Hizi ndio Hofu mbili ulizozaliwa nazo, nyingine ni uongo.

Hofu ndio kikwazo kikubwa cha wewe kushindwa kufikia mafanikio makubwa.
Hofu ya kushindwa, hofu ya kukataliwa, hofu ya kifo na nyingine nyingi zimekuwa zinakurudisha nyuma kila siku.
Habari njema ni kwamba hofu hizi sio sehemu ya maisha yako bali umejifunza tu. Hivyo ina maana unaweza kuondokana nazo kama zilivyokuingia.
Mtoto mdogo anazalia na hofu mbili tu; hofu ya kuanguka na hofu ya sauti kali.
Hofu nyingine zote umejifunza hivyo jifunze tena kuondokana nazo.
Jua kwamba unaweza kufanya mambo makubwa na hata ukishindwa sio mwisho wa dunia.
Nakutakia kila la kheri,
TUKO PAMOJA.

0 comments: