Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.

Kushindwa ni jambo ambalo haliwezi kukwepeka. Ila tofauti kubwa ya wale waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ni wale waliofanikiwa waliweza kuendelea hata baada ya kushindwa na wasiofanikiwa walikata tamaa baada ya kushindwa.

Kila mmoja wetu anapenda kufikia mafanikio makubwa kwenye jambo analofanya, inaweza kuwa kazi, inaweza kuwa masomo, inaweza kuwa biashara, inaweza kuwa chochote ambacho ni muhimu kwako.

SOMA; Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

Kuna vitu vitatu ambavyo vinawafanya watu wengi sana kushindwa kufikia mafanikio japo wanayatamani sana. Leo utajiongeza na vitu hivyo ili uweze kuviepuka na kufikia mafanikio unayotarajia.

1. Kuhsindwa kuendana na watu wengine.

Mafanikio sio kitu ambacho unaweza kukifikia wewe mwenyewe. Mafanikio yako yanategemea sana ushirikiano wako na watu wanaokuzunguka. Kama umeajiriwa kuna bosi wako, wafanyakazi wenzako na hata wafanyakazi walioko chini yako. Kama unafanya biashara kuna wateja, wafanyabiashara wenzako, wafanyakazi wako na kadhalika. Watu wote hawa wanaokuzunguka wana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yako. Ukiweza kushirikiana nao watakupa ushirikiano mzuri na utafikia mafanikio. Ukishindwa kushirikiana nao vizuri itakuwa vigumu sana kwako kufikia mafanikio.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

2. Kukata tamaa.

Kama tulivyoona hapo juu, tofauti ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni kwamba waliofanikiwa huendelea kufanya hata wanapokutana na magumu, ila wasiofanikiwa hukata tamaa haraka wanapokutana na vikwazo au changamoto. Kama kweli una kiu ya kufanikiwa inabidi uwe king’ang’anizi hata pale mambo yanapoonekana ni magumu.

3. Kuahirisha mambo.

Tabia ya kuahirisha mambo imewazuia watu wengi sana kufikia mafanikio. Mtu anaweka malengo na mipango lakini inapofikia kweye utekelezaji anaahirisha. Tabia ya kuahirisha inamfanya mtu kushindwa kuchukua hatua haraka na hivyo kukosa fursa nzuri za kupata mafanikio.

Epuka mambo hayo matatu kama kweli una kiu ya kufikia mafanikio. Kama utaendele akuyaendekeza utaona siku zinapota ila hakuna mabadiliko kwenye maisha yako.

Mwaka huu 2015 unahitaji nini tena ili kufanikiwa? Kila unachohitaji unajifunza kupitia AMKA MTANZANIA, KISIMA CHA MAARIFA, JIONGEZE UFAHAMU, na MAKIRITA AMANI. Kilichobaki ni wewe tu kuchukua hatua.

Nakutakia kila la kheri.

SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.

 

0 comments: