Mambo sita yatakayokufanya uwe na furaha zaidi.
Furaha sio kitu ambacho unapewa na mtu. Ni kitu ambacho kinatoka ndani yako mwenyewe. Kuna baadhi ya mambo ukifanya unaongeza furaha yako. Haya hapa ni sita kati ya mambo hayo.
1. Fanya mazoezi.
Kufanya mazoezi kunafanya mwili kuwa imara na hivyo kuweza kufanya mambo mengi unayotaka. Hakuna kitu kinachoondoa furaha kama kuumwa.
2. Pata usingizi wa kutosha.
Tafiti zinaonesha kwamba ukosefu wa usingizi unachangia sana kwenye msongo wa mawazo kitu ambacho kitakuondolea furaha.
3. Kaa mbali na simu yako.
Kukaa na simu yako masaa 24, kupokea kila simu, kujibu kila ujumbe na kuangalia kila kinachoendelea kwenye mtandao ni moja ya njia zinazochangia kukosa furaha. Zima simu yako kwa muda fulani, au iweke kwenye hali ya kimya kwa muda fulani.
4. Jumuika na watu halisi.
Katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii unaweza kuona unajumuika na watu kwa kuchat kwenye mtandao. Kama unakosa muda wa kujumuika na watu kwenye ulimwengu halisi ni chanzo cha kukosa furaha.
5. Jitolee kitu kwa ajili wengine.
Kutoa kunaongeza furaha. Usiseme huna cha kutoa, unaweza kujitolea muda wako kusaidia wasio na uwezo au kuelimisha wengine.
6. Shukuru kwa ulichonacho.
Kama kila wakati unalalamika kuhusu ugumu wa maisha au vitu ulivyokosa huwezi kuwa na furaha. Shukuru kwa vitu ulivyonavyo na hata kwa maisha unayoishi, utakuwa na furaha na utapata zaidi.
Fanya mambo haya sita na utakuwa na furaha kwenye maisha yako.
TUKO PAMOJA.
10/13/2014 07:40:00 PM
|
Labels:
MBINU ZA MAISHA
|
This entry was posted on 10/13/2014 07:40:00 PM
and is filed under
MBINU ZA MAISHA
.
You can follow any responses to this entry through
the RSS 2.0 feed.
You can leave a response,
or trackback from your own site.
0 comments:
Post a Comment