Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 2

Habari ndugu msomaji. Ni imani yangu kuwa u mzima na unafuatilia mwendelezo wa makala hii. Wiki iliyopita tuliangalia siri mojawapo ya kuondokana na msongo wa mawazo wa kukosa muda ambayo ni kuandika ratiba ya kazi zako. Ni imani yangu kuwa ulipanga ratiba kwa wiki iliyopita na unaweza kutushirikisha matokeo ya upangaji wa ratiba yalikusaidia kiasi gani kwa kuweka maoni hapo chini. Kama hukusoma makala ya wiki iliyopita isome hapa; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi.

Inawezekana mara nyingine ulisahau kama uliweka ratiba na kujikuta ukifanya vitu ambavyo si muhimu na viko nje ya ratiba yako. Usikate tama na kuamua kuacha kabisa kuandika ratiba. Endelea kuandika ratiba na kuifuatilia baada ya muda utazoea na kujikuta kila mara unaandika na kukamilisha ratiba yako uliyojiwekea.

Kama ulifanikiwa kuandika ratiba na kuifuata napenda kukupongeza sana. Endelea kufanya hivyo inakupa urahisi wa kukamilisha mipango yako bila ya kuzongwa na mawazo na kuchanganyikiwa. Tuendelee na siri nyingine.

2. Amka mapema asubuhi.

Hakikisha kuwa unaamka asubuhi sana, saa kumi na moja ni muda mzuri. Muda huu ni wa utulivu, akili bado inanguvu na hakunamtu anaweza kukusumbua kwa wakati huu. Angalia ratiba yako kwa siku husika na endelea na kukamilisha majukumu uliyojiwekea kwa siku hiyo. Kama una kazi za kusoma au kuandika basi huu ni muda mzuri sana wa kufanya hivyo kwani akili inakuwa na nguvu.

Ukiamka mapema siku nzima inakuwa ni ya kuchangamsha tofauti na mtu ambaye ataamua kuamka saa mbili asubuhi. Kuchelewa kuamka hukufanya ujisikie mchovu na kushindwa kufanya shughuli kwa ufanisi.

Wengi wetu huamka kwa mawazo tu na sio kimwili. Yaani unatega saa ikuamshe saa kumi na moja lakini kengele ikilia unaizima na kuanza kufikiri mawazo ya kuamka na fikra hizo zinakufanya ukae kitandani mpaka saa mbili asubuhi. Usifanye hivyo, kengele ikikuamsha amka kwakua unafanya hivyo kwa faida yako na ni kwaajili ya kupunguza wingi wa majukumu uliyonayo. Fanya zoezi la kuamka mapema asubuhi wiki hii na uzingatie ratiba yako ya siku.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuishi Maisha Yako Kwa Ukamilifu.

3. Lala masaa ya kutosha.

Kuna tofauti ya idadi ya masaa ya kulala kutokana na umri na aina mbalimbali ya watu. Watoto, vijana na wazee wanatofautiana katika idadi ya masaa wanayotakiwa walale. Kulingana na maelekezo ya wataalamubinadamu mwenye umri wa kati yaani ambaye si mtoto wala si mzee anashauriwa alale muda wa masaa saba hadi nane kwa usiku mmoja. Kupumzika huku ni salama kiafya kulingana na maelezo ya wataalamu. Si vizuri mtu kulala masaa chini ya sita, ingawa hali hii inatofautiana kati ya mtu na mtu.

clip_image002Kama utalala masaa saba na ukasinzia sana mchana basi inamaanisha hukupumzika vizuri hivyo jaribu kuongeza nusu saa. Na inawezekana pia baada ya masaa sita na nusu kuisha usingizi unakuishia. Huwezi kujilazimisha kuendelea kulala kwasababu inatakiwa ulale masaa saba. Amka na uendelee na ratiba zako.

Mapumziko ya kutosha ni mazuri kiafya pia huhuisha akili na mwili na kuvipa nguvu ya kufanya kazi tena.

SOMA; BIASHARA LEO; Hawa Ndio Wateja Rahisi Kuwapata Kwenye Biashara Yako.

Asante kwa kuwa nami naomba tukutane tena wiki ijayo. Endelea kufanyia mazoezi vitu hivi vitatu tulivyojadili na utupe maoni kama kunamabadiliko uliyoyapata.

Kama unaswali, maoni au ushauri usisite kuwasiliana nami.

MWANDISHI: ESTHER NGULWA

MAWASILIANO: 0767 900 110 / 0714 900 110

estherngulwa87@gmail.com

Makala imeangaliwa muundo na lugha fasaha na Rumishael Peter ambaye ni Mhariri wa vitabu/makala za Kiswahili na Mjasiriamali Email: rumishaelnjau@gmail.com simu 0713 683422.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunza mambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

0 comments: