Hatua Tatu Za Kujua Kama Wazo Lako La Biashara Zuri.

Linapokuja swala la kufanya biashara watu wengi hupenda kutafuta ji wazo gani la biashara ni bora na linaweza kuwapatia faida.
Ukweli ni kwamba wazo moja la biashara haliwezi kuwa bora kwa watu wote. Wazo linaweza kuwa bora kwangu ila kwako likawa sio zuri au lisiweze kukuletea mafanikio.
Wazo bora la biashara linategemea na mtu anayetaka kufanya biashara yako.
Watanzania tumekuwa hatupendi kuumiza akili kutengeneza mawazo yetu ya biashara na hivyo kukimbilia kuiga, kitu ambacho kinatuumiza sana baadae.
Sasa leo hapa utajiongeza na hatua tatu za kutengeneza wazo lako la biashara ambalo litakuletea faida kubwa.
Wazo bora la biashara lina sifa hizi tatu;
1. Kitu unachopenda.
Hatua ya kwanza kabisa ya wazo bora la biashara ni kitu ambacho unapenda kufanya. Kama unapenda kitu unakuwa na shauku nacho na kupenda kukifuatilia zaidi.
2. Kitu ambacho upo tayari kukifanya.
Kupenda tu kitu hakutoshi, je upo tayari kukifanya? Je upo tayari kufanya kazi na kumwagika jasho? Je upo tayari kuvumilia hata pale mambo yatapokuwa magumu?
3. Kuleta thamani kwa wengine.
Sifa ya tatu ya wazo zuri la biashara ni kuwa thamani kwa wengine. Je watu wapo tayari kulipia bidhaa au huduma itakayotokana na wazo lako la biashara? Kama haliwezi kutengeneza thamani huna biashara.
Tumia njia hizi tatu kutengeneza wazo lako la biashara ambalo litakufikisha kwenye mafanikio.
Usiige tena, tumia akili yako, angalia mazingira yanayokuzunguka.

0 comments: