Maswali Matatu Kwa Anayetaka Kuwa Mjasiriamali Kujiuliza Kutoka Kwa Richard Branson.

Richard Branson ni bilionea mwingereza ambae anamiliki makampuni ya VIRGIN. Chini ya virgin kuna makampuni karibu 400 na yote yako chini ya Richard.

branson

Richard Branson ni mmoja wa mabilionea ninaowakubali sana kwa sababu pamoja na utajiri mkubwa alionao bado anapata muda wa kuwafundisha watu wengine kupitia makala zake na vitabu vyake.

Leo nakushirikisha maswali matatu ambayo Richard anasema kila anayetaka kuwa mjasiriamali ni lazima ajiulize ili aweze kuwa na safari yenye mafanikio.

1. Je elimu ya juu ni muhimu kwangu?

Richard anasema ujiulize swali hilo kwa sababu pamoja na kwamba elimu ni muhimu bado haiwezi kuchukua nafasi ya kazi kubwa unayotakiwa kufanya unapoanza ujasiriamali. Hivyo kama unaendelea na elimu ya juu ili kupata ujuzi zaidi ni vizuri ila kama unataka kurudi shule ili kukwepa maamuzi magumu unayotakiwa kufanya kama mjasiriamali unapoteza muda wako.

2. Je napenda kuwa na bosi?

Richard anasema alianza biashara biashara akiwa mdogo sana kwa sababu hakuwahi kufikiria kufanya kazi chini ya mtu. Hivyo kama unaona huwezi kufanya kazi chini ya mtu basi ujasiriamali ndio njia yako.

3. Wanaonizunguka wanafikiriaje?

Richard anasema kama huwezi kuamua, omba ushauri kwa wale wanaokuzunguka. Wanaweza kukupa ushauri mzuri sana wa nini unaweza kufanya.

Angalizo; kwa mazingira yetu kuwa makini sana maana watu wako wa karibu wanaweza kuwa nao ni waoga kwenye ujasiriamali hivyo wakakuogopesha na wewe.

Kwa msaada zaidi tafuta mlezi (mentor) ambaye amewahi kufanya unachotaka kufanya na yeye atakuongoza.

Jiulize na kujibu maswali hayo matatu ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye ujasiriamali.

Nakutakia kila la kheri.

TUKO PAMOJA.

0 comments: