Katika Kula Ujana Usifanye Mambo Haya Matano, Utajutia Maisha Yako Yote.

Wakati wa ujana ndio wakati ambao watu wengi wanajaribu mambo mbalimbali. Sio kitu kibaya kwa sababu katika kujaribu huku mambo mbalimbali ndio unaweza kujua ni kitu gani utakomaa nacho kwenye maisha yako.
Katika kula ujana usifanye mambo haya matano, maana ukiyafanya utajutia maisha yako yote.
1. Usivute sigara.
Fanya starehe zote lakini usivute sigara. Uvutaji wa sigara una athari kubwa sana kwenye afya yako hasa utakapokuwa mtu mzima. Sigara ina kemikali zaidi ya elfu moja zinazochangia kuleta kansa. Kila unapovuta sigara moja unapunguza dakika 14 za kuishi.
2. Usiwe mlevi.
Kunywa pombe sio kitu kibaya ila kuwa mlevi ni tatizo kubwa sana kwako. Maisha yako yatakuwa magumu sana baadae kama utaendekeza ulevi. Japokuwa sio vibaya kunywa pombe ila bado ina madhara kwa afya yako.
3. Usifanye ngono zembe.
Ukiendekeza ngozo zembe unaweza kupata ugonjwa ambao hautibiki na hivyo kushindwa kufikia mafanikio unayotegemea baadae. Jilinde sana hasa kwenye ngono.
4. Usiharibu haiba na heshima yako.
Katika kula ujana usifanye jambo lolote ambalo litaharibu heshima yako. Kwa kufanya hivyo unaweza kushindwa kutumia fursa zitakazokujia baadae.
5. Usitumie madawa ya kulevya.
Fanya kila starehe lakini usijaribu kuonja madawa ya kulevya. Mara madawa haya yanapoingia kwenye mwili wako hauwezi kurudi katika hali ya kawaida. Epuka sana madawa ya kulevya, yataharibu mfumo wako wote wa mwili.
Kula ujana ila zingatia na epuka mambo hayo matano.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.

0 comments: