Sababu 5 Zinazokufanya Wewe Kuishia Kukopa Kila Siku.

Watu wamekuwa wakifanya kazi kila siku ili kuweza kupata pesa ya kuendesha maisha yao ya kila siku . lakini wengi wao wamekuwa na desturi ya kuwa na madeni kila siku na kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo .Kuna madeni ya aina mbili nayo ni madeni ya Mabaya na mazuri .Mazuri ni yale unayokopa kwa ajili ya kuanzisha mradi Fulani na mabaya ni yale ya kukopa kwa ajili ya kula na siyo kuzalisha .Hivyo basi madeni haya ndio yana kufanya wewe kubaki kuwa masikini na kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.

Tuangalie sababu hizo ni zipi zinazokufanya wewe kila siku unaishia kukopa .

1. KUTOWEKA AKIBA.

Wahenga wanasema hivi Akiba haiozi ,hivyo basi kumbe kujiwekea akiba itakusaidia wewe kuondokana na madeni ya kila siku na kuachana na kukopa kabisa.Unaweza kujiwekea akiba kila siku kulingana na kipato chako ambacho una kipata kupitia biashara yako au mshahara wako wa mwezi .Haijalishi una kipato kikubwa kiasi gani kama wewe ni mtu wa kutumia tu bila kuweka akiba wewe ni masikini,

FAIDA ZA KUWEKA AKIBA

· Itakusaidia kwenye dharura ya ghafla inayoitaji hela

· Itakusaidia kupata mtaji

· Akiba haiozi

· Akiba ni ulinzi wako

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

2. KUTEGEMEA CHANZO KIMOJA CHA MAPATO

Hili ni tatizo kwa watu wengi kutegemea chanzo kimoja cha mapato mfano,mtu anategemea chanzo kimoja tu cha mapato yaani Ajira .Huwezi kufikia katika eneo la kujidai ,eneo la kuwa na uhuru wa kipesa (comfort zone)kwa kutegemea chanzo kimoja cha mapato.Ili kuepukana na madeni kila siku ambayo hayana tija kwako .Anza leo kuwa na vyanzo vya mapato yaani ’’ multiple streams of income ,money machines’’.

Fanya vyanzo vyako vya mapato kuwa kama matawi ya mti utakuwa na uhuru wa kifedha.

3. KUISHI JUU YA KIPATO CHAKO

Hili ni tatizo kwa watu wengi ,kujiingiza katika gharama zisizo za kilazima mfano ,mtu anapokea mshahara laki na nusu halafu matumizi yake ni zaidi ya laki tatu.

Je unafikiri mtu atayaepuka madeni ya kila siku?­­­­ jibu ni hapana. Anza kuishi chini ya kipato chako leo ,acha tabia ya kuigaiga Fulani amenunua simu mpya na wewe unataka ununue ili mradi tu na wewe uonekane upo kwenye chati kumbe unajimaliza mwenyewe bila kujijua. Haijalishi unakipato kikubwa kiasi gani yakupasa uishi chini ya kipato chako. “whatever your income live below your means

SOMA; Hii Ndio Sababu Kwa Nini Watu Wanafurahia Pale Unapoanguka...

4. KUTOJILIPA

Watu wengi wanafanya kazi sana na wana walipa watu wengine lakini wanajisahau kujilipa wao kwanza .Wewe ndio mfanyaji kazi unatakiwa kujilipa kwanza wewe.

pay yourself first” jilipe kwanza wewe 10% ya kipato chako hii itakusaidia sana kujiwekea akiba na kuondokana na kukopa kila siku.Anza leo kujilipa kama ulikuwa haujui hii fungua akaunti maalumu kwa ajili ya kuhifadhi pesa yako na usiiguse ndani ya miaka miwili utakuw mtu mwingine.

SOMA; Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

5. KUISHI BILA YA KUJIWEKEA BAJETI YA MATUMIZI YAKO

Kuishi bila ya kuwa na bajeti ya matumizi yako kwa mwezi ,wiki, siku ni sawa na kusafiri bila ya kujua unapokwenda. Ukiwa na bajeti itakusaidia kujua matumizi yako ya kila siku na kuweza kujiepusha na kukopa hivyo basi anza leo kuwa na bajeti yako ya matumizi.

‘’ ukijua unapokwenda katika safari yako utafika uendako’’

Makala hii imeandikwa na DEOGRATIUS KESSY ambaye ni mwandishi,mjasiriamali na mwamasishaji unaweza kuwasiliana naye kwa kupitia simu namba 0717101505 au kwa barua pepe (Email) deokessy.dk@gmail.com

ASANTE !

0 comments: