Mambo Matatu Muhimu Yatakayokuletea Mafanikio.



Katika maisha ya binadamu kuna mambo matatu ambayo mtu anapaswa kuwa nayo ambayo yanaweza kumsababishia mafanikio. Mambo hayo matatu ni kama yafuatavyo;
1.      Kuwa na Maono
Kuna aina mbili za maono nayo ni maono makubwa na maono madogo na ni uamuzi wa mtu kuwa na maono makubwa au madogo. Maono ni kuwa na picha au ishara halisi ya maisha yako ambayo unatarajia kuwa nayo. Hivyo basi ukiwa na maono makubwa katika maisha yako ndivyo navyo mafanikio yako yanakuwa makubwa. Kwa hiyo maono ya mtu yanaweza kusababisha mafanikio makubwa.
2.      Kuwa na Ndoto
Kuna watu wengi wanaota ndoto lakini walio na ndoto ni wachache sana. Wako watu wengi wanaota usiku lakini wanaokumbuka nimeota ndoto gani ni wachache sana.
Ndoto ambazo ninaziongelea hapa siyo hizo za kuota usiku bali ni zile ambazo labda umekaa au umetembea huku unaona kitu au vitu kwa macho yako au ukakumbuka kuwa uliona vitu vikubwa vizuri na ukaanza kujisemea mwenyewe moyoni peke yako au hata kuwashirikisha wengine kuwa ungependa kuwa na hiki au kile au vile.
Watu ambao wanatembea katika ndoto na wenye ndoto katika maisha yao ni wale ambao wakati mwingine huwa wanatembea na ramani za nyumba au picha za nyumba  kubwa na nzuri au hata kuwa na picha nzuri ya gari ndani ya nyumba zao vitu hivi huwa vinamsukuma huyo kwa nguvu zote kwa kujituma ili kukamilisha ndoto yake .
Hivyo basi ni muhimu kila mtu kuwa na ndoto ya maisha yake ambayo yatasababisha kuwa na mafanikio makubwa.
3.      Kuwa na Malengo
Sasa ili uweze kukamilisha mpango wa ndoto yako au maono yako ni lazima uwe na malengo. Huwezi kuwa na lengo au malengo kama huna ndoto au maono. Malengo au lengo yanasaidia ,linakuwezesha ,linakuhamasisha  umetoka wapi? Uko wapi? Na unaenda wapi? Lengo litakuelekeza kuwa gari hii ni ya shilingi ngapi? Na pesa hizi nitazipataje?
Mafanikio yoyote katika maisha ni uamuzi wa mtu mwenyewe yaani kuwa na maono, ndoto na malengo. Hivyo basi yatupasa tuandike malengo, maono, ndoto katika maisha yetu.
Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com au unaweza kutembelea tovuti yake www.actualizeyourdream.blogspot.com

0 comments: