Tabia KUMI Za Watu Waliofanikiwa Sana(PICHA)
Tabia ndio msingi wa mafanikio. Wote tunajua kwamba tofauti kubwa kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa inaanzia kwenye tabia. Ukiwalinganisha watu hawa wawili utaona utofauti mkubwa sana kwenye tabia zao.
Leo hapa UTAJIONGEZA na tabia kumi ambazo kama na wewe utaweza kujijengea utajiweka kwenye nafasi kubwa ya kuendelea kufanikiwa, KWA SABABU TAYARI UMESHAFANIKIWA.
Hapa nitaweka picha ambayo nimeipata kwenye mtandao wa ADDICTED TO SUCCESS, pitia tabia hizi kumi na zifanyie kazi.
Kwa kifupi tabia hizi ni;
1. Kujifunza kila siku.
2. Kujijengea picha kwenye akili.
3. Weka vipaumbele.
4. Matumizi mazuri ya fedha.
5. Kuamka mapema.
6. Kuweka malengo.
7. Kula vizuri, kufanya mazoezi.
8. Kujiimarisha kiakili.
9. Kutengeneza mtandao.
10. Kujenga tabia nzuri.
Jijengee tabia hizi kumi na mafanikio hayataondoka kwako kamwe.
1/30/2015 01:19:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Tabia KUMI Za Watu Waliofanikiwa Sana(PICHA)
Tabia ndio msingi wa mafanikio. Wote tunajua kwamba tofauti kubwa kati ya watu waliofanikiwa na wale ambao hawajafanikiwa inaanzia kwenye tabia. Ukiwalinganisha watu hawa wawili utaona utofauti mkubwa sana kwenye tabia zao.
Leo hapa UTAJIONGEZA na tabia kumi ambazo kama na wewe utaweza kujijengea utajiweka kwenye nafasi kubwa ya kuendelea kufanikiwa, KWA SABABU TAYARI UMESHAFANIKIWA.
Hapa nitaweka picha ambayo nimeipata kwenye mtandao wa ADDICTED TO SUCCESS, pitia tabia hizi kumi na zifanyie kazi.
Kwa kifupi tabia hizi ni;
1. Kujifunza kila siku.
2. Kujijengea picha kwenye akili.
3. Weka vipaumbele.
4. Matumizi mazuri ya fedha.
5. Kuamka mapema.
6. Kuweka malengo.
7. Kula vizuri, kufanya mazoezi.
8. Kujiimarisha kiakili.
9. Kutengeneza mtandao.
10. Kujenga tabia nzuri.
Jijengee tabia hizi kumi na mafanikio hayataondoka kwako kamwe.
1/30/2015 12:51:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.
Mpaka sasa unajua kwamba tofauti kubwa ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa inaanzia kwenye fikra zao. Kama bado hujajua ndio nakuwambia leo na nitakuambia mawazo ya aina tano ambayo yanaua kabisa mafanikio yako.
Tunajua kwamba kuwa na mawazo chanya ni kitu muhimu sana ili kufikia mafanikio. Hivyo kuepuka mawazo hasi ni hatua ya kwanza ya kufikia mafanikio. Ila mawazo ya aina tano tutakayokwenda kujifunz ahapa leo yanaweza yasionekane kama ni hasi na ndio maana watu wengi wanashindwa kuyatambua mapema.
SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya
Kwa kujua mawazo haya na jinsi ya kuyaepuka itakuwa msaada sana kwako kufikia mafanikio.
1. Mimi sio mtaalamu.
Mara nyingi sana umekuwa ukitumia sababu hii kwamba unashindwa kufanya zaidi kwenye kazi yako au biashara yako kwa sababu huna utaalamu mkubwa. Sawa huenda ni kweli huna utaalamu mkubwa ila je unachukua hatua gani?
Kumbuka hakuna mtu aliyezaliwa na utaalamu wowote, vitu vyote tunajifunza hapa duniani. Hivyo kama kuna utaalamu ambao unajua utakusaidia sana kwenye kazi au biashara zako anza kujifunza. Kwa bahati nzuri tunaishi kwenye dunia ambayo kujifunza sio lazima uende darasani, popote ulipo unaweza kujifunz ana kutendea kazi yale uliyojifunza na baada ya muda ukawa mtaalamu.
SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.
2. Hicho kimeshafanyika.
Kuna wakati ambapo unapata wazo zuri la kufanya kitu ambacho kitakufaidisha sana kwenye kazi au biashara. Ila unapofuatilia kwa makini unagundua kwamba kuna watu wengine tayari wanafanya. Kwa kuwa na mawazo ya aina hii unajiondoa mwenyewe kwenye safari ya mafanikio.
Hata kama kitu kimefanyika na watu wengi kiasi gani, kama ndio kitakachokusaidia kifanye. Ila wewe kifanye kwa utofauti na upekee ili uweze kunufaika zaidi. Kama kuna biashara unayotaka kufanya na ukakuta wengine wanaifanya unatakiwa kufurahi kwa sababu tayari una uhakika kwamba soko lipo, hivyo kazi yako ni kujua jinsi gani utavutia na kuwabakiza wateja kwenye biashara yako.
3. Sina ‘connection’
Ni kweli kabisa na pia nilishaandika kwamba haijalishi unajua nini bali unamjua nani, mafanikio yako yatategemea sana na watu unaojuana nao na walioko kwenye mtandao wako. Hivyo ni rahisi sana kuamini kwamba kwa kuwa hujuani na watu waliofanikiwa basi huwezi kufanikiwa.
Swali ni kwamba unataka watu waliofanikiwa waje wakutafute wewe? Wakutafute kwa sababu gani? Wewe ndio unatakiw akuanzisha kitu hiki. Angalia ni watu gani ambao unahitaji kuwa nao kwenye mtandao wako, kisha angalia ni kitu gani unaweza kuwasaidia. Omba nafasi ya kuwasaidia kitu hiko na utakuwa umeanzisha connection muhimu sana kwako. Ndio watu wenye mafanikio ni vigumu sana kuwapata ila kama kweli unataka kuwapata utafanikiwa kuwapata.
4. Sina hela.
Angalau hii ni sababu ambayo karibu kila mtu anaitumia wakati mmoja au mwingine. Kwa nini huanzi biashara, sina mtaji. Kwa nini biashara yako haikui, sina fedha. Kwa nini hujafikia mafanikio, sina fedha. Sawa huna fedha, swali ni je unataka nani aje akuletee fedha hapo ulipo? Hakuna, kama unasubiri unapoteza muda wako bure. Anzia hapo ulipo, anza na ulichonacho. Kama unataka kuanza biashara anza na kiasi kidogo unachoweza kuanzia, endelea kukua na pale unapokuwa makini utaanza kuona fursa nyingi za kukuza biashara yako. Lakini kama utasema huna fedha, huna mtaji na ukaendelea kulala, nakutakia usingizi mwema.
SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
5. Nimejaribu sana lakini nashindwa.
Umesema nijifunze ili niwe mtaalamu, nimeshajifunza sana lakini siwezi.
JIBU; Bado hujajifunza vya kutosha, au haupo makini kwenye kujifunza kwako. Anza tena na jua ni nini hasa unachotaka. Usikate tamaa mpaka utakapofikia.
Umesema hata kama kitu kimefanywa naweza kukifanya na nikafanikiwa, nimeshajaribu hivyo lakini napata hasara tu.
JIBU; Unafanya kama kila mtu anavyofanya, weka ubunifu, jitofautishe, usiwe wa kawaida.
Unasema kama nahitaji connection nianze mimi kutafuta yule ninayetaka connection yake, nimejaribu sana, nimeenda ofisini kwa mtu niliyetaka kupata connection yake masecretary wamenizuia, wameniambia niandike barua na nieleze shida zangu nitapewa wa kunisaidia ila sio yule ninayemtaka.
JIBU; Ongeza juhudi, badili mbinu za kuweza kumpata mtu huyo, anza kufikiria ni jinsi gani unaweza kumsaidia, mwandikie kila unachofikiri kitamfanya atake kujua ni nani amempa mawazo hayo mazuri. Wakati huo huo kuwa bora kwenye kile unachokifanya, watu watakuongelea na moja kwa moja utapata nafasi ya kuonana na waliofanikiwa zaidi.
Unasema nianze kidogo hata kama mtaji sina, hata hicho kidogo sina, nilijaribu kuanz akidogo nimepata hasara na sasa sina hata pa kuanzia.
JIBU; Kama huna hata kidogo cha kuanzia kuna uwezekano mkubwa hujui unachotaka kufanya. Kama ulianza kidogo na umeshindwa, anza tena, ndio safari ya mafanikio ilivyo.
Hizo ndio fikra tano za kuondokana nazo ili uweze kufikia mafanikio. Kumbuka pamoja na yote haya maamuzi yanabaki kwenye mikono yako. Ukiamua kuyatumia haya kwenye maisha yako, utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa. Ukiamua kuachana nayo utaendelea hivyo ulivyo.
Nakutakia kila la kheri.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
1/29/2015 01:17:00 PM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Njia KUMI Za Kuboresha Maisha Yako Ya Kibiashara.
Ili kuweza kufanikiwa kwenye biashara na hata kwenye maisha unahitaji kuwa na malengo na mipango, kufanya kazi kwa bidii na maarifa na hata kuwa na mtizamo chanya kwenye kile unachofanya na hata maisha yako kwa ujumla.
Hakuna kitu kinachowarudisha watu nyuma kama kutokuwa na malengo, uvivu na mtazamo hasi.
Pamoja na mambo hayo muhimu kuna njia kumi unazoweza kuzitumia na ukaboresha maisha yako ya kibiashara kwa kiasi kikubwa sana.
1. Kubali changamoto.
Hakuna barabara iliyonyooka, hivyo hivyo biashara yoyote utakayofanya, hata kama ingekuwa rahisi kiasi gani ina changamoto zake. Unapokutana na changamoto, ikubali na kisha anza kuitatua. Ukianza kuikimbia unajijengea matatizo makubwa baadae.
SOMA; Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.
2. Jitegemee.
Ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara unayofanya, kuna wakati utahitaji kufanya maamuzi magumu na uweze kuyasimamia. Maamuzi hayo yanaweza yasiwe mazuri au yasiwapendeze wengi. Ni lazima uweze kujtegemea na kujisimamia kwenye biashara yako. Kama utaendesha biashara kwa kutegemea wengine wanafanya nini ndio uige, huwezi kufanikiwa.
3. Zione fursa.
Katika kila hali unayokutana nayo kwenye biashara, zione fursa mbalimbali zinapokuzunguka. Unapopata changamoto angalia ni fursa gani unayoweza kuitoa kwenye changamoto hizo. Kuwa na kiu ya kuangalia fursa na utaanza kuziona nyingi sana zinazokuzunguka.
4. Cheka.
Hata kama unafanya biashara inayokuhitaji uwe makini kw akiasi gani, unahitaji muda wa kucheka. Unahitaji muda ambao unawez akufanya utani wa hapa na pale na ukafurahia na kucheka. Kuna faida kubwa sana kwenye kucheka, inakuongezea kujiamini na kinga ya mwili pia.
SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.
5. Wasaidie wengine.
Utapata chochote unachotaka kwenye maisha kama utaweza kuwasaidia watu wengi zaidi kupata kile wanachotaka. Ifanye biashara yako kuwa sehemu ambayo watu wanajua matatizo yao yatapata suluhisho na utapata wateja wengi sana.
6. Kuwa na dhumuni la maisha yako.
Mbali na malengo na mipango ya kibiashara na hata maisha, kuwa na dhumuni kubwa la maisha yako. Hiki ni kitu ambacho utakiishi na ndio kitakusukuma wewe kuweka juhudi zaidi ili kuweza kufikia dhumuni hilo.
7. Kuwa tayari kubadilika.
Unachoamini leo, kesho kinaweza kisiwepo kabisa. Biashara inayolipa leo, miaka michache inaweza isiwepo kabisa. Hivyo wakati wowote kuwa tayari kubadilika. Soma alama za nyakati na kuwa tayari kuchukua hatua kabla mambo hayajakwenda hovyo.
8. Zungukwa na watu chanya.
Hakikisha unazungukwa na watu ambao wana mtizamo chanya kama ulivyo wewe. Hawa watakuwezesha wewe kuendelea na mtizamo wako. Ila kama utazungukwa na watu wenye mtizamo hasi, ni vigumu sana kuweza kuendelea na mtizamo wako.
SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya
9. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa.
Hili ndio hitaji la msingi kabisa, maelezo yanajitosheleza. Kama haupo tayari kufanya kazi kwa bidii na maarifa, achana na biashara, kafanye vitu vingine, na sina wazo ni kitu gani hakihitaji kazi. Kama utakipata tushirikishe.
10. Acha kuwa mwathirika.
Kama unataka kukuza biashara yako unahitaji kuacha kuwa na mawazo ya kiathirika. Pale jambo lolote linapotokea, acha kufikiri kwamba kwa nini limetokea kwako, au kwamba una bahati mbaya. Badala yake chukua hatua ya kubadili mambo. Kama umefanya makosa jifunze na usirudie tena.
Mafanikio kwenye biashara sio kitu rahisi sana ila pale unapojipanga vizuri utaona yanakuja yenyewe bila ya wewe kuteseka sana. Fanya mambo yale ya msingi na jali sana biashara yako na wale wanaokuzunguka. Bila kusahau, jifunze sana, wekeza sana kwenye rasilimali muhimu kwako ambayo ni akili yako.
SOMA; Kurasa 365 Za Mwaka 2015, Fursa Muhimu Kwako Kujifunza.
1/28/2015 02:02:00 PM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Mambo KUMI Ya Kufanya Ili Usiishi Maisha Ya Majuto.
Maisha ya majuto sio maisha mazuri kuishi. Ni maisha ambayo yatakufanya ukose furaha na hivyo kuona maisha yako hayana thamani.
Lakini pia majuto mengi ambayo watu wanaishi nayo ni ya kujitengenezea wenyewe iwe kwa matendo yao au kwa mitazamo yao.
Leo utajiongeza na mambo KUMI unayoweza kuanza kufanya leo ili uweze kusihi maisha yasiyokuwa na majuto.
1. Jali afya yako. Hiki ni kitu muhimu sana, ukiwa na afya mbovu utajutia mambo yote ya hovyo uliyofanya yakakupeleka kwenye afya mbovu.
SOMA; NENO LA LEO; Acha Kujiandaa Kuishi…
2. Tenga muda wa kufanya vitu unavyovipenda. Hata kama una kazi ngumu kiasi gani, tenga muda kila siku wa kufanya vitu ambavyo unavipenda kweli kwa moyo wako.
3. Pata muda wa kupumzika, cheka , cheza.
4. Sema kile ambacho unataka kusema. Unafiki utakufanya ujute sana baadae.
5. Badili mtazamo wako.
6. Usiumizwe na yaliyopitwa, usiogopeshwe na yajayo, ishi leo.
SOMA; UKURASA WA 19; Ishi Leo..
7. Kubali kwamba kuna vitu huwezi kuvibadili.
8. Acha kukimbiza fedha na mali, toa huduma nzuri na fedha zitakufuata zenyewe.
9. Shukuru kwa maisha uliyonayo, hata kama ni magumu kiasi gani.
10. Onesha upendo kwa kila mtu anayekuzunguka.
Maisha ni yako na una uamuzi wa kuyaishi vile unavyotaka kama tu hauvunji sheria na taratibu. Chagua kuishi maisha ambayo utayafurahia kila siku ili uweze kuwa na maisha bora. Fanya mambo hayo kumi kuanzia leo na maisha yako yataanza kubadilika.
1/27/2015 01:00:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.
Kushindwa ni jambo ambalo haliwezi kukwepeka. Ila tofauti kubwa ya wale waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni wale waliofanikiwa waliweza kuendelea hata baada ya kushindwa na wasiofanikiwa walikata tamaa baada ya kushindwa.
Kila mmoja wetu anapenda kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo analofanya, inaweza kuwa kazi, inaweza kuwa masomo, inaweza kuwa biashara, inaweza kuwa chochote ambacho ni muhimu kwako.
SOMA; Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.
Kuna vitu vitatu ambavyo vinawafanya watu wengi sana kushindwa kufikia mafanikio japo wanayatamani sana. Leo utajiongeza na vitu hivyo ili uweze kuviepuka na kufikia mafanikio unayotarajia.
1. Kuhsindwa kuendana na watu wengine.
Mafanikio sio kitu ambacho unaweza kukifikia wewe mwenyewe. Mafanikio yako yanategemea sana ushirikiano wako na watu wanaokuzunguka. Kama umeajiriwa kuna bosi wako, wafanyakazi wenzako na hata wafanyakazi walioko chini yako. Kama unafanya biashara kuna wateja, wafanyabiashara wenzako, wafanyakazi wako na kadhalika. Watu wote hawa wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yako. Ukiweza kushirikiana nao watakupa ushirikiano mzuri na utafikia mafanikio. Ukishindwa kushirikiana nao vizuri itakuwa vigumu sana kwako kufikia mafanikio.
SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.
2. Kukata tamaa.
Kama tulivyoona hapo juu, tofauti ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni kwamba waliofanikiwa huendelea kufanya hata wanapokutana na magumu, ila wasiofanikiwa hukata tamaa haraka wanapokutana na vikwazo au changamoto. Kama kweli una kiu ya kufanikiwa inabidi uwe king’ang’anizi hata pale mambo yanapoonekana ni magumu.
3. Kuahirisha mambo.
Tabia ya kuahirisha mambo imewazuia watu wengi sana kufikia mafanikio. Mtu anaweka malengo na mipango lakini inapofikia kweye utekelezaji anaahirisha. Tabia ya kuahirisha inamfanya mtu kushindwa kuchukua hatua haraka na hivyo kukosa fursa nzuri za kupata mafanikio.
Epuka mambo hayo matatu kama kweli una kiu ya kufikia mafanikio. Kama utaendele akuyaendekeza utaona siku zinapota ila hakuna mabadiliko kwenye maisha yako.
Mwaka huu 2015 unahitaji nini tena ili kufanikiwa? Kila unachohitaji unajifunza kupitia AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA, JIONGEZE UFAHAMU, na MAKIRITA AMANI. Kilichobaki ni wewe tu kuchukua hatua.
Nakutakia kila la kheri.
SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
1/26/2015 02:00:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Vitu VITATU Vinavyoathiri Kipato Chako Na Jinsi Ya Kukiongeza.
Katika mfumo wa uchumi tunaoishi sasa hivi duniani, ni dhahiri kwamba kipato chako kinaathiriwa na vitu vingi sana.
Kipato chako kinaweza kuathiriwa na hali ya uchumi inavyokwenda. Kwa mfano mfumuko wa bei unapokuwa mkubwa, kipato chako kinaweza kisitoshe matumizi yako. Lakini hii ni nguvu ya nje ambayo huwezi kuiathiri.
Kipato chako pia kinaathiriwa na mambo ambayo yanatokana na wewe binafsi na mambo haya unawezakuyabadili ili kubadili kipato chako.
Leo tutajadili vitu vitatu muhimu vinavyoathiri kipato chako na jinsi unavyoweza kuvitumia kubadili kipato chako.
Ni ukweli usiopingika kwamba kila mtu anapenda kipato chake kiongezeke, ila sasa unaanzia wapi kukiongeza? Jua vitu hivi vitatu na vifanyie kazi.
1. Unafanya nini.
Kitu cha kwanz akabisa kinachoathiri kipato chako ni unafanya kitu gani? Yaani ni shughuli gani unayofanya ili kujitengenezea kipato? Unafanya biashara? Umeajiriwa? Kama unafanya biashara je ni biashara gani? Na kama umeajiriwa je una utaalamu gani? Tunajua kabisa vipato vinatofautiana na kutokana na kile unachofanya. Kipato cha mwalimu hakiwezi kuwa sawa na cha daktari. Kipato cha boda boda hakiwezi kuwa sawa na cha dala dala.
Kuongeza kipato chako kwenye njia hii ni kuhakikisha unafanya kitu ambacho kina uwezekano mkubwa wa kutengeneza kipato kikubwa.
SOMA; HADITHI_FUNZO; Aliyenusurika Kufa Kutokana Na Tabia Yake Nzuri.
2. Unafanya kwa ubora gani?
Tumeona vipato vinatofautiana kutokana na vitu tofauti. Vile vile ndani ya fani moja au biashara moja, bado vipato havilingani. Watu wawili wanaweza wote kuwa walimu wenye kiwango sawa cha elimu lakini vipato vikawa tofauti. Watu wawili wanaweza kuwa wanaedesha boda boda na wanapaki eneo moja lakini vipato vikawa tofauti. Kwa yule ambaye anafanya kwa ubora wa hali ya juu kipato chake lazima kitakuwa kikubwa.
Hakikisha kile ambacho unakifanya unakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.
3. Ugumu wa kukubadili.
Kipato chako pia kinaathiriwa na ugumu wa kukubadili wewe kwenye hiko unachofanya. Pata picha wewe unafanya kazi ambayo ni wewe tu unaweza kuifanya, hii ina maana kwamba kama usipokuwepo kazi yako haiwezi kufanywa na mtu mwingine hivyo thamani ya kipato chako inakuwa kubwa. Hali kadhalika kama unafanya biashara kwa kiwango ambacho mteja wako hawezi kukipata sehemu nyingine, lazima utakuwa na kipato kikubwa.
Anza sasa kujitengenezea mazingira ya wewe kuw avigumu kubadilishwa. Na sio ufanye hivyo kwa kuwafanyia wengine majungu, ila kwa kujiboresha zaidi na hivyo kufanya kazi au biashara yako kwa ubora wa hali ya juu.
Chukua hatua leo ili kuboresha kipato chako, acha kulalamika, maamuzi ni yako.
SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.
1/23/2015 02:00:00 PM | Labels: BIASHARA, MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Okoa Muda Huu Muhimu Ambao Unaupoteza Kila Siku Na Kukuchelewesha Kufikia Mafanikio.
Kuna muda mwingi sana ambao unaupoteza kila siku na kwa kufanya hivyo unajichelewesha kufikia mafanikio.
Kumbuka muda una thamani kubwa kuliko fedha kwa sababu muda ukishapotea haurudi tena, ila ukipoteza fedha leo kesho unaweza kupata nyingine.
SOMA; UKURASA WA 09; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na Wengi.
Muda huo unaopoteza ni ule unaotumia kusema mabaya ya wengine, au kuonesha mapungufu ya wengine.
Ni kweli kwamba wengine wanaweza kuwa wana mapungufu makubwa, wanaweza kuwa wanakosea sana ila wewe kutumia muda wako kuyasemea hayo hakutakusaidia kwa vyovyote kufikia mafanikio unayotarajia.
Kwa mfano wewe ni mfanya biashara na unatumia muda wako mwingi kusema jinsi gani wafanyabiashara wengine wanakosea, au wanamadhaifu. Kwa kufanya hivi hauna tofauti na wao. Ni heri kutumia muda wako mwingi kuimarisha biashara yako.
SOMA; Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.
Inawezekana wewe ni mchungaji ambae una kanisa, ila unatumia muda wako mwingi kusema jinsi gani wachungaji wengine wana mapungufu au wana mabaya. Ni vyema ukatumia muda huo vizuri kuwaonesha watu ni kipi sahihi kinachotakiwa kufanywa.
Inawezekana wewe ni mwanasiasa na unatumia muda mwingi kuonesha madhaifu ya chama kingine au mgombea mwingine. Hii haitakusaidia kushinda uchaguzi, ni vyema kutumia muda wako mwingi kuwaeleza watu utawafanyia nini na watakuona upo makini.
Sisemi tusikemee mabaya, ila hii isiwe agenda yetu kuu, labda kama ndio agenda yako na kama ndivyo hujui unachokifanya au itakuwa vigumu kifikia mafanikio.
Kumbuka kitu chochote ambacho hakipo kwenye malengo na mipango yako ni kelele kwako. Achana nacho mara moja na wekeza nguvu zako kwenye kukuza kile unachofanya.
SOMA; USHAURI ADIMU; Unapokutana Na Tatizo Jiulize Jambo Hili Moja La Msingi.
1/22/2015 04:15:00 PM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Vitu Vitatu Vitakavyokufanya Uwe Na Hamasa Ya Kufikia Mafanikio.
Hamasa ni kitu muhimu sana ili uweze kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya.
Hii ni kwa sababu katika njia yoyote utakayopita utakutana na vikwazo na pia katika yale utakayofanya utapata changamoto.
Bila ya kuwa na hamasa kubwa utaishia njiani kwa kukata tamaa haraka sana.
Uzuri ni kwamba unaweza kuhamasishwa na pia unaweza kujihamasisha mwenyewe.
Unahamasishwa unaposoma vitabu ja makala nzuri kama hizi unazosoma hapa kwenye JIONGEZE UFAHAMU, MAKIRITA AMANI, AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Baada ya kupata hamasa hii unaweza sasa kuendelea kujihamasisha mwenyewe.
Ili kujihamasisha mwenyewe unahitaji kuwa na vitu hivi vitatu muhimu;
1. Kujisimamia.
Kama unajua kwamba unaweza kujisimamia mwenyewe unakuwa na hamasa kubwa sana ya kufanya vizuri. Hakuma mtu ambaye anapenda kupangiwa kila kitu cha kufanya, unapokuwa na nguvu ya kujipangia na kujisimamia unakuwa na hamasa ya kutekeleza mipango yako.
2. Kubobea.
Kama wewe ni mtaalamu wa kitu unachofanya unakuwa na hamasa kubwa ya kufanya kitu hiko. Kama umebobea na unatoa vitu ambavyo kila mtu anavikubali utahamasika kufanya zaidi ili wengi zaidi wanufaike na kile unachotoa.
SOMA; Kitu hiki kimoja ndio kitakufanya uanze.
3. Dhumuni.
Kama una dhumuni zuri la kuwasaidia wengine kwa kile unachofanya utahamasika kufanya zaidi. Kwa kuwa unajua watu wanakiutegemea kwa unachofanya na wanategemea kitu bora, hutotaka kuwaangusha. Hii itakuhamashisha ufanye zaidi na zaidi.
Hivyo ndio vitu vitatu muhimu unavyohitaji ili kujihamasisha. Habari njema ni kwamba kama huna vitu hivyo unaweza kujifunza. Na utajifumza kwa kujiunga ma KISIMA CHA MAARIFA ambapo mimi na wewe tutakuwa karibu zaidi.
Karibu sana.
1/21/2015 02:25:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Sheria NANE Za Kufanikiwa Kwenye Biashara Kutoka Kwa Warren Buffett.
Warren Buffett ni mmoja wa watu matajiri sana duniani. Utajiri wake huu ameupata kupitia biashara na uwekezaji. Alianza biashara akiwa na miaka 11 na sasa ana miaka 83. Kwa miaka zaidi ya 60 ambapo amekuwa kwenye biashara una uzoefu wa kutosha kutufundisha sisi ni vitu gani vya kuzingatia kwenye biashara.
Hizi hapa ni sheria 8 za kufanikiwa kwenye biashara kutoka kwa Warren Buffett.
1. Tulia wakati wa matatizo/changamoto.
Katika biashara kuna wakati ambao utakutana na changamoto na matatizo mbalimbali. Huu ni wakati ambao Warren anatushauri tutulie badala ya kuvurugwa na hatimaye kuharibu kila kitu.
SOMA; Maswali Matatu Kwa Anayetaka Kuwa Mjasiriamali Kujiuliza Kutoka Kwa Richard Branson.
2. Zungukwa na watu wazuri.
Kama unafanya biashara kwa kushirikiana na mtu au watu wengine, hakikisha watu hawa wana maadili mazuri na wanandoto kubwa ya mafanikio kama uliyonayo wewe.
3. Ng’ang’ania kile unachokitaka.
Warren anashauri kwamba usiache lengo lako kuu kwa sababu kuna vitu vizuri umeviona pembeni, kufanya hivi kutakuletea kushindwa.
4. Weka gharama chini.
Hakikisha gharama za kuendesha biashara yako zinakuwa chini sana ili uweze kuuza kwa bei ambayo wateja wako wanaweza kuimudu na wewe kupata faida.
SOMA; Hakuna Anayejua Anachofanya, Na Huo Ndio Uzuri Wa Maisha.
5. Toa zawadi kwa wafanyakazi wako.
Warren anashauri kwamba pale wafanyakazi wanapofanya vizuri uwape zawadi hata kama ni ndogo kiasi gani. Hii inawafanya waone unajali.
6. Epuka matatizo.
Warren aliwahi kumwandikia mshirika wake kwenye biashara hivi “nachotaka kujua ni wapi nitaenda kufa hivyo nisiende hapo kamwe”. Kama unataka kufanikiwa kwenye biashara unahitaji kuepuka matatizo maana matatizo mengi yanasababishwa na wewe mwenyewe.
7. Fanya kuwa ndogo.
Buffett anasema kwamba biashara inapokuwa kubwa sana inakuwa vigumu kubadilika na urasimu unakuwa mkubwa kiasi cha kuwachosha wafanyakazi na hata wateja. Anashauri kurahisisha uongozi wa biashara hivyo hata ikikua sana bado ionekane ni ndogo na rahisi kuongoza na kuwasiliana.
8. Linda heshima yako.
Buffett anasisitiza kwamba heshima yako ni kitu muhimu sana kwenye mafanikio ya biashara. Anashauri kuwa mwaminifu na kutofanya kitu chochote ambacho usingependa kiripotiwe kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti. Anasisitiza hili kwa kauli hizi mbili;
Poteza hela za biashara na nitakuelewa, poteza sifa ya biashara na nitakuwa mbaya sana kwako.
Inakuchukua miaka 20 kujenga heshima na dakika tano kuiharibu. Ukifikiria hili utafanya mambo kwa tofauti.
Tumia sheria hizi nane kwenye maisha yako ya kila siku na ya biashara na zitakusaidia sana kufikia mafanikio.
SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya
1/21/2015 11:54:00 AM | Labels: BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO | 3 Comments
Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.
Kama kila siku una matatizo ya fedha, na karibu kila mtu ana matatizo haya, huenda kuna mambo mawili unayoyafanya kimakosa sana.
Jambo la kwanza kipato chako ni kidogo.
Jambo la pili matumizi yako yanazidi kipato chako.
Leo tutajadili jambo la pili na siku nyingine tutajadili jambo la kwanza. Hiyo endelea kutembelea mtandao huu wa JIONGEZE UFAHAMU ili uweze kujifunza mambo hayo mazuri ambayo yataboresha maisha yako.
Ili kuweza kurudisha usimamizi mzuri kwenye fedha zako, hatua ya kwanza kabisa ni kubana matumizi. Unaweza kufikiri kwa nini hatujaanza kujadili kuongeza kipato, ila kama utaongez akipato kwa tabia uliyonayo ya matumizi mabovu bado utarudi pale pale.
Leo tubane kwanz ama matumizi halafu kwenye makala ijayo tutaongeza kipato.
Zifuatazo ni njia kumi za kubana matumizi kwa mwaka huu 2015.
1. Tengeneza bajeti. Bajeti yako ni muhimu na ndio itakayokuongoza kwenye matumizi yako ya fedha. Jua kila mwezi utatumia kiasi gani na gawa kwenye wiki na hata siku. Iheshimu bajeti yako.
2. Nunua vitu kwa jumla. Kama ni vitu vinavyohusiana na matumizi muhimu ya nyumbani nunua kwa jumla. Hii itakufanya ununue kwa bei nzuri na pia kuweza kwenda na bajeti yako.
3. Sitisha huduma ambazo hutumii. Kama kuna huduma umejiunga nazo ambazo hutumii sana sitisha. Hii inaweza kuwa malipo ya kuangalia tv, malipo ya kuhudhuria mazoezi, malipo ya gharama za simu na kadhalika.
4. Usinunue vitu hovyo. Ukikutana na mtu anauza nguo hata kama umeipenda kiasi gani usiinunue kama hukuwa na ratiba hizo.
5. Epuka sana mikopo. Kama kitu sio muhimu sana kwao, usiingie kwenye mkopo ili kukipata, mikopo ni mzigo ambao unakupotezea fedha nyingi.
6. Punguza starehe. Punguza kiasi ambacho unatumia kwenye starehe kama kula kwenye hoteli kubwa, kutumia vilevi, kwenda kwenye kumbi za starehe na kadhalika.
7. Nunua vitu vyenye ubora, hata kama ni ghali. Unaweza kufikiri kununua vitu vya bei rahisi ni kubana matumizi ila ukawa ndio unaongeza matumizi zaidi. Nunua kitu chenye ubora hata kama ni bei ghali, utakaa nacho muda mrefu zaidi na hivyo kuepuka kupoteza fedha kwenye kununua mara kwa mara.
8. Nunua vitu ambavyo unavihitaji kweli na sio unavyotamani. Kwa mfano nguo, nusu ya nguo zako hujazivaa mwaka mmoja uliopita. Sasa unanunua nyingine za nini? Acha kupoteza fedha.
9. Andaa vitu unavyoweza kuandaa mwenyewe badala ya kufikiria kununua tu. Pendelea kupika chakula badala ya kununua chakula kilichopikwa.
10. Acha kutaka kuonekana. Usifanye mambo kwa sababu kila mtu anafanya. Usinunue simu mpya kwa sababu kila mtu ana simu mpya. Fanya kitu ambacho unakitaka kweli na sio kwa sababu kila mtu anakifanya.
Tumia mbinu hizi kumi na uanze kupunguza matumizi yako mwaka huu 2015. Katika makala ijayo tutajadili njia kumi za kuongeza kipato chako mwaka 2015.
Kila la kheri.
1/20/2015 01:00:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Wajasiriamali Wenye Mafanikio Hufanya Mambo Haya Matano Kila Siku.
Kila mtu ana maelezo yake ya mafanikio. Neno mafanikio lina maana tofauti kw akila mtu. Lakini licha ya utofauti huo bado kwa ujumla mafanikio ni kuwa bora kama unavyoweza kuwa.
Na mafanikio sio kitu ambacho kinatokea mara moja. Hutaamka siku moja asubuhi halafu paa mafanikio hao hapo.
SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kutoka Kimaisha Kwa Kuanza Na Mshahara Mdogo.
Mafanikio yanatokana na jinsi unavyoishi kila siku. Kuna tabia ndogo ndogo unazofanya kila siku ambazo zikikusanyika pamoja ndio zinaleta mafanikio au kushindwa.
Yafuatayo ni mambo matano ambayo wajasiriamali wenye mafanikio hufanya kila siku. Yasome na wewe uanze kuyafanya ili uweze kufikia mafanikio.
1. Wako tayari kujaribu tena hata pale wanaposhindwa.
Haijalishi wameshindwa mara ngapi, wajasiriamali wenye mafanikio huendelea kujaribu tena na tena. Na hawajaribu tu kama wajinga(kwa kurudia kile kile walichofanya) bali wanatumia walichojifunza na kubadili mbinu wanazotumia na hatimaye kupata mafanikio.
SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ni Kitu Unachotakiwa Kufanya Kila Siku.
2. Huzikabili hofu zao.
Moja ya vitu vinavyowarudisha watu wengi nyuma ni hofu. Wajasiriamali wenye mafanikio sio kwamba hawana hofu, wanazo ila wanaamua kuzikabili. Wanaingiwa na hofu ila nwanajua hii ni hofu na wanaipuuza na kuendelea na mipango yao.
3. Wanajitengenezea nidhamu binafsi.
Wajasiriamali wenye mafanikio makubwa wanajua ya kwamba nidhamu binafsi ndio msingi wa mafanikio. Hivyo kila siku hujijengea nidhamu binafsi ili waweze kutekeleza majukumu yao, kuaminika zaidi na kuweza kufikia mafanikio. Wako tayari kufanya kazi ngumu leo ili baadae wapate matunda mazuri. Hawakimbilii kufanya vitu vya kuwafurahisha kwa sasa.
4. Hutenga muda wa kupumzika.
Pamoja na kupenda kufanya kazi kwa bidii na maarifa, wajasiriamali wenye mafanikio wanajua kwamba miili yao haiwezi kufanya kazi muda wote. Hivyo hutenga muda maalumu kwa ajili ya kupumzika ili kurejesha nguvu kwenye miili yao.
5. Hutoa bila ya kutegema kupokea.
Wajasiriamali wenye mafanikio hutoa kwa wengine bila ya kutegemea kupokea. Kama ni bidhaa au huduma wanatoa, hutoa zaidi ya wanavyolipwa.Kwa njia hii huendelea kuwa bora zaidi na kutengeneza wateja wengi, faida kubwa na mafanikio makubwa.
Hayo ndio mambo matano yanayofanywa na wajasiriamali waliofanikiwa, anza sasa kuyafanya na wewe kila siku. Kitakachotokea utaona mwenyewe.
1/19/2015 06:02:00 PM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Vyanzo Viwili Vya Vikwazo Vinavyokuzuia Kufikia Mafanikio
Maisha ni magumu, angalau kila mtu wnalikubali hilo.
Kila jambo unalofanya kwenye maisha kuna vikwazo au changamoto ambazo utakutana nazo.
Lakini changamoto hizi haziyokei tu hewahi, bali zina vyanzo vyake.
Kuna vyanzo viwili vya changamoto zinazokufanya mpaka sasa hujafikia mafanikio makubwa.
1. Vikwazo vya kimwili.
Hivi ni vikwazo vinavyoonekana, ujana, uzee, ugonjwa, ulemavu, ufupi, kukosa uzoefu na vingine vingi ambavyo vinaweza kukufanya uone huwezi kuendelea na mapambano.
2. Vikwazo vya kiakili.
Hivi ni vikwazo ambavyo vipo kwenye mawazo yako. Hofu, kutokujiamini, wasiwasi na kukosa uvumilivu. Vikwazo hivi vinakufanya uamini kwamba huwezi kuendelea tena pale unapokutana na changamoto kubwa.
Jambo jema na la kufurahia ni kwamba vikwazo vyote hivi unaweza kuvishinda.
Kama utajifunza kutoka kwa walioshinda licha ya kuwa na vikwazo mbalimbali unaweza na wewe kuchukua hatua na kubadili maisha yako.
Anza sasa kujifunza ili uboreshe maisha yako.
1/18/2015 12:18:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Kitu Hiki Kimoja Ni Lazima Kitokee Kwenye Maisha Yako, Japo Hukipendi.
Tukiangalia historia ya dunia tokea enzi na enzi, tunaona jinsi ambavyo watu wamepitia changamoto mbalimbali.
Tunaona jinsi ambavyo tawala kubwa kama Roma zilivyopigania ukuaji wa utawala wao na hata kufikia kufa kabisa.
Tumeona watu wakitokea kwenye maisha magumu, kujaribu vitu vipya kushindwa lakini kuwa vinganganizi na hatimaye wakafanikiwa.
Kitu kimoja ambacho naweza kukuhakikishia kitatokea kwenye maisha yako ni changamoto au vikwazo.
Haijalishi utapata elimu kiasi gani, haijalishi utakuwa na fedha kiasi gani na haijalishi utakuwana na hadhi kiasi gani. Kila ngazi utakayokuwa unapitia kwenye maisha yako utakutana na changamoto na vikwazo.
Tunaweza kusema changamoto hizi ni njia ya dunia kutupa mitihani ili tuoneshe kama kweli tuko tayari kupata kile tunachotaka.
Katika changamoto yoyote utakayopitia hata iwe kubwa kiasi gani, unaweza kufanya moja kati ya haya mawili;
1. Kukubali changamoto hiyo iwe ndio mwisho wako na kutoendelea na mapambano ya kupata kile ulichotaka.
2. Kutumia changamoto hiyo kukua zaidi na kukupa nguvu na hasira ya kupata kile ulichokuwa unataka.
Uchaguzi ni wako, kama utaamua kukubali kukata tamaa kila la kheri.
Kama utaamua kiendelea na mapambano licha ya changamoto unazokutana nazo weka email yako hapo juu ili uendelee kupata mbinu za kupambana na changamoto hizo.
TUPO PAMOJA.
1/18/2015 11:35:00 AM | Labels: FIKRA TOFAUTI, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Mbinu 9 Za Kukuwezesha Kuamka Asubuhi Na Mapema Ukiwa Na Nguvu.
Kuamka asubuhi na mapema ni moja ya siri ya watu wenye mafanikio makubwa. Hii ni kwa sababu asubuhi na mapema akili inakuwa vizuri na hivyo kuweza kufanya majukumu yanayohitaji kutumia vizuri akili yako.
Pamoja na muda huu kuwa mzuri sana kwa kutekeleza majukumu, sio rahisi sana kuamka asubuhi. Watu wengi wamekuwa wakijaribu kuamka asubuhi lakini wanaishia kuzima alamu zao na kurudi kulala.
Leo hapa UTAJIONGEZA na mbinu 9 zitakazokuwezesha kuamka mapema na ukiwa na nguvu.
1. Soma kitabu au jarida dakika 30 kabla ya muda wa kulala.
2. Usile au kunywa pombe mda mfupi kabla ya kulala.
3. Weka simu au kompyuta yako mbali, mwanga wa simu na kompyuta hupunguza usingizi.
4. Usijiwekee majukumu mengi ya kufanya asubuhi. Fanya yale ambayo ni muhimu tu.
5. Panga kupata kifungua kinywa kizuri, hii itakuhamasisha kuamka mapema.
6. Fanya mazoezi, sio lazima yawe magumu.
7. Kunywa maji, itarudisha maji uliyopoteza kwa siku nzima.
8. Weka alarm yako kwenye chumba kingine ambapo utalazimika kuamka ili ukaifuate.
9. Pata jua la kutosha.
Unaweza kupitia mbinu hizi kwenye picha hapo chini.
1/18/2015 08:03:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments