Kesho ni siku muhimu sana kwako, na itumie kufanya jambo hili moja muhimu.

Kesho ni tarehe moja mwezi wa kumi na mbili. Maana yake ni kwamba ni siku ya kwanza ya mwezi wa mwisho wa mwaka huu 2014.
Kuanzia kesho zitakuwa zimebaki siku 30 tu mwaka uishe!
Je mwaka huu 2014 uliendaje kwako?
Je malengo na mipango uliyojiwekea umeyatimiza!
Tumia siku ya kesho kutafakari mwaka huu umekwendaje.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.

Sheria Kumi Za Familia Za Kuzingatia


NENO LA LEO; Uwekezaji Unaolipa Riba Kubwa Sana

An investment in knowledge pays the best interest. –Benjamin Franklin

Uwekezaji kwenye elimu/ujuzi ndio uwekezaji unaolipa riba kubwa sana.

Anza sasa kuwekeza kwenye ujuzi na elimu yako, jifunze mambo mapya na yafanyie kazi.

Jinsi unavyojifunza zaidi ndivyo unavyoongeza thamani yako na hivyo kuongeza kipato chako.

Nakutakia siku njema.

UMUHIMU WA KUSOMA ZAIDI NA KUSOMA KILA MARA;

i. Jinsi unavyoishi jifunze jinsi ya kuishi, hakuna anayejua kila kitu.
ii. Viongozi bora wa uchumi mpya watakuwa ni wale wanaoweza kufikiri vizuri.
iii. Kufikiri vizuri kunajengwa na kusoma sana.
iv. Unachohitaji ili kubadili maisha yako moja kwa moja ni wazo moja tu kutoka kwenye kitabu sahihi.
v. Beba kitabu popote unapokuwa, ukiwa unamsubiri mtu soma, ukiwa kwenye foleni soma. Usipoteze muda wako kulalamika.
vi. Kama hujasoma kitu kizuri leo, hujaishi siku ya leo. Na kusoma huku sio habari, bali kitu kinachoweza kukusogeza karibu na malengo yako kweny maisha.
Kupata nafasi ya kusoma zaidi tembelea www.voraciousreaderstz.blogspot.com

Mambo matatu yatakayokufanya uishi maisha marefu.

Magonjwa mengi yanayowafanya watu kufa wakiwa na umri mdogo yanatokana na mtindo wa maisha tunaochagua.
Magonjwa kama presha ya juu, kisukari na hata kansa yanatokana na mitindo mbalimbali ya maisha.
Hapa nakushirikisha mambo matatu unayoweza kuanza kuyafanya leo na ukapunguza nafasi ya wewe kupata magonjwa haya na hivyo kuishi miaka mirefu.
1. Kula vizuri.
Naposema kula vizuri namaanisha ule mlo kamili. Kula mafita kidogo na kwa mtu mzima kula wanga kidogo. Kula matunda na mboga ,boga kwa wingi na pia kunywa maji mengi.
2. Fanya mazoezi.
Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako. Na mazoezi sio lazima ulipie gym au kukimbia barabarani japo hiyo ni sehemu nzuri ya mazoezi.
Unaweza kuchagua kutembea kwa miguu badala ya kupanda gari, kupanda ngazi badala ya kupanda lifti na kusimama na kufuata kitu mwenyewe badala ya kuagiza uletewe.
3. Usivute sigara.
Kila unapovuta sigara moja unapunguza dakika 14 za maisha yako. Sigara ina kemikali zaidi ya elfu moja zinazosababisha kansa. Karibu kila kansa inayompata binadamu inaweza kuchochewa na uvutaji wa sigara.
Na sigara sio lazima uvute wewe, hata ule moshi unaovuta kutoka kwa watu wanaovuta sigara una athari kubwa kwa afya yako.
Hayo ndio mambo matatu ambayo unaweza kuanza kuyafanya leo na ukaboresha afya yako na kyongeza siku zako za kuishi.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
www.kisimachamaarifa.co.tz
www.amkamtanzania.com

NENO LA LEO; Siku Mbili Muhimu Sana Kwenye Maisha Yako.

The two most important days in your life are the day you are born and the day you find out why. –Mark Twain

Siku mbili muhimu sana kwenye maisha yako ni siku uliyozaliwa na siku uliyojua kwa nini ulizaliwa.

Najua wengi tunajua siku tulizozaliwa ila ni wachache sana wanaojua kwa nini walizaliwa.

Kama bado hujajua kwa nini ulizaliwa kwaribu tusaidiane kujua kwa nini ulizaliwa, yaani ni nini hasa unatakiwa kufanya na maisha yako.

Andika email yenye kichwa cha habari KWA NINI NILIZALIWA na maelezo mengine muhimu kuhusu wewe kisha tuma kwenye email ushauri@kisimachamaarifa.co.tz

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Kuhusu Kuendesha Siku Au Kuendeshwa na Siku.

Either you run the day, or the day runs you. –Jim Rohn

Kwenye siku yako ni labda unaiendesha siku au siku inakuendesha wewe.

Unaiendesha siku pale ambapo unakuwa na malengo na mipango yako ambayo unaifuata.

Unaendeshwa na siku pale ambapo unafanya kile kinachotokea mbele yako.

NINAJUA UNAJUA UNACHOTAKIWA KUFANYA, FANYA SASA, LEO HII ILI UWEZE KUIENDESHA SIKU YAKO.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Unachohitaji Ili Kubadili Maisha Yako.

You can never cross the ocean until you have the courage to lose sight of the shore. –Christopher Columbus

Huwezi kuivuka bahari mpaka pale utakapokuwa na ujasiri wa kupoteza taswira ya ufukwe.

Tunapenda vitu vizuri lakini tunaogopa kupoteza tulivyo navyo. Huwezi kupata vitu vipya kama hutaacha hivyo ulivyonavyo sasa.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; MUDA MZURI WA KUPAMDA MTI.

The best time to plant a tree was 20 years ago. The second best time is now.

Muda mzuri wa kupanda mti ilikuwa miaka 20 iliyopita. Muda mwingine mzuri ni sasa.

Kila kitu kinahitaji maandalizi ya muda mrefu. Hivyo ili kuwa na maisha bora baadae inabidi uanze kufanya mabadiliko sasa.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; FURSA UNAZOZIKOSA.

You miss 100% of the shots you don’t take. –Wayne Gretzky

Unakosa asilimia 100 ya fursa ambazo hujazichukulia hatua.

Acha kuendelea kusita sita, unapoteza fursa nyingi na muda wako pia.

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa.

Nakutakia siku njema.

Hivi ndivyo shauku inavyokufanya kuwa mteja bila ya kupenda.

Sasa hivi tumekuwa watu wa kuendeshwa na shauku inayotokana na hisia. Na hii imetufanya tuwe wateja kwa wanaoweza kuzitumia hisia na shauku zetu.
Kwa mfano;
Kuna tofauti gani kwa anayenunua simu mpya iliyotoka leo kwa kusubiria muda mrefu na atakayekuja kuinunua kesho wakati kumetulia?
Kuna tofauti gani kati ya anayesikia habari mpya leo, BREAKING NEWS na atakayeisikia kesho?
Kuna tofauti gani kwa atakayekuwa wa kwanza kusambaza habari na ambae hatakuwa na haraka hiyo?
Yote haya na mengine mengi hayana tofauti ila yanatufanya tuwe wateja wa matoleo mapya, habari zilizovunjika na mbaya zaidi kusambaza habari ambazo hatuna uhakika nazo ili tu uwe wa kwanza......
Huna haja ya kuwa wa kwanza katika mambo haya, ni kujiongezea tu msongo.

NENO LA LEO; Kuhusu Fedha Kutonunua Furaha.

Watu wote wanaosema fedha haiwezi kununua furaha nao hawana fedha za kuwatosha. Sijawahi kumsikia tajiri akitumia kauli hiyo kwamba fedha haiwezi kununua furaha.

Hivyo basi badala ya kukubali tu kauli hiyo kwa nini usiifanyie majaribio? Kuwa na fedha nyingi halafu uone kama kweli zinaweza kununua furaha au la.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Tofauti Ya Washindi Na Washindwa.

Winners make goals... losers make excuses!

Washindi wanatengeneza malengo, washindwa wanatengeneza visingizio.

Amua leo kuwa mshindi na weka malengo na mipango mikubwa kwenye maisha yako. Acha sasa kutafuta visingizio.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Kuhusu Kujitetea.

It will do no good to argue if you're in the wrong. If you're right, you don't need to.

Kama umekosea au uko upande ambao sio sahihi, kujitetea hakuwezi kusaidia. Kama uko sahihi huna haja ya kujitetea.

Nakutakia siku njema.

NENO LA LEO; Mwalimu Bora.

The best teachers teach from the heart, not from the
book.

Mwalimu bora anafundisha kutoka moyoni na sio kutoka kwenye vitabu.

Nakutakia siku njema.