Mambo matatu yatakayokufanya uishi maisha marefu.
Magonjwa mengi yanayowafanya watu kufa wakiwa na umri mdogo yanatokana na mtindo wa maisha tunaochagua.
Magonjwa kama presha ya juu, kisukari na hata kansa yanatokana na mitindo mbalimbali ya maisha.
Hapa nakushirikisha mambo matatu unayoweza kuanza kuyafanya leo na ukapunguza nafasi ya wewe kupata magonjwa haya na hivyo kuishi miaka mirefu.
1. Kula vizuri.
Naposema kula vizuri namaanisha ule mlo kamili. Kula mafita kidogo na kwa mtu mzima kula wanga kidogo. Kula matunda na mboga ,boga kwa wingi na pia kunywa maji mengi.
2. Fanya mazoezi.
Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako. Na mazoezi sio lazima ulipie gym au kukimbia barabarani japo hiyo ni sehemu nzuri ya mazoezi.
Unaweza kuchagua kutembea kwa miguu badala ya kupanda gari, kupanda ngazi badala ya kupanda lifti na kusimama na kufuata kitu mwenyewe badala ya kuagiza uletewe.
3. Usivute sigara.
Kila unapovuta sigara moja unapunguza dakika 14 za maisha yako. Sigara ina kemikali zaidi ya elfu moja zinazosababisha kansa. Karibu kila kansa inayompata binadamu inaweza kuchochewa na uvutaji wa sigara.
Na sigara sio lazima uvute wewe, hata ule moshi unaovuta kutoka kwa watu wanaovuta sigara una athari kubwa kwa afya yako.
Hayo ndio mambo matatu ambayo unaweza kuanza kuyafanya leo na ukaboresha afya yako na kyongeza siku zako za kuishi.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
www.kisimachamaarifa.co.tz
www.amkamtanzania.com
11/29/2014 04:50:00 PM
|
Labels:
MBINU ZA AFYA
|
This entry was posted on 11/29/2014 04:50:00 PM
and is filed under
MBINU ZA AFYA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment