Showing posts with label UONGOZI. Show all posts
Showing posts with label UONGOZI. Show all posts
Sifa Unazotakiwa Kuzitambua Kwa Kiongozi Anayeweza Kuleta Mabadiliko.
Habari na karibu ndugu
mpenzi msomaji wa blogu hii ya JIONGEZE UFAHAMU. Ni matumaini yetu umekuwa na
wiki ya mafanikio sana.
Leo tutaangalia sifa
unazotakiwa kuzitambua kwa mtu unayetaka awe kiongozi au unamtegemea awaongoze.
- Tabia
Mtu
mwenye tabia nzuri au njema anakuwa na uaminifu, utiifu, nidhamu, kutegemewa,
uvumilivu, kujitambua na pia anakuwa na bidii katika kazi. Wakati kwa upande
mwingine mtu asiye na tabia njema au nzuri anakuwa hana uwezo wa kuwajibika kwa
matendo yake, hawezi kukamilisha kazi kwa wakati, na pia hatimizi ahadi au
majukumu yake.
- Kuhamasisha
Mtu
ambaye anajua wapi anaelekea anakuwa na uwezo wa kuhamasisha wengine wafuatane
nae kutokana na ahadi au mambo mazuri yanayopatikana kule anakoelekea. Kwa hiyo
unahitaji kuangalia mtu Yule ambaye anafuatwa na watu wazuri na sio wale walio
wa kawaida kabisa pia angalia huyu mtu anamtazama nani kama mtu anayemhamasisha
bila shaka kwa Yule anayefaa kuwa kiongozi utamkuta anamfuatilia mtu ambae pia
ni kiongozi na ana sifa njema
- Mtazamo chanya
Tafuta
mtu Yule ambaye hana vizuizi katika akili yake kwa kuona jambo Fulani
haliwezekani bali awe ni Yule mwenye nia ya kujaribu pamoja na kuwaza chanya
kuwa atafanikiwa katika lile atendalo na anakuwa hazuiwi na vikwazo binafsi.
- Ufanisi mzuri katika kuwasiliana
Viongozi
wazuri ni wale ambao wanaweza kuwasiliana vema, wanakuwa wanajihusisha vema na
wale wanaoongea nao kwa kuweza kumtazama ana kwa ana pamoja na kuwa na tabasamu
kwa Yule anayeongea naye. Kiongozi mzuri si Yule anayeweza kuwasilisha ujumbe
wake lakini pia anakuwa na uwezo mzuri wa kusikiliza pia wale anaowaongoza.
- Kujiamini
Bila
kujali hali gani katika wakati husika kiongozi pamoja na kundi wanapitia ,
kiongozi mzuri ni Yule anayekuwa anayejiamini na kuwa na ujasiri kuwa yeye
pamoja na timu anayoiongoza wanaweza kusogea hatua kutoka walipofika
- Nidhamu
Kiongozi
ni Yule mwenye nidhamu anayeweza kutawala hisia zake na pia ana uwezo wa
kusimamia au kutawala muda wake jinsi ya kuutumia ili kumsaidia kupata
mafanikio kwa ajili yake na timu anayoiongoza
- Rekodi nzuri ya mafanikio
Ni
vizuri ukacheki historia yake ya nyuma ya utendaji wa mtu. Na kiongozi mzuri
utakuta ana rekodi nzuri ya utendaji
Mwandishi: Goodluck Moshi
Mawasiliano:
Whatsapp:
+255 753 201 994, Telegram: +255 658
201 994, Barua pepe:
eng.gmoshi@gmail.com Facebook:
Goodluck Moshi
Pia unaweza kutembelea
blog yake www.stadizamafanikio.blogspot.com
kujifunza zaidi.
6/04/2015 07:30:00 AM | Labels: UONGOZI | 0 Comments
Jinsi ya Kuwaandaa Kuongoza Viongozi Watarajiwa (Chipukizi)
Habari
na karibu ndugu mpenzi msomaji wa blogu hii ya JIONGEZE UFAHAMU. Ni matumaini
yetu umekuwa na wiki ya mafanikio sana.
Leo
nitazungumzia namna ya kuwaandaa watu wenye sifa za uongozi ambao umewatambua
upo nao katika timu yako katika taasisi. Kuwaandaa viongozi hawa watarajiwa
kunahusisha wewe ambaye tayari ni kiongozi pamoja na hao viongozi watarajiwa ,
nah ii inaweza kulinganishwa kwa kiasi Fulani kama unawawapatia mafunzo.
1. Tengeneza Mahusiano na
Viongozi Chipukizi Unaowaandaa
Viongozi
chipukizi ambao umeshawatambua unahitaji kuwafahamu, kuwasikiliza historia za
maisha yao ili uweze kuwajua zaidi ya vile unavowajua tu kiofisi. Huhitaji
kujua kuhusu uwezo au ubora wao tu bali unahitaji pia kujua kuhusu madhaifu yao
pia ili uweze kujua namna ya kuwafanya wakamilifu kwa hayo mapungufu
uliyoyatambua. Na ukiweza kujenga mahusiano mazuri maanake utafanya wakupende
na pia kuongeza nia na kiu kwao kujifunza kutoka kwako
SOMA; Hatua 6 za Kuwalea Viongozi Watarajiwa (Chipukizi)
2.
Washirikishe
ndoto yako
Wakati
unaendelea kuwafahamu usiwaache wao peke yao tu wakuambie ya kwao, na wewe pia
unahitaji kuwashirikisha pi historia ya maisha yako na unahitaji kwenda hatua
ya ziada kwa kuwashirikisha ndoto yako kuhusiana na taasisi ambayo unaiongoza.
Na hii itawasaidia kujua ni wapi unataka kwenda na hivo kujiunga kujitoa
kufuatana nawe mpaka mwisho wa safari yako
3. Waombe utayari wao
kujitoa kiuongozi
Moja
ya kiungo muhimu ambacho kinaweza kumfanya kiongozi chipukizi kuwa kiongozi
mwenye mafanikio, ni utayari wa kujitolea kiuongozi. Ni muhimu sana kwa hawa
viongozi chipukizi unaowaandaa wawe wamejitoa kwa ajili ya uongozi pamoja na
taasisi. Na unahitaji kuwaeleza gharama ambayo itawachukua kwa wao kuwa
viongozi, na jambo la muhimu ni uwe mkweli kuhusu mambo ambayo watahitaji
kuzingatia au kuyajua hata kabla ya hatua yenyewe ya kufanya maamuzi ya
kukubali kuweza kujitoa kiuongozi.
4. Weka malengo kwa ajili
ya ukuaji
Viongozi
hawa chipukizi wanahitaji kujua malengo yaliyo fasaha ambayo wanatakiwa
kuyapigania au kuyafanikisha, nah ii itawasaidia kujua ni nini wnatakiwa
kufanya na pia ni vitu gani vinatarajiwa kutoka kwao. Jambo muhimu zaid la
kuzingatia ni unapoweka malengo zingatia malengo yawe yako wazi, fasaha na
yanayoeleweka. Malengo yawe ni sahihi kwao lakini pia yawe yanaweza kupimika.
Baada ya kuyafahamu hayo malengo ni vizuri yawekwe katika maadnishi ili kila
mmoja aweze kujitoa kikamilifu katika malengo hayo
5. Weka mambo ya msingi
sawa
Ni
muhimu sana kuweka misingi kwa kuwaelewesha majukumu yao na wayafahamu kwa
undani. Weka kwa ufasaha mategemeo yako kwao lakini pia na wao wajue vipaumbele
ni vipi katika majukumu yao. Na uhakikishe wanaweza kujua tofauti kati ya kazi
iliyo ya umuhimu sana na ile kazi yenye umuhimu kiasi.
6.
Mfumo
wa ufundishaji unaofaa
Kuna
hatua tano muhimu zinazoweza kukupatia matokeo mazuri hasa inapohusisha
kuwaandaa kiuongozi viongozi chipukizi
i.
Kuwa mfano kwanza kwa
kila unachotaka waweze kukifanya
ii.
Wafundishi au waelekeze
iii.
Simamia maendeleo ya
kile unachowaelekeza
iv.
Wahamasishe
v.
Wape fursa pia ya
kutengeneza viongozi kati yao viongozi chipukizi
7. Simamia maendeleo yao
bila kuacha
Ni
muhimu ukawa na mikutano iliyo rasmi na isiyo rasmi pia ili kuweza kujua
mahitaji, matatizo ambayo wanakumbana nayo pia. Na hii itakusaidia kuwapatia
vifaa sahihi zaidi na kuendelea kuwapa ujasiri na kuwahamasisha.
Mwandishi:
Goodluck Moshi
Mawasiliano:
Whatsapp:
+255 753 201 994, Telegram: +255 658
201 994, Barua pepe:
eng.gmoshi@gmail.com Facebook:
Goodluck Moshi
Pia
unaweza kutembelea blog yake www.stadizamafanikio.blogspot.com
kujifunza zaidi.
5/28/2015 07:30:00 AM | Labels: UONGOZI | 0 Comments
Subscribe to:
Posts (Atom)