Hii ndio faida ya kushindwa.

Moja ya vitu vinavyowazuia watu wengi kufikia mafanikio ni hofu ya kushindwa. Unaona kushindwa kama adui mkubwa ambae hupaswi hata kukutana nae.
Unakosea sana unavyofikiri hivyo. Kushindwa kunaweza kuwa kitu kizuri na kuwa na faida kubwa kwenye maisha yako.
Unaposhindwa unakuwa umejifunza ni njia au kitu gani hakifanyi kazi vizuri ja hivyo huwezi kurudia tena.
Unaposhindwa unakuwa imara zaidi na hivyo kuweza kufikia makubwa zaidi. Kumbuka mawimbi makali ndio yanayopima uhodari wa nahodha.
Hivyo usiendelee tena kuogopa kushindwa. Tumia kushindwa kama sehemu ya kujifunza na kukua zaidi.
Weka malengo makubwa na yafanyie kazi.
Nakutakia kila la kheri,
TUKO PAMOJA.

0 comments: