Mambo Kumi(10) Kuhusu Maisha Tunayoweza Kujifunza Kutoka Kwa Miti.
Miti niviumbe hai kama sisi, na ili kuendeleakuwa hai kuna mbinu mbalimbali ambazo viumbe hawa hutumia. Leo tutajiongeza na mambo kumi kuhusu maisha ambayo tunaweza kujifunza kwa kuangalia maisha ya miti.
1. Miti haijiwekei kikomo cha kukua, inakua mpaka mwisho wa uwezo wao.
Tofauti na mwanadamu ambaye anaweza kujiwekea kikomo cha mafanikio kwenye maisha yake, miti hukua biala ya kuchoka. Haijalishi hali ni mbaya kiasi gani miti huendelea kukua.
Ni muhimu kuendelea kukua kila siku.
2. Mapambano yao ya kuishi yanaifanya miti kuwa bora zaidi.
wakati baadhi ya watu wakikutana na matatizo wanazidi kuwa wadhaifu na wengine hata kukatisha maisha yao, miti inapokutana na matatizo ndio inazidi kuwa imara zaidi. Miti inapopata upepo ambao unatishiakuingoa kupeleka mizizi mbali zaidi ardhini. Inapokosa maji hupeleka mizizi mbali zaidi na hii yote huifanya kuwa imara.
3. Miti inachukua kile inachohitaji ili kuishi.
Miti inazungukwa na madini mbalimbali, lakinihuamua kuchukua madini yale inayohitaji kwa ukuaji wake tu. Ni muhimu kwetu kuwa wachaguzi wa vile ambavyo ni muhimu kwa maisha yetu.
4. Miti hufuata mwanga.
Bila ya kujali ni matatizo kiasi gani ambayo miti inapitia, mara zote huelekea upande wa mwanga. Mti unaweza kuwa umezungukwa na magugu, unawezakuwa unaliwa na wanyama wengine lakini hii haizuii yenyewe kuendelea kufuata mwanga ili kukua.
Ni muhimu kuangalia upande wa ukuaji hata kama upo kwenye matatizo.
5.Miti imejifunza kubadilika kutokana na mazingira.
Unapofika wakati wa kiangazi ambapo maji ni shida, miti hupunguza majani ili kupunguza maji yanayopotea kupitia majani hayo. Kiangazi kinapoisha na maji kuwa ya kutosha, hutoa tena majani.
Jifunze kubadilika kutokana na hali ya maisha.
6. Inatengeneza thamani kwa viumbe wengine.
Miti inatengeneza thamani kubwa sana kwenye maisha ya viumbe wengine. Miti inatoa hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe hai wote, inatoa chakula, inatoa kivuli na mengine mengi.
Hakikisha maisha yako yanakuwa na thamani kwa watu wengine.
7. Miti inaishi maisha yao wenyewe.
Mti hata ukiwa wenyewe unaendelea na maisha, na hata unapokuta kundi la miti, kila mti unakuwa na maisha yake wenyewe. Miti haiigani au kutaka kujionesha kwa wengine.
Ishi maisha yako, usiige ya wengine na wala usifanye mambo ili kuonekana.
8. Miti inatoa zaidi ya inavyopokea.
Miti inapokea maji, madini, na mwanga wa jua. Lakini inatoa chakula, hewa ya oksijeni, inaondoahewa ya kabondayoksaidi, inatoa kivuli, inatoa malazi na hata ikifa inatoa rutuba.
Mara zote penda kutoa zaidi ya unavyopokea, utapata mafanikio makubwa.
9. Miti ni vinganganizi.
Ili kuendelea kuwa hai miti ni vinganganizi na haikati tamaa. unaweza kukata mti leo na baada ya siku chache ukaota tena. Inajua kwamba maisha ni magumu na hivyo imejiandaa kushinda kwambinu zote.
Kuwa kinganganizi ili uweze kufikia malengo yako.
10. Miti imejijengea ulinzi wao wenyewe.
Kwa kuwa maisha ni magumu miti nayo imejifunza kuwa migumu. Ili isiliwe na viumbe wengine baadhi ya miti imejijengea vitu vya kuzuia isiliwe. Ili isipoteze maji mengi miti inayoota jangwani ina majani madogo sana ambayo pia ni miiba. Hii inaisaidia kuweza kuishi na pia kupunguza maji yanayopotea na kuepuka kuliwa na viumbe wengine.
Jipange najiwekee ulinzi kwa kuwa kuna watu wengi sana wanaokurudisha nyuma.
Tumia masomo hayo kumi kuboresha maisha yako.
Kumbuka kujifunza kila siku ni hitaji muhimu la wewe kufikia mafanikio.
1/11/2015 06:00:00 PM
|
Labels:
MBINU ZA MAISHA
|
This entry was posted on 1/11/2015 06:00:00 PM
and is filed under
MBINU ZA MAISHA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment