Tumia dakika hii moja kutatua matatizo yako ya kifedha.
Ukiacha hewa ya oksijeni tunayovuta, fedha ni kitu cha pili muhimu sana kwenye maisha ya kila mtu. Kama unapinga hilo acha kusoma hapa na usiendelee kulalamika kwamba maisha ni magumu.
Sasa leo chukua dakika moja tu kufanya mambo yafuatayo ambayo yatabadili muelekeo wako wa kifedha.
Matatizo makubwa unayopata kuhusu fedha yanatokana na matumizi mabaya ya fedha.
Sasa kuanzia leo kabla hujafanya maamuzi ya kutumia fedha, chukua dakika moja kujiuliza je matumizi unayofanya ni sahihi? Je watakuwezesha kufikia malengo yako? Je ni muhimu kwa maisha yako na ustawi wako?
Kama jibu ni hapana achana na matumizi hayo na wekeza fedha yako mahali ambapo utazalisha.
Kama hujui ni wapi unaweza kuanza kuwekeza fedha yako kidogo na ikazalisha weka maoni hapo chini na nitakupa siri moja kuhusu uwekezaji unaoweza kuanza kufanya.
Nakutakia kila la kheri,
TUKO PAMOJA.
10/06/2014 08:46:00 PM
|
Labels:
MBINU ZA MAISHA
|
This entry was posted on 10/06/2014 08:46:00 PM
and is filed under
MBINU ZA MAISHA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment