Mbinu 9 Za Kukuwezesha Kuamka Asubuhi Na Mapema Ukiwa Na Nguvu.
Kuamka asubuhi na mapema ni moja ya siri ya watu wenye mafanikio makubwa. Hii ni kwa sababu asubuhi na mapema akili inakuwa vizuri na hivyo kuweza kufanya majukumu yanayohitaji kutumia vizuri akili yako.
Pamoja na muda huu kuwa mzuri sana kwa kutekeleza majukumu, sio rahisi sana kuamka asubuhi. Watu wengi wamekuwa wakijaribu kuamka asubuhi lakini wanaishia kuzima alamu zao na kurudi kulala.
Leo hapa UTAJIONGEZA na mbinu 9 zitakazokuwezesha kuamka mapema na ukiwa na nguvu.
1. Soma kitabu au jarida dakika 30 kabla ya muda wa kulala.
2. Usile au kunywa pombe mda mfupi kabla ya kulala.
3. Weka simu au kompyuta yako mbali, mwanga wa simu na kompyuta hupunguza usingizi.
4. Usijiwekee majukumu mengi ya kufanya asubuhi. Fanya yale ambayo ni muhimu tu.
5. Panga kupata kifungua kinywa kizuri, hii itakuhamasisha kuamka mapema.
6. Fanya mazoezi, sio lazima yawe magumu.
7. Kunywa maji, itarudisha maji uliyopoteza kwa siku nzima.
8. Weka alarm yako kwenye chumba kingine ambapo utalazimika kuamka ili ukaifuate.
9. Pata jua la kutosha.
Unaweza kupitia mbinu hizi kwenye picha hapo chini.
1/18/2015 08:03:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Usianze Biashara Kama Hujui Kitu Hiki Kimoja.
Kama mwaka huu 2015 umepanga kuanza biashara usifanye kosa moja ambalo huwa linafanywa na wafanyabiashara wengi wanapoanza.
Usianze biashara kama hujui miaka mitano ijayo biashara yako itakuwa imefika wapi.
Ni muhimu sana kuwa na picha kubwa ya biashara yako ili unapoanza usisahau ulipotaka kufika.
Kama utaanza biashara ukiwa hujui miaka mitano utakuwa wapi hutafika popote. Maana biashara itakapoanza kukuchanganya utajikuta ukihangaika na matatizo yanayokusonga na kusahau kukuza biashara yako.
Pata picha ya kule unakokwenda kabla hata ya kuanza safari.
1/16/2015 06:29:00 PM | Labels: BIASHARA, MBINU ZA BIASHARA | 0 Comments
Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.
Tumejifunza sana kuhusu tabia za mafanikio. Na fikiri utakuwa unajua tabia kadhaa ambazo ukiwa nazo unaweza kufikia mafanikio unayotarajia kwenye maisha yako.
Lakini pamoja na kujua tabia hizo mbona watu wengi bado wanashindwa kufikia mafanikio?
Jibu rahisi ni kwamba wanaendelea kung’ang’ania tabia zile zile ambazo zinawafanya wasipate mafanikio.
SOMA; Huu Ndio Ushauri Muhimu Sana Wa Kuishi Nao Kila Siku Kwenye Maisha Yako.
Tabia hizo ni zipi basi? Zipo nyingi kulingana na makundi mbalimbali ya watu ila hizi saba zipo kwa watu wote ambao hawana mafanikio.
1. Kuahirisha mambo. Watu wote ambao hawajafanikiwa wana tabia ya kuahirisha mambo. Wataweka malengo na mipango mizuri sana ila wanapofika kwenye utekelezaji wanaanza kuahurisha. Wanajishawishi watafanya kesho cha kusikitisha ni kwamba kesho yao huwa haifiki.
2. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Hii ni tabia nyingine ya watu wasiokuwa na mafanikio, wanataka wafanye kazi, huku wanaangalia tv, wanachat kwenye simu na kuwa kwenye mitandao ya kijamii. Akili moja huwezi kuigawa kwenye mambo yote hayo na bado ikawa na ufanisi mzuri.
SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.
3. Kukubali kushindwa. Pale wanapokutana na changamoto au kikwazo wanakimbilia kusema wamejaribu ila wameshindwa.
4. Kupenda kuiga. Watu wasiokuwa na mafanikio hawana muda w akukaa na kufanya ubunifu wao wenyewe, wao hupenda kuiga kila kitu na mwishowe kujikuta kwenye wakati mgumu.
5. Hawajui njia bora za kujumuika na wengine. Watu wasiokuwa na mafanikio hawajui jinsi ya kujumuika na watu wenye mafanikio ili wajifunze mengi kutoka kwao.
6. Kufanya chochote ili waambiwe ndio. Watu wasiofanikiwa ni watu ambao wanapenda sana kuwaridhisha watu. Hujaribu kufanya chochote kile ili kuwafurahisha wengine na hivyo huishia kuwa na maisha magumu.
SOMA; Maisha Sio Rahisi Lakini Ni Mazuri Kama Hivi...
7. Kuhukumu. Watu wasiokuwa na mafanikio ni wazuri sana kuhukumu wengine. Hupend akufuatilia maisha ya wengine na kuhukumu kila jambo ambalo wanalifanya.
Epuka tabia hizi saba kama kweli unataka kufikia mafanikio kwenye maisha yako. Kama utaendelea kuzishikilia utajaribu kila mbinu lakini mafanikio hutoyaona.
1/16/2015 04:32:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Mbinu Kumi(10) Za Kuepuka Kuchoka Sana 2015.
Bado tupo kwenye mwanzo wa mwaka, na mwanzo wa mwaka kila mtu anakuwa na nguvu kubwa sana ya kufanya majukumu yake. Huu ni muda ambao kila mtu anakazana kujaribu kutimiza malengo yake.
Kadiri siku zinavyozidi kwenda watu wengi huanza kuchoka na mpaka kuja kufika mwezi wa kumi au kumi na moja asilimia kubwa ya watu wanakuwa wamechoka sana kiasi cha kushindwa kuwa na uzalishaji mzuri.
Hali hii ina madhara sana katika ufanisi wetu wa kazi na hata biashara. Na kama kweli unataka kufikia mafanikio makubwa, unahitaji kuwa kwenye ufanisi mkubwa kwa angalau mwaka mzima au wiki 50 kati ya wiki 52 za mwaka.
Leo hapa UTAJIONGEZA na mbinu 10 za kuepuka kuchoka sana mwaka huu 2015.
1. Upe mwili wako kazi. Kama kazi zako ni za ofisini au za kukaa, kufanya hivyo kila siku kutaufanya mwili wako uwe hovyo sana. Hivyo ni vyema kuupa mwili wako kazi, fanya mazoezi, cheza, tembea, kimbia, na hii ni kila siku.
2.Pata muda wa kutosha wa kulala. Kulingana na kazi zako unaweza ukasema huwezi kupata muda wa kutosha wa kulala, ila kulala kutaufanya mwili wako kuwa na nguvu na hata akili yako kuwa na ubunifu. Anza kulala nusu saa kabla ya muda wako wa kawaida wa kulala. Pia pata muda kidogo wa kulala mchana kama inawezekana kwako.
3. Pata dakika tano za kufanya tajuhudi/taamuli.
Hizi ni dakika chache ambapo unakaa kimya na kuondoa mawazo yote kwenye kichwa chako. Njia rahisi ya kufanya hili ni kukaa sehemu iliyotulia na kufunga macho yako kisha kuanza kuhesabu pumzi zako. Itakusaidia sana kusafisha akili yako.
4. Weka orodha ya vitu unavyoshukuru kuwa navyo. Haijalishi una matatizo kiasi gani kuna vitu unafurahi kuwa navyo, huenda ni familia inayokupenda, huenda ni biashara nzuri. Weka orodha hii na ipitie kila siku.
5. Kuwa na muda maalumu usiku ambapo unazima vifaa vyako vyote, yaani kompyuta, simu, tv na chochote kile. Fanya muda wako wa kupumzika kuwa wa kupumzika kweli.
6. Kuwa na picha inayokupa furaha na kukuhamasisha. Inaweza kuwa picha ya mtoto wako au kitu chochote. Itumie picha hii pale unapoona uvivu wa kufanya jambo.
7. Jisamehe. Kuna makosa mengi umeyafanya kwenye maisha yako, acha kuendelea kujitesa, jisamehe na songa mbele.
8. Kuwa mkarimu, wasaidie wengine, utaona mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako.
9. Tumia kipaji ulichonacho. Hata kama kazi au biashara unayofanya sio inayohusisha kipaji chako, tenga muda ambao utafanya kipaji chako. Kwa kufanya hivi utakuwa na nguvu na hamasa kubwa utaporudi kwenye kazi yako.
10. Fanya jambo moja kwa wakati. Kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja kutachangia wewe kuchoka haraka sana. Fanya jambo moja likiisha ndio uanze jambo jingine.
Hizi ni mbinu rahisi unazoweza kuanza kuzitumia leo ili kuhakikisha mwaka mzima unakuwa na ufanisi mkubwa sana.
Nakutakia kila la kheri.
1/16/2015 10:23:00 AM | Labels: BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Vitu Vitatu Vinavyoathiri Kipato chako Kwenye Chochote Unachofanya.
Katika uchumi tunaoishi, kipato chako kitategemea vitu vitatu;
- Nini unafanya. Kama unachofanya ni muhimu sana, basi hata kipato chako kitakuwa kikubwa.
- Unakifanya kwa kiwango gani. Kama unafanya kwa viwango vya juu sana basi kipato chako kitakuwa kikubwa. Kama unafanya kawaida basi kipato chako kitakuwa cha kawaida.
- Ugumu wa kukubadilisha. Kama ni vigumu kupata mtu mwingine anayefanya kama wewe basi thamani yako itakuwa kubwa na kipato chako kitakuwa kikubwa pia. Kama ni rahisi kupata mwingine, yaani unachofanya kila mtu anaweza kukifanya thamani yako itakuwa ndogo na kipato chako kitakuwa kidogo pia.
Hii ni sahihi kwenye kazi, biashara na hata shughuli yoyote ya kiuchumi unayofanya. Jitahidi uwe bora zaidi na kipato chako kitakuwa kikubwa sana. Haijalishi ni kazi au biashara gani unayofanya, kinachojali ni ubora unaotoa.
Dunia inalipa ubora.
1/15/2015 07:30:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Hii Ndio Hasara Ya Kutokuwa Na Malengo.
Kama huna malengo kwenye maisha yako, mtu mwenye malengo atakuajiri umtimizie malengo yake.
Kama huna ndoto kubwa kwenye maisha yako, mtu mwenye ndoto atakuajiri umkamilishie ndoto yake.
Na kama hujui unaelekea wapi na maisha yako, utajikuta unafuata kundi ambalo pia halijui linaelekea wapi.
Ni wakati sasa wa wewe kuacha kupoteza muda.
Kaa chini leo na uandike malengo yako, kisha weka mipango na anza kufanyia kazi mipango hiyo mara moja.
Kumbuka kauli mbiu ya mwaka huu ni JUST DO IT...
Usipoteze muda, anza sasa.
1/14/2015 08:12:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Maswali 12 Muhimu Ya Kujiuliza Ili Kuweza Kufikia Mafanikio.
Mafanikio ni kitu ambacho kila mtu anakazana kukifikia. Japokuwa kila mmoja wetu ana maana yake ya mafanikio, kila mmoja kuna kitu ambacho anapifana kukipata kwenye maisha yake.
Kitu hiki ambacho kila mmoja wetu anakipigania sio rahisi kupatikana. Ndio maana kuna watu wengi wanahangaika lakini bado wanaishia kukata tamaa.
Leo hapa UTAJIONGEZA na maswali kumi na mbili muhimu ya kujiuliza ili uweze kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya.
Jiulize na kujijibu maswali haya ili uweze kujua unaelekea wapi. Ingekuwa vizuri zaidi kama majibu yako utayaandika kwenye karatasi.
1. Ni kitu gani ninachotaka kwenye maisha?
2. Ni yapo machaguo yangu?
3. Ni dhana gani ambayo unatengeneza?
4. Nina majukumu gani?
5. Ninawezaje kufikiria tofauti na ninavyofikiri sasa?
6. Watu wengine wanafikirije kwa jambo hili ninalofikiri mimi?
7. Ni kitu gani ambacho nimejifunza kutokana na makosa ambayo nimewahi kufanya?
8. Ni kitu kitu gani ninachokosa au ninachokwepa?
9. Ni hatua gani ninazoweza kuchukua ili kuelekea kule ninakotaka?
10. Ni maswali gani muhimu nayotakiwa kuendelea kujiuliza na pia kuuliza wengine?
11. Nawezaje kubadili hali mbaya ninayopitia ili kuwa nzuri na kufaidika nayo?
12. Ni kitu gani kinawezekana?
Jiulize maswali hayo mara kwa mara kila wakati ambapo unakutana na changamoto au kikwazo na hata pale unapoweka malengo mapya.
1/14/2015 04:44:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
Mwaka huu nitaongeza kipato changu…
Mwaka huu nitafungua biashara yangu…
Nwaka huu nitaacha ulevi….
Mwaka huu nitaanza kufanya mazoezi…
Ndio tumekusikia na malengo yako ni mazuri sana, lakini je unakumbuka malengo haya haya uliyaweka mwaka jana? Na mwaka mwingine uliopita? Kwa nini hujayafikia mpaka sasa.
Kushindwa kujiuliza maswali haya kunakufanya uendelee kushindwa kufikia malengo yako.
Sababu kubwa ya watu kushindwa kufikia malengo yao inatokana na wao kutojua njia sahihi ya kuweka na kufikia malengo hayo. Leo hapa utajiongeza na sababu kumi kwa nini malengo yako hayatatimia mwaka huu 2015 ili uweze kuziepuka.
1. Unaweka malengo ambayo hayaeleweki.
Kwa mfano lengo “mwaka huu nitaongeza kipato” sasa kama kipato chako kwa mwezi kilikuwa milioni moja mwaka huu unaongeza na kufikia milioni moja na elfu kumi umetimiza malengo yako. Lakini kiuhalisia umeshindwa, unapoweka lengo hakikisha unajua ni kiasi gani unataka kufikia.
2. Huna njia ya kujipima.
Kama umeweka malengo halafu nuna njia ya kujipima kama kweli uko kwenye njia sahihi umejiandaa kushindwa. Kitu chochote ambacho hakiwezi kupimwa hakiwezi kufanyika. Jua ni kiwango gani unataka kufika na kila baada ya muda uweze kujitathmini umefika wapi.
3. Unaweka malengo ambayo hayapo ndani ya uwezo wako.
Japokuwa hakuna kisichowezekana, lakini ni vigumu sana kwako wewe kuweka malengo ya kutengeneza bilioni moja kwa mwaka huu wakati kwa sasa kipato chako ni laki mbili kwa mwezi. Kuweka lengo kama hili kunakukatisha tamaa badala ya kukusukuma kulifikia.
4. Huandiki malengo yako.
Kama unajisemea malengo yako na kuyaacha kichwani, subiri baada ya siku chache utakuwa umesahau kila kitu. Malengo na mipango yako yote ni lazima uiandike vizuri kwenye kitabu au karatasi.
5. Unaishi kwenye mazingira ambayo hayachochei malengo yako.
Kama watu wanaokuzunguka hawaoni umuhimu wa kuweka malengo na kuboresha maisha yao, upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kwenye malengo yao.
6. Unakata tamaa pale unapokutana na changamoto kidogo.
Changamoto ni sehemu ya safari hii ya kufikia mafanikio. Kama kila ukikutana na changamoto kidogo unakata tamaa itakuwa vigumu sana kwako kufikia mafanikio makubwa.
7. Unapoteza muda.
Muda ni muhimu sana kwako wewe kuweza kufikia malengo yako. Kama bado unaendelea kupoteza muda huwezi kufikia malengo yako.
8. Huna mfumo wa kukuwajibisha.
Kwa asili binadamu ni wavivu, kama ukijiwekea malengo yako mwenyewe kwa siri, hata usipoyafikia au kuyavunja unajua hakuna atakayejua au kukuuliza. Tafuta mtu ambaye anaweza kuwa anakufuatilia ili kujua kama unaendelea na malengo yako au la. Wakati mwingine tangaza hadharani, kwa mfano kama unataka kuacha pombe, mwambie kila mtu kwamba naacha kunywa pombe, kwa njia hii utaona aibu kunywa kwa sababu kila mtu anajua umesema unaacha.
9. Unaangalia na kusikiliza wengine wanafanya na kusema nini.
Popote ulipo umezungukwa na watu ambao hawajui maisha yao yanaelekea wapi. Hawana malengo yoyote na hawaoni umuhimu wake. Kama utajilinganisha na watu hawa huwezi klusonga mbele kamwe.
10. Umegoma kubadilika.
Kama unataka kuishi maisha yale yale ambayo umekuwa unaishi kila siku halafu unataka ufikie malengo yako nakushauri uache kujidanganya, hakuna kitu kama hiko. Unahitaji kubadilika wewe kwanza ndio mabadiliko mengine yatokee kwenye maisha yako.
Yafanyie mambo hayo kazi ili uweze kufurahia kufikia malengo yako.
1/14/2015 09:00:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Vipande Kumi Vya Ushauri Bora Kuwahi Kutolewa.
Tunaishi kwenye dunia ambayo kuna njia nyingi sana za kujifunza ili kufikia malengo yetu.
Unaweza kujifunza kwa kufundishwa, yaani kusoma au kukaa darasani au kupata aina yoyote ya mafunzo. Hii ni njia nzuri ya kujifunza.
Pia unaweza kujifunza kwa kushindwa kutokana na makosa yako. Yaani pale unapofanya jambo ukashindwa unajifunza njia ambayo imekufanya ushindwe ni nini na kutokurudia tena. Hii ni njia bora ya kujifunza maana hutosahau.
Njia nyingine unayowez akutumia kujifunza ni kupitia makosa au uzoefu wa watu wengine. Hapa unasoma au kuangalia kile ambacho watu waliofanikiwa wamefanya au hawafanyi na wewe kufanya kama wao. Hii ni njia bora sana ya kujifunza kwa sababu inakupunguzia muda ambao ungepoteza kwa kusubiri ujifunze kwa makosa yako mwenyewe.
Leo hapa utajiongeza kwa vipande kumi vya ushauri bora kuwahi kutolewa. Uchukue kama ulivyo na ufanyie kazi.
1. Haijalishi kama utatumia masaa 1000 kufanya kitu, kama unafanya kwa kukosea ulichojifunza ni jinsi ya kufanya kitu kwa kukosea.
2. Kama utamlaumu mtu mwingine usitegemee mabadiliko yoyote.
3. Usibishane na mjinga, atakayekuwa anaangalia kwa pembeni hatojua tofauti yenu.
4. Acha kuchukulia kila kitu binafsi, hakuna anayekufikiria wewe zaidi ya unavyojifikiria mwenyewe.
5. Kama unataka kukumbuka kitu kiandike mahali.
6. Fanya chochote unachofanya kama wewe ndio mtaalamu uliobobea, kila mtu atakuacha uendelee na kile unachofanya.
7. Jua ni kitu gani unachopenda kufanya, halafu fikiria ni jinsi gani mtu anaweza kukulipa kwa wewe kufanya kitu hiko.
8. Kama umekosea kubali kosa, kama uko sahihi kaa kimya.
9. Nunua kile ambacho utakitumia.
10. Mara zote kuwa na mpango, na mipango mingi itashindwa.
Hivyo ndio vipande kumi vya ushauri bora kuwahi kutolewa. Chukua ushauri huo na ufanyie kazi.
1/13/2015 09:00:00 AM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Hatua Tatu Za Kujua Kama Wazo Lako La Biashara Zuri.
Linapokuja swala la kufanya biashara watu wengi hupenda kutafuta ji wazo gani la biashara ni bora na linaweza kuwapatia faida.
Ukweli ni kwamba wazo moja la biashara haliwezi kuwa bora kwa watu wote. Wazo linaweza kuwa bora kwangu ila kwako likawa sio zuri au lisiweze kukuletea mafanikio.
Wazo bora la biashara linategemea na mtu anayetaka kufanya biashara yako.
Watanzania tumekuwa hatupendi kuumiza akili kutengeneza mawazo yetu ya biashara na hivyo kukimbilia kuiga, kitu ambacho kinatuumiza sana baadae.
Sasa leo hapa utajiongeza na hatua tatu za kutengeneza wazo lako la biashara ambalo litakuletea faida kubwa.
Wazo bora la biashara lina sifa hizi tatu;
1. Kitu unachopenda.
Hatua ya kwanza kabisa ya wazo bora la biashara ni kitu ambacho unapenda kufanya. Kama unapenda kitu unakuwa na shauku nacho na kupenda kukifuatilia zaidi.
2. Kitu ambacho upo tayari kukifanya.
Kupenda tu kitu hakutoshi, je upo tayari kukifanya? Je upo tayari kufanya kazi na kumwagika jasho? Je upo tayari kuvumilia hata pale mambo yatapokuwa magumu?
3. Kuleta thamani kwa wengine.
Sifa ya tatu ya wazo zuri la biashara ni kuwa thamani kwa wengine. Je watu wapo tayari kulipia bidhaa au huduma itakayotokana na wazo lako la biashara? Kama haliwezi kutengeneza thamani huna biashara.
Tumia njia hizi tatu kutengeneza wazo lako la biashara ambalo litakufikisha kwenye mafanikio.
Usiige tena, tumia akili yako, angalia mazingira yanayokuzunguka.
1/12/2015 08:15:00 PM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
Njia Kumu(10) Za Kupata Utajiri Na Mafanikio.
Fedha ni muhimu na kila mmoja wetu anakazana kila siku ili kupata fedha za kumtosha kuendesha maisha yake. Na pia tunakazana kupata fedha zaidi ili angalau kuwa na uhakika wa chochote kitakachotokea mbeleni.
Hivyo kujua njia za kupata fedha na hata kuwa tajiri ni muhimu ili usijikute ukihangaika sana na mwishowe kushindwa kupata unachotaka.
Katika kitabu cha RICH HABITS, The daily success habits of wealthy individuals, mwandishi Tom Corley amechambua tabia ambazo ameziona kwa watu matajiri na hata masikini katika utafiti aliofanya.
Zifuatazo ni tabia ambazo watu wenye mafanikio wanazo;
1. Kuweka malengo.
Watu wenye mafanikio wanaongozwa kwa malengo na mipango, watu hawa wana malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu na kila siku wanafanyia kazi malengo yao.
2. Kujifunza kila siku.
Watu waliofanikiwa wana tabia ya kujifunza kila siku. Huangalia njia za kuongeza maarifa yao, hujisomea na kuhudhuria semina mbalimbali zinazowafanya kuwa bora zaidi.
3. Kujali afya.
Watu waliofanikiwa wanajali sana afya zao. Wanakula vizuri na kufanya mazoezi mara kwa mara. Pia huepuka vyakula ambavyo sio vizuri kwa afya.
4. Kuweka mbele vitendo.
Watu wenye mafanikio ni watu wa kujali vitendo zaidi kuliko maneno. Ni watu ambao wakishasema wanafanya jambo fulani basi wanalifanya mara moja na sio kuvuta muda mpaka kusahau wanachotaka kufanya.
5. Wana mtizamo chanya muda wote.
Watu wenye mafanikio ni watu ambao wana mtizamo chanya juu yao binafsi na hata kuhusu maisha. Wanaamini wanaweza kufanya kile wanachotaka kufanya na hii huwafanya wafanikiwe zaidi.
6. Kuweka akiba.
Watu wenye mafanikio ni watu ambao huwa wanaweka akiba katika kila kipato wanachopata. Watu hawa huweka akiba kwanza na ndio kufanya matumizi. Wanaweka akiba asilimia 10 mpaka 20 ya kipato chao.
7. Kudhibiti matumizi.
Watu wenye mafanikio huishi chini ya kipato chao. Ni watu ambao hudhibiti matumizi na kuweza kuishi chini ya kipato wanachopata, wakitaka kuongeza matumizi wanaongeza kwanza kipato. Kwa njia hii wanaepuka kuingia kwenye madeni.
8. Kutokupoteza muda.
Watu wenye mafanikio wanaepuka sana kupoteza muda bila ya kufanya jambo la msingi. Watu wengi wenye mafanikio wanaangalia tv sio zaidi ya saa moja kwa siku.
9. Kufanya zaidi ya wanavyotegemewa.
Watu wenye mafanikio hufanya zaidi ya wanavyotegemewa kufanya. Kama wanategemewa kutoa huduma kwa kiwango fulani wao hupitiliza na kuwafanya kuwa wa thamani sana.
10. Kutokata tamaa.
Watu wenye mafanikio wameshindwa mara nyingi sana ila hawakukata tamaa. Wamekuwa na uvumilivu na pia ni vinganganizi mpaka wameweza kufikia mafanikio makubwa.
Je wewe unataka kufikia utajiri na mafanikio? Njia ndio hiyo hapo, kazi ni kwako sasa.
Nakutakia kila la kheri.
1/12/2015 05:01:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO, MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Maazimio Matano Muhimu Ya Fedha Kwa Kila Kijana Kuweka Mwaka Huu 2015.
Bado tupo kwenye msimu wa mwaka mpya na huu ni wakati muhimu wa kuweka maazimio na malengo mbalimbali ili kuboresha maisha yetu zaidi.
Huenda tayari umeshaweka malengo na mipango yako ya mwaka 2015, leo tutakumbushana mambo machache ambayo ni ya muhimu sana kuyajumuisha kwenye malengo yako ya mwaka huu 2015.
Kama bado hujaweka malengo mpaka leo bado hujachelewa, unaweza kukaa chini leo na kuandika malengo yako kwenye karatasi na kuanza kuyafanyia kazi.
Kama huna mpango wa kuweka malengo kabisa kwa mwaka huu pole…
Yafuatayo ni maazimio muhimu kuweka kwenye malengo yako ya kifedha kwa mwaka huu 2015;
1. Weka akiba zaidi ya ulivyoweka mwaka jana.
Kama mwaka jana ilikuwa unaweka akiba, mwaka huu ongeza kiwango cha akiba unachoweka. Kama huna utaratibu wakujiwekea akiba kabisa anza na kuweka pembeni asilimia 10 ya kile unachopata. Ukipata elfu kumi, weka elfu moja pembeni. Ukipata laki moja weka elfu kumi pembeni. Baada ya muda mfupi utaona mabadiliko makubwa ya kifedha kwenye maisha yako.
2. Punguza madeni yako.
Madeni ni mzigo, madeni ni utumwa, mtu anayekudai anaweza kunyanyasa utu wako muda wowote. Mwaka huu weka azimio la kupunguza madeni yako na kama ikiwezekana lipa yote kabisa. Kaa chini na wale wanaokudai na wape pendekezo la njia rahisi kwako kuwalipa kisha anza kuwalipa. Utanunua uhuru wako ulioupoteza.
3. Tengeneza, badilisha bajeti yako.
Ni muhimu sana kuishi kwa bajeti, kama mpaka sasa huna bajeti tafadhali sana tengeneza bajeti yako leo. Amua ni kiasi gani utakachoishi nacho kwa siku, wiki na hatimaye mwezi. Na jitahidi sanakuishi kwa kiasi hiko, usinunue vitu kwa tamaa tu, nunu kile ulichopanga kwenye bajeti. Kama umepanga mwezi huu hununui nguo, usishawishike kununua nguo hata ukikutana nayo nzuri kiasi gani, nguo nzuri huwa haziishi. Siku ambayo bajeti yako inaruhusu utapata nzuri kuliko uliyokutana nayo.
4. Jifunze kuhusu uwekezaji.
Bila shaka uwekezaji ni somo gumu sana kwa vijana. Wengi hawapendi kusikia kitu hiki na huona ni kitu kinachohitaji elimu kubwa. Ukweli ni kwamba uwekezaji ni rahisi na ni njia rahisi kwako kukuza kipato chako. Kuna aina nyingi za uwekezaji, kuna uwekezaji wa kununua mali, uwekezaji wa fedha na kadhalika. Unaweza kuanza kujifunza hapa hapa kwa kubonyeza maandishi haya
Soma; Hivi ndivyo unavyoweza kutajirika kwa kuanza na shilingi elfu moja.
5. Jijengee nidhamu ya fedha.
Kama hutakuwa na nidhamu ya fedha, yote tuliyojadili hapo juu hayataweza kukusaidia. Mara zote tumia pungufu ya unachokipata, yaani matumizi yako yasizidi mapato yako. Na pia kwenye kuweka akiba weka akiba na inayobaki ndio ufanye matumizi. Ukifanya matumizi ili inayobaki ndio uweke akiba hutabakiwa na kitu.
Wewe kama kijana ni muhimu sana kwako kujijengea misingi imara ya kifedha na kiuchumi. Weka maazimio hayo matano muhimu mwaka huu 2015 na anza kuyafanyia kazi.
1/12/2015 11:20:00 AM | Labels: FEDHA, SOKO LA HISA(DSE) | 0 Comments
Mambo Kumi(10) Kuhusu Maisha Tunayoweza Kujifunza Kutoka Kwa Miti.
Miti niviumbe hai kama sisi, na ili kuendeleakuwa hai kuna mbinu mbalimbali ambazo viumbe hawa hutumia. Leo tutajiongeza na mambo kumi kuhusu maisha ambayo tunaweza kujifunza kwa kuangalia maisha ya miti.
1. Miti haijiwekei kikomo cha kukua, inakua mpaka mwisho wa uwezo wao.
Tofauti na mwanadamu ambaye anaweza kujiwekea kikomo cha mafanikio kwenye maisha yake, miti hukua biala ya kuchoka. Haijalishi hali ni mbaya kiasi gani miti huendelea kukua.
Ni muhimu kuendelea kukua kila siku.
2. Mapambano yao ya kuishi yanaifanya miti kuwa bora zaidi.
wakati baadhi ya watu wakikutana na matatizo wanazidi kuwa wadhaifu na wengine hata kukatisha maisha yao, miti inapokutana na matatizo ndio inazidi kuwa imara zaidi. Miti inapopata upepo ambao unatishiakuingoa kupeleka mizizi mbali zaidi ardhini. Inapokosa maji hupeleka mizizi mbali zaidi na hii yote huifanya kuwa imara.
3. Miti inachukua kile inachohitaji ili kuishi.
Miti inazungukwa na madini mbalimbali, lakinihuamua kuchukua madini yale inayohitaji kwa ukuaji wake tu. Ni muhimu kwetu kuwa wachaguzi wa vile ambavyo ni muhimu kwa maisha yetu.
4. Miti hufuata mwanga.
Bila ya kujali ni matatizo kiasi gani ambayo miti inapitia, mara zote huelekea upande wa mwanga. Mti unaweza kuwa umezungukwa na magugu, unawezakuwa unaliwa na wanyama wengine lakini hii haizuii yenyewe kuendelea kufuata mwanga ili kukua.
Ni muhimu kuangalia upande wa ukuaji hata kama upo kwenye matatizo.
5.Miti imejifunza kubadilika kutokana na mazingira.
Unapofika wakati wa kiangazi ambapo maji ni shida, miti hupunguza majani ili kupunguza maji yanayopotea kupitia majani hayo. Kiangazi kinapoisha na maji kuwa ya kutosha, hutoa tena majani.
Jifunze kubadilika kutokana na hali ya maisha.
6. Inatengeneza thamani kwa viumbe wengine.
Miti inatengeneza thamani kubwa sana kwenye maisha ya viumbe wengine. Miti inatoa hewa ya oksijeni ambayo ni muhimu sana kwa maisha ya viumbe hai wote, inatoa chakula, inatoa kivuli na mengine mengi.
Hakikisha maisha yako yanakuwa na thamani kwa watu wengine.
7. Miti inaishi maisha yao wenyewe.
Mti hata ukiwa wenyewe unaendelea na maisha, na hata unapokuta kundi la miti, kila mti unakuwa na maisha yake wenyewe. Miti haiigani au kutaka kujionesha kwa wengine.
Ishi maisha yako, usiige ya wengine na wala usifanye mambo ili kuonekana.
8. Miti inatoa zaidi ya inavyopokea.
Miti inapokea maji, madini, na mwanga wa jua. Lakini inatoa chakula, hewa ya oksijeni, inaondoahewa ya kabondayoksaidi, inatoa kivuli, inatoa malazi na hata ikifa inatoa rutuba.
Mara zote penda kutoa zaidi ya unavyopokea, utapata mafanikio makubwa.
9. Miti ni vinganganizi.
Ili kuendelea kuwa hai miti ni vinganganizi na haikati tamaa. unaweza kukata mti leo na baada ya siku chache ukaota tena. Inajua kwamba maisha ni magumu na hivyo imejiandaa kushinda kwambinu zote.
Kuwa kinganganizi ili uweze kufikia malengo yako.
10. Miti imejijengea ulinzi wao wenyewe.
Kwa kuwa maisha ni magumu miti nayo imejifunza kuwa migumu. Ili isiliwe na viumbe wengine baadhi ya miti imejijengea vitu vya kuzuia isiliwe. Ili isipoteze maji mengi miti inayoota jangwani ina majani madogo sana ambayo pia ni miiba. Hii inaisaidia kuweza kuishi na pia kupunguza maji yanayopotea na kuepuka kuliwa na viumbe wengine.
Jipange najiwekee ulinzi kwa kuwa kuna watu wengi sana wanaokurudisha nyuma.
Tumia masomo hayo kumi kuboresha maisha yako.
Kumbuka kujifunza kila siku ni hitaji muhimu la wewe kufikia mafanikio.
1/11/2015 06:00:00 PM | Labels: MBINU ZA MAISHA | 0 Comments
Tabia Mbaya KUMI(10) Zinazopunguza Ufanisi Wako.
Huenda unatamani kufanya zaidi ya unavyofanya sasa lakini kila ukijitahidi huoni mabadiliko. Huenda una ufanisi mdogo kiasi kwamba kila mtu anakuona wewe ni mvivu sana.
Sio kweli kwamba wewe ni mvivu bali kuna tabia ambazo zinakufanya ushindwe kutekeleza majukumu yako kwa wakati.
Leo utajiongeza na tabia kumi mbaya ambazo zinakufanya uwe na uzalishaji mdogo na ukiweza kuziepuka utaongeza uzalishaji wako.
1. Unzanza siku yako bila ya kuipangilia. Usipopangilia siku yako utafanya nini utajikuta unafanya chochote kinachotokea mbele yako.
2. Unaangalia facebook au email kila baada ya dakika kumi. Kama mawasiliano yako yanakufanya uwe na shauku kubwa ya kutaka kujua ni nini kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii itakuwa vigumu sana kwako kukamilisha majukumu yako kwa wakati.
3. Unasubiri muda muafaka ndio ufanye ulichopanga kufanya. Kuna wakati unafikiri kama kitu fulani kikitokea basi nitafanya kitu fulani, mwishowe unaishia kutokufanya kabisa.
4. Unajaribu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Mwishowe unaishaia kushindwa kumaliza hata moja, kama mtu anayekimbiza sungura wawili, hakamati hata mmoja.
5. Unagoma kujifunza vitu vipya. Dunia ya sasa karibu kila kazi imerahisishwa sana. Kuna utaalamu mwingi ambao unaweza kuutumia kurahisisha kazi yako, ila unapogoma kujifunza unabaki nyuma.
6. Unasubiri mpaka dakika ya mwisho ndio ufanye jambo. Unapokuwa na muda wa kufanya jambo mara nyingi huwa unaona ni mwingi, ni mpaka muda unapokaribia kuisha unaona kwamba ulipoteza muda mwingi.
7. Unalaumu vifaa unavyofanyia kazi. Labda unasema kompyuta unayotumia ipo taratibu sana, mashine unayotumia inakurudisha nyuma. Hizi zote ni sababu ambazo hazina msingi.
8. Huna muda maalumu wa kula. Kama huna muda maalumu wa kula au wakati mwingine unaacha kula itakuwa vigumu sana kwako kuweza kuwa na nguvu ya kutekeleza majukumu yako.
9. Unatumia muda mwingi sana kupanga. Inawezekana unapanga, halafu unakaa unafikiria mipango yako, baadae unapanga tena. Kwa kupanga huwezi kutimiza chochote, unatakiwa kufanya kazi.
10. Huapati usingizi wa kutosha. Kama kila siku unachelewa kulala na kuamka umechoka ni vigumu sana kuweza kutekeleza majukumu yako.
Epuka tabia hizo kumi mwaka huu 2015 ili uweze kuongeza ufanisi wako.
1/11/2015 09:57:00 AM | Labels: MBINU ZA BIASHARA, MBINU ZA KAZI | 0 Comments
Hatua Nne Muhimu Unazohitaji Kupitia Ili kufikia Mafanikio Makubwa 2015.
Mwaka umeanza na mwaka unakaribia kukomaa. Kila mwanzo wa mwaka watu wengi huweka malengo mablimbali ya kufanya kwenye mwaka husika. Huenda na wewe umeweka malengo mengi kama ambavyo umekuwa ukifanya miaka iliyopita.
Lakini pia watu wengi wanaoweka malengo huwa hawayafanyii kazi hata kidogo. Zaidi ya asilimia 85 ya watu wanaoweka malengo husahau malengo yao wiki sita baada ya mwaka mpya.
Ili na wewe usiwe mmoja wa watu ambao wanasahau malengo yao au wanashindwa kuyafikia kuna hatua nne muhimu za kufuata ili kuhakikisha unafikia mafanikio makubwa kwenyemaisha yako.
Hatua hizo nne ni kama ifuatavyo.
1. Amua ni nini unataka kwenye maisha yako.
Ni lazima uamue ni kitu gani hasa unataka kwenye maisha yako. Jua kwa usahihi na kwa uhakika na uweze kusema kwa sentensi fupi ni nini unataka kwenye maisha yako.
2. Amua ni gharama gani upo tayari kulipa.
Kama ulikuwa hujui ni kwamba HAKUNA KITU CHA BURE, yaani huwezi kupata kitu pasi na kutoa kitu. Hivyo ili uweze kupata kile unachotaka kwenye maisha lazima uwe tayari kulipa gharama. Inaweza kuwa unahitaji kufanya kazi zaidi, au gharama nyingine yoyote.
3. Weka vipaumbele vyako.
Baada ya kuamua unataka nini, na baada ya kujua ni gharama gani upo tayari kulipa, weka vipaumbele vyako. Amua ni vitu gani utafanya na vingine vyote sema hapana. Jifunze kusema hapana itakusaidia sana kwenye maisha yako.
Soma; Mambo 30 ya kusema hapana mwaka 2015.
4. Fanya kazi.
Yote hayo tuliyojadili hapo juu yanachangia asilimia 1 ya mafaniko. Asilimia 99 ya mafanikio yako itatokana na kazi. Ni lazima ufanye kazi sana, hakuna longolongo hakuna janja janja.
Soma; Misingi mitatu ya kujijengea mwaka 2015.
Fuata hatua hizo nne na anza haraka kufanyia kazi malengo yako. Nina hakika utaweza kufikia mafanikio makubwa. Ila kumbuka kwamba itakuchukua muda, maana mafanikio sio kitu cha kutokea papo kwa hapo.
Nakutakia kila la kheri,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
1/10/2015 07:54:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments