Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.

Mahusiano unayojenga na watu kibiashara yanaweza kuwa ya aina mbili;
1. Uhusiano ambao kila mmoja anafaidika(win - win)
2. Uhusiano ambao mmoja ananufaika zaidi ya mwingine(win - lose)
Kwa bahati mbaya sana kwenye mazingira yetu mahusiano yaliyotawala ni ya aina ya pili.
Watu wengi watakaotaka kujenga mahusiano ya kibiashara na wewe watataka kiunufaika zaidi yako.
Kuwa mjanja, angalia mbali.
Ukiona uhusiano wa aina hii kimbia, hautakufikisha mbali.

Siri Moja Kubwa Ya Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Unapokuwa mjasiriamali elimu yako ndio imeanza. Kwa kweli ili uweze kuwa juu kwenye ujasiriamali ni lazima uendelee kutafuta maarifa yatakayokufanya wewe na biashara yako kuwa bora zaidi.
Mjasiriamali anayeacha kujifunza ni mjasiriamali anayeacha kufaidika.
Wajasiriamali wanajifunza kupitia kusoma vitabu, kujifunza kuhusu watu waliofanikiwa, kusoma majarida yanayohusiana na wanachofanya, kuhudhuria semina na makongamano na njia nyingine nyingi.
Je wewe unatumia njia ipi kujifunza?

Siri Moja Kubwa Ya Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Unapokuwa mjasiriamali elimu yako ndio imeanza. Kwa kweli ili uweze kuwa juu kwenye ujasiriamali ni lazima uendelee kutafuta maarifa yatakayokufanya wewe na biashara yako kuwa bora zaidi.
Mjasiriamali anayeacha kujifunza ni mjasiriamali anayeacha kufaidika.
Wajasiriamali wanajifunza kupitia kusoma vitabu, kujifunza kuhusu watu waliofanikiwa, kusoma majarida yanayohusiana na wanachofanya, kuhudhuria semina na makongamano na njia nyingine nyingi.
Je wewe unatumia njia ipi kujifunza?

Unapokuwa Tayari Kuingia Kwenye Ujasiriamali Fanya Vitu Hivi Vitano.

Kuna watu ambao wangetamani kuwa wajasiriamali. Wanapoona mafanikio ya wajasiriamali wakubwa wanatamani sana kama wangekuwa wao.

Hijalishi unatamani kiasi gani kuwa mjasiriamali, tamaa yako tu haitakuwezesha kufikia mafanikio katika ujasiriamali. Ni lazima uwe na misingi ambayo utaisimamia ndio uweze kuona mafanikio makubw akupitia ujasiriamali.

Kwanza ni lazima uondoke kwenye kutamani na uingie kufanya na ukishaingia kufanya uwe tayari kukabiliana na lolote litakalojitokeza mbele yako.

SOMA; Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

Leo hapa UTAJIONGEZA na vitu vitano muhimu vya kufanya unapokuwa tayari kuingia kwenye ujasiriamali.

1. Usianze tena kujishuku.

Ukishaamua kwamba wewe umechagua njia ya ujasiriamali, sahau kuhusu kujishuku na kuanza kuwa na wasi wasi kama kweli utaweza. Kikubwa ni nia yako ya kufikia mafanikio kupitia ujasiriamali. Matatizo, changamoto na vikwazo kila mtu anavipitia. Hivyo acha kuwa na wasi wasi kama utaweza na jitoe kwa asilimia 100 kufanya kile ambacho umeamua kufanya.

Kwenye ujasiriamali hakuna kujaribu, kuna kufanya. Fanya sasa na ondoa wasi wasi na hofu.

SOMA; SIRI YA 20 YA MAFANIKIO; Iendee Dhahabu...

2. Kuwa na mshauri.

Kuna ushauri wa bure ambao unapatikana kila mahali kwenye maisha yetu ya kitanzania. Ushauri kama, biashara fulani inalipa kweli yani, ukianza kuifanya tu, utapata mafanikio makubwa. Ukimuangalia anayekupa ushauri huo nae amesikia kwamba biashara hiyo inalipa.

Sasa hawa sio washauri ambao nakuambia uwe nao. Nakuambia uwe na mshauri ambaye anaelewa ni nini hasa anachokuambia. Mtu ambaye amekuwa kwenye safari ya ujasiriamali na anaujua ugumu wa safari hiyo. Mtu ambaye hatakuwa mnafiki kwako kukuambia mambo ili tu kukupa moyo na kukufurahisha, bali atakuambia ukweli, na ukweli huu utakufanya uweze kutumia mazingira yako vizuri kufikia mafanikio.

SOMA; UKURASA WA 43; Ushauri Wa Bure Una Gharama Kubwa.

3. Jitengenezee utaratibu wako wa kila siku, ambao utauheshimu.

Tofauti ya ujasiriamali na kazi zingine ni kwamba kwenye ujasiriamali wewe unajiongoza mwenyewe. Hakuna atakayekugombeza au kukutishia kukufukuza kazi kama utakuwa mzembe. Na hii ni hatari kubwa sana kwa sababu kama huwezi kujiongoza mwenyewe utashindwa kwenye ujasiriamali.

Njia rahisi ya kuweza kuanza kujiongoza mwenyewe ni kuwa na utaratibu wako wa kila siku ambao utaufuata na kuuheshimu. Ipangilie siku yako kabla hujaianza na weka vipaumbele kwenye malengo na mipango yako kwenye maisha na kupitia ujasiriamali unaofanya.

4. Acha kukaa na watu ambao wanakurusisha nyuma.

Tumeshajadili hili mara nyingi sana kwamba wewe ni wastani wa watu watano ambao wanakuzunguka. Hivyo kama umezungukwa na watu watano ambao hawana malengo yoyote kwenye maisha yako, ni vigumu sana wewe kuweka malengo na kuyasimamia. Hivyo wewe unapoamua kuingia kwenye ujasiriamali usikubali kukaa tena na watu ambao mawazo yao yanakurudisha wewe nyuma. Wewe unajua kwamba kwenye ujasiriamali, hasa wakati wa mwanzo unaweza kujikuta unafanya kazi mpaka masaa 16 au 20 kwa siku, lakini rafiki zako wanataka kila siku jioni mkutane mkipata moja moto na moja baridi, hii hutaiweza wewe kama mjasiriamali, niamini.

SOMA; UKURASA WA 11; Watu Hawa Wanakurudisha Nyuma.

5. Kuza mtandao wako.

Tumesema sana hili pia, haijalishi unajua nini bali unamjua nani. Unapoamua kuingia kwenye ujasiriamali hakikisha kila mtu anayehusika na aina ya ujasiriamali unaofanya anajua kuhusu wewe na kile unachofanya. Angalia watu muhimu ambao unahitaji ushirikiano wao, watafute, angalia ni jinsi gani unaweza kuwasaidia ili nao wakusaidie, kukua zaidi.

Kama unafikiri kwenye ujasiriamali utashinda kwa jeshi la mtu mmoja umepotea njia, ongea na watu wengi uwezavyo, wajue unachofanya na wao watakuunganisha na watu wengi zaidi.

Haya ndio mambo matano muhimu sana ya wewe kufanya pale unapoamua kwamba ujasiriamali ndio maisha yako. Na miaka sio mingi kila mtu atahitaji kuwa mjasiriamali, hivyo ni vyema kama utaanz akujiandaa mapema.

Kwa ushauri wowote kuhusu biashara na ujasiriamali tafadhali tuma email kwenda ushauri@kisimachamaarifa.co.tz

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio kupitia ujasiriamali.

TUPO PAMOJA.

Makirita AMANI 

Maswali Matatu Muhimu Ya Kujiuliza Kwenye Wazo Lako La Biashara.

Hakuna changamoto kubwa kama kupata wazo zuri la biashara na ambalo litakuwezesha kupata mafanikio na mafanikio makubwa.

Japo nimeshaandika mara nyingi sana jinsi ya kutengeneza wazo zuri la biashara, bado maswali mengo ninayopata kutoka kwa wasomaji ni wazo gani la biashara ni zuri na lenye faida.

Leo tutajifunza maswali matatu muhimu ya kujiuliza kwenye wazo lolote la biashara ili kujua kama litakuletea faida.

SOMA; Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.

Muhimu ni kujua kwamba kila wazo la biashara ni zuri na linaweza kuleta faida. Changamoto ni jinsi gani unaweza kulitekeleza wazo hilo ili liweze kukuletea faida hiyo. Kupitia maswali haya matatu utaweza kuliweka wazo lako vizuri na hatimaye kuweza kutengeneza biashara kubw akupitia wazo hilo.

1. Je nawezaje kulipwa kwa wazo hili?

Jiulize swali hili muhimu sana kwamba unawezaje kulipwa kwa wazo ulilonalo. Unawezaje kulipwa kwa kile unachopenda kufanya?

Tuseme labda unapenda kuchora, je unawezaje kulipwa kwa kuchora? Hapa unaweza kupata majibu kama kuchora kazi za kisanaa, kuchora ramani za majengo, kuanzisha jarida la vibonzo na mengine mengi.

2. Je nitalipwa kiasi gani kutokana na wazo hili?

Kupata uhakika wa kulipwa kutokana na wazo bado hakutoshi wewe kujihakikishia biashara. Swali jingine muhimu la kujiuliza ni nitalipwa kiasi gani kwa wazo hili? Ni lazima ujue kiwango ambacho unaweza kulipwa kutokana na wazo lako. Na pia uone kiwango hiko unacholipwa kitakuwezesha kuendelea na biashara hiyo.

Kwenye mfano wetu wa kuchora hapo juu, huendakuchora vibonzo kunalipa, ila kuchora ramani za majengo kunaweza kulipa zaidi.

SOMA; Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.

3. Je kuna njia ambayo naweza kulipwa zaidi ya mara moja?

Wazo zuri la biashara ni lile ambalo unaweza kulipwa zaidi ya mara moja. Kama una biashara ambayo mtu akishanunua ndio imetoka na hawezi kurudi kwako tena ni vigumu sana kutengeneza biashara endelevu.

Ila kama utakuwa na njia ya kuweza kulipwa zaidi ya mara moja, au mteja kuja tena na tena utaweza kujenga biashara nzuri na yenye mafanikio makubwa.

Jiulize na kujijibu maswali hayo matatu na utaweza kulijenga wazo lako la biashara na likakuletea mafanikio makubwa sana.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Usianze Biashara Kama Hujui Kitu Hiki Kimoja.

Weka Pamoja Vitu Hivi Vitatu Na Tayari Wewe Ni Mjasiriamali Mwenye Mafanikio Makubwa.

Kama tayari una kundi la watu wanaokufuata, na wanaosikiliza unachosema, ila huna cha kuwauzia, huna biashara.

Kama una bidhaa au huduma unayouza ila hakuna mtu yuko tayari kununua huna biashara.

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Kama una bidhaa au huduma unayouza na watu wapo tayari kununua ila huna njia rahisi ya wateja kuweza kukulipa huna biashara.

Kama ukiwa na bidhaa au huduma unayouza, ukawa na watu ambao wako tayari kuinunua, na ukawa na mfumo mzuri wa watu kukulipa ili kuipata, hongera una biashara kubwa ambayo itakuletea mafanikio.

Kwa kuweza kufikia vigezo hivyo vitatu na kuviweka pamoja wewe ni mjasiriamali mwenye mafanikio.

Kila la kheri.

SOMA; Huyu Ni Mjasiriamali Mwenye Hamasa Kubwa sana. Unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwake.

Huyu Ni Mjasiriamali Mwenye Hamasa Kubwa sana. Unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwake.

Moja ya vitu ambavyo vitakuwezesha wewe kufanikiwa kwenye ujasiriamali ni kupend akile unachokifanya. Kama kweli unapenda unachofanya, utakuwa na hamasa kubwa sana ya kukifanya.

Hamasa hii ndio inakuwezesha kuvuka vikwazo, kuwa mbunifu na kuweza kufikia mafanikio makubwa sana.

Kuna mjasiriamali mmoja mkubwa sana duniani ambaye ana hamasa kubwa sana ambayo huwa inawashangaza wengi. Pamoja na mafanikio makubwa aliyonayo, bado haoni shida kufanya mambo madogo madogo ambayo yanamfanya azidi kufikia mafanikio makubwa.

Mjasiriamali ninayemzungumzia ni Richard Branson. Huyu ni raia wa uingereza na anamiliki kampuni kubwa ya Virgin Group ambayo ina kampuni zaidi ya 400 chini yake. Huyu ni mmoja wa watu matajiri sana duniani, akikadiriwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 4.9.

branson

Leo hapa utajiongeza na baadhi ya mambo anayofanya Branson ambayo yatakufanya na wewe uwe na hamasa zaidi kwenye ujasiriamali unaofanya.

Katika ufunguzi wa hotel mpya chini ya kampuni yake ya Virgin, kulikuwa na tetesi kwamba Richard alikuwa anawatembelea wateja wake usiku na kuwafurahisha zaidi.

branson 2

Tetesi hizo zilithibitishwa na Branson mwenyewe pale alipowatembelea wateja chumbani kwao na kuwasomea hadithi wakati wa kulala. Kama ambavyo wazazi huwa wanawasomea watoto wao hadithi.

branson 3

Unaweza kuona ni kitu kidogo ila kinajenga picha kubwa sana kwake na kwa biashara zake. Hii inaonesha jinsi anavyojali biashara zake na anavyotoa huduma bora kwa wateja.

Angalia video ya tukio zima hapo chini;

Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Hakuna maisha mazuri kama ya ujasiriamali, kama unajielewa na unaweza kujisimamia, ujasiriamali ni maisha yenye uhuru mkubwa sana.

Unapokuwa na wazo la ujasiriamali mwanzoni ni kama moto unawaka ndani yako. Unakuwa na hamasa kubwa sana ya kutekeleza wazo lako na unakuwa na mapenzi makubwa kwa unachofanya.

Ila kwa bahati mbaya sana unapoingia kwenye ujasiriamali na kuanza kufanya biashara zako za kila siku ni rahisi moto huu kuzimika na kujikuta unakosa hamasa ya kuendelea. Na pale unapokutana na changamoto, ambazo ni lazima ukutane nazo ni rahisi kukata tamaa.

Leo UTAJIONGEZA na njia tatu za kufanya moto wa ujasiriamali uendelee kuwaka kwenye nafsi yako. Hii itakufanya uendelee kuwa na hamasa kubwa na kupenda kile unachofanya. Hata utakapokutana na changamoto itakuwa rahisi sana kwako kuzitatua na kuendelea ili kufikia mafanikio makubwa zaidi.

SOMA; UKURASA WA 35; Usijaribu Kumfurahisha Kila Mtu.

1. Washa moto wa ujasiriamali kila siku.

Kila siku kabla ya kuanza siku yako, washa moto wa ujasiriamali kwenye nafsi yako. Unawashaje moto huu? Ni rahisi, kila siku jikumbushe ni nini ambacho kilikufanya uingie kwenye ujasiriamali unaofanya. Kama sababu yako ni kubwa, kwa kujikumbusha kila siku na kujiambia sababu hiyo itakuwa hamasa kubwa ya wewe kufanya mambo makubwa kwa siku hiyo.

Kila siku jikumbushe kilichokufanya uingie kwenye ujasiriamali.

2. Penda matatizo/changamoto.

Kwa sehemu kubwa kilichokufanya uingie kwenye ujasiriamali ni kutatua matatizo ya watu, au kuwapatia njia bora zaidi. Katika mchakato huu na wewe pia utaingia kwenye matatizo au changamoto mbalimbali.

Kama utaziogopa changamoto hizi, itakuwa rahisi kwa wewe kukosa hamasa ya kuendelea. Ila kama utayapenda matatizo na changamoto unazokutana nazo, utazipatia ufumbuzi na utaweza kuendelea na safari.

SOMA; NENO LA LEO; Viti Viwili Ambavyo Kila Mtu Anataka Kwenye Maisha.

3. Usikubali majukumu ya kila siku kukupoteza lengo lako.

Wewe kama mjasiriamali ulianza na wazo moja, lakini kwenye kutekeleza wazo hilo umeingia kwenye biashara ambayo ina vipengele vingi sana. Kwa kujaribu kufanya kila eneo la biashara yako kunaweza kukuchosha na ukasahau lengo lako kubwa lilikuwa nini.

Chagua mambo machache ambayo unayapenda kweli kuyafanya na yafanye vizuri sana, hii itakupatia hamasa kubwa ya kuendelea kufanya zaidi. Mambo mengine yote tafuta watu wanaoweza kufanya na waajiri wafanye mambo hayo.

Kadiri unavyofanya vitu vichache vinavyokuhamasisha, ndivyo unavyopata majibu mazuri na ndivyo moto wa ujasiriamali utaendelea kuwaka ndani yako.

SOMA; #HADITHI_FUNZO; Mbinu Rahisi Iliyomwezesha Jenerali Kushinda Vita Ngumu.

Hatua TANO Za Kuongeza Uzalishaji Wako Ili Kufikia Mafanikio.

Kuna usemi mmoja maarufu sana unaosema “ukiendelea kufanya unachofanya sasa, utaendelea kupata matokeo unayopata sasa”. Kwa lugha nyingine kama unataka kubadili matokeo yako, ni lazima uanze kwa kubadili kile unachofanya.

Ili uweze kufikia mafanikio zaidi ya uliyonayo sasa, kwa sababu mpaka hapo ulipo tayari una mafanikio, unahitaji kubadili njia unazotumia sasa. Na kitu cha kwanza kabisa kubadili ni uzalishaji wako.

Uzalishaji tunaozungumzia hapa ni ile kazi au thamani unayotoa kwa wengine kwa muda unaofanya kazi. Hivyo kama utazalisha thamani zaidi kwa muda mfupi maana yake una uzalishaji mkubwa. Na hii ni njia nzuri ya kufikia mafanikio kwenye chochote unafanya, iwe ni kazi au biashara.

Kiuchumi, utajiri au thamani ya kampuni, mtu binafsi na hata jamii kwa ujumla unapimwa kwa ongezeko la uzalishaji.

SOMA; Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Leo UTAJIONGEZA na hatua tano unazoweza kutumia na ukaongeza uzalishaji wako na hatimaye kufikia mafanikio zaidi.

Hatua ya kwanza na rahisi kabisa ya kuongeza uzalishaji wako ni kuwa bora kwenye majukumu yako. Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kuendelea kujifunza zaidi. Kama unafanya biashara, ijue vizuri biashara yako na ongeza juhudi. Kama umeajiriwa, unajua majukumu yako kikazi, yatekeleze vizuri.

Hatua ya pili ni kutafuta mtu ambae anaweza kufanya hiko unachofanya na kwa bei rahisi kisha unampa afanye. Kama ni mfanyabiashara maana yake unatafuta watu wa kukusaidia. Kama ni ajira unafanya kazi na watu wengine ambao wanakusaidia. Ukweli ni kwamba kazi inayofanyika kwa timu inafanyika kwa uzalishaji mkubwa.

SOMA; Tabia Mbaya KUMI(10) Zinazopunguza Ufanisi Wako.

Hatua ya tatu ya kuongeza uzalishaji ni kutumia teknolojia iliyopo. Hapa unatafuta njia ambayo teknolojia inaweza kurahisisha kazi unazofanya. Kwa mfano badala ya kuandika kila barua kwa mkono, inaweza kuandikwa moja na zikatolewa kopi na mashine. Kila kazi inaweza kusaidiwa na teknolojia.

Hatua ya nne ni kuvumbua teknolojia mpya inayoweza kurahisisha kazi zako. Na ukifikia hatua hii unakuwa umetatua tatizo la wengi. Inawezekana kwa kila kazi unayofanya kuvumbua njia rahisi ya kiteknolojia ya kuirahisisha.

Hatua ya tano na ya mwisho ya kuongeza uzalishaji wako ni kujua vitu vinavyoleta uzalishaji mkubwa kwako na kufanya hivyo tu. vingine vyote unaacha kuvifanya kwa sababu vinakupotezea muda. Kwa mfano asilimia 80 ya mafanikio yako inatokana na asilimia 20 ya kazi unazofanya. Je ni kazi zipi hizo zinakuletea faida kubwa? Zijue kazi hizi na zifanye kwa ufanisi mkubwa na utaongeza uzalishaji wako.

SOMA; SIRI YA 4 YA MAFANIKIO; Itumie Sheria Ya Wastani Kukuletea Mafanikio.

Mwisho wa siku kinachoongeza uzalishaji ni pale unapojua kile chenye faida kwako na kukifanya. Hii ndio inayoleta faida kwenye makampuni, biashara na hata kazi. Wale wanaojaribu kufanya kila kitu huishia kuwa na uzalishaji mdogo. Wale wanaochagua vichache na kuvifanya vizuri huwa na uzalishaji mkubwa.

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Sifa TATU Unazohitaji Ili Kufanikiwa Kwenye Ujasiriamali.

Mafanikio kwenye ujasiriamali yanachangiwa na vitu vingi sana. Kupitia blog hii JIONGEZE UFAHAMU tumeshajifunza vitu vingi sana vinavyokuwezesha wewe mjasiriamali kufikia mafanikio makubwa.

Vitu kama kuweka malengo na mipango, kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuwa mwaminifu, kutokata tamaa na vingine vingi ni muhimu sana kw akila mjasiriamali ili aweze kufanikiwa.

Leo UTAJIONGEZA na sifa tatu muhimu ambazo zitakuwezesha kufikia mafanikio kupitia ujasiriamali.

SIFA YA KWANZA; Kuwa Mtu Wa Watu.

Kuwa mjasiriamali maana yake wewe upo kwenye biashara ya watu. Mafanikio yako yote kwenye ujasiriamali yatatokana na watu wanaokuzunguka. Watu hao ni wateja wako, wafanyakazi wako, wawekezaji, washirika na hata watu wengine wa karibu.

Jinsi unavyoweza kwenda vizuri na watu wengi ndivyo utakavyoweza kutengeneza mafanikio makubwa.

SOMA; Hatua Tatu Za Kujua Kama Wazo Lako La Biashara Zuri.

SIFA YA PILI; Kuwa na Nidhamu.

Nidhamu ndio kila kitu ndugu yangu. Unapokuwa mjasiriamali hakuna wa kukusimamia utekeleze majukumu yako. Kama utakuwa mtu wa kujiendekeza utajikuta unabaki nyuma kila siku. Ni lazima uwe na nidhamu ambayo itakufanya uweze kufuata malengo na mipango yako hata kama mazingira ni magumu kiasi gani.

SOMA; Tabia Mbaya KUMI(10) Zinazopunguza Ufanisi Wako.

SIFA YA TATU; Penda Unachofanya.

Safari ya ujasiriamali inaweza kuwa ndio safari ngumu kuliko safari zote duniani. Kama ulikuwa hujui hilo jua leo. Na kinachofanya iwe ngumu ni ukweli kwamba utashindwa. Na utashindwa mara nyingi kiasi kwamba kama haupendi kile unachofanya kwa roho moja utaishia kukata tamaa.

Penda sana kile unachofanya, penda kujifunza zaidi na penda kuwasaidia wengine kupitia unachofanya na mafanikio hayatakuwa na ujanja wa kukukimbia.

Hizo ndio sifa tatu muhimu za kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa kama mjasiriamali. Uzuri ni kwamba tabia hizi unawez akujitengenezea na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika mafanikio yako kwenye ujasiriamali.

SOMA; SIRI 50 ZA MAFANIKIO.