Sifa Unazotakiwa Kuzitambua Kwa Kiongozi Anayeweza Kuleta Mabadiliko.



Habari na karibu ndugu mpenzi msomaji wa blogu hii ya JIONGEZE UFAHAMU. Ni matumaini yetu umekuwa na wiki ya mafanikio sana.
Leo tutaangalia sifa unazotakiwa kuzitambua kwa mtu unayetaka awe kiongozi au unamtegemea awaongoze.
  1. Tabia
Mtu mwenye tabia nzuri au njema anakuwa na uaminifu, utiifu, nidhamu, kutegemewa, uvumilivu, kujitambua na pia anakuwa na bidii katika kazi. Wakati kwa upande mwingine mtu asiye na tabia njema au nzuri anakuwa hana uwezo wa kuwajibika kwa matendo yake, hawezi kukamilisha kazi kwa wakati, na pia hatimizi ahadi au majukumu yake.
  1. Kuhamasisha
Mtu ambaye anajua wapi anaelekea anakuwa na uwezo wa kuhamasisha wengine wafuatane nae kutokana na ahadi au mambo mazuri yanayopatikana kule anakoelekea. Kwa hiyo unahitaji kuangalia mtu Yule ambaye anafuatwa na watu wazuri na sio wale walio wa kawaida kabisa pia angalia huyu mtu anamtazama nani kama mtu anayemhamasisha bila shaka kwa Yule anayefaa kuwa kiongozi utamkuta anamfuatilia mtu ambae pia ni kiongozi na ana sifa njema


  1. Mtazamo chanya
Tafuta mtu Yule ambaye hana vizuizi katika akili yake kwa kuona jambo Fulani haliwezekani bali awe ni Yule mwenye nia ya kujaribu pamoja na kuwaza chanya kuwa atafanikiwa katika lile atendalo na anakuwa hazuiwi na vikwazo binafsi.
  1. Ufanisi mzuri katika kuwasiliana
Viongozi wazuri ni wale ambao wanaweza kuwasiliana vema, wanakuwa wanajihusisha vema na wale wanaoongea nao kwa kuweza kumtazama ana kwa ana pamoja na kuwa na tabasamu kwa Yule anayeongea naye. Kiongozi mzuri si Yule anayeweza kuwasilisha ujumbe wake lakini pia anakuwa na uwezo mzuri wa kusikiliza pia wale anaowaongoza.
  1. Kujiamini
Bila kujali hali gani katika wakati husika kiongozi pamoja na kundi wanapitia , kiongozi mzuri ni Yule anayekuwa anayejiamini na kuwa na ujasiri kuwa yeye pamoja na timu anayoiongoza wanaweza kusogea hatua kutoka walipofika
  1. Nidhamu

Kiongozi ni Yule mwenye nidhamu anayeweza kutawala hisia zake na pia ana uwezo wa kusimamia au kutawala muda wake jinsi ya kuutumia ili kumsaidia kupata mafanikio kwa ajili yake na timu anayoiongoza
  1. Rekodi nzuri ya mafanikio
Ni vizuri ukacheki historia yake ya nyuma ya utendaji wa mtu. Na kiongozi mzuri utakuta ana rekodi nzuri ya utendaji

Mwandishi: Goodluck Moshi
Mawasiliano:
Whatsapp: +255 753 201 994, Telegram: +255 658 201 994, Barua pepe: eng.gmoshi@gmail.com Facebook: Goodluck Moshi
Pia unaweza kutembelea blog yake www.stadizamafanikio.blogspot.com kujifunza zaidi.

0 comments: