Showing posts with label HABARI ZA UWEKEZAJI. Show all posts
Showing posts with label HABARI ZA UWEKEZAJI. Show all posts

Soko la Hisa la Dar: Fursa ya kipekee kwa wajasiriamali wazalendo Tanzania

 

Soko letu limekuwa likiwanufaisha zaidi wageni na wananchi wa nchi jirani ambao hulitumia kikamilifu kujinufaisha na wazalendo wengi kutoelewa nini kinachoendelea. Kwa wale waliokwisha jitosa, huwezi amaini jinsi wanavonufaika na kuwekeza zaidi na zaidi.

Leo kidogo tutupe jicho kwenye hii sekta ya hisa… Si sekta ngeni sana ila kwa hapa nchini wananchi wengi hawajaigundua na kushiriki kikamilifu kama nchi jirani na Tanzania. Wenzetu Kenya wamejitahidi kwenye ushiriki wa soko lao la Hisa la Nairobi (Nairobi Stock Exchange). Na kwa Afrika Mashariki, hili Soko la Hisa la Nairobi ndilo soko kubwa kuliko yote.

Dar-es-Salaam-Stock-Exchange

Pamoja na changamoto zake, hili soko lina faida kubwa kwa wale walioligundua na wanaoendelea kulitumia. Kuna mjasiriamali mmoja, yeye alinunua hisa za Twiga mwishoni mwa miaka ya 90 au mwanzoni mwa miaka ya 2000 zikiwa zinauzwa kati ya 200-300 kwa kipande. Leo hii kipande hicho hicho cha Twiga Cement kinauzwa kati ya 2500-2006 kiasi cha miaka 13 tu mbele.

Mdau huyu wa soko hilo anakiri kama angejua ukuaji ni wa kiasi hiki basi angenunua zaidi ya hizo alizonunuaga. Na ameendelea kuongeza vipande vyake kila awezapo. Anadai yeye hupenda kuwekeza kwenye hisa sababu hakuna usumbufu wa uendeshaji . Ukishanunua hisa unakaa na kungoja zipande ama zishuke ili na wewe uuze za kwako. Anakiri kuwa soko hili limemnufaisha sana na anawashauri wengine wajiunge nalo wapate kunufaika pia.

Wengi wetu wenye mitaji midogo midogo tunaweza kunufaika kwa kujiunga na hili soko la hisa la Dar es Salaam na kununua vipande kwa pesa tuliyonayo. Vipande vingi vimeonesha kupanda thamani yake ikiwemo hisa za makampuni ya bia (TBL na SBL), Saruji (Twiga  na Simba ) na Bank kama NMB. Kama mwekezaji mzalendo, ukijitosa ukanunua hisa zako za 2,000,000 leo, baada ya miaka 4 unaweza kuziuza hata kwa faida kubwa tu bila kuteseka na usumbufu wa uendeshaji kama zilivyo biashara nyingine.

Upande wa pili soko hili la hisa pia lina magumu yake kama kupotea kwa mtaji wako kutokana na kushuka kwa thamani ya vipande. Hili kwa mfano, limewaathiri wawekezaji walionunua hisa za CRDB na TOL ambazo zimekuwa zikikumbwa na kushuka kwa thamani mara kwa mara. Muhimu ni kuwa makini tu kwa kuchagua vyema ni hisa zipi ununue na kampuni ipi uwekeze.

Soko letu limekuwa likiwanufaisha zaidi wageni na wananchi wa nchi jirani ambao hulitumia kikamilifu kujinufaisha na wazalendo wengi kutoelewa nini kinachoendelea. Kwa wale waliokwisha jitosa, huwezi amaini jinsi wanavonufaika na kuwekeza zaidi na zaidi.

Huu ni wito wangu kwenu wazalendo wenzangu, mkajiunge na soko la hisa la Dar es Salaam na kufaidi matunda yake!

Chanzo cha makala haya ni FIKRA PEVU.

Kuhusu Uwekezaji Tanzania

UWEKEZAJI TANZANIA ni mtandao unaokupatia maarifa na taarifa mbalimbali za uwekezaji kwa hapa nchini Tanzania.
Kupitia mtandao huu utajifunza fursa mbalimbali za uwekezaji na pia kupata taarifa zinazohusu uwekezaji.

 AINA ZA UWEKEZAJI TANZANIA.

Kwa bahati nzuri sana kuna aina nyingi sana za uwekezaji Tanzania. Kuna kila rasilimali na fursa mbalimbali za uwekezaji. Ugunduzi wa mafutra na gesi unaoendelea kufanyika Tanzania unaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi sana.
Kuna aina mbalimbali za uwekezaji zinazoweza kufanyika Tanzania.

1. Uwekezaji wa mali.

Tanzania kuna arhi kubwa sana ambapo mtu anaweza kununua na kuendeleza kwa kujenga majengo ya kibishara na hata makazi.
Pia ardhi hii inaruhusu kilimo na hivyo mtu unaweza kuwekeza kwenye kilimo cha biashara.

2. Bishara.

Kwa kuwa uchumi wa tanzania unakua kwa kasi sana mtu yeyote anayweza kuwekeza kwenye biashara anaweza kuapata faida kubwa. Biashara za bidhaa na huduma zinakua kwa kasi sana kutokana na ongezeko la watu na muingiliano wa kimataifa.

3. Uwekezaji katika maliasili na gesi.

Tanzania ina gesi nyingi sana ambayo bado haijachimbwa. Hii inatoa fursa kubwa sana ya uwekezaji.

4. Uwekezaji wa hisa na vipande.

Hii ni fursa nzuri ya uwekezaji kwa watu ambao wana miotaji kidogo. Soko la hisa la dar es salaa limeorodhesha makampuni mbalimbali ambayo mtu anaweza kununua hisa.
Pia dhamana ya uwekezaji UTT, inatoa fursa kwa watu kununua vipande na vipande hivyo kuongezeka thamani na hivyo kunufaika zaidi.
Kuna fursa nyingi sana za uwekezaji ambazo utajifunza kupitia mtandao huu.