Showing posts with label MBINU ZA AFYA. Show all posts
Showing posts with label MBINU ZA AFYA. Show all posts

SIKU YA UKIMWI DUNIANI; Mambo Kumi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ukimwi.

Kila tarehe 01/12 ya kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya UKIMWI. Siku hii imepewa heshma yake kutokana na madhara yake makubwa kwa watu wanaoupata.

Wakati tukiwa kwenye siku hii ya UKIMWI jiongeze na mambo haya kumi muhimu.

1. UKIMWI HAUUI.

UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga mwilini. Hivyo kinga yako inapopungua unatoa nafasi ya magonjwa mengine kukushambulia. Hivyo kinachowaua wagonjwa wa ukimwi sio ukimwi wenyewe bali magonjwa nyemelezi.

2. UKIMWI ni tofauti na VIRUSI VYA UKIMWI.

Ukiambukizwa virusi vya ukimwi leo, hauna ukimwi. Unawez akukaa na vizsi hivi kwa muda hata wa miaka kumi na pale kinga ya mwili inaposhindwa kukulinda na magonjwa ndio unakuwa na UKIMWI.

3. Wagonjwa watatu wa kwanza wa UKIMWI Tanzania waligunduliwa katika hospitali ya Ndolange mkoani Kagera mwezi November 1983.

4. UKIMWI husambazwa kwa kupitia maji maji ya mwilini. Yanayoongoza ni damu, na yenye kiasi kidogo ni mate, machozi na majimaji ya ukeni.

UKIMWI TZ

5. Njia kuwa ya kusambaza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine ni kufanya mapenzi bila ya kujikinga. Njia nyingine ni kuchangia vitu vikali kama sindano na pia mama kwenda kwa mtoto.

6. Mpaka leo hakuna tiba wala kinga ya UKIMWI. Baadhi ya tafiti zimeonesha matokeo mazuri ila hakuna ambayo imedhibitishwa kutumiwa kama kinga au dawa.

7. Afrika chini ya jangwa la sahara ndio sehemu yenye maambukizi makubwa ya UKIMWI, asilimia 80 ya watu wenye ukimwi duniani wako Africa chini ya jangwa la sahara. Wakati idadi ya wanachi walioko Afrika chini ya jangwa la sahara ni asilimia 10 tu ya idadi ya watu wote duniani.

8. Wanawake wana hatari mara nane zaidi ya kuambukizwa ukimwi kuliko wanaume.

9. Mikoa inayoongoza kwa UKIMWI Tanzania ni Njombe ukifuatiwa na Iringa na mikoa yenye maambukizi madogo ni Pemba, Unguja na Lindi.

10. Mapambano ya UKIMWI yanaanza na mimi na wewe. Njia nyingine za maambukizi zimeweza kuzuiwa kwa kiasi kikubwa ila njia moja ndiyo yenye changamoto na njia hiyo ni kupitia kufanya mapenzi.

Tushirikiane kuutokomeza UKIMWI.

Mambo matatu yatakayokufanya uishi maisha marefu.

Magonjwa mengi yanayowafanya watu kufa wakiwa na umri mdogo yanatokana na mtindo wa maisha tunaochagua.
Magonjwa kama presha ya juu, kisukari na hata kansa yanatokana na mitindo mbalimbali ya maisha.
Hapa nakushirikisha mambo matatu unayoweza kuanza kuyafanya leo na ukapunguza nafasi ya wewe kupata magonjwa haya na hivyo kuishi miaka mirefu.
1. Kula vizuri.
Naposema kula vizuri namaanisha ule mlo kamili. Kula mafita kidogo na kwa mtu mzima kula wanga kidogo. Kula matunda na mboga ,boga kwa wingi na pia kunywa maji mengi.
2. Fanya mazoezi.
Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako. Na mazoezi sio lazima ulipie gym au kukimbia barabarani japo hiyo ni sehemu nzuri ya mazoezi.
Unaweza kuchagua kutembea kwa miguu badala ya kupanda gari, kupanda ngazi badala ya kupanda lifti na kusimama na kufuata kitu mwenyewe badala ya kuagiza uletewe.
3. Usivute sigara.
Kila unapovuta sigara moja unapunguza dakika 14 za maisha yako. Sigara ina kemikali zaidi ya elfu moja zinazosababisha kansa. Karibu kila kansa inayompata binadamu inaweza kuchochewa na uvutaji wa sigara.
Na sigara sio lazima uvute wewe, hata ule moshi unaovuta kutoka kwa watu wanaovuta sigara una athari kubwa kwa afya yako.
Hayo ndio mambo matatu ambayo unaweza kuanza kuyafanya leo na ukaboresha afya yako na kyongeza siku zako za kuishi.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
www.kisimachamaarifa.co.tz
www.amkamtanzania.com

Faida Kumi za Kula Matango

Ukweli Kuhusu Afya ya Wanaume; Kwa nini Wanaume Wanakufa Wadogo Kuliko Wanawake.

Web-infographic

Faida 13 kiafya za kucheka.

Laughter-Infographic1

JE WAJUA; Madhara Ya Kula Huku Unaangalia Tv

Imekuwa ni jambo la kawaida kwa mtu kula huku akiangalia tv, simu au kompyuta.
Wakati mwingine mtu anaweza kuwa anakula huku anasoma kitabu, gazeti au jarida.
Hiki ni kitu hatari sana kwa afya yako. Tabia hii inakusababishia uzito wa mwili uliozidi(obesity) au kiribatumbo.
Hii inatokana na kwamba wakati unakula huku unafanya jambo jingine akili yako inakuwa haipo kwenye chakula na hivyo kula chakula kingi sana.
Badili tabia hii sasa ili kula kwako kuwe ni afya.
Tenga muda wa kula na usiingiliwe na kitu kingine.
Nakutakia afya njema.