Hii ndio njia ya uhakika ya wewe kufikia mafanikio.
Mafanikio sio ajali au bahati. Ni kitu ambacho kila anayekitafuta anaweza kukipata kama atafuata njia sahihi ya kuzipata.
Nikuulize swali moja, kama unataka kupika mkate na hujui jinsi ya kupika mkate unafanya nini?
Jibu ni kwamba utatafuta njia yankujifunza kupika mkate. Iwe ni kusoma kitabu, kuangalia mapishi au vinginevyo.
Sasa ni kuulize ni lini umewahi kujifunza kuhusu mafanikio?
Sasa umeshapata jibu la kwanza kwa nini hufanikiwi, ni kwa sababu hujifunzi kuhusu mafanikio.
Leo nakupa njia ya uhakika ya kufikia mafanikio.
Jifunze vile ambavyo watu wenye mafanikio wanafanya na wewe uvifanye. Jifunze kwa kuongea nao na kwa kusoma vitabu vinavyohusu mafanikio.
Fanya kile wanachofanya, usijaribu kutafuta njia mpya, muda ni mfupi sana tumia njia hizo zilizodhibitishwa.
Anza kufanya hivyo sasa, na kama hujui pa kuanzia weka maoni yako hapo chini na nitakuambia uanzie wapi.
Nakutakia kila la kheri kwenye kuelekea kwenye mafanikio.
TUKO PAMOJA.
10/10/2014 05:33:00 PM
|
Labels:
MBINU ZA MAISHA
|
This entry was posted on 10/10/2014 05:33:00 PM
and is filed under
MBINU ZA MAISHA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment