinazoonyesha kilimo ni kama chaguo la mwisho. Mara kadhaa utasikia watu wakisema kama mjini pamekushinda rudi kijijini ukalime. Hapa wakimaanisha kilimo ni kama shughuli za ya kishamba na ndio chaguo la mwisho ukishashindwa kila kitu.

SOMA; Matumizi Mawili Ya Mbegu Za Mahindi.

Kwa bahati mbaya sio mjini tu ndiko wanakodharau kilimo hata kijijini kwenyewe wapo watu wengi wanaona kilimo ni kama adhabu fulani. Nakumbuka nikiwa kijijini kwetu baada kumaliza kidato cha sita na kupata nafasi ya kwenda kusoma kilimo Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Morogoro baadhi ya ndugu waliumia sana kusikia kwamba naenda kusomea kilimo tena chuo kikuu. Ndugu mmoja alidiriki kuniambia mwanangu naona umepoteza dira yaani unaenda kusomea kilimo chuo kikuu, sasa kweli huko kuna hela? si bora ungeenda hata upolisi ambapo unaanza kupata hela mapema na ajira ni uhakika. Yaani huoni wenzako wanasomea uhasibu kozi nyingne zenye hela. Lakini niliamini ipo siku moja watageuza mtazamo walio nao na mimi ndio nitakua chachu ya mageuzi hayo ya fikra.

SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

Hoja ninayoijenga hapa ni kwamba sisi wenyewe ndio tumekua chanzo cha kufanya vibaya kwa kilimo chetu kwa sababu ya fikra potofu tulizonazo juu ya kilimo. Tunasahau kwamba kilimo ni biashara kama zilivyo biashara nyingine. Hivi tunajifunza nini tunapoona makampuni makubwa yanawekeza kwenye kilimo? Mfano mji wa Arusha kuna Makampuni zaidi ya 20 ya wawekezaji wa nje ambao wamewekeza kwenye kilimo cha maua, mboga mboga, matunda na hata nafaka. Hivyo hivyo kwenye mikoa mingne kuna uwekezaji kutoka nje. Wakati sisi tunachukulia kilimo kama jambo la hovyo hovyo wenzetu wanaingiza teknolojia kwenye kilimo. Mfano nimewahi kufanya kwenye kampuni moja inayozalisha mbegu chotara ambayo ipo Arusha ambapo nilikua Meneja Msaidiz kwenye kitengo cha Operesheni na Uzalishaji ambapo wana mwagilia kwa kutumia mfumo wa kompyuta (Computerized Irrigation system). Huhitaji kuwepo ili mashamba yamwagiliwe hata ukiwa haupo una seti mitambo automatiki kazi inaendelea. Pia mimea inawekewa feni za kisasa ili kudhibiti hali ya hewa( joto na unyevunyevu kwenye hewa au humidity) ili kuhakikisha mbegu inakua na ubora wa hali ya juu.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Lakini swali la kujiuliza je walianzia wapi hadi wakafika hapo? Jibu ni kwamba walianzia mbali sana, kampuni yenyewe ina zaidi ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwake, na ilianzishwa kama kama kampuni ya familia huko nchini Uholanzi mnamo mwaka 1938, mwanzilishi alianza kwa kuuza mbegu za mbogamboga kwa wakulima wenzie, baadaye akaanza kidogokidogo kuzalisha mbegu leo hii ndio kampuni inayoongoza duniani kwa kuzalisha mbegu chotara za mbogamboga. Kwa sasa imesambaa zaidi ya nchi 20 duniani ikiwemo Tanzania na ni kampuni ya mabilioni ya hela. Hivi sasa kampuni inaongozwa na mjukuu yaani aliyeianzisha aliiongoza akamwachia motto wake naye akaiongoza leo hii mjukuu ndiye CEO na bado inakua kwa kasi sana. Japo mwanzilishi alianzia katika hali duni na ya chini sana lakini alikua na maono makubwa na alikua kiipenda kazi yake.

SOMA; Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

Tunachojifunza hapa ni kwamba hatuhitaji mabilioni ya hela kufika walikofika wenzetu, hayo yote kwa sasa hayatatusaidia. Ndio maana kila mwaka tunatenga mabilioni ya hela lakini kilimo chetu bado hikipigi hatua. Tunasahau kwamba hatuwezi kubadilisha nje wakati ndani bado hatujabadilika. Vijana wengi tunataka pesa za haraka haraka tukiambiwa tuwekeze kwa malengo ya kuanza kupata faida miaka 3 au 5 mbele hakuna nayetaka kusikia hiyo habari. Tunakosa uvumilivu. Angalia hata matajiri wengi wa Tanzania kilimo ndicho kiliwatoa. Baadhi ya watu ambao nimekua nikiwafuatilia ni Bilionea Eric Shigongo. Leo hii tunamwona Shigongo hapo alikofika amefanya sana kilimo, amelima sana mananasi huko pwani na ni biashara iliyokua inamlipa sana. Sasa hivi anawekeza kwenye madini na biashara nyingine kubwa lakini mweynyewe anakiri kilimo ndicho kilimtoa.

Hitimisho: Niseme tu napenda kutambua juhudi za watu ambao wameanza kuamka na kuchukulia kilimo kama uwekezaji unaolipa. Wapo watu amabo wameadhamiria kufanya kitu katika kilimo. Natamani kuona watanzania wengi tukifuata nyayo zao. Lazima tubadili fikra zetu lazima tuwe na mitazamo chanya kuhusu kilimo. Asanteni sana tukutane wiki ijayo katika makala nyingne ya kilimo.

Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana nae kwa simu 0763 071007 au 0658 587029 au email daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Jinsi ya kuchagua Kampuni ya kuwekeza katika Soko la Hisa

Unapohitaji kuingia kwenye uwekezaji katika Hisa swali la kwanza utajiuliza je ni kampuni gani inafaa kuwekeza. Swali hili ni zuri kwa mwekezaji kwa sababu anahitaji kuweka pesa yake katika sehemu salama na ambayo itafanya biashara yake izidi kukua. Kuchagua kampuni inayofanya vizuri katika soko la ni jambo gumu kwa watu wengi hasa ambao hawana ujuzi kuhusu uwekezaji katika Hisa. Leo tutaangalia mbinu ambazo zitamsaidia mtu ambaye hana ujuzi kuhusu uwekezaji ili aweze kuchagua kampuni ya kuwekeza katika soko la Hisa.

SOMA; Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Kwa kuanza kuwekeza sasa ndipo unapoanza kujifunza kuhusu uwekezaji katika Hisa. Na ukiendelea kusoma makala kama hizi utaendelea kukuza uelewa katika uwekezaji katika Hisa na kuweza kuwekeza bila wasiwasi.

Kampuni ambazo ni nzuri kwa ajili ya kuwekeza kwa mtu ambaye ana ujuzi mdogo

1. Wekeza katika Kampuni ambayo unaipenda/unaifahamu

Katika kampuni ambazo zimesajiliwa katika soko la Hisa kuna kampuni ambayo utakuwa unaipenda. Anza kuwekeza toka katika Kampuni hiyo kwa sababu unaipenda hata kama haitafanya vizuri utakuwa mvumilivu na kusubiri kwa kipindi kijacho.

2. Wekeza katika kampuni kubwa

Katika soko la Hisa kuna Kampuni kubwa na ndogo, kwa mwekezaji ambaye anafuatilia taarifa katika soko la Hisa ni rahisi kufahamu kampuni kubwa na kampuni ndogo ambazo zimesajiliwa katika soko la Hisa, Ukiwekeza katika kampuni kubwa una hatari ndogo kuweza kupoteza mtaji wako.

SOMA; Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.

3. Wekeza kwa Kampuni ambayo inauza hisa zake kwa mara ya kwanza (IPO)

Njia nzuri kwa mwekezaji ambaye anao ujuzi mdogo kuweza kuwekeza katika soko la Hisa. Ni vizuri kuanza kuwekeza katika Kampuni ambazo zinauza Hisa zake kwa mara ya kwanza katika soko. Mara nyingi bei zake huwa chini ya thamani halisi hivyo ni rahisi bei kuongezeka zikisajiliwa katika soko. Nunua hisa kwa kampuni ambazo zinakaribia kusajiliwa katika soko la Hisa. Ili kufahamu kampuni ambazo zinauza hisa zake kwa mara ya kwanza tembelea www.dse.co.tz au nitakuwa natoa taarifa kupitia blog hii ya Jiongeze ufahamu au www.wekezamtanzania.blogspot.com .

SOMA; Maswali Matatu Kwa Anayetaka Kuwa Mjasiriamali Kujiuliza Kutoka Kwa Richard Branson.

Jinsi kuchagua kampuni inayofanya vizuri

Ufanisi wa Kampuni husika

Hapa tunaangalia ufanisi wa kampuni yenyewe kutokana na taarifa zake za fedha. Kwa mwekezaji anayeanza ataangali vitu vifuatavyo katika taarifa za fedha za kampuni

· Revenue/Sales/Interest income (Ukuaji wa mauzo)

· Net Income (Faida baada ya kutoa gharama zote pamoja na kodi)

· Earnings per share (kwa kiasi gani kila hisa imepata toka kwenye faida ya kampuni)

· Share Price (Bei za hisa kwa kipindi fulani)

· Dividend (Ukuaji wa gawio)

Kwa vitu ambavyo nimevionyesha hapo juu utaangalia katika taarifa za fedha za kampuni kupitia website ya DSE na kama unapata shida unaweza kunitafuta kwa mawasiliano nitakayoweka hapo chini.

Ili uweze kufanya kwa urahisi utaandaa table kama iliyopo hapo chini ili kuweza kujua ni kampuni ipi imefanya vizuri. Ili uweze kufanya uamuzi sahihi unatakiwa kulinganisha kampuni ambazo zinafanya biashara inayofanana.

2012

2013

MAKAMPUNI

Details

Ongezeko %

Nafasi

NMB

Interest income

287,923

355,686

23.5

3

Net Income

97,401

133,906

37.5

2

Earnings per share (EPS)

195

267.81

37.3

1

Share Price

1,120

2,620

133.9

1

DCB

Interest income

18,600

24,665

32.6

2

Net Income

1,908

3,711

94.5

1

Earnings per share (EPS)

50

55

10

3

Share Price

620

490

-20.9

3

Mabadiliko ya bei kwa kampuni zilizo katika soko la Hisa

Ni vizuri ukawa na taarifa ya mabadiliko ya bei za Hisa kwa Kampuni ambazo zipo katika soko la Hisa kwa miaka miwili nyuma. Ili uweze kufahamu ongezeko la bei za Hisa katika soko. Taarifa hizi zitakuasidia kujua kama kampuni bei zake zinaongeze, zinapungua au zinashuka kwa miaka miwili. Taarifa hizi utazipata kupitia website ya DSE.

Mwandishi: Emmanuel Mahundi

Mawasiliano emmanuelmahundi@gmail.com/0714445510

Kwa kujifunza zaidi tembelea www.wekezamtanzania.blogspot.com

Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Za Watu.

Hofu ya kuongea mbele za watu ni hofu kubwa inayotawala katika maisha ya watu wengi sana duniani. Inasemekana kuwa zaidi ya robo tatu ya watu wote duniani hukabiliwa na hofu hii. Kuna watu hofu hii ni kubwa hata kuliko hofu ya kifo. Dalili za hofu hii ni kama kutetemeka, kutoka jasho mikononi na mfadhaiko. Hofu si kitu zaidi ya hali ya kiakili (state of mind) ya kuogopa kitu ambacho mara nyingi hakipo au hakiwezi kutokea. Katika maisha yetu hakuna jinsi ambayo tutaweza kukwepa kuongea mbele za watu, hivyo basi penda ama tusipende yatupasa na kutulazimu kujifunza kuongea mbele za watu. Hofu hii ina madhara makubwa hasa katika fani zetu na maisha yetu ya kila siku. Kuna njia kadhaa za kujijengea uwezo na kuondoa hofu hii, ambazo ni:

1. Kujiandaa vyema

Mojawapo ya njia ya kuepusha hofu hii ni kujiandaa vyema kwa kitu ambacho utakiwasilisha mbele ya hadhira. Kujua vizuri mada husika kutakupunguzia hofu kwa kiasi kikubwa. Pia hakikisha kwamba vifaa ambavyo utavitumia kuwasilisha mada yako mfano kompyuta, projekta n.k vinafanya kazi vyema na unajua kuvitumia. Kutokufanya kazi kwa vifaa hivi kutakufanya kuwa na mfadhaiko (panic) ambao mwishowe huleta hofu.

SOMA; Hizi ndio Hofu mbili ulizozaliwa nazo, nyingine ni uongo.

2. Fanyia mazoezi unachotaka kuwasilisha

Ili uweze kufanya vyema katika nyanja yoyote kama michezo na masomo yakubidi ufanye mazoezi ya kutosha ili uweze kumudu. Vivyo hivyo katika kuongea ama kuhutubia, andika yanayopasa kuwasilishwa na fanyia mazoezi ili uweze kujibu swali lolote ambalo litaulizwa. Ila wakati wa kuwasilisha si vyema kusoma kila kitu ulichoandika bali tumia tu kama mwongozo wako. Hii itakusaidia sana kuondoa hofu na kuweza kuimarika.

3. Ondoa hofu ya kukataliwa

Hofu ya kukataliwa inatawala vichwa vya watu wengi sana. Hii ni kwa sababu hakuna mtu anayependa kukataliwa. Kama nilivyosema mwanzo kuwa hofu si kitu zaidi ya hali ya kiakili uliyojijengea mwenyewe ambayo pia waweza kuiondoa ukitaka. Watu wamekuwa wakihofia kuhusu kuchukiwa kwa mada zao, mwonekano na vitu vinavyofanana na hivyo. Kumbuka umati uliokusanyika umekusanyika kwa ajili yako, hivyo wewe ni wa thamani mbele yao.

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

4. Lenga kutimiza ulichopanga

Inashauriwa kulenga katika yale uliyopanga. Ongea katika lugha inayoeleweka na punguza misamiati migumu ili uweze kuvutia wasikilizaji. Usiongee haraka haraka na weka msisitizo kwa kurudia mambo ya msingi.

5. Fanya mazoezi mbele ya kioo kikubwa

Wataalamu wanashauri kufanya mazoezi mbele ya kioo kikubwa ili uweze kujitazama mwonekano wako kwa ujumla na jinsi unavyowasilisha mada yako. Hii itakusaidia kuweza kujiamini kwani utachukulia kama upo mbele ya hadhira. Kwa njia hii utajigundua udhaifu na ubora wako hivyo kuurekebisha.

6. Rekodi na usikilize sauti yako

Watu wengi huchukukia sauti zao na jinsi wanavyoongea. Hivyo basi jijengee tabia ya kujirekodi na kusikiliza sauti yako ili uweze kuizoea. Pia kama una uwezo jirekodi video pale unapowasilisha mada. Itakusaidia kujua sehemu ya kurekebisha na pia jua kwamba huwezi kufanya kitu usichokipenda, hivyo zoea sauti yako na namna yako ya kuongea (voice flow).

SOMA; NENO LA LEO; Kitu Kimoja Kitakachokujengea Kujiamini Na Kujithamini.

7. Fanyia kazi upumuaji wako (breathing) na mazoezi mepesi

Ongeza uwezo wa kupumua kwa kufanya mazoezi ya viungo (physical exercises). Pumua katika hali ya taratibu pale unapowasilisha mada yako. Inashauriwa pia kupumua kwa nguvu pale unapokabiliwa na hofu, lakini si vizuri kufanya hivyo mbele za watu. Mazoezi mepesi ya viungo kabla ya kuhutubia yataongeza mzunguko wa damu na oksijeni katika ubongo wako.

8. Wasilisha mada yako mbele ya mtu mwingine

Mojawapo ya njia nzuri ya kukabiliana na hofu hii ni kuwasilisha mada yako mbele ya rafiki yako/zako, ndugu na jamaa pia. Hakikisha mtu huyo ni yule unaemuamini. Mwambie mtu huyo/watu hao udhaifu wako na uwe mkweli mara zote. Watakusikiliza, kukuuliza maswali, kukukosoa na hata kukurekebisha. Tegemea kuwa hiyo ndiyo hadhira yako na chochote watakachokirejesha ni sawa na ambavyo hadhira yako itafanya.

9. Tafuta muelekezaji wako (Mentor)

Hakuna mtu ambaye amefanikiwa sana kwa kufanya kila kitu peke yake. Ukigundua tatizo lako, mtafute mtu ambaye unajua ana uwezo huo na umwambie akuelekeze. Wakati mwingine itakulazimu kwenda darasani kujifunza kama kutakuwa na madarasa ya namna hiyo.

SOMA; SIRI YA 35 YA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kujijengea Kujiamini.

10. Wasilisha mada unayoipenda/ Penda unachokiwasilisha

Kuwasilisha unachokipenda itakufanya ukione cha muhimu na utapenda kuwashirikisha. Kitu unachokipenda utakiwasilisha kwa umakini, kwa moyo, hamasa na kwa akili yako pia. Hivyo basi utakuwa umeondokana na hofu hii kwa asilimia kubwa sana.

11. Jifunze misamiati mingi

Ili uweze kuzungumza vizuri ni lazima uijue vyema lugha husika. Kuwa na misamiati mingi ya neno moja itakusaidia kuwasilisha mada yako bila kulazimika kukariri neno kwa neno hiyvo kutotakiwa kuogopa kulisahau neno husika. Kutokuwa na misamiati kutafanya wasikilizaji kuchukulia kwamba hujui unachowasilisha mbele yao. Cha muhimu ni kuilewa mada/ hotuba yako kabla hujaiwasilisha.

12. Relax na usiogope jinsi wasikilizaji wako watakavyokuchulia

Hakikisha akili yako haijasongwa na mawazo wakati unawasilisha maada yako au unaongea mbele za watu kwani hii itakusababisha kutoongea vizuri, kusahau na hata kuchanganya mambo. Pia kuwa huru kuwasilisha unachowasilisha bila kuogopa watu kwani siku zote hutaweza kuridhisha kila mtu. Kuna ambao watafurahi, watakereka na wengine watakuwa wanawasiliana kwa simu. Usiwatilie maanani sana kwani watakufanya ushindwe kuendelea vyema.

SOMA; SIRI YA 24 YA MAFANIKIO; Fanya Licha Ya Kuwa Na Hofu.

13. Usiongee haraka haraka

Kuongea haraka haraka kutakufanya uishiwe na pumzi mapema. Hii itakufanya mwishowe ufadhaike (panic) na ushindwe kuendelea. Hii inaweza pia kuwafanya wanaokusiliza wakereke na kushindwa kuendelea kukusikiliza kwa umakini. Pia unashauriwa kukielewa unachowasilisha ili isikulazimu kusoma mada/hotuba yako neno kwa neno

14. Kuwa na maji karibu

Ni muhimu kuwa na maji safi ya kunywa ili uweze kulainisha koo pale unapohisi kukaukiwa na maji au kuhisi koo linakaba. Ni muhimu yawe kwenye chombo ambacho ni rahisi kutumia, mfano glasi. Mbali na maji, hushauriwi kutumia vinywaji vyenye sukari kwani vitakufanya kupungukiwa na maji wakati unaongea. Pia usitumie vinywaji vyenye caffeine maana vitaongeza kasi ya mapigo ya moyo na kusababisha mfadhaiko wa mwili na akili.

Asante kwa kusoma Makala hii

Makala hii imeandikwa na ; Nickson Yohanes

Mwandishi ni mjasiriamali na mhamasishaji

Unaweza kuwasiliana nae kwa;

Simu: 0712-843030/0753-843030

E-mail: nmyohanes@gmail.com

Pia unaweza kutembelea blog yake: www.lifeadventurestz.blogspot.com

Njia Mbili Za Uhakika Za Jinsi Ya Kupata Fedha.

Fedha ni chombo cha muhimu sana kwa kila mtu anayeishi chini ya jua yaani Duniani kwa ajili ya kukidhi mahitaji muhimu ya kibinadamu. Fedha ni chombo kinachotumika kuhalalisha mambo baina ya pande mbili yaani mtoaji na mpokeaji katika kulinganisha mapatano yaliyofikiwa katika hali ya kuuza au kununua.

Ni chombo ambacho kila mtu anahitaji kuwa nacho usidanganyike kwamba utapata miuzija ya kifedha ikuangukie lahasha! Pesa zinatafutwa ,zinategewa mitego watu wamekuwa hawana kitu kwa kusubiri muujiza wa kifedha uwaangukie. fedha huleta jawabu la mambo yote na fedha ni ulinzi’’

NJIA ZA KUPATA FEDHA

1. KUWA MBUNIFU

Njia moja wapo ya kupata,kuongeza fedha ni kuwa mbunifu ,buni njia mbalimbali za kukuingizia kipato yaani miradi. Kadiri unavyotega mitego ndivyo unavyopata pesa au ndivyo unavyonasa fedha zaidi.

Fedha haina mwenyewe wala upendeleo ,tabia ya fedha hufuata pale ilipotegwa jifunze kutega mitego mbalimbali ( vyanzo vya mapato) mwisho wa siku ,wiki,mwezi au mwaka utasema umepata pesa . Huwezi kufanikiwa kama wewe ni mtu wa kukaa tu ,tafuta kazi itakayokupatia kipato na tumia kipato hicho kuanzisha chanzo chako cha mapato.

Kila kitu kina gharama au bei hivyo basi lipia gharama au bei upate huduma na kumbuka kuwa hakuna kitu cha bure “There is no free lunch

Kuwa bora katika kile unachofanya utalipwa fedha ,utapata fedha kulingana na ubora wa bidhaa au huduma unayotoa.

SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.

2. KUWA MSHINDANI

Kama unafanya biashara na hujui mshindani wako hilo ni tatizo .Lazima umjuwe mshindani wako katika biashara yako au katika kile unachofanya ,mwandishi wa kitabu cha The Entrepreneur Mind ,Kevin Johnson amesema tafuta adui wako yaani mshindani wako ‘find your enemy’na akatoa mfano wa kampuni mbili jinsi ngani zina ushindani wa miongo mingi na kampuni hizo ni ni Apple chini ya mwanzilishi wake Steve Jobs na Microsoft chini ya Bill Gates au kampuni ya cocacola na pepsi hizi kampuni zote zinapigania kutafuta masoko na kila mmoja anamjuwa adui wake yaani mshindani wake kama makampuni makubwa duniani yanaushindani hata wewe unabidi umtambue mshindani wako katika biashara yako ili uweze kuwa bora zaidi.

SOMA; NAFASI MOJA YA KAZI; Changamkia haraka.

Ubora wa kitu utamvutia mteja hata kama hakuwa amekuja kwa ajili ya bidhaa pengine alikuwa anapita tu kando lakin akashawishika baada tu ya kuona huduma unayotoa au bidhaa unayouza. Mfano wa kampuni za simu hapa Tanzania kama vile Tigo,Vodacom au Airtell zina ushindani kila siku huyu katoa hiki leo mwenzake naye kesho kaja na kingine ushindani huu unawafanya waendeshe kampuni zao katika hali ya ushindani inayoleta ufanisi wa kifedha na cha kushangaza wote wanapata wateja .

Ushindi unaonekana kwa Yule atakayekuwa amevutia wateja wengi zaidi na kupata kipato kikubwa zaidi na kudumisha kiwango cha juu cha ufanisi. Ukiwa mtu wa ushindani utatumia bidii kujifunza zaidi na wala hutokubali kushindwa utafanya vitu vyako katika hali ya ubora ili upate ufanisi zaidi maana hakuna mtu anayependa vitu /bidhaa feki ,kila mtu anapenda vitu bora

SOMA; Usianze Biashara Kama Hujui Kitu Hiki Kimoja.

Mwandishi wa Makala hii ni DEOGRATIUS KESSY ambaye ni mwandishi mhamasishaji na mjasiriamali unaweza ukawasiliana naye kupitia namba ya simu ya mkononi 0717101505 au kupitia barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuwa Jasiri Na Kufanya Mambo Makubwa Zaidi Ya Unavyofikiria.

Nina imani umeshawahi kusikia au kusoma historia za watu tofauti tofauti na mara nyingine ukawaza kuwa watu hao walikua jasiri sana. Kuna watu mbalimbali waliowahi kuendesha nchi, kufanya vitu vya utofauti ambavyo kwa hali ya kawaida sio kila mtu anaweza kufanya, watu waliochukua maamuzi magumu ambayo sio rahisi kufikiria kwanini waliamua kuchukua maamuzi magumu kiasi hicho. Inawezekana wakati wanafanya maamuzi hayo hata watu wa karibu yao yaani ndugu na marafiki hawakuungana nao kwakua maamuzi hayo yalikuwa ni magumu mno, hivyo waliwakataza kufanya maamuzi hayo. Ukiwasoma au kuwasikia watu hawa unakubali kuwa watu hawa walikuwa na ujasiri mno.

Inawezekana pia kwenye familia yako kuna mtu jasiri wa namna hii katika eneo fulani la maisha,je na wewe pia ungetamani kuwa jasiri? Endelea kusoma makala hii mpaka mwisho na ufanyie kazi yale unayoyasoma kwa umakini ili uweze kuwa na ujasiri wa kufanya jambo lolote unalodhani ni zuri na litakuwezesha wewe kukamilisha ndoto za maisha yako.

SOMA; SIRI YA 14 YA MAFANIKIO; Tengeneza Ujasiri Wa Kufanikiwa.

VITU VITAKAVYOKUSAIDIA KUJENGA UJASIRI

Nimeorodhesha vitu hivi katika namba lakini haina maana kuwa kitu namba moja ndio cha muhimu zaidi kuliko namba ya mwisho. Vyote ni muhimu kulingana na nini unahitaji.

1. Weka malengo.

Nina imani sio mara ya kwanza unasoma kitu kama hiki. Mara nyingi umesoma na kusikia watu wakikuambia uweke malengo ya maisha yako. Malengo ya muda mrefu, malengo ya muda wa kati na malengo ya muda mfupi.

Kwanini kuweka malengo kunasaidia kukupa ujasiri?

Ukiorodhesha malengo yako unakuwa unafahamu ni nini unatakiwa ufanye, au njia gani uanatakiwa upite ili kufanikisha lile ulilokusudia katika maisha yako. Na katika kutimiza malengo kuna wakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu ambayo yatakuhitaji wewe kuwa na ujasiri ndani yako ili kuweza kuyafanya maamuzi hayo. Fanya maamuzi hayo na utimize lengo ulilokusudia .Kwa kufanya hivi utakuwa unajijengea ujasiri wa kufanya mambo mengine yaliyopo mbele yako hata kama ni makubwa kiasi gani.

SOMA; NENO LA LEO; Jinsi Ya Kuimarisha Ujasiri Wako.

2. F anya jambo moja baada ya jingine.

Ili uweze kuwa jasiri ni vizuri ufanye jambo moja kwa wakati. Kufanya jambo moja kwa wakati kunakupa urahisi wa kutafuta mbinu za kuweza kufanya jambo hilo. Ukiwa na mambo mengi kichwani unayohitaji kuyafanya na hauna mpangilio ufanye lipi kwanza, unaweza kufikia hatua ukachanganyikiwa na kuamua usifanye jambo lolote lile.

Unaona tu mbele yako kuna mambo mengi na wingi huo wa vitu vya kufanya unaweza kukuondolea ujasiri wa kukamilisha hata jambo moja. Ni vizuri kuandika katika karatasi unahitaji kufanya nini na uweke vitu hivyo katika vipaumbele kuwa unaanza na kipi na utafuatia kipi. Ukifanya vitu vyote kwa wakati mmoja utashindwa kukamilisha vyote, utajiona huwezi kufanya lolote na hivyo kukuondolea hata uthubutu kidogo ulipo ndani yako.

3. Pata taarifa sahihi za kitu unachotaka kukifanya.

Ni vizuri kupata taarifa sahihi za kitu unachotaka kukifanya ili upate ujasiri wa kufanya kitu hicho. Inawezekana kweli kitu unachotaka kukifanya kikawa ni kigumu, ukiwa na taarifa hizo unajiandaa tangu mwanzoni kwaajili ya kupambana na ugumu huo. Unatengeneza njia za kupana na ugumu huo. Unapata ujasiri wa kuendelea na lengo lako hata kama mambo yatakuwa magumu kwakua unafahamu kuwa ili kufanikisha lengo lako kunaugumu fulani inabidi uupitie. Hiyo inakupa ujasiri wa kupambana hadi kukamilisha kusudio lako.

Ukiwa hauna taarifa za kutosha juu ya kitu unachoenda kufanya, ukipata changamoto hata kama ndogo, au hata watu wakikukatisha tama, ni rahisi kuacha kufanya jambo ulilotaka kulifanya nakujiona huwezi kufanya jambo lolote kubwa katika maisha yako.

SOMA; UKURASA WA 60; Je Una Ujasiri Huu?

4. Maandalizi.

Ili kupata ujasiri wa kufanya jambo lolote lililopo mbele yako ni lazima kufanya maandalizi mapema.

Ukiwa na taarifa sahihi za kitu unachokwenda kukifanya ni rahisi kujua ni nini utahitaji, iwe ni vifaa au tabia fulani. Kwa mfano unahitaji kuwa mkulima mzuri wa kahawa na umepata raarifa sahihi kuhusu eneo kahawa zinapostawi, mtaji wake, soko na faida. Lakini pia umepata taarifa ni nini changamoto katika ulimaji wa kahawa. Basi maandalizi ya kutafuta eneo, mbegu, watu watakao kusaidia, jinsi ya kupambana na changamoto ulizoambiwa hufuatia. Kwa kufanya hivi unapata ujasiri wa kuendelea na kilimo chako huku ukitegemea matokeo mazuri mbeleni.

Asante sana kwa kuungangana nami katika makala hii ya leo. Tutaendelea kuangalia vitu vingine vitakavyokusaidia kujenga ujasiri wiki ijayo siku kama ya leo.

Nakutakia maisha yenye furaha.

MWANDISHI: ESTHER NGULWA

MAWASILIANO: 0767 900 110/ 0714 900 110

estherngulwa87@gmail.com

Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)

Watu wengi wanatamani kununua hisa kupitia soko la Hisa la Dar es salaam ila bado hawafahamu ni jinsi gani wanaweza kununua hisa wakiwa mahali popote pale Tanzania. Soko la Hisa limetengeneza njia rahisi ambayo kila mtu anaweza kununua hisa akiwa sehemu yoyote ile Tanzania.

Unapohitaji kununua Hisa katika soko la Hisa unatakiwa kuwa na email, akaunti ya bank na kuwa na mawasiliano brocker yoyote Yule ambaye amesajiliwa katika soko la Hisa.

SOMA; Soko la Hisa la Dar: Fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wazalendo Tanzania

Hivi ndivyo unavyoweza kununua Hisa

Baada ya kufanya maamuzi ya kampuni gani ya kununua katika soko la Hisa. Unaweza kutamfuta brocker ambaye amesajiliwa na soko la Hisa kwa ajili ya kununua hisa zako.

1. Wasiliana Brocker kwa ajili ya kununua hisa

Wasiliana na brocker yoyote ambaye amesajiliwa katika soko la hisa. Baada ya kuwasiliana na brocker ataomba email yako kwa ajili ya kukutumia fomu za kujaza. Utaprint fomu hizo ambazo zitakuwa mbili; moja kwa ajili ya taarifa zako binafsi na nyingine kwa ajili ya ununuzi wa hisa.

Hii ni orodha ya Brockers waliosajiliwa na soko la Hisa

· CORE securities Ltd; Mawasiliano Tel: +255 22 212 3103 au info@coresecurities.co.tz

· Orbit Securities Co. Ltd; Mawasiliano Tel: +255 22 211 1758 au orbit@orbit.co.tz

· Rasilimali Ltd; Mawasiliano Tel: +255 22 211 1711 au rasilimali@africaonline.co.tz

· Tanzania Securities Ltd; Tel: +255 22 211 2807 au info@tanzaniasecurities.co.tz

· Vertex International Securities Ltd; Tel: +255 22 211 6382 au vertex@vertex.co.tz

· Solomon Stockbrokers Co. Ltd; Tel: +255 22 211 2874 au solomon@simbanet.net

· E.A. Capital Ltd P.O. Box 20650, Dar es Salaam au Tel +255 779740818/ +255 784461759
EC@EACAPITAL-TZ.COM

· ZAN Securities  Ltd P.O. Box 5366, Dar es Salaam au Tel +255 22 2126415
info@zansec.com

2. Jaza fomu ulizopewa

Baada ya kuprint fomu ulizotumiwa utajaza kutokana na mahitaji ya fomu husika. Baada ya kumaliza kujaza fomu zako, utazi scan zote na kuzituma kama attachment kwenye email ya brocker na kusubiri majibu kutoka kwake.

SOMA; Msingi na ustadi wa kuwekeza kwenye Soko la Hisa

3. Utatumiwa kiasi cha kutuma na akaunti ya benki kwa ajili ya kuingiza pesa

Baada ya kutuma fomu zako kwa brocker atazipitia na kujua ni kiasi gani ulipie ili uweze kununua hisa hizo. Baada ya kupata akaunti ya benki ya utaingiza kiasi cha pesa ambacho umeambiwa kwenye akaunti ya kampuni ya brocker. Baada ya kulipia benki pesa za ununuzi wa hisa uta scan risiti ya benki.

4. Tuma risiti ya benki ambayo umescan kwenye email ya brocker

Baada ya kuscan risiti ya benki utatuma kwa brocker ili kuthibitisha kuwa umefanya malipo hayo kwenye akaunti yao na wewe ni muhusika. Baada ya kutuma atakujibu kuwa amepata na usubiri hisa zako kununuliwa.

SOMA; Hatua Muhimu Kuzifahamu Unapohitaji Kuwekeza Katika Hisa.

5. Subiri kununuliwa kwa hisa zako

Baada ya kupitia hatua zote, subiri kwa ajili ya kununuliwa kwa hisa zako. Kutoka na kupanda na kushuka kwa bei unaweza kumwambia kuwa brocker anunue hisa zako kulingana na bei ya soko hii ni kwa sababu wakati unajaza fomu ulipanga bei ya kununulia.

Kumbuka: Vitu vyote nilivyoelewa unaweza kufanya ndani ya siku moja ikiwa utawasiliana na brocker mapema na kufanya kwa uharaka. Vile vile unaweza tumia gmail akaunti kwa urahisi wa utumaji wa taarifa zako.

Mwandishi: Emmanuel Mahundi

Mawasiliano emmanuelmahundi@gmail.com/0714445510

Kwa kujifunza zaidi tembelea www.wekezamtanzania.blogspot.com