Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu UNPROFESSIONAL.
Habari rafiki, ni matumaini yangu waendelea vizuri. Wiki hii
tunaendelea na utaratibu wetu wa kushirikishana mambo 20 nilijifunza kwenye
kitabu. Leo tunaangazia kitabu
kinachoitwa UNPROFESSIONAL. Kitabu kimeandikwa na Jack Delosa. Kitabu hiki
kinaonyesha jinsi gani kijana Jack Delosa mwenye miaka 26 alivyoacha chuo na
kuanzisha biashara na kua milionea mdogo katika nchi ya Australia.
Unprofessional haimanishi kufanya mambo ya hovyo au kufanya mambo ya
kudharauliwa, Unprofessional ni njia ya kutoa changamoto kwa maisha ya mazoea
au kutoa changamoto kwa fikra za mazoea. Unprofessional ni Kubuni au kuvumbua
njia yako katika kusonga mbele kutengeneza kesho yako nzuri.
Karibu tujifunze mambo mengine
1. Usikubali sauti
yako ya ndani uzimwe na makelele ya sauti za watu huko nje. Hizo sauti za watu
wa nje zinataka uishi kama wao wanavyotaka...
Jifunze kujisikiliza, kuisikiliza sauti yako ya ndani ni muhimu sana.
2. Mjasiriamali
anayefanikiwa sana ni yule anayeweza kutengeneza vizuri ulimwengu ambao
haukuwepo. Ni yule anayeweza kutengeneza bidhaa au huduma ambazo hazikuwahi kuwepo
toka kuwepo kwa ulimwengu.
3. Kuna mambo
mengi ya muhimu katika dunia hii zaidi kuliko yale unayopaswa kujifunza
shuleni. Usifungwe kwenye kile ulichojifunza shule peke yake. Yapo ya muhimu na
mazuri sana ambayo hukuweza kujifunza shuleni. Kwa hiyo usiache kujifunza kisa
eti una degree 1 au 2 au 3….. Hata profesa anajua vichache sana, ukilinganisha
na vitu vilivyomo….
4.
Biashara haiwezi kukua kuzidi
mwanzilishi wake. Ukitaka biashara yako
ikue, lazima uanze kukua wewe kwanza. Ukiona biashara inadorora ujue mwanzilishi/mmiliki wake naye
kadorora. Kiwango chako cha kujifunza
ndicho kitakachoamua umbali gani biashara yako itafika.
5.
Ukiwa mjasiriamali lazima uwe
mchunguzi, mara zote uwe unavumbua
mipaka mipya ya fursa. See things invisible
6.
Kitu kikubwa katika dunia ya leo ni kuongeza thamani kwenye
maisha ya wengine na kuibadilisha dunia kua sehemu nzuri zaidi, Ukiweza kufanya
hivyo watu hawajali au hawataangalia kama una sifa rasmi au hauna, hawaangalii
wewe umesoma shule kiasi gani, kinachojalisha ni thamani gani unayoongeza kwa
watu na dunia.
7. Uhai wa
biashara yako utategemea thamani unayowapa wateja wako. Don’t let anyone,
especially the professionals, tell you any different
8. Usisubirie upewe
ruhusa au kibali, jiruhusu mwenyewe. Ruhusa/Kibali chako cha biashara ni uwezo
wa kua na ndoto ya vitu ambavyo havikuwahi kuwepo awali, na ujasiri wa
kuvijaribu.
9.
Kisababisho cha
kwanza kikubwa kinachosababisha kushindwa kwa biashara
nyingi hasa zinazoanza ni kukosa lengo
(focus). Waanzilishi wa biashara hizo wanataka kugusa kila kitu, kufanya vitu
vingi kwa wakati mmoja, matokeo yake hawafanyi vizuri kwenye jambo lolote.
Stick to the three rules of start-up: Focus. Focus. Focus.
10.
Mjasiriamali unapaswa uzungukwe na watu nadhifu/makini
kukuzidi wewe. Unatakiwa wewe ndio uwe
kilaza katika watu wanaokuzunguka. Wengi wetu tunapenda kuwepo kwenye makundi
ya watu ambao wanakubali na ambao tumewazidi uwezo wa kiakili au kiuchumi . Kwa
kawaida tunataka tukiwa kwenye makundi hayo sisi ndio tuonekane vichwa, na
tunapenda sisi ndio tuwe tunamiliki mazungumzo.
11.
Watu wa leo hakuna anayetaka kuuziwa, watu wanataka kununua
na siyo kuuziwa, unachotakiwa kufanya ni kumsaidia mteja wako aweze kununua.
Usijikite katika kuongea tu kuhusu biashara yako ili kumshawishi mtu anunue
bidhaa au huduma yako, bali mpe nafasi
mteja aeleze hitaji lake. It’s not about
‘selling’; it’s about providing the necessary leadership to enable your
customers to buy.
12.
Katika mwanzo wa biashara
mpya au mradi wowote mpya usiwekeze kwa kiwango kikubwa kwenye kitu
chochote kabla ya kujihakikishia kwamba huduma au bidhaa unayotaka kuitengeneza
ndiyo kitu wateja wanataka.
13.
Kama unaweza kupata kundi la watu ambao wanatafuta kile
unachotaka kuzalisha, basi kama ni vita basi umeshapata ushindi nusu. Nusu
iliyobaki itategemea na ubora wa bidhaa utakayo wapatia
14.
Wafahamu wateja wako vizuri. Katika biashara jinsi
unavyowafahamu/unavyowaelewa vizuri wateja wako, ndivyo utakavyoweza
kuwahudumia vizuri, na hii ndiyo itakayopelekea mafanikio ya biashara yako.
Jitahidi kujua kwa nini wananunua kwako, je wanapata wapi taarifa, Week end zao
hua wanakwenda wapi, marafiki zao ni kina nani, mara ngapi wananunua kutoka
kwako, kwanini wanapendelea bidhaa au huduma zako kuliko za washindani
wako, ndoto zao ni zipi, hofu za pia ni
zipi, wao wenyewe wanajionaje,
wanatamani kua nani. You need to get to know them better than they know
themselves. Kinyume na hapo utafunga biashara, au utaishia kua na biashara ya
kawaida sana.
15.
Anza kabla hujawa tayari. Hua hakuna muda muafaka wa kuanzisha
biashara, hakuna siku ambapo utakua na
muda wa kutosha, fedha au taarifa za
kutosha kuanzisha biashara, hakuna wakati ambapo utasema sasa niko tayari kila
kitu kipo sawa. Wajasiriamali halisi ni
wale wanaonza kuchukua hatua kabla hawajawa tayari. Wakati wengine wanahangaika
na kuweka mipango, kufanya utafiti au kusubiri, wajasiriamali halisi wao
wanaendelea kusonga mbele tu.
16.
Maono yako yanapokua makubwa ndio inakua rahisi kuyatekeleza.
Mara kadhaa tumekua tukijidanganya kwa kuamini kwamba tunapokua na malengo
madogo ndio inakua rahisi kuyafikia, lakini uzoefu umedhibitisha kwamba kinyume
chake ndio ukweli. Ukweli ni kwamba unapokua na maono makubwa ndiyo yanakua
rahisi kutekeleza, kwa sababu utapata watu ambao kweli watahamasishwa na maono
hayo na kutamani kua miongoni mwa maono hayo. Hakuna anayetaka kua sehemu ya
vitu vinyonge.
17.
Kikwazo kikubwa katika ukuaji wa kampuni au mashirika ni
pale waanzilishi/wamiliki wanapokua bado wanafikiri na kutenda vilevile kama
walipokua wakianzisha biashara hizo. Hii itakua kikwazo cha ukuaji mpaka pale
wamiliki watakapotambua kwamba wanasimamia kampuni au shirika ambalo linahitaji
uongozi wa tofauti kabisa na wakati wa uanzishwaji wake..
18.
Njia nzuri yenye ufanisi katika kujenga mahusiano mazuri na
soko lako unalolilenga ni kuwaelimisha wateja wako kuhusu suluhisho ambalo
wanafuata kwako kununua. Hii haimaanishi kuwaelimisha kuhusu biashara yako,
bali kuwaelimisha kuhusu suluhisho wanalokuja kutafuta kwako (bidhaa au huduma
unayouza). Kufanya hivyo utajenga imani kati ya wateja na biashara yako.
Regardless of what business you are in, today you are in the business of
education.
19.
Katika ulimwengu wa kibiashara ushawishi unajengwa kwa
kuzalisha kitu chenye maudhui makubwa (great content). Kama wewe ni mwandishi
hakikisha unayoandika yana uwezo wa kuongeza thamani kwa msomaji. Ukifanikiwa
kuandika vitu vyenye thamani, ushawishi kwa watu utakuja tu, utatengeneza
hadhira kubwa.
20.
Unapokua unataka kufanya ushirikiano wa kibishara wa
kimkakati (strategic partnership), kwanza fahamu ni kitu gani mwenzako
atanufaika nacho. Katika huo ushirikiano ni thamani gani uanyoweza kuitengeneza
mwenzako anufaike? Katika mwanzo wa
mazungumzo kitu cha msingi unapaswa kuonyesha jinsi gani huyo mshirika wa
kibiashara atanufaika kwanza. Ukitanguliza maslahi yako mbele hutafanikiwa.
What you want out of the partnership should be secondary.
Asanteni sana
Tukutane wiki
ijayo
Makala
hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri
katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au
barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com
6/01/2015 07:30:00 AM
|
Labels:
UCHAMBUZI WA VITABU
|
This entry was posted on 6/01/2015 07:30:00 AM
and is filed under
UCHAMBUZI WA VITABU
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment