Vitu Vitamu Muhimu Unavyohitaji Ili Kuingia Kwenye Biashara.
Ili kuingia kwenye biashara zama hizi unahitaji vitu vitatu tu;
i. Kidadavuzi mpakato(laptop)
ii. Simu ya mkononi yenye uwezo mkubwa(smartphone)
iii. Wazo.
Na wazo sio lazima liwe kubwa sana, linaweza kuwa wazo la kawaida sana ambalo wengine wanalipuuza.
Kama una vitu hivyo vitatu na hujui uanzie wapi niandikie kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Angalizo; uwe tayari kufanya kazi, sio lelemama...
12/13/2014 06:44:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Furaha.
Happiness is not something readymade. It comes from your own actions. –Dalai Lama
Furaha sio kitu ambacho kimetengenezwa tayari. Furaha inatokana na matendo yako mwenyewe.
Kama utakuwa na matendo yenye maana kwako na kwa wanaokuzunguka ni lazima yatakuletea furaha. Furaha hupewi na mtu mwingine.
Soma; HII NI HAKI YAKO YA KUZALIWA, USITEGEMEE KUPEWA NA WENGINE.
Nakutakia siku njema.
12/12/2014 07:30:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Mlango Mpya Wa Furaha
When one door of happiness closes, another opens, but often we look so long at the closed door that we do not see the one that has been opened for us. –Helen Keller
Mlango mmoja wa furaha unapojifunza, mlango mwingine unafunguka, lakini tunaishia kuangalia mlango uliojifunza kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kuona mlango mpya uliofunguka.
Acha kuangalia matatizo yako tuu, angalia pembeni na utaona fursa nyingi za kubadili na kuboresha maisha yako.
Nakutakia siku njema.
12/10/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Ni Mara Ngapi Unahitaji Kusimama Tena?
Fall seven times and stand up eight. –Japanese Proverb
Anguka mara saba, nyanyuka mara ya nane.
Haijalishi ni mara ngapi umeshindwa, cha msingi ni kuendelea tena.
Kukata tamaa ni mwiko kama kweli unataka kuyafikia mafanikio makubwa.
Nakutakia siku njema.
12/09/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Jambo Kubwa Na La Kushangaza.
We can easily forgive a child who is afraid of the dark; the real tragedy of life is when men are afraid of the light. –Plato
Tunaweza kumsamehe mtoto mdogo anayeogopa giza; ila jambo kubwa na la kushangaza kwenye maisha ni pale mtu mzima anapoogopa mwanga.
Ni kipi unachokiogopa kukifanya kwenye mwanga? Maana hiko ndio kinachokuzuia wewe kufikia mafanikio makubwa.
Nakutakia siku njema.
12/08/2014 07:12:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Hapa Ndio Unapoweza Kuanzia Na Hiki Ndio Unachoweza Kufanya.
Start where you are. Use what you have. Do what you can. –Arthur Ashe
Anzia hapo ulipo. Tumia hiko ulicho nacho. Fanya unachoweza.
Usipoteze tena muda kufikiri ni wapi pa kuanzia, uanze na nini au ufanye nini. Unachohitaji ni kuanza kupiga hatua na mambo mengine yote yatakwenda vizuri.
Nakutakia siku njema.
12/07/2014 08:17:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
KARIBU KWENYE MTANDAO WA AFYA IMARA
Kupitia mtandao huu utajifunza mbinu mbalimbali za kulinda na kuboresha afya yako.
Kama wote tunavyojua afya ni kiungo muhimu sana kwenye maisha yetu.
Bila kuwa na AFYA IMARA hatuwezi kufikia mipango na malengo tuliyojiwekea kwenye maisha yetu.
Tembelea mtandao huu kila siku ili uweze kujifunza kuhusu afya yako.
MAMBO UTAKAYOJIFUNZA KUPITIA AFYA IMARA.
Kupitia afya imara utajifunza mambo yafuatayo kuhusu afya;1. Dalili za magonjwa mbalimbali.
2. Jinsi ya kujikinga na magonjwa.
3. Mazoezi na afya.
4. Lishe kwa makundi mbalimbali ya watu.
5. Afya kwa makundi mbalimbali kama watoto, wanawake na wazee.
MASWALI NA USHAURI ZAIDI.
Kama una tatizo la kiafya ambalo ungependa kupata ushauri zaidi unaweza kuandika na ukapewa ushauri wa kitaalamu. Andika email kwenda afya@kisimachamaarifa.co.tz
Tujenge AFYA IMARA ili tuweze kuwa na maisha bora.
12/06/2014 07:13:00 PM | Labels: AFYA YA MTOTO, AFYA YA MWANAMKE, DALILI, JIKINGE, LISHE, MAZOEZI NA AFYA, MUONE DAKTARI | 0 Comments
Maswali matatu muhimu ya kujiuliza leo ili kujua muelekeo wa maisha yako.
Maswali matatu muhimu ya kujiuliza ili kujua ni nini unapaswa kufanya.
i. Ni kitu gani ambacho unajua unataka ukifanye ila bado unakipuuzia kukifanya?
ii. Ni kitu gani unaweza kukisimamia leo?
iii. Ni kitu gani haupo tayari kukiacha/kukiharibu hata kama kungetokea nini?
Kwa kujibu maswali haya utajua ni kipi muhimu kwako na anza kukifanyia kazi.
Kama bado unapata shida ya kujua ni kipi muhimu kwako karibu kwenye ushauri utakaokuwezesha kujijua zaidi. Andika email kwenda ushauri@kisimachamaarifa.co.tz
Nakutakia kila la kheri.
12/06/2014 06:53:00 PM | Labels: MBINU ZA MAFANIKIO | 0 Comments
NENO LA LEO; Chochote Unachotaka Kuwa Kipo Huku
Everything you’ve ever wanted is on the other side of fear. –George Addair
Chochote ambacho umewahi kutaka kipo upande wa pili wa hofu.
Acha sasa kuwa na hofu na chukua hatua kupata kile unachotaka.
Kumbuka hakuna kingine zaidi ya kuchukua hatua.
Nakutakia siku njema.
12/06/2014 07:45:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Umepangiwa Kuwa Mtu huyu…
The only person you are destined to become is the person you decide to be. –Ralph Waldo Emerson
Mtu pekee uliyepangiwa kuwa ni yule unayeamua kuwa.
Kama unaamua kuwa na mafanikio utakuwa nayo kweli na kama unaamua kuwa wa hovyo utakuwa wa hovyo.
Maamuzi ni yako, uchaguzi ni wako.
Nakutakia siku njema.
12/05/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Vikwazo.
Obstacles are those frightful things you see when you take your eyes off the goal. –Henry Ford
Vikwazo ni yale mambo ya kutisha unayoyaona pale unapoondoa macho yako kwenye malengo yako makubwa.
Ukishaweka malengo na mipango yako usiangalie tena pembeni, utaona mambo mengi ambayo yatakukatisha tamaa.
Nakutakia siku njema.
12/04/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuepuka Kupingwa.
There is only one way to avoid criticism: do nothing, say nothing, and be nothing. –Aristotle
Kuna njia moja pekee ya kuepuka kupingwa; usifanye chochote, usiseme chochote na usiwe chochote.
Vinginevyo chochote utakachofanya lazima kuna mtu atakupinga au kukukosoa.
Fanya kile unachoona ni sahihi kufanya na komaa nacho mapaka ufikie mafanikio.
Nakutakia siku njema.
12/03/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
NENO LA LEO; Jinsi Ya Kuua Hofu
If you hear a voice within you say “you cannot paint,” then by all means paint and that voice will be silenced. –Vincent Van Gogh
Kama unasikia sauti ndani yako inayokuambia huwezi kuchora basi kwa njia yoyote ile hakikisha unachora na sauti hiyo itanyamazishwa.
Usikubali kukatishwa tamaa na nafsi yako mwenyewe. Fanya kile unachohofia na hofu itakufa yenyewe.
Natutakia siku njema.
12/02/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments
SIKU YA UKIMWI DUNIANI; Mambo Kumi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ukimwi.
Kila tarehe 01/12 ya kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya UKIMWI. Siku hii imepewa heshma yake kutokana na madhara yake makubwa kwa watu wanaoupata.
Wakati tukiwa kwenye siku hii ya UKIMWI jiongeze na mambo haya kumi muhimu.
1. UKIMWI HAUUI.
UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga mwilini. Hivyo kinga yako inapopungua unatoa nafasi ya magonjwa mengine kukushambulia. Hivyo kinachowaua wagonjwa wa ukimwi sio ukimwi wenyewe bali magonjwa nyemelezi.
2. UKIMWI ni tofauti na VIRUSI VYA UKIMWI.
Ukiambukizwa virusi vya ukimwi leo, hauna ukimwi. Unawez akukaa na vizsi hivi kwa muda hata wa miaka kumi na pale kinga ya mwili inaposhindwa kukulinda na magonjwa ndio unakuwa na UKIMWI.
3. Wagonjwa watatu wa kwanza wa UKIMWI Tanzania waligunduliwa katika hospitali ya Ndolange mkoani Kagera mwezi November 1983.
4. UKIMWI husambazwa kwa kupitia maji maji ya mwilini. Yanayoongoza ni damu, na yenye kiasi kidogo ni mate, machozi na majimaji ya ukeni.
5. Njia kuwa ya kusambaza ugonjwa huu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine ni kufanya mapenzi bila ya kujikinga. Njia nyingine ni kuchangia vitu vikali kama sindano na pia mama kwenda kwa mtoto.
6. Mpaka leo hakuna tiba wala kinga ya UKIMWI. Baadhi ya tafiti zimeonesha matokeo mazuri ila hakuna ambayo imedhibitishwa kutumiwa kama kinga au dawa.
7. Afrika chini ya jangwa la sahara ndio sehemu yenye maambukizi makubwa ya UKIMWI, asilimia 80 ya watu wenye ukimwi duniani wako Africa chini ya jangwa la sahara. Wakati idadi ya wanachi walioko Afrika chini ya jangwa la sahara ni asilimia 10 tu ya idadi ya watu wote duniani.
8. Wanawake wana hatari mara nane zaidi ya kuambukizwa ukimwi kuliko wanaume.
9. Mikoa inayoongoza kwa UKIMWI Tanzania ni Njombe ukifuatiwa na Iringa na mikoa yenye maambukizi madogo ni Pemba, Unguja na Lindi.
10. Mapambano ya UKIMWI yanaanza na mimi na wewe. Njia nyingine za maambukizi zimeweza kuzuiwa kwa kiasi kikubwa ila njia moja ndiyo yenye changamoto na njia hiyo ni kupitia kufanya mapenzi.
Tushirikiane kuutokomeza UKIMWI.
12/01/2014 01:00:00 PM | Labels: MBINU ZA AFYA | 0 Comments
NENO LA LEO; Kisasi Bora
The best revenge is massive success. –Frank Sinatra
Kisasi bora ni mafanikio makubwa.
Kama mtu amekufanyia jambo baya na unataka kulipa kisasi, kisasi bora kulipa ni kuhakikisha unafanikiwa sana.
Nakutakia siku njema.
12/01/2014 07:00:00 AM | Labels: NENO LA LEO | 0 Comments