Mambo Matano Ya Uongo Uliyojifunza Shuleni.
Shule ni nzuri sana maana ndio imetuwezesha kusoma, kuandika na kuhesabu. Vitu vitatu muhimu sana ambavyo unavitumia kwenye maisha yako yab kila siku.
Shule hii hii imekufundisha mambo mengine ya uongo ambayo yamekuwa kikwazo kwako kufikia mafanikio.
Haya hapa ni mambo matano ya uongo uliyofundishwa shuleni.
1. Ukifeli shule umefeli maisha.
Umeaminisha kwamba kama utafeli darasani basi maisha yatakuwa magumu sana kwako. Ukweli ni kwamba hakuna uhusiano wa karibu kati ya kufeli shule na kufanikiwa maishani.
2. Umekuja mwenyewe na utaondoka mwenyewe.
Hii ni tabia ambayo umejengewa shuleni ya kufanya mambo mwenyewe ndio maana hata mtihani unapewa mwenyewe. Kwenye mitihani ya maisha ukiifanya mwenyewe ni lazima ushindwe, unahitaji ushirikiano wa watu wengine.
3. Soma kwa bidii, faulu, pata kazi nzuri na utakuwa na maisha mazuri.
Kama bado unaamini hili angalia idadi ya wahitimu ambao hawana ajira au angalia maisha ya wafanyakazi wengi yalivyo magumu.
4. Kujilinganisha na wengine.
Shuleni ulikuwa unalinganishwa na wanafunzi wengine kama vile mnafanana kwa kila kitu. Na ndio maana mlikuwa mnapewa mtihani mmoja kisha unaambiwa umefel au kufaulu kulingana na matokeo ya wengine. Huu ni uongo, wewe ni tofauti kabisa na binadamu mwingine yeyote.
5. Kuna jibu moja sahihi.
Shuleni na hasa kwenye mitihani umefundishwa kwamba kuna jibu moja sahihi, ukipata umepata na ukikosa umekosa. Kwenye maisha ni tofauti kabisa, kuna majibu mengi sana na yote yanaweza kuwa sahihi au sio sahihi. Inategemea na wewe mwenyewe.
Achana na mawazo haya potofu uliyofundishwa shuleni. Jua maisha yako yako chini yako na juhudi na maarifa ndio vitakuletea mafanikio.
TUKO PAMOJA.
10/10/2014 10:08:00 AM
|
Labels:
MBINU ZA MAISHA
|
This entry was posted on 10/10/2014 10:08:00 AM
and is filed under
MBINU ZA MAISHA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment