NENO LA USIKU; Kabla ya kulala tafakari hiki.

Kama siku yako ya leo imekwenda vibaya, kumbuka kwamba huo sio mwisho wa dunia. Kuna kesho na kesho ni siku mpya unayoweza kufanya tofauti na kuweza kufanikiwa.
Kabla hujalala chukua kalamu na karatasi na uandike yafuatayo;
Mambo matatu uliyofanikisha na kufanikiwa leo.
Mambo matatu uliyopata changamoto au kushindwa leo.
Jiulize ni kipi cha kuendeleza kesho na kipi cha kubadilisha na kuboresha.
Ianze siku ya kesho ukiwa na hamasa kubwa.
Nakutakia kila la kheri, TUPO PAMOJA,

0 comments: