Kama Ulikuwa Hujui Bahati Inavyopatikana Soma Hapa.

Mara nyingi kwenye jamii zetu huwa tunawaona watu waliofanikiwa kama watu wenye bahati. Yaani walikutana na bahati ndio maana wamefikia mafanikio makubwa sana.
Inaweza kuwa kweli ila hujui nini maana ya bahati.
BAHATI NI PALE MAANDALIZI YANAPOKUTANA NA FURSA.
Hivyo ili na wewe upate bahati una kazi mbili za kufanya;
1. Kujiandaa kwa kiwango cha juu sana, weka mipango na jifunze.
2. Kutafuta fursa inayoendana na maandalizi yako.
Baada ya hapo mafanikio ni wewe tu kuendelea kuweka juhudi kubwa na kuendelea kujifunza kila siku.
TUPO PAMOJA.

0 comments: