Vitu Vitatu Vitakavyokufanya Uwe Na Hamasa Ya Kufikia Mafanikio.

Hamasa ni kitu muhimu sana ili uweze kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya.
Hii ni kwa sababu katika njia yoyote utakayopita utakutana na vikwazo na pia katika yale utakayofanya utapata changamoto.
Bila ya kuwa na hamasa kubwa utaishia njiani kwa kukata tamaa haraka sana.
Uzuri ni kwamba unaweza kuhamasishwa na pia unaweza kujihamasisha mwenyewe.
Unahamasishwa unaposoma vitabu ja makala nzuri kama hizi unazosoma hapa kwenye JIONGEZE UFAHAMU, MAKIRITA AMANI, AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA.
Baada ya kupata hamasa hii unaweza sasa kuendelea kujihamasisha mwenyewe.
Ili kujihamasisha mwenyewe unahitaji kuwa na vitu hivi vitatu muhimu;
1. Kujisimamia.
Kama unajua kwamba unaweza kujisimamia mwenyewe unakuwa na hamasa kubwa sana ya kufanya vizuri. Hakuma mtu ambaye anapenda kupangiwa kila kitu cha kufanya, unapokuwa na nguvu ya kujipangia na kujisimamia unakuwa na hamasa ya kutekeleza mipango yako.
2. Kubobea.
Kama wewe ni mtaalamu wa kitu unachofanya unakuwa na hamasa kubwa ya kufanya kitu hiko. Kama umebobea na unatoa vitu ambavyo kila mtu anavikubali utahamasika kufanya zaidi ili wengi zaidi wanufaike na kile unachotoa.

SOMA; Kitu hiki kimoja ndio kitakufanya uanze.
3. Dhumuni.
Kama una dhumuni zuri la kuwasaidia wengine kwa kile unachofanya utahamasika kufanya zaidi. Kwa kuwa unajua watu wanakiutegemea kwa unachofanya na wanategemea kitu bora, hutotaka kuwaangusha. Hii itakuhamashisha ufanye zaidi na zaidi.
Hivyo ndio vitu vitatu muhimu unavyohitaji ili kujihamasisha. Habari njema ni kwamba kama huna vitu hivyo unaweza kujifunza. Na utajifumza kwa kujiunga ma KISIMA CHA MAARIFA ambapo mimi na wewe tutakuwa karibu zaidi.
Karibu sana.

0 comments: